Ndugu Ankal Michuzi, asante sana kwa kazi murua ya kutuhabarisha. Ninakuomba wewe au mdau ye yote anisaidie kutatua huu utata ulionigubika kwa muda mrefu sasa – kuhusu viashiria vinavyotangulia jina la mtu tutumiavyo wakati wa kumwita, kuandika au kutoa habari juu yake.
Hii inatokea kila siku hususan katika vyombo vya habari vinapokuwa vinaandika habari juu matukio mbalimbali. Kuhusu wabunge, hakuna utata: wanawaashiriwa “Mheshimiwa” (Mhe). Kuhusu Rais, kuna utata kidogo: katika picha rasmi ya kutundika ukutani ameashiriwa “Ndugu” lakini kwingineko anaashiriwa “Mheshimiwa”.
Kuhusu wananchi wa kawaida (akina sisi pangu pakavu) ama tunaashiriwa “ndugu” au “Bw./Bi.” Je, ni vigezo vipi vinavyotumika kujua matumizi sahihi ya “ndugu”, “mheshimiwa”, na “Bwana/Bibi”? Kwa mfano, katika moja ya picha ulizotutundikia jana (Feb 23, 2010) iliyobeba kichwa cha habari “Msajili wa Magazeti Atembelea Uhuru na Mzalendo Leo” maelezo yaliyoambatishwa yalikuwa kama ifuatavyo:

"Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Uhuru Publications Ndugu Josiah Mufungo (kushoto)akimwonyesha Maktaba ya Ofisi yake Mkurugenzi Msaidizi na Msajili wa Magazeti wa Idara ya Habari (Maelezo) wa pili (Kushoto) Ndugu Raphael Hokororo alietembelea Ofisi hiyo kwa ajili ya kujifunza,na wa pili((Kulia) ni Msajili Msaidizi wa Idara ya Habari Ndugu Ismail Ngayonga,aliefutana nae.Na wa kwanza (Kulia) ni Mkutubi wa Maktaba hiyo ndugu Mussa Hassan akielezea kitu kwa Mkurugenzi huyo leo jijini Dar."

[ANGALIZO: katika picha hiyo inaonekana bado ofisi hiyo wametundika picha ya zamani ya Ndugu Rais JK. Washauriwe kuweka ile mpya!!!!].

Ninatanguliza shukrani
Mdau Muttabazi Bwenge

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Umesahau mbona hujaeleza kwanini wewe unajisalimisha kama MDAU badala ya Ndugu au Bwana. Hapo nazidi kuchanganyikiwa na kuparaganyikiwa zaidi

    ReplyDelete
  2. Sasa kwanini mimi pia nikifa naitwa MAREHEMU na Mwenye nafasi kubwa anaitwa HAYATI? Jamani si wote tumekufa? au mwenye nafasi anaenda na nafasi yake huko kuzimu? Namimi "pangu pakavu" nabakia kuwa mlala hoi?
    Haya namimi pia sijui maana nimechakua kuwa Mdau na siyo Ndugu. Kwahiyo...Wenu Mdau-NY, USA

    ReplyDelete
  3. Ndugu yangu Bwege hiyo isikupe shida sana. Siku hizi hata ile maana iliyokusudiwa kuhusu hicho kiashiria wala haipo.

    Maana yake siku hizi imelenga kwenye "kuwa na kitu". Kama upo kwenye kundi la kuwa na vitu then utaitwa mheshimiwa.

    ReplyDelete
  4. basi tu maujiko/kujiona uko juu kuliko wengine yasiyo na maana yanaboa kishenzi

    asa "mheshimiwa"for what??

    ReplyDelete
  5. Kuitwa mheshimiwa ililazimishwa na baadhi ya wabunge ikatungiwa sheria. Mtu anatakiwa aitwe mheshimiwa kutokana na matendo yake yanayompa hadhi mbele ya jamii anayoishi.

    Waheshimiwa wa kulazimisha hawana maana manake hao hao wanaitwa mafisadi, watuhumiwa wa wizi n.k huo uheshimiwa uko wapi???

    ReplyDelete
  6. kuna mtu anaitwa Mzee, siyo kwamba amezeeka. Utakuta ni kijana anaitwa na watu wanaomzidi umri Mzee fulani kwa sababu ya pesa, cheo n.k. kama wewe ni choka mbaya-pangu pakavu hakuna atakayekuita mheshimiwa....

    ReplyDelete
  7. SWALI JUU YA SWALI
    -------------------
    naomba nami kufahamishwa, kila ninapokwenda hospitalini au katika zahanati au maabara za kupima magonjwa, kila ninaye muona pale mara nyingi huwa hawana vitambulisho vya kuonyesha kuwa ni nani. sasa swali langu ni hili,je ni nani anayestahili kuitwa doctor? ni yeyote anaye tibu au kuna kuanzia ngazi maalum ambayo wanapaswa kuitwa doctor na wengine je tuwaiteje?mr/miss/mrs au? tafadhali nijulisheni nami pia!!!
    pia naomba nijulishwe ni kwanini daktari wakutibu anaitwa doctor,na mtu mwenye pHD ya fani yeyote ile pia anaitwa doctor? na viambata vyao vinakuwa vyote Dr? na je,daktari wa kutibu akiwa na phD je bado kiambata chake kinabaki kuwa DR au kinabadilika?
    SWALI lapili.
    *************
    inakuwaje madaktari wengine wanakuwa wamesoma miaka 4,wengine 5,wengine 6,wengine 7 n.k? je ina maana kwamba degree zao zinatofautiana kwa yale waliyo yasoma au inakuwaje?maana kama ukiangalia tofauti kati ya miaka 4-7 ni karibia tena miaka aliyosoma huyo wa miaka 4 sasa hii inakuwa imekaaje?
    asanteni kwa mtakao jibu.
    kimelanzoka.

    ReplyDelete
  8. Bi Kidude...teh teh teh teh!

    ReplyDelete
  9. Kuna wabunge walitunga sheria ya kuitwa 'waheshimiwa' kwa sababu 'wenzao' wanaitwa hivyo. Mimi ni kati ya walioshangaa kwa sababu nilidhani wale wabunge ni wenzetu sisi, kumbe sio. Sisi ni ndugu tu.
    Nadhani umefika wakati tuwarudishe 'down to earth'. Waheshimiwa gani wana tuhuma nzito za ufisadi namna hiyo? Kwa hiyo tuanze kuitana waheshimiwa. Kila mtu awe mheshimiwa, kama ilivyokuwa kila mtu ni ndugu enzi za Mwalimu. Au mnaonaje waheshimiwa?

    ReplyDelete
  10. Mdau unayeuliza swali la Dr, mtu mwenye shahada ya uzamivu kama PhD anatambulika kama Dr maana ni daktari wa falsafa.
    Kwa upande wa wataalamu wa huduma za afya, Dr ni mtu mwenye shahada ya MD. Wanaotibu wanajiita madokta kwa sababu ya uzito wa jina katika jamii. Ukweli ni kuwa wana majina ya fani zao lakini hawayapendi kwa mfano kuna waganga wasaidizi wa vijijini, waganga wasaidizi, matabibu, wauguzi, wakunga nk

    ReplyDelete
  11. Ndugu yangu BWEGE NINA HAYA MACHACHE PLZ SOMA KWA MAKINI.
    WAKATI WENZIO WANASOMA WEWE UMEKWENDA KUWINDA NDEGE NA MANATI YAKO LAIYI UNGEJUMUIKA MASCHOOL USINGE KUWA MBUMBU,(PILI)TUMEAMBIWA TUWAITE WANETU MAJINA MAZURI SIO KAMA LAKO NINA HAKIKA JINA LAKO BWEGE JAPO UNATAKA KUITWA 2PAC,,(TATU)matumizi ya kiswahili yanabadirika sana kutokana na sehemu inayotumiwa,PLZ USICHANGANYIKIWE UKAWA MBUMBU

    ReplyDelete
  12. LABDA TUISOME KWA KIZUNGU,
    Ankal Michuzi brother, thank you for the work murua the kutuhabarisha. Ninakuomba you or any member help me solve this controversy was onigubika for a long time now - about the indicators vinavyotangulia name during the call tutumiavyo, write or provide information on it.
    This happens every day especially in the media vinaandika When information on various events. About legislators, no contradiction: they waashiriwa "Mr." (Hon). About the President, there is little controversy: the official picture hanged on the wall has ashiriwa "brothers" but elsewhere he ashiriwa "Mr.".
    About ordinary (we were among dry) or we ashiriwa "brother" or "Bw. / Bi." What is the criteria used to know how the right use of "brother", "Mr.", and "Lord / Ms"? For example, in one of the image zotutundikia yesterday (Feb 23, 2010) iliyobeba head of information "Registrar of Newspapers and Liberty visits Mzalendo Leo" yaliyoambatishwa details were as follows:

    "Executive Editor Company Uhuru Publications Mufungo brother Josiah (left) he showed his Office Library Director and Assistant Registrar of Newspapers of the Department of Information (Translated) the second (left) Mr. Raphael Hokororo he etembelea the Office for the study, and the second ((right) is the Assistant Registrar of the Department of Information Ngayonga Dear Ismail, was the first efutana nae.Na (right) is the Librarian of the Library Mussa Hassan brothers explaining things to the Director in Dar today. "

    [NOTE: the picture still seems to have been hanged on the office of the old image of the Dear President JK. Washauriwe put the new !!!!].

    Ninatanguliza thanks

    ReplyDelete
  13. Mdau, picha iliyotundikwa ya nani unasema? Kitu gani kimekutambulisha kuwa pisha hiyo ni ya Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete? Nini tofauti yake, kwani hatambuliki kuwa ni yeye? Umeitambuaje? Haya mambo mnayokuza wadau, hebu angalieni kwanza yasije yakasababisha hoja zisizo na msingi sana kwa mpendwa Mheshimiwa wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete. Amependekeza kuandikwa neno Ndugu, kwa vile anajua yeye ni ndugu wa wananchi wa Tanzania. Mdau, wewe ndiyo unataka kumharibia Rais wetu aonekane vinginevyo!!
    Nilitembelea ofisi moja katika kijiji kimoja kilichoko mbali sana na makao makuu ya wilaya. Nilikuta picha huko ya Mheshimiwa huyo huyo. Wanakijiji kwa kumpenda Rais wao walichangishana na kwenda kununua ile picha ya kwanza inayomtambulisha kabisa Rais wetu. Kijiji kile hakina zahanati karibu pale. Hivi utakwenda hapo kwenda kuwazungumzia kuondoa picha eti ya zamani ya Rais jamani!!

    Nilifanya utafiti wangu binafsi kutaka kufahamu juu ya utata wa ile picha, nilimwita mtoto wa kama miaka 4 au 5. Nikanyoosha kidole kumwuliza, je ile picha unafahamu ni ya nani? Mtoto alijibu kitoto kabisa, "mmh, si ya Rais ile". Nikauliza Rais, nani anaitwa? jibu, "mmh, si Kikwete"
    Nilifarijika kuona hata mtoto wa umri ule anaitambua picha ya Rais wake.
    Hoja yangu hapa ni kwamba, picha zile hazitolewi bure. Ili kupata hiyo mpya inatakiwa kununua kwa Tsh 15,000/=. Kwa vile ile ya zamani mwenyewe Mheshimiwa haitaki, basi hiyo mpya ajitolee kuwabadilishia watu wake bure? Mbona picha za kugombea au za kuomba kura zinatolewa bure, tena nyingi sana? Au kwa sababu mnatuomba kura?, halafu mkipata, mnaanza kuzikana au kuzichukia picha zenu? Sidhani kuwa ndivyo alivyofikia Mheshimiwa katika hatua hiyo?
    Hivi ninyi washauri, hamumsihi kabisa Mheshimiwa akaliangalia hili?

    Mbona picha za Baba wa Taifa zipo za aina mbalimbali, akiwa kijana, akiwa shambani, nk, wala hakuwahi kuikataa picha yake hata moja kwa sababu fulani?

    Nadhani, hiyo inayosemwa inaonyesha alikuwa na uchovu, kwa mtu kama mimi ilikuwa ndiyo ya kujivunia kuona kuwa, kweli ulifanya kazi kuitaka nchi hii na watu wake.

    Mheshimiwa, tunakuomba, uienzi picha yako ya kumbukumbu ya mara tu ulipopata Ukuu wa nchi hii njema yenye utulivu na amani.

    Ni mimi Mtoa maoni, Mtanzania.

    ReplyDelete
  14. mdau uliye uliza kuhusu Dr, doctor ni kama inavyoelezewa hapa:
    Doctor of Medicine (MD, from the Latin Medicinæ Doctor meaning "Teacher of Medicine") is a doctoral degree for physicians (medical doctors). The degree is granted by medical schools.

    It is a first professional degree (qualifying degree) in some countries, including the United States and Canada, although training is entered after obtaining at least 90 credit hours of university level work (see second entry degree). In other countries, such as United Kingdom and India, the MD is either an advanced academic research degree similar to a PhD or a higher doctorate.[1] In Britain, Ireland, and many Commonwealth nations, the qualifying medical degree is instead the Bachelor of Science in Medicine, Bachelor of Medicine, Bachelor of Surgery (MBBS, BMBS, BM BCh, MB BCh BAO, or MBChB).
    kuhusu kwanini wengine wanasoma miaka 4,5,6,7,n.k hii inategemeana na sehemu pamoja na mahitaji ya sehemu hiyo. kumbuka kwamba hata tanzania kulipo jitokeza hitaji la waalimu baada ya kuanzishwa sekondari nyingi,ilibidi kufupisha muda wa kutrain waalimu ili kukidhi mahitaji.
    kuna nchi nyingi zilijaribu pia kufunza madaktari kwa miaka 4 kama china,zimbabwe,n.k lakini baadaye waligundua kuwa muda huo hautoshi kutokana na uzito wa fani yenyewe na mahitaji ya kiwango wanachotaka,hivyo wakalazimika pia kuongeza muda. hivyo hilo ni swala la mahitaji na sehemu.
    kama kunatofauti inakuwa hailengi kuathiri namna ya kutibu,bali inapunguza tu baadhi ya vitu kama fundamental medicine na sio clinical medicine,pia na vitu kama phylosophy,languages,pamoja na masomo mengine ya sayansi ya jamii ambayo kwa huyo anayesoma miaka 7 yeye hulazimika kuyasoma yote in full length. hii system hufuatwa na wale waliodumisha asili ya fani hii waliorithi mfumo wa kirumi(latin) ambapo ili kuitwa mwalimu wa kitu flani katika jamii ulipaswa kuwa umeiva katika kila nyanja,ili uweze kufundisha jamii na kutatua matatizo yao kwa kutumia approach tofauti.
    nadhani umepata mwanga kidogo. kuhusu viashiria,hivi pia hutegemea na nchi na lugha.
    kwa tanzania, tuna kada nyingi za afya,kuachilia MD=MO,pia kuna AMO,MA=CO,RMA.ambao hao hutibu pia ktk ngazi tofauti,na pia kuna paramedics ambao husaidia katika kufanya vipimo ktk idara tofauti,na pia kuna wauguzi wa ngazi mbalimbali pia.na wote hushirikiana ili kukusaidia wewe afya yako irejee katika uimara wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...