

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Ankal!
ReplyDeletekumbe huwa unatoka "bling bling" bila ze fulanazzzz! uko makini na matukio. keep it up
Mkuu,
ReplyDeleteSamahani Professor Omar Shaban wa Simba Wanyika ambaye alikuwa anapiga rhythm guitar na co-composer wa Sina Makosa alifariki mwaka 1998.
Mdau 1:25PM Nakusifu, una kumbukumbu nzuri sana. Lakini ukiangalia vizuri hapo juu nadhani imeandikwa Prof omar Jnr (junior).
ReplyDeleteHuyu bwana alikuwa na uwezo wa kuchukua nafasi ya Professor Omar Shaban na kufanya vitu (kupiga rithym) kama alivyokuwa akipia Prof Omar. Ndiyo sababu mashabiki wa les Wanyika, Super Wanyika, Simba Wanyika Original na Mashabiki wa muziki kwa ujumla hapa Kenya walimpa hili jina la Prof. Junior.
Hadi leo anafahamika hivyo. Na hata juzi ameongea na watangazaji wa radio na TV ya hapa Kenya na wamemuita jina hilo-hilo.
Siku yoyote njoo hapa Nairobi, uliza mashabiki wa muziki wa wakati huo watakuambia wanamfahamu Prof Junior.
Huyu bwana amepigia bendi zote za Wanyika (Simba, Les, Super), amerekodi nyimbo nyingi sana akiwa na bendi hizi, amepiga na Virunga pia na baadae akaanzisha bendi yake iliyokuwa ikiitwa MAS System (Muungano All Stars), na huko pia walitoa album zao.
Baadhi ya nyimbo zilizovuma sana za Simba Wanyika Original kama vile shilingi Yaua, Barua kwa Mama, Tufurahi na wana wanyika na zingizo sizikumbuki vizuri, alishirikiana na kina George Peter na Wilson Peter Kinyonga kuzitunga na kurekodi.
Huyu bwana ni kati ya wanamuziki wale ambao huchuka low profile. Hasikiki sana lakini anajina kubwa sana kati muziki hasa hapa kenya na East Africa.
Bwana Prof. Junior kama umeshafanya nyimbo zako mpya tafadhali tuletee hapa Nairobi.
Mdau, Huruma Estate Nairobi.
(Mshabiki mkubwa sana pale kidongo)
OMBI LANGU AU WAZO LANGU MKUU KABLA YA KUTOA TAARIFA ZA MTU MWELEWESHE MBLOG YA JAMII NI YA KIMATAIFA HIVYO AKUAKIKISHIE MAUJIKO ANAYO KWAMBIA NI KWELI UKU UKIMTAZAMA USONI.ABUU OMARI ALIKUWA UDA JAZZ MBONA UKWEKA HIYO KAENDA KENYA ENZI ZA MKUMBO WA BORABORA YA MAREHEMU SUPER SAX TWAHIRI MOHAMED,KAMA MDAU HAPO JUU ANAVYOSEMA PROFESA OMARI ALIFARIKI 1998,BAADA YA VUNDUMUNA YA KINA KANKU KELLY NA NSILU WA BANSILU KURUDI TOKA JAPANI KUNA MWANAMUZIKI MWINGINE WA KONGO ALIPATA MKATA HUKO NA KUMCHUKUA FRESH JUMBE KISHA ABUU AKAFUATA,MWABIE NIVIZURI KUWEKA HISTORIA YAKE KAMA YEYE ITAMSAIDIA VIATU VYA PROFESAR OMARI VIKUBWA HAVIMTOSHI.PLEASE TUSIPOTOSHE UKWELI KWA UJIKO WA MUDA LETS TELL THE CHILDREN TRUTH.
ReplyDeleteAnon Sun Feb 14, 02:35:00 PM
ReplyDeleteHuyu Bwana Abuu Omar Prof. Junior hakuwa katika Wanyika ya ligi kubwa ya kina Wilson, George na William Kinyonga, Professor Shaban Omar, Maiko Beche, Issa Juma, Victor Boniface, Twahir Super Sax, Maneno Shaban Ali na wengineo. Abuu alipita kidogo wakati wa Simba Wanyika iliyochovuka na alipunguzwa kwa lugha ya kigeni alipewa redundancy.
HUYU JAMAA NI WA SIKU NYINGI ILA MAJUU NDO HAKUSEMI UONGO BADO ANAONEKANA KIJANA, NA KAMA SIKOSEI AMAOA MAMA WA KI-AMERIKA AMBAYE NI PROFESSOR WA TAALUMA CHUO KIKUU KIMOJA HUKO JAPAN, KWAO ASILIA NI MMWERA WA NACHINGWEA LAKINI WAZEE WAO WALIKUJA DAR SIKU NYINGI SANA TU, KWA WALE WALIOYOWAHI KUFANYIA KAZO NBC HEAD OFFICE ALIKUWA NA MDOGO WAKE PALE SITOMTAJA JINA HAPA KWA VILE SINA IDHINI YAKE NAYE KAMA SIKOSEI YUPO NJE NCHI GANI SIJUWI, NI MWANAMUZIKI WA SIKU NYINGI ILA NI YULE AMBAYE HAPENDI MAUJIKO. LOW PROFILE MAN.
ReplyDeleteMdau uliyeitaja Vundumuna umenikumbusha yule mpiga bezi Mganda Sammy Kasule yule mwendawazimu alikuwa analikung'uta bezi utafikiri kaliumba yeye na kina Mondo wa Mondondee na yule Mkongo mwingine aliyekuwaga Boma Liwanza. Jamaa wako wapi?
ReplyDelete