Bosi wa DAWASCO Mh. Alex Kaaya

Na Veronica Kazimoto, MAELEZO
Afisa mtendaji mkuu wa DAWASCO Mhandisi Alex Kaaya amewaambia wakazi wa Kimara Baruti kuwa watapata mgao wa maji mara mbili kwa wiki kama hakutakuwa na hitilafu itakayojitokeza kwenye mitambo kuanzia hivi sasa.
Akizungumza wakati wa kujibu maswali ya wananchi jana kufuatia malalamiko yaliyokuwepo katika eneo hilo hususani katika suala la maji Mhandisi Kaaya amewaambia wananchi hao kuwa upatikanaji wa maji ya kuaminika unategemea ukarabati wa mitambo na uboreshaji wa miundombinu na mabomba.

“Ninawaomba wananchi muelewe kwamba ili kutatua tatizo hili la maji inabidi mradi ambao unatekelezwa hivi sasa wa ukarabati wa mitambo kwa asilimia 100, uboreshaji wa miundombinu na mabomba kwa asilimia 95 na kupanua mtambo wa usambazaji wa maji kwa asilimia 95 ukamilike kabisa,” alisisitiza Kaaya.

Hata hivyo Mhandisi Kaaya amesisitiza kuwa suala la mgao wa maji ni lazima kutokana na ongezeko la watu katika jiji la Dar es Salaam ambalo linahitaji maji kwa wingi kuzidi uwezo wa vyanzo vya maji.

Mpaka sasa maeneo yaliyofanyiwa matengenezo tayari yameshaanza kupata maji. Maeneo hayo ni pamoja na Kimara kin’gongo, Kimara temboni, maeneo ya Kilungule, Baruti pamoja na eneo lote la Msewe.

Kaaya ameyataja maeneo ambayo hayajapata maji kuwa ni Golani, Bakery na Bonyokwa, hata hivyo Mhandisi huyo amesema jitihada ya kuyapatia maji maeneo hayo zinaendelea kufanyika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. HIVI KWANINI WASOMI WETU MNASHINDWA KUTATUA TATIZO LA MAJI DAR WAKATI MMEZUNGUKWA NA VYANZO VYA MAJI?

    ReplyDelete
  2. mie niliogopa kuona picha nikidhani kuna habari mbaya. yaani tangazo la mgao wa maji hadi picha? kweli ufanisi umepungua.

    ReplyDelete
  3. Kaka hii yote ni Umaskini...ila yanamwisho ipo karne tatizo la maji litakuwa historia. Haingii akilini kabisa maji pale Rufiji kibao mtu anasema vyazo vya maji vichache...while bili zinaletwa majumbani hata kama maji hayatoki!

    ReplyDelete
  4. Mhandisi huyu amekosea naomba nimrekebishe. Maji wakazi wa Kimara tunapata maji masaa takribani saba tu kwa wiki na si mara mbili kwa wiki. Na hilo si jipya tumeshalizoea Diwani wetu Bwana Mlingo kajenga shule shauli ya shida zetu za maji. Kama atabisha bwana Michuzi njoo hapa kimara bucha tukuoneshe tanki lililozinduliwa kwa mbwembwe na Mkuu wa Mkoa wa kitambo kile Bwana Makamba huku bomba zote zikielekezwa kwa diwani.
    Ila tunawashukuru DAWASCO kwa kutuwekea mita maana tulikua tukiwalipa mishahara bure tu zile sh.22500 kwa mwezi huku maji bomani ni kila baada ya miezi 2.

    ReplyDelete
  5. HIVI NDUGU YANGU WA JUU, TATIZO NI WASOMI AU SERIKALI NA SERA ZAKE NA SIASA KATIKA KILA MAAMUZI? WASOMI HAWANA SHIDA KAMA WAKIWEZESHWA, KILA KITU KINAWEZEKANA. SHIDA YETU KUBWA NI WATOA MAAMUZI WA SERIKALINI HUWA HAWAONI UMUHIMU WA KUFANYA HAYA MAMBO KWANI WANAOGOPA WAKITENGENEZA MAJI YAKATOKA BILA SHIDA SASA KURA WATAOMBAJE UCHAGUZI UNAOFUATA? KURA ZINAOMBEWA KWA KUTUMIA MATATIZO YETU. HII NDIO TABIA YA VIONGOZI WETU, KUTUMIA MATATIZO YETU WANAYOYALEA MAKUSUDI KUOMBEA KURA.
    TUNA KAZI SANA...

    Mzozaji

    ReplyDelete
  6. miundombinu ya maji ya darisalama ni ya mwaka gani? na ilitengenezwa kwa ajili ya kukidh mahitaji ya watu wangapi? na hivi sasa dar ina watu wangapi?

    Kama serikali haiwezi kujenga miundo mbinu inayokidhi mahitaji ya maji ya darisalama, basi inabidi kuja darisalama kutoka nje ya mkoa wa morogoro na pwani iwe kwa VISA.

    ReplyDelete
  7. kwa maana hiyo hawa watu kimara wataoga mara mbili kwa wiki????
    mdau money uk.

    ReplyDelete
  8. Kaaya...inamana kwamba kwasababu vyanzo havitoshelezi watu ndio basi tena siku zote itakua mgao? Je watu wanavyozidi kuja kila siku si itafika wakati maji yataisha kabisa? Ni aibu sana kiongozi mkubwa kabisa dawasco kutamka maneno hayo. Angalia majiji mengine afrika kama Cairo, Joburg, Nairobi mbona wao wana maji yakutosha. Tena cairo ndio wako jangwani kabisa na maji wanayo! Inabidi Dawasco mfanye mpango wa kutoa maji kwenye vyanzo vingine ili kukidhi kwa asilimia 100 mahitaji ya maji ya wakazi wa dar!

    ReplyDelete
  9. hamna lolote..hawa jamaa mara nyingi wanapofanya kazi zao wanashindwa kumua jambo lolote kwa long term..wewe anagali barabara wanajenga wanashindwa kujuwa kama kunahitajika mitaro hadi waje siku ingine wameshamaliza kutengeneza barabara wake kubomoa..hii ni akili gani...weken mfumo wa kudumu muda mrefu..tumieni akili yenu kama mnavyojiita miundo mbinu.KILA KITU KIWE MGAO MGAO BASI SITOSHANGAA KUAMBIWA KUTAKUWA NA MGAO WA NETWORK...

    ReplyDelete
  10. Bro Michu, kila mwaka Viongozi we2 wanakwenda majuu zaidi ya mara 10, hv awaulizii jambo gani wafanaye au ki2 gani wanunue ili 2ondokane na tatizo la maji na umeme. Uwezo wa kununua vifaa hivyo 2navyo ila Serikali ye2 ina2didimiza. 2taishi maisha haya mpaka ln? Inaniuma sana, 2naishi maisha ambayo wa2 wa ulaya wameishi miaka 120 iliopita. Serikali badirikreni mtaiba mpaka ln? Kumbukeni duniani 2napita!!

    ReplyDelete
  11. Hivi huyu Mhandisi bado anaiongoza Dawasco? nafasi yake si ilishatangazwa siku nyingi tu na nasikia usaili ulishafanyika au ndo siasa zenyewe za bongo. Dawasco iliingia kwa mbwembwe lakini kwa muda iliyokaa chini ya huyu bosi imedhihirisha kushindwa kutekeleza majukumu yake.
    "Tanzania bila bakora hatutaendelea"

    ReplyDelete
  12. Mimi ni mkazi wa kimara mwisho nakaa upande wa kushoto ukitokea mjini karibu na shule ya Sec ya Midland, kwa kweli hatuna mgawo wa maji hata kwa wiki mara 1 hatupati kbs maji mwaka wa 6. Na tumewekewa mabomba kila nyumba na mita zetu yapata hata miezi 8 na zaidi sasa hayajawahi kutoa maji, cha kushangaza kimara hiyo hiyo upande wa kulia ukitokea mjini wao wanapata maji mara 2 kwa wiki jnne na alhamisi, sasa nikijiuliza tatizo liko wapi sipati jibu, nabaki nashangaa tu, tunanunua maji ndoo 250 hadi mia 500 kwa wenye mikokoteni ya maji. Kwa kweli tunapata shida sana sana sisi wakazi wa kimara mwisho. Bora watuambie tatizo ni nini. Tutashukuru km na sisi tutakuwa kwenye huo mgao, mm kwa upande wangu wakitupa hata mara moja kwa wiki yatatutosha tu kwani tushapata tabu miaka mingi sana sasa!!!!

    ReplyDelete
  13. Namshauri bwana Kaaya kufuatilia hili jambo kwa ukaribu yy mwenyewe kwani sisi wakazi wa Kimara tumechoshwa na tatizo hili ambalo ni la muda mrefu sana na ufumbuzi wake hatuujui hadi leo hii kila siku tunaambiwa kuna matatizo upande wetu kwa ss wakazi wa kimara mwisho upande wa kushoto ukitokea mjini, tumebaki njia panda huku wenzenu wa upande wa pili wa barabara wakipata maji kwa kweli inatusikitisha sana tumebaki tunayatazama mabomba tuliyofungiwa na wachina miezi zaidi ya sita sasa mwisho wa yote vibaka wataanza kuiba mita kabla hata maji hayajaanza kutoka!!!

    ReplyDelete
  14. nanukuu
    "hata hivyo mhandisi Kaaya amesisitiza kuwa suala la mgao wa maji ni lazima kutokana na ongezeko la watu katika jiji la Dar esa salaam ambalo linahitaji maji kwa wingi KUZIDI UWEZO wa VYANZO VYA MAJI"

    ipo kazi pale eti msomi km uyu anapojibu kisiasa kisa asipoteze mkate wake...ungwini tuuu shule za bongo no practical kazi kutaka kuajiriwa tu.

    ata me nilifikiri tangazo la msiba/ajali hii picha khaaa

    ReplyDelete
  15. Mie nimeanza ishi kimara toka mwaka 2008 kwa mwaka jana ndio hao wachina wakaanza weka hayo mabomba na mpaka mwaka jana nimehama mwezi wa isa kwa kweli maji yalikuwa hayatoki kwa upande wa king'ongo yanatoka huku msikitini na sehemu hizi za juu yaani yanapopita magari kuelekea huko kwa komba ila ukishuka pale maduka matatu kwenda kule kwa choo hakuna maji kabisa ila mabomba wameka hata kwenye magofu ambayo hajamaliziwa kujenga kila siku ni hadith tu yatatoka mwezi huu mara mwezi ujao na cha kushangaza wanaleta bill za maji hao dawasco je watu walipe hewa au maana maji hayatoki kabisaaaaaaaaa na kwa upande wa bonyokwa ndio hakuna maji kabisa tunasubiri hayo mabomba yatoke vyura labda maji tunanunua kila siku ziendazo kwa mungu jamani hawana hata huruma ndoo 200 mpaka mia 300 kwa wale wenye magari na mikokoteni dumu mia 500 je ndio maisha bora haya,wajaribu kufikiria coz tumechoka kudanganywa kama watoto wadogo na wakati mwingine hata hao wauza maji wanaleta maji ya chumvi mtu unagundua baadae wakati wa kufua labda or km wataka kunywa na pia ni hatari kwa maisha yetu sisi watumiaji coz hatujui wakati mwingine hao wauza maji wanatoka nayo wapi may be ya visima huko wanakuja kutuuzia sie ambapo si salama.

    Dawasco wajirekebishe tumechoka kudanganywa hasa sie wakazi wa kimara bonyokwa.NA WAJARIBU KUJIFIKIRIA JE YANGEKUWA KWAO WANGEKAA KIMYAAAAAAA SI AJABU HUKO KWAKE MAJI MPAKA YA KUMWAGILIA BUSTANI WAKATI SIE TUNAPATA SHIDA YA KUNUNUA MAJI

    ReplyDelete
  16. Mie nimeanza ishi kimara toka mwaka 2008 kwa mwaka jana ndio hao wachina wakaanza weka hayo mabomba na mpaka mwaka jana nimehama mwezi wa isa kwa kweli maji yalikuwa hayatoki kwa upande wa king'ongo yanatoka huku msikitini na sehemu hizi za juu yaani yanapopita magari kuelekea huko kwa komba ila ukishuka pale maduka matatu kwenda kule kwa choo hakuna maji kabisa ila mabomba wameka hata kwenye magofu ambayo hajamaliziwa kujenga kila siku ni hadith tu yatatoka mwezi huu mara mwezi ujao na cha kushangaza wanaleta bill za maji hao dawasco je watu walipe hewa au maana maji hayatoki kabisaaaaaaaaa na kwa upande wa bonyokwa ndio hakuna maji kabisa tunasubiri hayo mabomba yatoke vyura labda maji tunanunua kila siku ziendazo kwa mungu jamani hawana hata huruma ndoo 200 mpaka mia 300 kwa wale wenye magari na mikokoteni dumu mia 500 je ndio maisha bora haya,wajaribu kufikiria coz tumechoka kudanganywa kama watoto wadogo na wakati mwingine hata hao wauza maji wanaleta maji ya chumvi mtu unagundua baadae wakati wa kufua labda or km wataka kunywa na pia ni hatari kwa maisha yetu sisi watumiaji coz hatujui wakati mwingine hao wauza maji wanatoka nayo wapi may be ya visima huko wanakuja kutuuzia sie ambapo si salama.

    Dawasco wajirekebishe tumechoka kudanganywa hasa sie wakazi wa kimara bonyokwa.NA WAJARIBU KUJIFIKIRIA JE YANGEKUWA KWAO WANGEKAA KIMYAAAAAAA SI AJABU HUKO KWAKE MAJI MPAKA YA KUMWAGILIA BUSTANI WAKATI SIE TUNAPATA SHIDA YA KUNUNUA MAJI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...