Super Malik (shoto) na Muddy Clever
BENDI kongwe ya muziki wa Dansi nchini ya Msondo Music imewanyakuwa waimbaji, Hamisi Tenguweni'Super Maliki' akitokea bendi ya Makoba Bandi ambapo amewai kuimbia bendi ya TOT plas na Shikamoo Jazz zote za jijini Dar es salaam pamoja na Mohamedi Mwerevu 'Muddy Clever' akitokea bendi ya Maruni Komando,ambapo ameshawai kuimba katika bendi za Nyota Soundi Afrika na Lessi Wanyika zote za Kenya

Msemaji wa Msondo Rajabu Mhamila 'Super D' ameiambia Globu ya Jamii kuwa wameamua kuwachukuwa waimbaji hawo kwa kuwa wana uwezo wa kuisaidia bendi na sasa wameshaanza kupanda katika jukwaa la bendi hiyo ambapo mpaka sasa tunajipanga kutoa nyimbo mpya za mwaka uhu baada ya mwaka jana kutambulisha albamu yetu ya huna shukrani na kuwa ipo mtaani kwa sasa inauzwa,

Wakati huohuo, bendi hiyo kwa sasa imekuwa ikitoa burudani za wazi katika kuwaweka karibu wapenzi wake ambapo kila jumamosi Msongo wanakuwa katika viwanja vya TCC Chan'gombe na jumapili huwa Leaders Club.
Mpaka sasa Msondo wana nyimbo mbili mpya moja ni 'Lipi jema' uliotungwa na Eddo Sanga na 'Dawa ya Deni kulipa' wa Isihaka Katima 'DJ Papa upanga'

"Sambamba na burudani hizo pia tumejipanga kutoa nyimbo mpya kila baada ya wiki tatu ili kukamilisha albamu ya mwaka huu mapema kadri iwezekanavyo", alisema Mhamila

Akitoa wito kwa wapenzi wa bendi hiyo kuhudhulia kuona maonesho yao popote yafanyikapo kwani kuna burudani ambazo azihitaji kuadithiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Sasa Viatu jamani huko Tanzania... yaani inatia huruma ukiangalia hivyo viatu.

    ReplyDelete
  2. hivi haya majina ya wasanii wetu huwa wanakurupuka tu na kujjipachika? manaake nafikiria, yaani mtu kaamka asubuhi na kuamua jina langu la kisanii litakuwa muddy clever..au super danger n.k!?

    ReplyDelete
  3. mimi sishangai majina ya wasanii hata bendi za muziki wa kibongo maana ukiyafikiria utacheka sana. wewe fikiria kipindi cha miaka ya nyuma kidogo kila bendi ya muziki ilijiita ni jazz band,wakati muziki waliokuwa wanapiga hauna hata ukaribu wowote na jazz,hapo ndipo nikifika nachoka kabisa.
    tabora jazz band,shikamo jazz band,n.k

    ReplyDelete
  4. Jamani.. bendi zetu nazo ebu waangalie hawo viatu nguo zao yaani utafikili kama siyo bendi kubwa.. au na mavazi nayo ni ukongwe.. au siyo msondo ngoma labda nimekosea kusoma.....tutashida saaana sisi tanzania loo! wadhamini wenu wa safari wako wapi....viatu chini suruali hizooo lo!! at kiwi akuna... bwana eeeh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...