Wadau,
Google sasa kupitia simu yao ya nexus wako katika hatua za mwisho za kuanzisha teknolojia mpya yaani simu yenye kamusi yaani mtu unapiga na kuongea kiswahili unaset anayepokea apokee lugha gani ie Kihindi au kiingereza akiitikia kwa kihindi au kiingereza unasikia kiswahili hivyo sasa itarahisisha wafanya biashara na watu wa professionals mbalimbali kuongea na kusikia lugha nyingi ulimwenguni. Hivyo siyo ishu upresent kazi kwa kiswahili wasikiaji wanaweza kuwa wahispaniola.

Sambo Maganga,
Research Scientist,
Ifakara Health Institute,
P. O. Box 53,
Ifakara, Morogoro,
United Republic of Tanzania,
mobile: +255 713 709 064/783 713 757

Nb. Tafadhali usiniulize swali ambalo linaweza kujibiwa na google.com na usiprint hii email ili uokoe miti labda kama kuna ulazima wa kufanya hivyo.
kwa habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. mimi ninavyofikiria itategemeana na service provider. Sasa kama hiyo simu unaitumia bongo hiyo service inaweza isipatikane. Watu ambao wanaishi nchi za ulaya na america ndio wanaweza kufaidi service hii..ni kama vile service ya GPS ambayo katika simu inategemeana na plan yako na service provider.

    ReplyDelete
  2. Yes I can....What about you?February 18, 2010

    Kumbe wewe ume copy na kupaste alafu unajiita Research wewe vipi bana,Nikajua wewe mwenyewe umeifanyia kazi hiyo kitu kumbe ume copy??

    ReplyDelete
  3. Hebu acheni uswahili wenu na story zenu za mitaani hiyo ya kutafasili kibena na ki-zaramo labda mtengeneze bongo

    ReplyDelete
  4. Hao ndo marisacha wetu wa kibongo bana wanarisachi risachi za watu wengine hahaha mie naona tuwaite watoa habari za risachi za wanarisachi au vp

    ReplyDelete
  5. jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

    Huyu mtafiti kosa halilolifanya ni kuandika wadhifa wake. Lakini ametoa habari, kwa kizungu wanasema ame report. NUKTA. Kwani hamjaipenda habari hiyo?

    mdau florian rweyemamu

    ReplyDelete
  6. Maganga umetoka kwenye utafiti wa kichaa cha mbwa Malinyi Mororgoro sasa unafanya Utafiti wa simu?Ongera sana au ndo Masters yako unayo fanya hapo London?Ifakara wanakusubili sana...

    ReplyDelete
  7. maganga kazi yako ni kutafiti jinsi mmbu wanavyozaliana haya mambo waachie wenyewe

    ReplyDelete
  8. Manganga unasema usiulizwe swali mabalo linaweza kujibiwa na google!! Je mimi nisiejuwa kutumia computer wala Kugoogle ninaekimbizana na 500 ya chai asubuhi itakuwajeee huku hakauna interney cafe na hata zikiwepo sina nduruuuuuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...