
Habari ankal!
Naomba uwawekee wadau picha ya mataa (traffic lights) ya pili hapa jijini Arusha. Zimewekwa hivi juzi juzi tu. Ni traffic lights za pili hapa Arusha na zimewekwa kwenye makutano ya barabara ya Mianzini. Traffic lights za awali zipo pale Sanawari. Arusha kuna waka waka sasa.
Mdau Mwandamizi A-Taun.
badilisha hiyo windscreen haraka
ReplyDeletekaka hicho kioo vipi? sheria zetu za bongo bado zinaruhusu magari kama hayo kutembea barabarani? wadau nijibu tafadhari
ReplyDeleteDu na hizo taa zimepinda kwa kwenda mbele!!!!
ReplyDeletewataweza kuzitumia?
ReplyDeletemataa mapya barabara za zamani
ReplyDeleteannon #1 umenivunja mbavu
ReplyDeletemaana me picha kuiona tu wazo ilo likanijia jaman wee mtoa mada gari kioo vipi?au ndo mambo yetu yaleee ya wizi wa magari arusha?ulikuwa wasave nini?
maana ilo shimo mh!!
Ni vyema hata zile za mjini zikawekewa solar panels.Inaonyesha hizi zinatumia solar power. Kama ni kweli hata za Dar ziwe hivyo kuachana na adha ya kukatika umeme.
ReplyDeletetrafiki huyo, atakukamata, badilisha kioo, au uweke karatasi ya bima nasi tujue moja.
ReplyDeletemsicheke jamani wanakomaga tuu mama yeyoo (wamama wa kimasai) wakati wa kuvuka wanakimbia haswa yani ni waoga hao full speed
ReplyDeleteUhuru road (Sokoine road) tunahitaji mataa hasa maeneo ya Friends Corner, barabara ya kutokea idara ya Maji inapoingia karibu na Mount Meru Posta na Kilombero sokoni karibu na Shoprite na Ngarenaro barabara ya Nairobi. Na kule Impala kwenye junction ya kwenda kijenge na njiro.
ReplyDeleteHata hivyo tunaishukuru Manispaa. Iongeze bidii
Wadanganyika tumekuwa nyuma sana hivi vitu vyote ni haki yetu kuwekewa na sio hisani,vitu kama maji,umeme,barabara,shule,nk ni haki yetu kupata bilashida maana tunalipa kodi,tuamke ndugu zangu
ReplyDeleteukiangalia zaidi kupitia tundu la kioo,hilo bomba la chuma chakavu limeunganishwa kizalendo pale gerezani, big up wachaga!
ReplyDeleteMACHALII NAONA WAMEBAKI KUSHANGA NA MATAA. HIYO NDIO KARNE YA 21, ACHENI USHAMBA. WAKIKUYU NA WAGANDA WANAVAMIA HUO MJI, SHAURI YENU.
ReplyDeletetatizo moja lilopo ni kwamba wavuka kwa miguu hawafati taa bana yani unakuta watu wamesimama kama wanariadha wanaosubiri filimbi ya kuanza mbio arafu wanatimka mbio wanavuka du aibu ukiwaambia si mfate taa wanajibu tufate taa kwani sisi magari??
ReplyDeletemaskini naona machalii wote walijaazana hapo kuangalia mataa yakiwakawaka hongera mmepata maendeleo makubwa sana kupata Robot light.akina mama yoyo ndo stori kwa sasa
ReplyDeleteabadilishe kioo gari yake? alipiga picha akiwa kwenye teksi...wayu wengine bwana
ReplyDeleteHizi taa ni tabu kwelikweli huko A-town. Mashabiki wa Simba wakifika hapo wakikuta taa ya kijani imewaka wanagoma kwenda wanadai hawawezi kuamrishwa na Yanga...nao wa Yanga wakifika hapo wakikuta imewaka taa nyekundu wanakatiza kitemi tu wanadai wanaikomoa Simba....!
ReplyDelete