Mjomba naomba nafasi kurusha shida yangu kwa wanaglobu!
Mimi ni mpenzi wa mbwa sana tu, natafuta DOBERMAN PINCHER (JIKE) na ROTWEILLER (DUME) puppies kwa ajili ya kufuga.
Aliyenao, au anayefahamu nitakapowapata naomba awasiliane nami kwa barua pepe
Angalizo; “wawe pure breed” tafadhali
Weekend njema
Mdau Semesozi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Duu! Mbwa shoka hao, hakuna mpole hata mmoja kati yao. Cheki na polisi labda.

    ReplyDelete
  2. Mkubwa, sasa huyo dume unamtaka wa nini?

    ReplyDelete
  3. sema mimi napenda KUFUGA MBWA sio kusema mimi ni mpenzi wa mbwa au kiswahili hakina maneno mengi

    ReplyDelete
  4. Sasa wee anon wa tarehe 28/02 11:00 unamsahihisha na kwa misingi gani kwani wewe hujui kua umbwa ni shemeji zetu??? Ebo

    ReplyDelete
  5. guys: nasahihisha lugha kama nilivyoelekezwa na mdau! NAPENDA KUFUGA MBWA na ninahitaji Doba na Rotty (Doba Jike na Rotty dume). Kuhusu namhitaji dume wa nini kwa nini hujauliza jike wa nini? Ni bora kama huna cha kusema ukae kimya. Tusitumie networking vibaya. Shukran, Semesozi

    ReplyDelete
  6. Hao mbwa uwatajao, ni wa kumwaga kule ukerewe! ila nasikia lazima uwe na kibali cha kuwafugia kwani mara nyingi huya wanauwa watoto si mchezo wee google tu utaona.

    Wakichukia wanaweza wakakung'ata hata wewe mwenyewe.

    Mimi ningekushauri utafute German-Shefferd.kwani ni wazuri na kuwafundisha ni rahisi. Na kama ni kwa matumizi ya ulinzi binafsi basi wanafaa.

    ni hayo

    Mdau wa Tanangozi Iringa

    ReplyDelete
  7. Asante sana mdau wa Tanangozi kwa ushauri!

    Kama nilivyosema napenda ufugaji wa mbwa, tayari ninao German Shepherd kadhaa, niliwahi kuwa na Doba (siyo pure breed). Nia yangu ni kuwatumia kwa ulinzi na pia kama hobby. Najua walivyo hatari...hasa Rotty; ila nafuga kwa kuzingatia masharti ya kitaalamu na usalama!
    Asante, sasa una maanisha UKEREWE au UK-Rewe?

    ReplyDelete
  8. Huku Ukerewe kuna mtu kashtakiwa baada ya mbwa wake Rott dume kumvunua vufu la kichwa mtoto wa miaka 5 aliyekuwa anacheza kwenye park, kama si babake kupambana naye huyo mbwa huyo mtoto angalikufa. Nimesoma hiyo story jana tu kwenye yahoo na kuona picha za huyo mtoto alivyoshonwa na kuwa na kovu kichwani kuanzia sikio moja hadi lingine.

    Hivi huyu Rott nini sijui ni mbwa wa kawaida au mbwa mwitu au chui asiye na madoa? Tafuta hiyo link kwenye yahooutaikuta hiyo story. Au unataka kufanya cross breeding?

    ReplyDelete
  9. Ukiwa na rotweiller au doberman hakikisha hauwaachi mbwa hao na watoto. Zimetokea kesi nyingi sana za mbwa hao, hasa rotweiller, kuua watoto. Kuna mbwa wengine ambao si hatari sana kwa watoto lakini wanafaa kwa ulinzi.

    ReplyDelete
  10. mbwa hao inaonekana dili hata kamari unaweza ukawachezesha..

    ReplyDelete
  11. yani hii blog/globu inakufanya uwe chizi kwa kucheka peke yako dah!!

    yani ninacheka apa???

    wee annon 28feb,4:18pm

    kazi ipo umu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...