Mwenyekiti wa DP, Mchungaji Christopher Mtikila akisisitiza jamabo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana kuhusu kuwashirikisha wagombea binafsi katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010. Kushoto ni Mkurugenzi wa Liberty International Foundation.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mch Mtikila atakumbukwa na Historia Yetu kwa kusimamia hili la mgombea Binafsi Tanzania.

    Nampongeza na Kumshukuru Sana.

    NE,
    Reading, UK

    ReplyDelete
  2. ni kweli mkuu kama ulivyosema hapo juu huyu jamaa nampa sifa zake,amepigania haki ya wa tanzania kwa kiasi kikubwa pia natumaini anapaswa kuheshimiwa katika wana democrasia wazuri tanzania,sawa binadamu hatupo kamilifu,lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni

    ReplyDelete
  3. Mtikila atakumbukwa (1) alipoibuka 1986/87 katika forum yake iliyokuwa ikiitwa Liberty Desk huku akitetea siasa ya makaburu wa Afrika kusini na kuitukana ANC na Mandela akidai eti ANC ni chama cha kikomunisti na magaidi. Mwafrika yoyote aliyeitetea "apartheid" ni msaliti mkubwa dhidi ya Waafrika na wanyonge. (2) Alipotaka kuleta "apartheid" Tanzania. (3) Alipotukana Waislamu na Uislamu katika toleo moja la BBC FOCUS IN AFRICA 1993. (4) Aliposherehekea kifo cha baba yetu wa Taifa mpendwa, Mwalimu Nyerere, sauti ya mnyonge, 1999,wakati taifa likiwa kenye msiba : uchochezi uliopelekea kufungwa (wananchi fleti za Breweries walitaka kumshughulikia kabla ya polisi kumwokoa.) (5)Uchaguzi wa 2005 alpata kura chini ya 40,000. Liberty International Foundation inafadhiliwa na maracist wa Marekani waliompinga Mh. Obama 2008. Tuamke. Kujua kutukana tu si ukombozi wa mnyonge. A LUTTA CONTINUA. LONG LIVE MWALIMU'S MEMORY!!! LONG LIVE MADIBA MANDELA!!! MUNGU IBARIKI AFRIKA! MUNGU IBARIKI TANZANIA!!! Mwanaharakati daima.

    ReplyDelete
  4. Zungu Wa MbiziFebruary 16, 2010

    Kuna mambo mengi huwa sikubaliani na Mchungaji Mtikila.....Lakini hili la mgombea binafsi ninakubaliana naye kwa aslimia zote. Tafadhali Mchungaji hakikisha mwaka huu wa uchaguzi sheria hii ya mgombea binafsi inaanza kutumika...All the best!

    ReplyDelete
  5. huyo Mtikila bado pia ni mkoloni,kutetea maslahi ya wachache wenye tamaa ya madaraka, sio ukombozi wa mtanzania, tunataka watu wenye kulinda na kuwatetea walio wengi wenye kuteseka tz, mfano rushwa, polisi, mahakama, n.k ni nani atafaidika na ugombea binafsi.kumtetea mnyonge ndio silaha ya kweli, tuondolee takataka yako mtikila.

    ReplyDelete
  6. Mbona tumetoa maoni kumpongeza Mchungaji Mtikila na mmekataa kuyatoa. Tungekuwa tunamkashifu mngeyatoa upesi sana! Nbona anapokamatwa mnatoa habari upesi na kuruhusu maoni hadi 70?

    ReplyDelete
  7. Namuunga mkono Anon wa tatu @03:45 p.m. Nakumbuka kabisa makabrasha ya mtikila (liberty desk) ya
    1980's alipokuwa akiitaka serikali ya TZ iache kuisaidia ANC na alipofanya party ya soda kusherehekea kifo cha hayati mwalimu Nyerere 1999. Huyu mtu anatumiwa na maadui wa mtu mweusi (kina Falwell, Robertson, n.k.). Wanaharakati wazalendo, huu si wakati wa kulegeza kamba; sharti tupambane vikali ideologically na kisiasa. Tusikubali kamwe kupoteza dira tuliyowekewa na kina Samora Machel, Nkrumah, Cabral, Nyerere, Mandela. Nyinyi apologists wa mtikila, pesa za kununua nyumba mikocheni, masaki, n.k. mtikila kazipata wapi??? Huyo si mtetezi wa wanyonge ; ni kibaraka hatari anayechochewa na chuki na hostile foreign interest. Sitamwita "mchungaji" hata siku moja, siasa yake inapingana 100% na mafundisho ya Bwana Yesu!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...