BALOZI WETU UINGEREZA ASEMA IKO HAJA KUKAZA MASHARTI YA KUWASAFIRISHA WAFANYAKAZI WA NDANI MAJUU
Na Freddy Macha, London
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Mwanaidi Maajar, amependekeza kukazwa sheria za kuwalinda wafanyakazi wa ndani wanaosafirishwa kufanya kazi za utumishi nchi za kigeni.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mheshimiwa Mwanaidi Maajar, amependekeza kukazwa sheria za kuwalinda wafanyakazi wa ndani wanaosafirishwa kufanya kazi za utumishi nchi za kigeni.
Akiongea nami jana Jumapili mjini London, Mama Maajar alikuwa akitoa maoni kuhusu kukamatwa na kuchunguzwa na polisi kwa baadhi ya waajiri wa Kitanzania hapa Uingereza wanaowaleta wafanyakazi wa ndani na kutotimiza ahadi walizowapa kabla ya safari.
“Tunachokiona ni kuvunjwa kwa makubaliano ya kuaminiana kati ya wafanyakazi na waajiriwa,” alisisitiza.
Mwezi Desemba mwaka jana maofisa wawili wa polisi wa Kiingereza walisafiri Bongo kwa majuma mawili kama sehemu ya uchunguzi wa mateso aliyofanyiwa Bi. Zubeda Ali na waajiri wake, mjini Birmingham toka 2007.
Waajiri hao, Bwana na Bibi Shariff, ambao wamewekewa dhamana hadi kesi yao itakapofikishwa tena mahakamani mwezi ujao walitiwa hatiani mwezi jana kwa mashtaka ya kusafirisha wanadamu kinyume cha matakwa yao na kukiuka masharti ya uhamiaji.
Mwishoni mwa wiki jana mwajiri wa mfanyakazi mwingine wa makamo mzawa wa Kondoa alihojiwa na polisi wa London baada ya mfanyakazi huyo kupelekwa hospitali akiwa na ugonjwa wa kuvimba miguu (Varicose Veins).
Bibiye alifanya kazi kutwa kucha bila mapumziko wala likizo na kulala jikoni. Mshahara wake mdogo (shilingi elfu 20) alipewa mwisho wa mwaka si kwa mwezi. Mwajiri wake alimwita kwa kengele kama mbwa badala ya kutumia jina lake. Kwa sasa anahifadhiwa na kutetewa na chama kinachopigania maslahi ya wafanyakazi wa ndani (Kalaayan) na Umoja wa Wanawake wa Tanzania London (TAWA).
Balozi Maajar kasema wafanyakazi hawa wa ndani hudanganywa kwamba watalipwa vizuri na waajiri wao. “Wakiambiwa watalipwa shilingi laki mbili ughaibuni wanaona nyingi lakini punde wanakutana na maisha tofauti na yale waliyoahidiwa.”
Mheshimiwa Maajar alisema Ubalozi wa Tanzania umekuwa ukishirikiana na taasisi mbalimbali husika hapa, polisi wa Uingereza na TAWA kuwasaidia wanawake hawa.
Ila alisema tatizo hili halipo UIngereza tu. “Karibuni nimesoma habari mtandaoni kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa wafanyakazi wa Kibongo nchi za Uarabuni.”
Aliendelea kueleza kuwa wengi wa waajiri hawa ni watu wanaoheshimiwa Bongo na hawakubali kwamba wanachokifanya si kizuri. Wamezoea kuwafanya binadamu wenzao watumwa.
“Iko haja ya kuwafichua maana majina yao yameshawekwa hadharani hapa na kesi ziko mahakamani. Je, watajisikiaje kama hawa wanawake wangekuwa binti zao?”
mtu yeyote anayemnyanyasa mfanyakazi wa ndani ni mpumbavu maana hawa ni watu muhimu sana na wanaweza kutuua dakika moja kwa kuwa wanatupikia chakula wanatufulia, maji ya kunywa wao ndiyo wanatupa wanaweza hata kutulisha sumu wakitaka ni basi tu hatujui umuhimu wao wanaweza hata kuwatesa watoto kwa kulipiza kisasi kwa wazazi wanaowatesa na kuwanyima au kuwapunja haki zao. wakati umefika sasa kuwapenda mahouse girl tena kwa kuwaita majina mazuri kama house manager and so forth
ReplyDeletewa-tz wenzangu hivi mbona tuna roho za kinyama kiasi hiki katika hili mimi binafsi sio bongo ,Europe, middle east na far east watanzania ndio wakwanza kufitini watoto wa kwa kuwarubuni kwa ahadi hewa mshara hewa akijua kwamba akisha mpata na kumtuma uko anafanya anavyotaka yeye boss coz hana pakwenda na most of these are real educated ecducated.wanafanya hivyo kwa sababu mtoto hawezi kurudi nyumbani kwa sababu hana uwezo ya kujilipia nauli ndugu zangu kila mmoja wetu mwenye mafanikio kuna mahala alipopitia au kuanzia maisha ni magumu ila tuweni na moyo wa huruma kumbukeni kila mmoja wetu ni mchunga na ataulizwa na sote kwa mungu tutarejea.
ReplyDeleteHivi unamleta Binadamu mwenzako Ulaya kwenye hali ya hewa ya baridi namna hii, halafu unamwambia alale jikoni.
ReplyDeleteKwa nini tunakuwa na roho mbaya hivi kwa binadamu wenzetu jamani???!!!
Kwanza angeanza na maafisa Wa balozi zetu ambao wanatabia ya kuchukuwa watu au ndugu Kama watumishi Wa ndani na hawalipi mishahara.cha ajabu hata bima za afya hawalipi kwa watu wanaowapeleka.Mishahara Yao ni chakula na vijisenti kidogo.
ReplyDeleteUshahidi tunao chunguzeni watumishi wote Wa balozi za Tanzania duniani
Halafu ndio mnataka mrudi Bongo kwa gea ya uraia wa nchi mbili mje mtunyanyase zaidi!
ReplyDeletemimi nilishatoa maoni hapa kuwa "hii ni roho mbaya utakuata mama akirudi nyumbani hausigeli anatetemeka,haruhusiwi kula chakula meza moja na wanafamilia nk.. uncivilized act" ile siku jamaa aliyeleta mada ya nafasi hausigeli nyumbani, cha ajabu wengi walimshambulia jamaa kuwa ni kama mlemavu/mtemi na zaidi walikuwa akina mama, wengi walidai ndio kazi yake na analipwa.
ReplyDeletehaya sasa wema unaanzia nyumbani kabla ya kutoka nje vinginevyo itakuwa ni unafiki
kwakweli maisha ya wadada wakiafrika nje ni ya majonzi sana wanadhalilishwa sana mfano ni waethiopia wengi ktk nchi za kiarabu
Tena haswaa maafisa wa kibalozi wengi wanachukua watoto huku wengine wa ndugu zao wengine wafanyakazi halafu hawawalipi au mabalozi ule mshahara anaotakiwa kumlipa mfanyakazi anachukua yeye anaishia kumpa mtumishi vijisenti - wapo wengi tu jamani chunguzeni anzeni kusafisha balozi zetu kwanza alafu mje kwa watu binafsi
ReplyDeleteLeo nimesoma kwenye gazeti la The citizen hapa Tanzania/16Feb. Hao Shariff ni watanzania wenye asili ya kiAsia ndio wale wale (Wahindi wenye passport 2 ya UK na TZ) Jamani roho imeniuma sana,kweli na baridi yote hiyo na ma snow huko London anathubutu kumlaza mtu jikoni? I am sure hapo hamna hata heater wala blanket!!! Shame on you Shariff's... MUNGU atawalaani. Lakini Mama Maajar kwanini ubalozi usimpe hifadhi na kumsaidia matibabu huyo mama maskini ya mungu? mnamuachia apewe hifadhi na watu baki? au mrudisheni nyumbani...Very sad!
ReplyDeleteduh nipo miaka mingi ulaya lakini hii kali...lakini sishangai. hawa jamaa tena kesi ikakamilika waweke nye black list ya tanzania.....
ReplyDelete