Jerry Muro na wengine wawili wakitoka selo na kuingiwa kwenye chemba ya mahakama ya kisutu leo kusomewa mashataka ya kula njama ya kula rushwa ya shilingi milioni 10.

Angalizo: Hii kesi imeshafika pahala pake na hatma ya washtakiwa iko mikononi mwa Mahakama na si vinginevyo. Hivyo mdau unapoleta maoni ambayo yanaweza kuingilia mwenendo wa kesi hii tafadhali nakusihi uwe makini tuheshimu Mahakama tafadhali. Samahani lakini kama nitakuwa nimewakwaza, si mnajua tena mambo ya kei vii oww ei.....

- Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 32 mpaka sasa

  1. Haitian Courts! Haitian Justice! Yaani serikali inatumia pesa za walipa kodi kuendesha kesi za kipuuzi kusikiliza mtu ambaye serikali ilithibitisha ni mwizi aliyekuwa anaiibia serikali!!! Kuna kesi za watu walioonewa zinapigwa kalenda tu.

    Ndio maana hata mafisadi papa wameachwa vimekamatwa vidagaa. Kwa mtindo huu lolote linaweza kumpata Jerry! Laana Tupu

    ReplyDelete
  2. we michuzi acha hizo kijana, sasa maoni yataingiliaje mwenendo wa kesi??? au umeyachoka maoni yetu??? sikutegemea kama ungekuwa na mawazo kama hayo kijana. sasa tusipoongea unataka tukaongelee wapi??? au Kova amewaonya kuwa hataki vyombo vya habari mtoe maoni ya watu??? you can't be serious man sioni ni kwa jinsi gani maoni kwenye blog yako yanaweza kuingilia mwenendo wa kesi iliyoko mahakani kisutu. Badilisha kauli kijana umechemka. hata oni langu lisi[poona mwanga wa jua lakini ujumbe umeupata. kama wewe muoga basi bora ufunge blog yako, wewe unataka tuongelee harusi tu. haiiniingii akilini and can't the words are from you.

    ReplyDelete
  3. mimi nashangaa sana serikali yetu,insu hii ya Jerry Haina hata wiki mbili tayari ipo mahakamani,izo inshu kubwakubwa za vigogo wa serikali mabilioni ya pesa zinachukua miezi na miezi kufika kortini,hiyo pingu inayosemekana Jerry anamiliki na tumeona hadi risiti ya serikali iweje auuziwe??mwenyemakosa nani aliyenunua ama serikali iliyomuuzia?ni aibu sana kwa Taifa.

    ReplyDelete
  4. kwa swala hili i support Michuzi. yeye ni professional journalist, anaelewa kuwa anaweza kufungwa jela kwa kuruhusu maoni yanayoenda kinyume na sheria.

    tatizo watu hawajui sheria zinasemaje, na pia hawataki kujishughulisha kuelewa.

    kuna kitu kinaitwa contempt of court, huruhusiwi ku-publish au kutangaza maoni yanayokinzana na kesi iliyoko mahakamani.

    ungemwuliza Michuzi kwa utaratibu kwanini? angekuelewesha sababu, badala ya kubwabwaja wakati hujui unakosoa nini.

    ReplyDelete
  5. Kazi kweli kweli!!!! Mwaka huu sijui? tuombe uzima tu, sijui utaishije. Kwa vitisho mhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  6. hapo sasa patamu kakak jerry hao hawafanyi utani watakumaliza ndugu yangu kama wameamua kukupeleka mahakamani juwa wazi ushahidi umekamilika na hawana shaka lolote .umekwisha mdogo wangu

    ReplyDelete
  7. Hahahaha naungana na anon wa 04:45:00PM hapo juu, kweli Mzee wa fulanaaz unazeeka sasa. Hilo "angalizo" mbona limekaa kiujimaujima. Au hii ni Exit Strategy ya Polisi na watu wa usalama mmeitwa kuhakikisha sauti hazisikiki tena?. Hebu jibu maswali yafuatayo kwanza.

    1. Blog yako imesajiliwa kwa mujibu wa sheria ya vyombo vya habari TZ? au ni mali ya "Google USA"

    2. Iweje maoni yaingilie muendenendo wa kesi wakati sidhani hata kama mahakimu wa TZ wanajua kutumia mtandao zaidi ya kuwapatia makarani kutype mashauri yao kwenye Ms Word?, Je jeshi la polisi linafanya uchunguzi kupitia maneno ya kwenye blog?

    3. Wewe michuzi ukichukua maoni yetu na kuyapeleka daily news ndiyo utakuwa unaingilia muenendo wa kesi lakini ukiyaacha hapa basi ujue ni mali ya "Google" na wanajamii wote wanaopenda uhuru wa kutoa na kusoma mawazo mbalimbali

    4. Najua umeweka disclaimer ili usiingie matatani kama Jerry maana sasa hivi mnatishwa sana kwani kumbuka Jerry naye yupo TBC chombo cha serikali pia, so hakikisheni hamuingizwi kwenye matatizo kwa kuitwa kufanya kazi na watu msiowajua?

    ReplyDelete
  8. Angalizo: Hii kesi imeshafika pahala pake na hatma ya washtakiwa iko mikononi mwa Mahakama na si vinginevyo. Hivyo mdau unapoleta maoni ambayo yanaweza kuingilia mwenendo wa kesi hii huenda yasione mwanga wa jua hivyo usijisumbue na hata ulalame vipi haitosaidia. Tuheshimu Mahakama tafadhali - Michuzi
    ===================================
    Michuzi, with all due respect, kwa nini hairuhusiwi kutoa maoni juu ya shauri hili humu? Ni mara ya kwanza kuona ONYO hili kwenye blog hii. Kwa sababu gani? Kuna nini? Itaathiri vipi mwenendo wa kesi iwapo kamanda wa polisi kanda ya Dar mwenyewe alikuwa anatumia vyombo hivi kuwa 'parade" watu ambao bado ni watuhumiwa tu? Kama wafuatiliaji wengine, ninaomba utueleweshe hapo. Vinginevyo, kwa mtazamo wangu, ninaomba maoni / mawazo yote humu yaone "mwanga wa jua" (kutumia msemo wako) ili sote tuelimike. Ninawakilisha

    ReplyDelete
  9. Mtoto wa CoastFebruary 05, 2010

    Michuzi, Shukrani kwa angalizo.

    Lakini ukweli unabaki kuwa blogu hii ni kijiwe binafsi (personal property).

    Ndio maana wengine huwa tunasema kuwa matangazo toka Ikulu au Wizarani hayawezi kuwekwa officially hapa kwako ila unayachukuwa tu kuyaendeleza katika hiki kijiwe kwa yeyote anayeweza kufaidi.

    Hivi kweli Michuzi unatuambia kuwa hata nyumbani kwake Afande Kova sasa hawajadili au kutafakari kesi hii eti kwa kuogopa kuingilia mahakama.
    Au Maafande wakiwa kwenye kijiwe (mesi) yao hawazungumzii kabisa hii kesi?

    Kuna sehemu kweli kama Bungeni au katika Press conference au mihadhara au katika media za umma kesi hii sasa haijadiliwi.

    Tunaposema hii ni blogu ya jamii hatuna maana kuwa inamilikiwa na jamii bali tuna maana kuwa inajali ustawi wa wananchi basi!


    Hata hivyo kwa nini tunafikiri kuwa kuathiri Kesi lazima kuanze sasa mbona mengi yamesha semwa na kutundikwa katika jamii?
    Kama kuna Prosecutor au Hakimu yeyote ataamua kujilegeza na kutotumia taaluma yake na au kutupilia maadili ya kazi yake sasa basi anaweza pia kufanya hivyo wakati wowote lakini AJUE KUWA NAYE ANASUBILIWA KUONEKANA KATIKA HUKUMU ITAKAYOTOLEWA NA JAJI WA MAJAJI SIKU YA KIYAMA NA MALIPO HUANZA HAPA HAPA DUNIANI.

    ReplyDelete
  10. Wewe Mithupu naona sasa unatumiwa...!!

    ReplyDelete
  11. Mie namiliki pingu aina ya CABLETISER Hahahahah je kwa IQ ya polisi wa kibongo anaweza jua kama ni pingu pia???????

    ReplyDelete
  12. Waandishi wengi walicheka pale Kova aliposema kuwa "kwa nini Jerry ana pingu....?" na kuwa yeye kuwa "investigative reporter" pingu hazihusiani na kazi yake. Pengine (Kova)ana ukweli hapo. Mimi pia ni mwandishi na ninazo pingu (ki-halali) kwa kuwa mpenzi wangu anapenda tutumie hizo wakati tukijamiiana. Je ni kosa? Ninaomba mwongozo.

    ReplyDelete
  13. Nchi hii wananchi hawathaminiwi kabisa. Kwa mtazamo wa serikali wananchhi ni wapiga kura tu. Ndio maana kila mtu kapewa kitambulisho cha mpiga kura kwa haraka sana. Wakati vitambulisho vya taifa zoezi lake gumu. Watanzania ni ma "zombies" wanaokwenda kupitisha chama tawala kila wakati wa uchaguzi. Hii nchi ni ya MANJAGU NA CHAMA TAWALA. Wengine Vitisho tu!

    ReplyDelete
  14. ...Ankali ni ushauri wa kisheria umeupata mpaka kuweka "ONYO" au ni COPY and PASTE....????
    Hebu ona hii
    "Mwanzoni mwa mwaka huu Thesun Newspaper ilidokeza kuna kocha wa Ligi kuu ya UK alionekana kunako/siko hawakuweza kumtaja kwa jina wakati ule.
    Lakini baada ya Mahakama kupiga chini maomba ya Terry kuhusu kutaka kufichiwa mafyoso yake, then ndo wakawa wamefungulia bomba. Watu wamemtaja Avram kama mzee aliyeonekana chobisi.
    Ona sasa jamaa walivyotumia logic...kumbuka ni issue mbili tofauti lakini watu wametumbikiza akili!
    Je, hapa kwa Michu hakuna pa kutokea au???

    ReplyDelete
  15. siamini na nasema tena siamini na wewe michuzi unatumiwa na unaogopa serikali

    ebu tupe sababu nzito 3 maoni yetu umu ndani yatakuponza wewe au sie tunaochangia (sheria inasemaje)

    SIJAWAI BOREKA NA KUKKUONA WA AJABU TOKA NIANZE SOMA HII BLOG,,kumbe sio ya jamii??unatupa sisi angalizo/warning!!

    pili apa sio maswala ya kukwazana km unavodai,ni kuelewa/kueleweshwa ktk ili,,,siamini kila kitu Tz kimetawaliwa na mafisadi papa

    Mungu ingilia kati

    ReplyDelete
  16. we anony wa 04:59 unaijua sheria wewe??? au anabwabwajabwabwaja tu?? hicho ulichoandika hapo unakijua mapana yake na wigo wake?? wewe sasa ndo unaeropokaropoka bila kufikiri. hata wanasheria waliobobea huwa wanatoa maoni yao wakati kesi tena nyeti zikiendelea mahakani, na wanajua sheria inawaruhu kufanya hivyo sasa wewe na kidigrii chako kimoja na sheria za kukariri darasani na bado hujapractice kama lawyer unakurupuka tu. umesahau kesi nyeti ya Zombe?? mbona wanasheria wakubwa waliobobea kitaifa na kimataifa walikuwa wakifuatwa na waandishi wa habari kuhojiwa kuhusu kesi yenyewe na mwenendo mzima na walikuwa wakitoa maoni yao na yanarushwa kwenye tv na magazetini na hata michuzi mwenyewe mzee wa libeneke alikuwa akituhabarisha. hata alipofariki mshatakiwa mwenza wanasheria waliongea sana 5tu kuhusu maoni na mwenendo na hatma ya kesi sasa wewe usikuruppukie kitu ambacho uelewa wako bado ni mdogo. hicho ulichokitaja hapo nina uhakika hukifahamu kiundani. hicho kidigrii kakiongezee ujuzi nenda law school kwanza.
    halafu wewe na michuzi mmeshasahu kuwa officially mahakani imefika leo, lakini hukumu kama hukumu alishaianza Kova long time tu, hapo mnasemaje?
    Hebu acheni watu waongee.

    ReplyDelete
  17. mbona kesi za kina liumba na lowassa na chenge maangalizo yalikuwa hamna wadau?ndio maana mm naona hii kesi ni FTIZI TU LAZIMA ULIWE KAMA KARATA3 VILE KARATA YA MCHEZO UNAONYESHWA HALAFU BADO WANAKUPIGA BAO TU..tatizo lingine la michuzi anatuona kama vile wachangiaji wake wote ni wahuni vile..kwa mahakama zipi basi hizo za kibongo zenye haki au kuvurugiwa kesi wakati kesi pochi lako tu

    ReplyDelete
  18. Hakuna mahali popote duniani ambapo utawashinda polisi mahakamani. Polisi na mahakama ni maswahiba na hii ni popote duniani. Hata marekani watu wanauawa na polisi mara kwa mara na wakienda mahakamani polisi watashinda. Nitashangaa kama bongo itakuwa tofauti

    ReplyDelete
  19. Huyo DADA MWENGINE PEMBENI NANI? KWAHIYO WAPO WANNE? MH KOMENTIIIII JAMANI LEO VILIO TUNABANIWAAAAA HAHAHAAH. UHURU WA MAONI UKO WAPI???????? MH JAMANI TUWE MAKINI ANKAL WETU ASIJE BULOGI YAKE IKAZIMWA BUREE MH> KIPANYA aKa PAZI.

    BWAWA 3 EVERTON 1.

    ReplyDelete
  20. WANAWAKE BWANA UTAWAJUWA TU WAPO KWENYE NGAZI WANALOLIONGEA MAJUNGU TUUUUUUU. HAWANA MOJA WALA MBILI SASA CHEKA BASI NDIO NINI? JIHESHIMUNI.

    ReplyDelete
  21. CHANGA LA MACHO KUDIVERT ATTENTION FROM DODOMA! BUNGE LITAISHA HAKUNA CHOCHOTE CHA MAANA THEN HII KESI ITAKUFA KIAJABU AJABU

    ReplyDelete
  22. wewee ankl kova amekutisha nini??mbona unataka kutulimit ktk kutoa maoni.Acha woga hilo sio dili.FANYA KAZI KIJANA!!!!

    ReplyDelete
  23. Waandishi wa habari bwana!!! Sasa ankal ameweka ANGALIZO kwa lengo la kupiga biti watu wasitoe maoni yatakayokinzana na kesi iliyo mahakamani,huku akijua wazi kuwa watu wataacha kuhoji ili kujua ukweli wa sakata la Jerry,na badala yake watataka kuhoji ni kwanini ankal amepiga biti hilo,na hatimaye kuteka mawazo ya watoa maoni wengi kwa kuyahamishia kwenye ANGALIZO hilo badala ya sakata la Jerry.Ankal acha janja ya nyani bwana,mambo ya kiintelijensia hayo.Watu tunataka kujua kama kweli swala ni million 10 au ni njama za*****Message sent Ankal.

    Potz.

    ReplyDelete
  24. Samahani kama nitakuwa nje kidogo na topic,hivi naona kesi ya Jerry imevaliwa njuga wakati pia kuna kesi nyingine mbona zimezimika hivi hivi,vipi ule uchunguzi wa nyumba ya Gavana umeishia wapi au mie ndio nipo nyuma?maana kama hii kitu haipo tena kama imepotea hewani,pia je' kama wameamua kumfatilia hivi jerry watafanyaje kuhusu watu wanaosadikika kumpiga kipigo mpaka umauti kumfika Fundikira?kwa kweli Tz tunasikitisha mambo yakushikiliwa na kuchunguzwa hayafanywi ila wanashikilia kupoteza pesa kwa mambo ambayo sio kabisa.

    ReplyDelete
  25. Jerry Muro is fake!

    Risiti ya pingu ya Jery Muro ni kanjanja na ana kesi mpya ya kujifu ya kufoji document ya serikali

    Mwenyewe alikanusha hana risiti

    Mzinga wanakanusaha kumuuzia na hawawezi kuuza pingu hizo kwa raia.

    Maoni kibao kama ya waganga wa kienyeji mwishi wake ndio huo.

    Bongo kila kitu rushwa, utapeli na kanjanja

    ReplyDelete
  26. Jamani eh huyu michuzi hana kazi,sasa comet kama hazitaki si asipublish tu,haya na ashasema hataki hizo commet ujue KOVA maoni yamemgusa kwa hiyo jihadharini UHURU WA PRES NA SPEECH HAUPO TANZANIA KABISA,na hawa mapolisi wetu yani kikesi hikii kimepelekwa utafikiri cha kupindua nchi,polisi hawataki kushindwa na wao,wakati rushwa kibao na watu wamepewa muda hadi kurudisha.

    ReplyDelete
  27. angalizo, umechemka mithupu

    ReplyDelete
  28. Mimi kila siku Mzee wa Ankal....nanhii nilikuwa namshaka naye lakini leo za mwizi ni 40. Sisi maoni yetu na mahakama yanahusiana nini? Tutake radhi muungwana unakuwa hujatundea haki kabisa wanajamii.
    Unajua huwa tunapiga kelele hapa kuhusu mafisadi lakini sijawahi kusikia hata siku moja Mzee wa Ankal akatuma vijana wake waweze kufikisha maoni yetu yeye akishapata maji ya kunywa sisi tunaumiza vidole kutoa maoni yetu hapa lakini hayafiki popote.
    Mdau Ukerewe

    ReplyDelete
  29. mimi nasema hapa tulipofika ni pazuri sana kuona muandishi amefanya kosa kushitakiwa lakini jee na wale askari mbona hatujaona kushitakiwa au mkuki kwa nguruwe tuu naomba msaada wa jibu

    ReplyDelete
  30. Kila siku naona TZ inavyoharibu na kuangamiza vipaji vya watu wake. Sasa hata mimi na kipaji changu cha kupiga box naogopa kurudi huko TZ maana najua kitaangamia tu.

    =Nawasilisha.=

    ReplyDelete
  31. Everybody lies, Cops lie,Lawyers lie, witnesses lie ,the victim lie so a trial is a contest of lies! Everybody in the courtroom knows this!

    ReplyDelete
  32. ankali ya leo kali ;

    kajisemae mama yangu hii umeunzuza maana ukichemsha waweza kula khaaaaa !!!

    naona unakofia mbili sasa ehh !!

    usinibanie comment yangu

    villager

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...