yanga imara
Mechi ya kwanza ya Simba na Yanga mwaka huu itafanyika jumapili april 4, kwenye uwanja wa Kalmia, kufuatia mechi itakayochezwa jumamosi kati ya Stars united na Maryland united japo uwanja itakapochezwa mechi hiyo bado kutangazwa.

Mtayarishaji wa mpambano huo wa Stars na Maryland United,Cyprian,amesema kutakua na nyama choma siku hiyo ya jumamosi april 3,na mechi hii ni re-union ya wachezaji wote wa maryland united na kutakuwa na zawadi maalum kwa wachezaji wazamani wa timu hiyo.

Wachezaji Watanzania waliowahi kuichezea Maryland united ni Liberatus Mwang'ombe,Vicent Ndusilo,Chiwa Mwombela,Elvis Dotto na Yahaya Kheri,na Cyprian ameiomba Stars united wachezaji hao wachezee Maryland united siku hiyo ya mpambano.

Salum Salum amesema yeye hana mkwara wowote,wachezaji hao wanaweza kuchezea timu hiyo,lakini wajue hawatakiwi kuifunga timu yao,mchezaji yeyote atakaeifunga timu yake ya Stars united ajue amefungiwa wewe chezea tu lakini ujue unatoa pasi tu
simba taifa kubwa


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mmependeza kuliko hata Yanga na Simba za kweli.

    ReplyDelete
  2. Duh hao simba wenyewe mbona wan vitambi hivi? hala hala jamani msije mka... uwanjani.

    ReplyDelete
  3. YANGA OYEEE....WAKO FIT, SIMBA KWISHA KAZI! CHALI KABISA!SIMBAVITAMBI.....KWANI HAO SIMBA WANAFIKIRI MASHINDANO YA KULA BAGA HAYO?

    ReplyDelete
  4. Teh, teh tehee!!!!yaani anon wa pili ulikuwa na mawazo kama yangu vitambi hivyo? Duh!

    ReplyDelete
  5. Hao Simba mbona vitambi vingi, mtatuahibisha

    ReplyDelete
  6. ,,,nyama choma,,,,duh!!

    mnatia aibu ivi saangapi mnakaa na kuota ivo vitambi???mwee kweli mswahili ni mswahili tu

    ReplyDelete
  7. Huyo mchezaji wa Simba (wa kwanza kushoto) naona alikuwa anajaribu kukificha kinundu chake lakini wapi kikaumuka tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...