Siku hizo 40, huhitimishwa na Sikukuu ya Pasaka ambayo ni ya ufufuko wa Yesu Kristo, hiyo ni kwa mujibu wa Wakristo.
Jumatano ya Majivu hukusanya waaumini wengi ndani ya makanisa kwa ajili ya ibada ya majivu, japo si siku inayoadhimishwa kwa shangwe na nderemo kama ilivyo siku za Krismasi na Pasaka, ambazo hutawaliwa na shangwe zaidi.
Maadhimisho ya siku hii huwa ni ya kipekee na waamini huiadhimisha kwa namna ya kipekee pia, ambapo hufurika kwa kishindo ndani ya makanisa kwani wengi hawaiachi ipite bure bila kuhudhuria ibada na kupakwa majivu kwenye paji la uso.
Hata kwa baadhi ya waumini ambao ni nadra kwao kuhudhuria makanisani, hujitahidi kuhudhuria ibada ya Jumatano ya Majivu na kushiriki katika adhimisho hilo la kuanza kwa kipindi cha Kwaresma.
Kwa kusoma zaidi:
-------------------------------------
KWA NIABA YA WADAU WOTE GLOBU YA JAMII INAWATAKIA KWARESMA NJEMA WADAU WOTE WATAOFUNGA KATIKA SIKU HIZI 40 KUANZIA LEO.
KWA NIABA YA WADAU WOTE GLOBU YA JAMII INAWATAKIA KWARESMA NJEMA WADAU WOTE WATAOFUNGA KATIKA SIKU HIZI 40 KUANZIA LEO.
-Michuzi


Tunakushukuru sana Mkuu wa wilaya na ankal wa blog ya jamii. Na mimi nakutakia Kwaresima njema pamoja na wadau wenzangu wote ktk blog yetu.
ReplyDeleteAsante sana Michuzi kwa kuwa mtu wa watu wote. Na sisi wakristu tutakukumbuka katika sala zetu wakati huuu wa kwaresma.
ReplyDeleteankal kwa kupigia debe ukatoliki?! mbona sikukuu za waislamu huzielezei kwa undani??
ReplyDeletenajua utabania maoani yangu kwani hupendi kukosolewa wewe!