JIJI ZIMA LA DAR LIMEZIZIMA KWA HABARI KWAMBA NDEGE MOJA YA ABIRIA IMEANGUKA KATIKA UWANJA WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE JIJINI DAR LEO NA KUUA WATO 50.
INGAWA NI KWELI KWAMBA KULIKUWA NA HEKAHEKA ZA VITENGO VYA DHARURA PAMOJA NA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA NA WANAHABARI KUKIMBILIA UWANJA WA NDEGE BAADA YA TAARIFA HIZO, SI UWONGO KWAMBA HILO LILIKUWA NI MOJAWAPO YA MAZOEZI YANAYOFANYWA KWA KUSTUKIZA ILI KUONA NI JINSI GANI WADAU WA DHARURA WATAWEZA KUITIKIA MWITO NA KWA KASI GANI.
AFISA HABARI WA MAMLAKA YA ANGA BW. ABEL NGAPEMBA AMEITHIBITISHA HILO NA KUSEMA ZOEZI LIMEENDA VYEMA NA KILA KIKOSI HUSIKA KILIWASILI UWANJANI KWA MUDA MZURI TU, NA KUWEZA KUZIMA MOTO WA MFANO WA NDEGE ULIOWASHWA KATIKATI YA UWANJA NA 'KUWAOKOA' MAJERUHI.
MWANDISHI WA GLOBU YA JAMII ALIYEKUWA MMOJA WA WANAHABARI WALIOKUWA WA MWANZO KUFIKA UWANJANI ANARIPOTI KWAMBA MILIO YA VING'GORA NA MAGARI YA DHARURA YA ZIMAMOTO NA AMBULENSI ZA HOSPITALI MBALIMBALI ZILIFANYA JIJI LA DAR KUZIZIMA KWA MUDA
Kaka Michu,
ReplyDeleteWazo zao lilikuwa zuri mno lakini tunatakiwa tutangaziwe watanzania kama kutakua na zoezi kama hilo sie wenye roho nyepesi kidogo tuache kupanda ndege na kuanza kutafuta nyungo za kusafiria
MWAMBIENI NABII YOHANA MASHAKA AJE ATENGENEZE BALABALA YA UWANJA WA NDEGE YA EAPOTI ILI AJALI ZISITOKEE KWENYE UWANJA HUO. YEYE NDO MGOMBEA WA UKONGA KWA HIYO KAZI KWAKE
ReplyDeletena wakati wa dharura ya kweli, je tutaitikia hivyo? Tanzania zaidi ya uijuavyo.
ReplyDeleteWananikumbusha mbaaali sana ... JKT Masange (Azimio la Arusha miaka ???). Umechoka hoi, waweka ubavu tu kwenye kitanda cha kamba, koplo fulani awasha moto ili kuruta muamke kwenda kuzima. Mkichelewa kuzima hadi 10 usiku ujue hakuna kulala tena. Duh! ilikuwa kazi kweri kweri!!!!
ReplyDeleteanony wa kwanza mngeambiwa zoezi then lisingefanikiwa,,,
ReplyDeletepambaf
ReplyDeleteAnnonymous wa kwanza umeangukia pua. Zoezi kama hilo ni la kawaida hata viwandani katika nchi zilizoendelea ili kuwapa watu zoezi katika kipindi cha dharura ya moto ama ajali. Sasa ukitangaza kama kutakuwa na zoezi hilo nani ataenda wakati anajua hakuna kilichotokea? Tutembee tuone na tutajifunza mengi kwa namufaa yetu .
ReplyDeleteThat is good;very good!!!
ReplyDeleteI don't think kama wanachofanya ni sawa kwani siku likitokea zali la kweli watu wanaweza wakafirkiri ni masihara then????? malizia mwenyewe
ReplyDelete