Ushabiki wote kando, nikupashe hili jambo,
Mimi bado mzalendo, hata unichape fimbo,
YANG...A yafwata mwendo, wa SIMBA tangu kitambo,
Katika TIMU za BONGO, SIMBA ni kiboko yao.

© 2010 Darda King

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mimi ni shabiki wa Simba lakini huwezi kuhitimisha kwamba kwa timu za bongo Simba ni kiboko bila kuweka vigezo. Kutegemeana na vigezo, Simba au Yanga inawezak uwa zaidi.
    Yanga wametwaa ubingwa wa nchi mara nyingi kuliko Simba kwa hiyo kwa kigezo hicho unaweza kusema Yanga ni zaidi. Yanga walishiriki Champions League ya Afrika kabla ya timu yoyote Tanzania.
    Kwa upande mwingine, Yanga wamekuwa wakiongoza kwa kuitia aibu nchi kwenye mashindano ya kimataifa. Waliposhiriki kwenye Champions League walikuwa wanatandikwa hadi mabao sita kama wamesimama. Simba waliposhiriki waliikosakosa nafasi ya kutinga nusu fainali katika mechi yao mwisho huko Ivory Coast. Simba wamepata kucheza fainali na pia nusu fainali katika mashindano ya Afrika.
    Labda kikubwa kinachotia uzito hoja ya uchokozi ya Darda King ni kwamba Yanga wameshawahi kupata kashfa ya kujaribu kutoa rushwa kwa refa wa mashindano ya kimataifa bila mafanikio wakaishia kufungiwa kushiriki soka ya kimataifa katika miaka ya themanini. Sijui ndio namna wanavyochukuaga ubingwa wa bongo...

    ReplyDelete
  2. Inategemea unatumia vigezo gani, ukiangalia ushindi wa kuchukua ubingwa wa nchi, Yanga wamechukua mara nyingi zaidi kwa hiyo ni zaidi kwa upande huo. Simba ni zaidi tena kwa mbali ktk mashindano ya kimataifa na rekodi ziko wazi, swali la kujiuliza ni kwanini mtu anayefanikiwa nchini azidiwe na mwingine wanapokuwa nje ya nchi?

    ReplyDelete
  3. Hivi nyinyi mwaujua mpira ama mwakurupuka tu... Chelsea imekuwa bingwa mara ngapi England na Imechukua ubingwa wa ulaya mara ngapi.. kwa maana hiyo wataka kusema inatoa rushwa ili iwe Bingwa.. Yanga Yanga hiyo yote gere tu inawatekenye.. acheni Yanga iitwa Yanga. Yanga Oyeeeeeee

    ReplyDelete
  4. asante kwa uchokozi. lakini naomba wadau mkumbuke na rekodi ya kutia mpira kwapani pia. simba wanavunja rekodi kwa kutia mpira kwapani mbele ya yanga mara mbili!
    halafu kufika fainali sio issue, jose mourinho aliwahi kusema kwamba hakuna rekodi ya kukaribia kufika ubingwa, la muhimu ni kuchukua ubingwa. simba haijawahi kuchukua ubingwa, walilikosa kombe la klabu bingwa afrika hapo dar es salaam kwa aibu mbele ya stalla abidjan. hakuna kiboko yao tanzania, wote wameoza!!!!

    ReplyDelete
  5. waswahili mbona mna tabia ya kuchanganyikiwa!Juma Kaseja si mlinda mlango wa Simba...sasa mbona yuko kwenye kikosi cha Yanga???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...