

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
WEKENI CCTV WANATUIBIA MIZIGO YETU SANA HAPO AIRPORT, UKIGUNDUWA HAPO HAPO UKIWAULIZA WALA HAWAKUSIKILIZI SO PLEASE WEKA CCTV AMBAO MAIN CONTROL YAKE IWE KWA MKURUGENZI WA KIWANJA WATU WASI ICHOKONOWE, KUNA WEZI SANA HAPO NA BANDARINI PLEASE CHONDE CHONE WAZIRI SIKIA KILIO CHETU WEKA CCTV NI AIBU WANAIBIA HATA WAGENI HAPO NI AIBU TUPU. WATALII WANALIZWA KILA SIKU NI AIBU CHONDE CHONDE
ReplyDeleteAnkal Michuzi, mimi nina maoni yafuatayo, maana sina njia nyingine ya kufikisha ujumbe kunakohusika isipokuwa hii blogu yetu ya Jamii. Nina uhakika wahusika kwa namna moja au nyingine ujumbe huu utawafikia.
ReplyDeletePamoja na nia nzuri ya serikali ya kuboresha miundombinu hapo Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere, serikali inabidi pia iboreshe rasilimali watu katika uwanja huo. Hii ni kutokana na utendaji kazi wa hali ya chini na wa ajabu uliopo hapo katika uwanja wa ndege. Kwa hiyo hata kama hicho kiwanja kitakuwa kizuri namna gani kama hakuna mabadiliko katika uendeshaji wake ni sawa sawa na kujenga tembo mweupe!
Kuna mengi yanaendelea hapo lakini kubwa na la kutia aibu ni hili la wafanyakazi wa kitengo cha Security ambao sijui wako chini ya nani hapo kuomba rushwa wazi wazi kwa abiria wanaosafiri bila woga wala aibu. Hili limenikuta mwenyewe wakati nikiwa nasafiri kwa ndege ya Shirika la ndege la Uingereza miezi michache iliyopita nikiwa nimeambatana na watoto wangu wadogo.
Kwanza mizigo yangu ambayo haikuwa mikubwa wala kuzidi uzito, sikubeba kitu kingine chochote zaidi ya nguo na viatu, ilipita kwenye scan kama kawaida. Kisha security aliyeko kwenye scan akaniambia peleka mzigo wako ukakaguliwe tena pale ufunguliwe. Sikuwa na wasi wasi wowote kwa sababu sikubeba chochote si mchele wala kahawa wala kitu chochote cha kutilia shaka, nikaupeleka mzigo wangu kwenye meza ya security kama nilivyoelekezwa. Huyo Security badala ya kukagua mzigo akawa ananiomba rushwa tena bila hata haya yuko "dada tuachie chai basi". Sijui alinifikiriaje, kwanza nilifadhaika watoto wangu kushuhudia kitu cha aibu kama hicho. Nilimjibu kagua mzigo wangu, pesa sina! Na niliuchuna sikutaka kuendelea na mjadala zaidi, ila nilikuwa makini nisibambikiwe vitu vya ajabu kwenye begi langu.
Ikabidi huyo Security asalimu amri, hawakukoma, mwingine naye akaanza kutaka kung'ang'ania mizigo yangu, bahati kila sehemu sio wote ni watumishi waovu, akatokea Security mmoja akawauliza hii mizigo ya huyu mama ina shida gani? Hawakuwa na majibu, nikacheck inn nikaingia ndani.
Sakata hilo halikuishia hapo, kwenye final check inn wakamtuma Security mwingine mwanamke aje apekuwe hand luggage yangu, humo akakutana na madocuments yangu niliyotoka nayo field ambayo nilikuwa naondoka nayo kwa ajili ya data analysis akaumbuka, lakini bado naye aliendelea kuniomba "eti tuachie basi dola ya chai". Sikuampa senti tano kwani tayari nilishafikwa kooni!
Hivi hali hii ya Security wa airpot ya Dar kuomba rushwa kinguvu tena bila woga wala aibu itaisha lini? Hivi inaonyesha nini wageni wanaoingia na kutoka nchini mwetu? Na hali hii inatokana na nini hasa? Mazingira mabaya kazini? Mishahara midogo? Au na wao wanatumwa na wakubwa zao kupeleka mapato mwisho wa siku?
Nasikia hawa Security wa airport hawana mikataba ya kueleweka ya kazi, wengi nasikia hawana uhakika wa ajira zao, hawajui kama mwezi huu ukipita mwezi ujao atakuwepo kazini. Hivi katika dunia ya leo wenzetu wanaimarisha Security za viwanja vyao, sie tunadharau Security ya uwanja wetu kwa kiasi hicho hivi tuko serious kweli?
Mswahili
we mswahili hapo juu kwa taharifa wale security asilimia 80 wote ni wanajeshi, maafsa upepelezi sema tabia chafu wanazo kuanzia wakubwa mpaka wadogo sasa hebu fikiri kama mkumbwa anajengewa nyumba ili atoe eneo la police wahindi wafanyie kazi sasa kwanini mimi nisifanye hivyo mdogo hapo kuna rusha lakini bandari na mahakama wamezidi ktk nchi hii
ReplyDelete