Na Mohammed Mhina,
wa Jeshi la Polisi

Polisi mkoani Kigoma wamefanikiwa kumkamata askari Jeshi anayetuhumiwa kuhusika katika tukio la kuwaua wenzake wawili kwa kuwapiga risasi mkoani humo.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma ACP Twaha Ramadhani, amesema leo kuwa mtuhumiwa huyo mwenye namba MT.81071 Pte Yusuf Haji Hussein (30) amabaye ni mzaliwa wa Zanzibar kijiji cha Mamba Unguja Kaskazini alikamatwa na Polisi jana usiku huko kwenye eneo la Ilagala wilaya ya Kigoma vijijini kiasi cha kilometa 30 kutoka Kigoma mjini na kilometa 70 kutoka eneo alikofanyia tukio hilo.
Kamanda Ramadhani amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa wakati wa operesheni ya kumsaka iliyoendeshwa na Polisi kwa kushirikiana na Askari wa JWTZ waliosambaa katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Amesema makachero wa Polisi wanaendele kumhoji mtuhumiwa huyo na anategemewa kufikishwa mahakamani mara baada ya kumalizika kwa mahojiano ya kina.
Usiku wa kuamkia Novemba 23, 2009 mtuhumiwa huyo akiwa kwenye Kambi ya JWTZ Manyovu katika wilayani Kasulu mkoani Kigoma anatuhumiwa kuwauwa enzake kwa kuwapiga risasi akitumia silaha aina ya SMG.

Askari waliouawa ni MT.84720 Pte Hildefonce Burunja Masanja(35) na MT.8528 Pte Rashid Hassan Nawawi (25) na mara baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alikimbia na kutokomea msituni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. saw tunaka na yule askari mwenzenu aliyemuua swet naye asakwe kwa bidii hii hii

    ReplyDelete
  2. Hamna lolote wanataka misifa tu, yule aliyehusika na mauaji ktk kesi ya zombe yuko wapi?Msilete utoto hapa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...