Bwana Michuzi Khabari.

Naomba uiweke khabari hii kwenye blog yetu ili wenzangu waifaidi. Ni kuhusu khabari zilizoletwa kitambo kumhusu bwana Mtoro, mbeba maboksi wa kwanza

Kuna wengi walitaka kujua zaidi kuhusu Bwana Mtoro na ilikuwa-kuwaje hata akawepo kwenye anga za Wajerumani (wengi wanaita kubeba Maboksi, kifupi KM). Kitabu chake nilisha kisoma na napenda na wengine wakisome.
Kabla sijawapeni kitabu chenyewe kwanza nitoe wasifa kidogo kumhusu Bwana Mtoro

1. Aliishi bagamoyo (NI mzaramo) na alikuwa ni informant wa Wajerumani, kwa uhasa, infoma wa Professor C. Velten (mkufunzi na mwana fasihi (linguistic) wa kijerumani)

Jamaa mwenyewe, yaani Mtoro alikuwa mwanafunzi wa Shehe Abubakar bin Taha’l Barawy kwenye masomo ya kiarabu na fasihi za lugha za mwambao

3. Alikuwa vilevile mfanyakazi (Clerk) wa Wajerumani (mtoza ushuru)


4. Prof Velten alipokutana na jamaa alipokuwepo pwani akifanya tafiti za lugha hasa lugha ya kiarabu na za kibantu alimpenda jamaa kwa akili alizokuwa nazo na juhudi.

Alikuwa ni kichwa (resources) kizuri sana kwa Velten kwenye hizi tafiti mbalimbali alizokuwa anazifanya na msaada. Velten alipo maliza kazi ilibidi amchukue kwenda naye Berlin kwa Lengo la kumsaidia kufundisha Kiarabu ambacho Prof. Velten alikijifunza na alikuwa na mpango wa kukifundisha
5. Jamaa alikuwa Handsome boy hivyo haikuwa shida kwake kupata mtoto wa Kijerumani na akaoa akazamia moja kwa moja. Ila kuna tetesi kuwa akina Prof. Velten walimfanyia mpango aoe ili asifikiri kurudi kwao Uzaramoni na kweli alishikwa akashikamana kweli kweli kwani hakuwahi kurudi “Ushenzini” kama walivyoita Wajerumani hadi kufa kwake

Uandishi wake
Jamaa alikuwa na akili sio uongo na aliweza kuandika tangu akiwa Bongo ya Bagamoyo na katika safari za ndani na akina Velten.

Velten aliendelea uwa rafiki yake wa karibu na kwauwa Velten aliuwa ni mwandishi, kazi zake zilimshawishi Mtoro kufuata nyayo za bwana wake. Kwa msaada wa Velten, Mtoro alikusanya makala (collections) zake na Velten akaziweka sawa zika chapishwa.

Velten alimsaidia sana hasa katika utaratibu wa uandishi wa wakati ule na aliandika preface ya kitabu.

Ijapo kitabu chaweza kuwa na makala ya waandishi wengine lakini sehemu kubwa sana iliandaliwa na bwana Mtoro
Lugha iliyotumika
Kiswahili alichokitumia Bwana Mtoro ni cha mwambao enzi hizo, ambacho kinaendelea kutumika kwa kiasi katika nchi ya Congo. Ukweli bwana Mtoro angeliishi leo akakutana na wacongomani wanao kisema kiswahili basi wangelisikilizana zaidi ya wabongo ambao kiswahili chao kimekua saana. mfano mzuri ni matumizi ya neno “kuhemea” maana yake shopping, n.k.
Unahamu ya kukisoma kitabu chenyewe?
kupata manuscript nzima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. I have been reading a lot about African explorers and African journals during colonial times. When I came across this book in Michuzis blog I was so pleased, that is until I ordered it, well I ordered then cancelled the order pronto. Amazon sells a paperback copy for £ 18.95.So I decided I did not want to read it afteral,the electronic copy is not very good,could I borrow someones copy?
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  2. Unaweza pia kumsoma hapa
    http://www.best.uni-mainz.de/modules/AMS/article.php?storyid=173

    ReplyDelete
  3. Leo pia nimesoma habari za Mtz mwingine aliyezamia kunako maboksi miaka hiyo huko Ujerumani, hadi akauawa katika kambi za mateso za hitler. Jama huyu, nadhani naye ni wa Bmoyo, unaweza kusoma habari zake kidogo hapa vhini (na picha yake icheki ktk Jamii Forum):


    JE WAFAHAMU KUWA KUNA MTANZANIA ALIYEUWAWA KATIKA ZILE KAMBI MAALUM ZA KUWATEKETEZA BINADAMU ENZI ZA HITLER? ANAITWA, BAYUME MOHAMED HUSSEIN.

    Bayume Mohamed Husen was born (Feb 22 1904) in Dar es Salaam, German East Africa, now Tanzania, and died (Nov 24th 1944) in Sachsenhausen concentration camp. (birth name: Mahjub bin Adam Mohamed). He was an African-German Askari and actor. Husen served in World War I in the protection force of German East Africa as a child soldier. After the war and the end of German colonial rule, he could not seem to connect to the service of Great Britain, which had Tanganyika as a "mandate". Temporary Husen worked in Zanzibar as a teacher and as a "boy", as a servant to British and German ships. In 1925 he was hired on to a ship of the German East African line as a waiter.

    In 1929 he went to Berlin to demand unpaid wages of his father's and his. The request was rejected by the Foreign Office on the grounds that the fund had already been settled. Attempting to return him to Africa, Husen opposed and instead he settled in Berlin. He worked as a waiter in the "Wild West Bar" at Potsdamer Platz in Berlin from April 1930 until his dismissal in 1935.

    From 1931 to 1941 Husen was also at the "foreign studies department," of the University of Berlin as a Swahili Language instructer/assistant. He instructed officials who were to be prepared for the planned subsequent recovery of the German colonies by the German Reich. For a relatively low salary, he worked under the founder of the German African Studies, a former missionary Diedrich Westermann.
    In April 1941 he resigned his duties at the university, apparently because of the humiliating treatment by a professor. In January 1933, three days before the appointment of Hitler as Chancellor, he married Mary Schwandner. In March 1933 they bore a son, Ahmed Adam Mohamed Husen. Another daughter, Anne Marie Husen, was born in September 1936. Both of the children died during childhood.

    Between 1934 and 1941, Bayume Mohamed Husen had starred in at least 23 German film productions. He had his first role in the movie titled "The Riders of German East Africa". In the movie "To New Shores" Husen 1937 stood alongside the main actors as an extra and also with small speaking roles. He occasionally took on the role of a consultant in the language of Swahili. His biggest role was also his last: Between August 1940 and February 1941 Husen played in the Nazi propaganda film, "Carl Peters" as Ramadan, a guide and interpreter of the "colonial pioneer," Carl Peters.

    In August 1941 he was arrested by the Gestapo( "Secret State Police") because of a relationship with a white woman (Aryan). Since there was no legal basis for a conviction - for blacks, there was indeed a ban on marriage, but no sex ban was with "Aryan women" - he transferred to the Sachsenhausen concentration camp. Shortly thereafter, his wife filed for divorce, probably under pressure from the Nazi authorities. After 3 years in the camp Husen died in November 1944 as a result of bad prison conditions. (ref: Bechhaus-Gerst. 2007)

    ReplyDelete
  4. Halafu mnasema ufisadi umeanza leo, kumbe umeanza tangu zamani, ama kweli tutakuwa na kazi kubwa sana ya kuondoa mlungula

    Hebu angalia Mtoro Bin Mwinyi anavyosimulia "a§-subuhitukaondoka, tukendaYangeyange. na mku-
    bwa wa Yangeyange Magembe. tulipoqaribia akasema:
    ^nipeni hongo, kama hamkutoa hongo, ntafanya vita, ni-
    wanyanganye mali yenu yote pia". tukatoa nguo kumi hongO; tukampa, akakataa. na sisi tukakataa vilevile
    kumpa zayidi. akaleta vita, tukapigana naye. wakaua
    watu wawili kwetu, wakachukua mizigo miwili ya bicja'a,
    na sisi tukaua watu watatu kwake.
    "

    ReplyDelete
  5. Mkmzira....that was absolutely fascinating, I had no idea and now I will pursue this subject further, shukran mara alf.
    Ewe mheshimiwa Kaka Trio, wasema ufisadi ulianza zamani kwa matumizi ya neno "hongo" neno hilo katika maana ya kiswahili cha asili ni MALIPO ie payment,matumizi ya neno hilo kwenye maana ya kisasa ni rushwa
    If you want to know where we are going to dont forget where we came from
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  6. wewe anony wa kwanza. Ingia mfukoni na nunua kitabu. Usipende vya bure. Buy the book. I have ordered mine already.

    ReplyDelete
  7. heee jamani sasa wee mtoa mada ndo maneno gani ayo???
    wala hueleweki uyu mbeba box alitokea congo full stop!!bagamoyo alifikia tu na kuaza makazi

    eti alioa mzungu wanawe wote wakafa (alishikwa akashikamana)

    mbona watumwa wa kiafrika wako duniani kooote tu ata asia walipelekwa sii ajabu watu km hawa wako ujeremani...nothing special/new

    khaaa

    ReplyDelete
  8. Ebwana eeeh Rushwa ni urithi wetu toka kwa mababu siunaona wadogo walikuwa wanaomba rushwa kwaaajili ya mkubwa wao ila wengine walikuwa hawana soni wanaomba wenyewe lol hayo si ndo mambo yanatokea sasahivi pia kwa maafande na maofisa wa sirikali rushwa is here to stay

    ReplyDelete
  9. JAMANI HIKI KITABU NITAWEZA KUKINUNUWA WAPI? AMAZON NIMEONA KWAK IJERUMANI TU. NISAIDIENI. PAZI.

    ReplyDelete
  10. Wacheni zenu hata Alivyoenda Urusi inaonesha Wamemuomba rushwa.

    ReplyDelete
  11. Sasa Anon si unaona hata Urusi nao wanayumbayumba kama sisi tu kwa shauri ya utendaji kazi legelege? kwanini Urusi haikokama western countries zingine? kwanini Europena union inajengeka lakini Urusi ilisambaratika? kwanini Marekani state zao hazijitengi kama zile za Urusi? Kwanini Afrika hatuungani?

    Jibu moja mlumgula, nakubali kiswhaili kimebadilika lakini pia wala rushwa wanaiita rushwa majina mengi, mfano 10%, kushika mkono, mlungula, system n.k. Kama ingalikuwa Mtoro alikuwa analipishwa kodi kwa ajili ya kupita maeneo hayo angendika ni kodi lakini kasema ilikuwa ni hongo, kina unatoa ili upate kupendelewa kiaina

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...