JK akipanda kiberenge tayari kukagua uharibifu wa reli uliofanywa na mafuriko kando ya mto Mkondoa huko Kilosa leo.
JK akikagua kingo za mto mkondoa uliofurika na kuleta hasara kubwa ya mali katika mji wa Kilosa.


JK akiangalia reli iliyosombwa na maji ya mto Mkondoa wilayani Kilosa leo asubuhi
Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Viongozi wa DECI wanamlilia Mungu huko jela. Wafuasi wa DECI wanamlilia Mungu huko Jela. Serikali iliwapa mkongoto na Mkullo akawaruka!

    Maoni yetu nayo yabanieni tu!

    ReplyDelete
  2. Mimi Naomba kumpongeza kikwete kwa juhudi kubwa z kuiinua nchi hii. Kikwete anasikiliza mahitaji ya watu na kwa kweli katika marais wote waliopita katika nchi hii Kikwete anastahili pongezi/ Tumwombee Mungu ampe afya njema na kuendelea kumwonyesha jinsi ya kutuongoza kwa ufanisi zaidi. Mungu akubariki Rais Kikwete kwa kazi nzuri!

    ReplyDelete
  3. WEWE MDAU WA USA NI MUUMINI AU VIZURI NIKUITE FANATIC WEWE NI MTU WA KUSIFU HATA KAMA HAUNA TAKWIMU KWANI HAUZIHITAJI BA KWAKO SIFA NI MUHIMU KULIKO UKWELI.

    ReplyDelete
  4. Hata mimi namuunga mkono mdau wa US ninamsifia JK kwa kazi anayoifanya, mwenye kukasirika akasirike mwenye kuumwa na aumwe. Kama Rais wa nchi anatimiza wajibu wake, sitegemei Rais afanye kazi za RC, DC, Mkurugenzi mpaka mtu wa chini.

    Kinachowasumbua ni uvivu tu wa kutaka kila kitu mfanyiwe na serikali nyie kazi kukaa vijiweni kusogoa siasa, hata maofisi mmegeuza vijiwe vya kusogoa siasa, badala ya kufanya kazi kutwa mpo kwenye mitandao mnablogu mara Jf, mara BF, hivi saa ngapi huwa mnafanya kazi za kujenga nchi saa ngapi?

    Na huyo mcheza kamari hapo juu, unategemea uliwe kwenye kamari kisha serkali ikulipe fidia? Ulisikia hayo yametokea wapi? Labda mwezini.

    Wengine mnashindwa kuona utendaji wa JK kutokana miwani myeusi mliyojivika ya imani zenu, hamna zaidi ya hapo angekuwa Joseph hata kama ana fanya madudu kama ya RADA mngemsifia, mbona tushawasoma siku nyingi! Kha wala hamtupi shida siku hizi.

    Mswahili

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...