JK akisalimia na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. William Lukuvi mara baada ya kuwasili jioni hii katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akitokea nje ya nchi kwenye ziara ya kikazi nchini Uturuki na Jordan. Kabla ya kutua Dar asubuhi alipitia Mwanza kufungua mkutano mkuu wa TAKUKURU
akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mara baada ya kuwasili kutoka ziara ya kikazi nchini Uturki na Jordan. Mwingine katika Picha ni Mzee Kingunge Ngombale Mwiru.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Jaman kingunge si apumzike tu sasa hivi anatakiwa awe nyumbani na wajukuu wanacheza na kula,mambo ya kukimbiakimbia aache sasa astaafu ameshatumikia nchi ya kutosha na kama kuvuna ameshavuna ya kutosha aachie vijana sasa wakimbiekimbie.

    ReplyDelete
  2. Kingunge hapo yupo kama nani? Manake sio waziri tena na sio mshauri wa Raisi. Nadhani alitangaza kustaafu, vipi mbona yupo hapo

    ReplyDelete
  3. Kingunge mbona yupo hapo?huyu mzee akae apumzike,tuwe na utamaduni wa kupumzika,sio busara kabisa,acha vijana wafanye kazi bwana.kacheze na wajukuu nyumbani,nyie ndo mnatuongezea foleni barabarani.

    ReplyDelete
  4. Mr. Kingunge bado ni mshauri wa rais. Ana miaka zaidi ya 80. Nakumbuka back in a day alikuwa mkuu wa itikadi ya elimu ya mafunzo, ya ushirikishwaji umma, ya sekretarieti, ya halmashauri kuu ya taifa.Na waziri asiyekuwa na wizara maalumu. na mshauri wa rais. Na mjumbe wa kamati kuu, ya halmashauri kuu ya taifa-central committee and NEC. Wooow!

    ReplyDelete
  5. Sasa kwanini raisi akiwa anarudi kutoka nje , inabidi viongozi wengi tu waende kumpokea Uwanja wa Ndege.

    Kwaninininni ?

    ReplyDelete
  6. where to, next...haiti? south africa? zuma kaowa juzi inabidi atembelewe kumpa pongezi.

    ReplyDelete
  7. Anon wa 10;21;00 pm na Anon wa 11;31;00 katafuteni kitabu "48 Laws of Power" by Robert Green. Ndiyo mtaelewa kwa nini Kingunge hawezi kuacha kwenda Airport kumpokea JK. That is part of the dynamics za principles za Machiavelli. Mlioenda shule mtaelewa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...