KAMPENI YA KITAIFA TANGU LINI IKAWA NA KIINGILIO????
Kaka Michu! Habari za siku?
Mimi ni mmoja wa wananchi ambao nilikwenda kushuhudia namna Malaria INAVYOKUBALIKA. Nasema hivyo nikiwa na sababu kadhaa za msingi:
1. Kwa kawaida Matamasha kama ya Kupambana na UKIMWI huwa bure Je, imekuwaje hili la Malaria liwe na Kiingilio? Je wafadhili wamefadhili nini?
2. Katika Kampeni hii ya Malaria kumekuwa na Matabaka mawili kuna walioitwa VIP na kuna akina sie KABWELA ambao tulichangishwa sh. 3000/- na hao wanaoitwa VIP wakaingia kwa DEZO (Bureeeee). Pamoja na kuingia kwao bure walifaidika na vifuatavyo:
i) Vinywaji vya kutosha tu
ii) Chakula kizuri tu
iii) Walipewa pia Chandarua kila aliye VIP
iv) Waliwekewa Viti na meza zilizopambwa
Jambo ambalo limenifanya mimi niandike ni kwamba inakuwaje waliolipa kiinglio watengwe yaani hata kumpa Chandarua!? halafu Chandarua anapewa Balozi ambaye ana uwezo wa kununua wakati mwananchi aliyeunga mkono kwa kulipa anatoswa? Je, asipokuja Tamasha lijalo utamlaumu?
Hao tunaowaita VIP wana uelewa tosha wa Malaria lakini huyu mwananchi wa kawaida anahitaji msaada. Kwa nini umnyime japo Net moja?
Nawaachia Wadau
By Kinyemela
Mimi ni mmoja wa wananchi ambao nilikwenda kushuhudia namna Malaria INAVYOKUBALIKA. Nasema hivyo nikiwa na sababu kadhaa za msingi:
1. Kwa kawaida Matamasha kama ya Kupambana na UKIMWI huwa bure Je, imekuwaje hili la Malaria liwe na Kiingilio? Je wafadhili wamefadhili nini?
2. Katika Kampeni hii ya Malaria kumekuwa na Matabaka mawili kuna walioitwa VIP na kuna akina sie KABWELA ambao tulichangishwa sh. 3000/- na hao wanaoitwa VIP wakaingia kwa DEZO (Bureeeee). Pamoja na kuingia kwao bure walifaidika na vifuatavyo:
i) Vinywaji vya kutosha tu
ii) Chakula kizuri tu
iii) Walipewa pia Chandarua kila aliye VIP
iv) Waliwekewa Viti na meza zilizopambwa
Jambo ambalo limenifanya mimi niandike ni kwamba inakuwaje waliolipa kiinglio watengwe yaani hata kumpa Chandarua!? halafu Chandarua anapewa Balozi ambaye ana uwezo wa kununua wakati mwananchi aliyeunga mkono kwa kulipa anatoswa? Je, asipokuja Tamasha lijalo utamlaumu?
Hao tunaowaita VIP wana uelewa tosha wa Malaria lakini huyu mwananchi wa kawaida anahitaji msaada. Kwa nini umnyime japo Net moja?
Nawaachia Wadau
By Kinyemela


he he he he! ama kweli tanzania tambarare! nakubaliana na point nyingi za mlalamikaji.
ReplyDeleteMKUU HII NDO TANZANIA, KARIBU SANA. NAONA SASA HIVI WATAPEWA URAIA WA NCHI MBILI SENKYU TO NABII YOHANA MASHAKA NA PROF. MEMBE WAZIRI WA NCHI ZA NJE.
ReplyDeleteHAWA VIP NI VIGOGO NA WATOTO WAO, WALALAHOI NDO SISI TUSOKUWA NA HOJA, LAZIMA ULIPE ILI WATU WENYE MAJINA MAKUBWA MEMBE ZAO ZIPAMBWE
umesema kweli mdau, siku hizi pesa nyingi ziko kwenye UKIMWI na TB, malaria inaachwa ili isaidie kuharibu ubongo wa watoto wa kiafrika kwa maana ya kupunguza uwezo wao kiakili baada ya kuugua malaria kali mara kwa mara. na hawa watoto ni wa walala hoi ili wasiweze kujinasua kwenye umaskini na wazidi kutawaliwa. Kwenye UKIMWI hakuna cha VIP au mlala hoi, tena UKIMWI unapenda VIP wanaoweza kula starehe kila siku.
ReplyDeleteKwa haraka haraka naona hilo tamasha lilikuwa haliwahusu makabwela, lilikuwa ni tamasha maalumu kwa ma-VIP wetu na ndio maana hata kikawekwa kiingilio ili kitumike kama kizuizi kwa choka mbaya kufika pale ndani ila kwa wale wabishi sana watalazimika kuoingia kwa kuchangia 3,000 na hawatapata huduma yoyote zaidi ya kuwaangalia kina Proffessor J nk. Hao waliopendelewa huduma za vyakula na vyandarua licha ya kwamba hata kuingia waliingia bure ni wale ambao hata malaria huwa wanaiona kwenye TV tu ila siku hiyo walipata tu nafasi ya kuja kuwaona kina Bi Kidude na kuchukua picha za kumbukumbu wakirudi kwao.
ReplyDelete..Du mshikaji kweli KAZINDUKA...kwa hali hii kitakuwa kweli kizazi cha mwisho kufa kwa malaria,...na usisemee hao makabwela walitoa buku tatu, wasemee wananchi walioko vijijini ambao sijui ni asilimia ngapi ujumbe huu umewafikia...ama ni Kizazi cha VIP ndo kinatakiwa kiwe cha mwisho kupata malaria na kina yaghe wacha wafe...shaurilao...
ReplyDeletethat's a busness mr Kinyemela,we call it a legitimate way to generate money for personal gain.hawa watu wanajua exactly wanachofanya,na utaamini wanajua wanachofanya pale utakapoona msaada wanaotoa ni mdogo kuliko viingilio vilivyolipwa siku hiyo ya kampeni.
ReplyDeleteitabidi nimuulize wife anipe updates on this issue
ReplyDeletehalafu mbona hujaweka picha yake 2nd week in a row?
lakini ili isiwe majungu ulitakiwa kueleza hiyo tamasha la malaria lilikuwa wapi na lini ili wanaohusika wamulikwe kirahisi namna nyingine unatuwekea taarifa ambayo hatujui tumlaumu nani!!!!
ReplyDeleteVIP haaa haaa haaa kwii kwiii kwiii. Tunataka wafadhili watugee vyandarua? Hiyo buku tatu ipeleke moja kwa moja kwenye chandarua.
ReplyDeletenakumbuka rais wa marekani(bush)alipouliza kuhusu vyandarua(ziara tz) aliambiwa nibei nafuu sana alafu yeye akaagiza vitolewe bure, litakuwa jambo la ajabu ikiwa ni kweli waliopewa ni hao wanaojifanya wakubwa na waheshimiwa,wakati walengwa ambao ndio wanaoliwa na mbu na kutozwa hizo tSH 3000 hawakufaidika, ""VIVA KIKWETE PINDA"
ReplyDeletehaya ndio yale yale ya Wyclef na haiti, hapo ndio ujue kila kitu deal na watu wanaangalia nini watapata kwa kuztoa misaada. kwakifupi ile ni business ndio bongo entrepreneurship iyo. ankal hili linabidi litolewa maelezo na ikibidi watu wawajibishwe maana mh. kikwete ametumika kuwatajirisha watu bila kujijua
ReplyDeleteHuyu Jamaa mtoa hii mada kweli kaona kwa jicho la tatu..
ReplyDeleteIla mi nasema ni vijimambo tu kwa mheshimiwa J 2 za K kuwarudia anayesema yupo nao karibu,vijana esp Bongo fleva! those 4+ years toka atoe ahadi kwao imekuwaje?
Now tunaenda October kwenye uchaguzi ndio tamasha la malaria?malaria ipo na imesahaulika kabisa,ila jamaa na jopo lake la ubunifu wa kuchukua kura ndio kaanza na ili baada ile kitu ya kilimo kwanza kushtukiwa na wachambuzi wa uchumi(ni blah blah tu),now anatoka na hii ya malaria.
And offcourse kitakachofuata ni tour all over the country, SHAVU HILO KWA VIJANA WA BONGO FLEVA (Ingawa ni vijisenti vya Muda tu)!!
-The Dreamer
Mdau, Miye sikwenda kwa sababu kubwa MBILI: 1) buku tatu napata kesto zangu mbili saaaaaffiiiii hivyo hakuna haja ya kulipa kiingilio kwenye "TAMASHA LA KITAIFA". 2) Mi ile nliona ni kama FIESTA tu (huwa siendi fiesta), tofauti ni kuwa mgeni rasmi alikuwa rais na barabara zilitengenezwa....
ReplyDeletechiggs
inasikitisha kwa kweli, nilishangaa sana na rais wetu anakubali kushiriki wakati akijua wanakufa kwa malaria kila siku ni masikini wa chini kabisa. unamuelimisha nani kama unawatenga maskini?ni hao watoto wa matajiri walio na uwezo wa kulipia kiingilio au hao VIP?tatizo waTZ ni waoga sana na tunaogopa sana kuongea ukweli, matokeo yake watu wanajiamulia kila kitu pasipo hata kuulizwa. ule ulikuwa ni mradi wa watu wachache wanufaike na hela ya wafadhili huku walengwa wakiwa hawana kitu.
ReplyDeletemlitumwa muende kwenye matamasha ya mafisadi?? msilalamike kutozwa kiingilio mmeyataka wenyewe - akili ku mchichwa
ReplyDeletehaya....yote kwa yote sawa ila jamani wanamuziki wetu wa ukweli tunawatenga hata kwenye hili...GURUMO,BICHUKA,DEDE,KIKII,MAPILI AHH.....OK najua huwa hawakubali kale ka biashara ketu ka pasenti
ReplyDeleteMdau wa saa 08:26:00 AM, nimekukubali umesema sawasawa kabisa....
ReplyDeleteupupu mtupu,,,mlitaka wenyewe kutozwa msingeenda!!
ReplyDeleteme hii kitu naona mchezo wa kuigiza kabisaaaaa,yani jibu la malaria zajulikana sio huu usanii
Mimi nilifikiri ni peke yangu naona hii kitu imekaa tenge!!! maana hii kali zaidi ya zote zilizowahikuwepo. Watakuja kumwambia presida tanzania iuze watumwa abroad nhi itapata maendeleo na nafikiri atakubali. Kama bao za kisigino zinaingia kwa njia ya tobo namna hii.
ReplyDeleteNaishia hapo maana mambo mengine hata kuchangia yanatia kichefuchefu. Tanzania imepotea njia......
Mimi wala siwalaumu wale VIP wakulaumiwa ni waandaaji amabo mpaka leo imenipa shida kujua ni nani aliandaa....mara sugu kasema idea ya kwake ila kuna watu wamempora....lakini pia waandaajin walikua kibiashara zaidi na wanjua wabongo ukiwaambia rayc na Profesa watakuwapo hata kama ni bure ukiambiwa ulipe buku 5 watatoa...ni aibu kweli and ma sure JK alikua hajui hilo...watuombe radhi
ReplyDeletehahahahaa mdau lile tamasha lilikuwa letu ma-VIP kwaajili ya uzinduzi wa kampeni ya kupambana na malaria.
ReplyDeleteNinyi pangupakavu tunajua mlikuja kuangalia wasanii tu ndo maana hatukuona haja ya kuwahudumia kwa chochote... kwani zile bia tungewapa ninyi msingegombana? hebu sema ukweli! msingetoana macho? sisemei chakula maana hapo mngetoana utumbo wallahi!!
mbona sisi tulihudumiwa wengine moja, wengine mbili, wengine 10 lakini kila mtu akaondoka kwa ustaarabu wake. hata nyie hamkugombana kwasababu zenu zilikuwa nyimbo tuu ndo maana mlizichangamkia sana.. ila pole kwa kutumezea mate. nakushauri usingojee tamasha lingine la zinduka utukomoe kwa kutokuja kwani lilikuwa moja tuu halitajirudia tena. pole sana!! duuh unatia huruma kweli kweli... tukutane pale Jackies nikununulie hata mbili tuu uridhike hahahaaa!!!!!....
HIVI KWELI WA-TZ BADO TUMELALA USINGIZI KIASI HIKI? TANGU LINI TAMASHA LA KITAIFA TENA LA UGONJWA HATARI LIKAWA NA KIINGILIO?
ReplyDeleteBE CAREFUL
KUMEKUCHA SASA, TUFIKIRI MARA MBILI YA TULIVOZOEA LA SIVYO TUTAKUWA TUNAIBIWA KILA SIKU TENA KUPITIA MIGONGO YA WAKUBWA LIVE MCHANA KWEUPE!
HI HAYO TU.
na siku ya uhuru tuwe tunalipa kiingilio kuingia pale neshno.nchi yetu ina mambo ya kipekee,sina hali
ReplyDeleteNA KWA MAZINGIRA YA PALE LEADER CLUB , NADHANI MAAMBUKIZI YA MALARIA YALIONGEZEKA SIKU HIYO
ReplyDeleteHILO LILIKUWA NI TAMASHA LA BIASHARA YA VYANDARUA NA SI KAMA MNAVYDHANI KUHUSU MARALIA, HOTUBA YA JK ILIWEKA UMUHIMU WA KWANZA BIASHARA YA VYANDARUA NI KINYUME KABISA NA WENGIWETU TULIVYOFUNDISHWA SHULE NJIA ZA MWANZO ZA KUANGAMIZA MBU, SASA HIVI TUNATAKIWA TUZALISHE MBU WENGI ILI BIASHARA YA VYANDARUA IENDELEE DAIMA. KWA KUWA LILIKUWA NI TAMASHA NA SI KAMPENI HIVYO ILIKUWA SAHIHI KULIPA ILI MUWEZE KUJIMWAYA.
ReplyDeleteHITU VINGINE WATANGANYIKA MNALALAMIKA BURE VIP HATA SIKU MOJA HAWALIPII KITU! WAKIENDA DISCO NURE, MPIRANI BURE LABDA JAKAYA NDIO KUNA SIKU NILIMUONA TAIFA AKIWA KATIKA FOLENI NA TIKETI YAKE!
ReplyDeleteKALI ZAIDI ANAGALIA ZIARA ZA VIONGOZI VIJIJINI NDIO ROHO ITAKUUMA, MTU ANAKWENDA NA VX THEN ANACHUKUA ZAWADI ZA MAGUNIA YA MAHINDI MADEBE YA NYANYA, MAHARAGE NA VITU VINGINE BUREEE KABISA KWA MTU MWENYE NYUMBA YA NYASI HATA KUPOZA KWA 5,000 HAKUNA.
SASA KWA TABIA ZA VIONGOZI WETU MNASEMAJE? VIONMGOZI WA MBIO ZA MWENGE WAKISAFIRI NA HUIO 'MOTO WA NYERERE'WANAKUSANYA ZAWADI KILA KONA WANAYOPITA KWA WALALAHOI.
SASA KULIPA BUKU MBILI UNALALAMIKA NINI WAKATI KUNA BAADHIO YA VIONGOZI WANAPEWA NA WAKULIMA VYAKULA NA MIFUGO KAMA MBUZI NA NG'OMBE, ITAKUJA KUWA HIYO BUKU TATU YAKO?
WENYE NACHO HUONGEZEWA NI KWELI MUWE NA KUMBUKUMBU JAMANI.
JAMANI, HIVI KUNA HATA KWELI YA KUWEKA TAMASHA LA MALARIA? KUNA ASIYEJUA KWELI KATIKA TANZANIA HII KUWA KUNA MALARIA? TENA YANAUA SANA?
ReplyDeleteSIKUONA, SIONI NA SITAONA HAJA YA KUWA NA TAMASHA, AU UZINDUZI KUHUSIANA NA MALARIA!!
TUMEONA YALEYALE TULIYOTAHADHARIAHSA TANGU MWANZO KUWA FEDHA HIZI ZA MALARIA ZA WAFADHILI HAZITATUMIKA KWA MALENGO KUSUDIWA. KINA WASANII WALIOPEWA KUHAMASISHA, WAMEHASISHA NINI? MNAMHAMASISHA NANI ASIYEJUA MALARIA JAMANI? HII NI NJI YA KUFUJA FEDHA ZA MSAADA ZA WALIPAKODI WENZETU WALIOTULETEA.
NADHANI INGEKUWA BORA KUNUNUA MADAWA MOJA KWA MOJA NA KWENDA KWENYE SEHEMU ZA MAZALIA NA MAFICHO YA MBU NA KUPULIZIA, MBU WANGEPUNGUA PENGINE. HAPA LENGO LINGEFIKIWA.
TANGU PALE TULIPOANZA KUONA WAHAMASISHAJI KWENYE LUNINGA HADI LEO WAMEKUFA WANGAPI TOKANA NA MALARIA?
TUACHENI USANII, TUWENI MAKINI KATIKA UTEKELEZAJI HALISI ILI KUJASTIFAI MATUMIZI YA FEDHA ZA WADHAMINI KIKWELIKWELI!
AAH. TANZANIA NA HASA WATANZANIA!!!!