Habari ankal!
Naomba uwawekee wadau picha ya mataa (traffic lights) ya pili hapa jijini Arusha. Zimewekwa hivi juzi juzi tu. Ni traffic lights za pili hapa Arusha na zimewekwa kwenye makutano ya barabara ya Mianzini. Traffic lights za awali zipo pale Sanawari. Arusha kuna waka waka sasa.
Mdau Mwandamizi A-Taun.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. badilisha hiyo windscreen haraka

    ReplyDelete
  2. kaka hicho kioo vipi? sheria zetu za bongo bado zinaruhusu magari kama hayo kutembea barabarani? wadau nijibu tafadhari

    ReplyDelete
  3. Du na hizo taa zimepinda kwa kwenda mbele!!!!

    ReplyDelete
  4. wataweza kuzitumia?

    ReplyDelete
  5. mataa mapya barabara za zamani

    ReplyDelete
  6. annon #1 umenivunja mbavu
    maana me picha kuiona tu wazo ilo likanijia jaman wee mtoa mada gari kioo vipi?au ndo mambo yetu yaleee ya wizi wa magari arusha?ulikuwa wasave nini?

    maana ilo shimo mh!!

    ReplyDelete
  7. Ni vyema hata zile za mjini zikawekewa solar panels.Inaonyesha hizi zinatumia solar power. Kama ni kweli hata za Dar ziwe hivyo kuachana na adha ya kukatika umeme.

    ReplyDelete
  8. trafiki huyo, atakukamata, badilisha kioo, au uweke karatasi ya bima nasi tujue moja.

    ReplyDelete
  9. msicheke jamani wanakomaga tuu mama yeyoo (wamama wa kimasai) wakati wa kuvuka wanakimbia haswa yani ni waoga hao full speed

    ReplyDelete
  10. ADILI NA NDUGUZEFebruary 23, 2010

    Uhuru road (Sokoine road) tunahitaji mataa hasa maeneo ya Friends Corner, barabara ya kutokea idara ya Maji inapoingia karibu na Mount Meru Posta na Kilombero sokoni karibu na Shoprite na Ngarenaro barabara ya Nairobi. Na kule Impala kwenye junction ya kwenda kijenge na njiro.

    Hata hivyo tunaishukuru Manispaa. Iongeze bidii

    ReplyDelete
  11. Wadanganyika tumekuwa nyuma sana hivi vitu vyote ni haki yetu kuwekewa na sio hisani,vitu kama maji,umeme,barabara,shule,nk ni haki yetu kupata bilashida maana tunalipa kodi,tuamke ndugu zangu

    ReplyDelete
  12. ukiangalia zaidi kupitia tundu la kioo,hilo bomba la chuma chakavu limeunganishwa kizalendo pale gerezani, big up wachaga!

    ReplyDelete
  13. MACHALII NAONA WAMEBAKI KUSHANGA NA MATAA. HIYO NDIO KARNE YA 21, ACHENI USHAMBA. WAKIKUYU NA WAGANDA WANAVAMIA HUO MJI, SHAURI YENU.

    ReplyDelete
  14. tatizo moja lilopo ni kwamba wavuka kwa miguu hawafati taa bana yani unakuta watu wamesimama kama wanariadha wanaosubiri filimbi ya kuanza mbio arafu wanatimka mbio wanavuka du aibu ukiwaambia si mfate taa wanajibu tufate taa kwani sisi magari??

    ReplyDelete
  15. maskini naona machalii wote walijaazana hapo kuangalia mataa yakiwakawaka hongera mmepata maendeleo makubwa sana kupata Robot light.akina mama yoyo ndo stori kwa sasa

    ReplyDelete
  16. abadilishe kioo gari yake? alipiga picha akiwa kwenye teksi...wayu wengine bwana

    ReplyDelete
  17. Hizi taa ni tabu kwelikweli huko A-town. Mashabiki wa Simba wakifika hapo wakikuta taa ya kijani imewaka wanagoma kwenda wanadai hawawezi kuamrishwa na Yanga...nao wa Yanga wakifika hapo wakikuta imewaka taa nyekundu wanakatiza kitemi tu wanadai wanaikomoa Simba....!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...