Ze fulanazzzzzzzzzzzz!
Hongera ankal kwa kazi nzuri ya kutuhabarisha wanajamii, naomba fulanazzzzzzzzz ya jamii ifike A-town fasta ili tuwakilishi vema globu yetu ya jamii.

Angalizo: Tunaomba utupe sehemu maalum
pa kununua ili kuepuka "made in Ungaltd"
Nawakilisha........
Mdau kutoka A-town.
----------------------
Mdau toka A-Taun usikonde wala nini.
Lete anwani yako kupitia issamichuzi@gmail.com ili uletewe ze fulanazzz moja kama kianzio. Nawashukuru pia wadau ambao wameshauri globu ya jamii itoe ze fulanzzz zenye kwaliti. hiyo haina shida. Naomba niwaeleze kwamba kauli niliyotoa na kuonekana ni ya kubughudhwa haikuwa hivyo bali ni katika kutesti zali kama wadau wako makini. Nimehakikisha hilo na naomba msamaha kwa yeyote niliyemkwaza. Haikuwa nia yangu kuudhi mdau yeyote.
Oda kama yako mdau zimepokewa toka sehemu mbalimbali duniani, ikiwa ni pamoja na Sauzi, Alaska, Tokyo, Saudia, UK, Canada, USA, China, Korea Kusini na Kaskazini, Algeria, India na sehemu kibao. Kwa kweli nimeguswa mno na oda hizo nami nitajitahidi kuzifanyia kazi.
Sio ze fulanazzz tu bali pia vitu kibao vinaandaliwa ikiwa ni pamoja na sun-visors, peni, mouse-pads, wallets na kadhalika. Hakuna kitachouzwa bali vyote vitatolewa bure kwa wadau kama shukurani ya kuendeleza libeneke.
Nawaheshimu na kuwapenda sana wadau wote.
Tufanye subira wakati vitu hivyo vinapoandaliwa na kutafutwa njia ya kuvigawa. Haitokuwa rahisi kiiivyo kumpatia kila mtu lakini hao wataopata zawadi hizo watakuwa wakala wa wengine wote wadau.
Kaa chonjo kuanza kupata zawadi ya Globu ya Jamii itapotimiza mdau wa milioni 7. Fuatilia mahesabu hapo chini kuume kujua siku itapowadia.
-Michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. kaka misoup tupo nyuma yako t-shirt tutauza suburi niende hkg kwa Jet lee uone nirudi lazma kariakoo kama kawa kwa bei mbaya usingesema broo.sasa kama mimi sitapata unategemea nini ndo mwanzo wa kwenda kwa babu kisa misuop hajanipa t-shirt bora nichonge zangu made in vungunguti na cha juu kidogo blog tunawakilisha ahsante kwa mchongo.

    ReplyDelete
  2. Ankal, nimefarijika sana kuona umechukua hatua hii ya kurejelea suala la kauli za wadau na wewe mwenyewe binafsi. Ndio customer service iliyopevuka. Wewe ni muungwana. Blogu/globu yako imekuwa kiungo cha wabongo kubadilishana mawazo juu ya masuala ya kijamii lakini pia kijiwe cha kutaniana of course bila kuchafua hewa. Hapa ndipo unapoona ule Utanzania tulioujua enzi hizo zilizopita. Watanzania wanapendana, wanakosoana, wanataniana, wanacheka hata pale wanapokuwa hawajui kama jioni watapata mlo wa kuweka mezani kwa familia zao!! Hii blogu huwa inanipa matumaini kuwa iko siku Tanzania itarejea kuwa Tanzania!!!
    Kilichokuwa kimenipa wasiwasi na sasa umeishanipa jibu ni huu utamaduni unaosambaa kama moto wa mabua kwamba mtu akikosolewa anakimbilia kujibu kuwa ni wivu, husuda, nk. Kukosoana sio kukosana bali ni kuboreshana (kwa mfano, tukubali kuwa clothing line ya Michuzi blog inaweza - na itaweza - kuboreshwa zaidi ya hapo ilipo). Ninakupongeza sana kwa uungwana na uchapaji kazi wako, na huu ni mfano wa kuigwa.
    Nitafurahi nikitumiwa fulana mbili. moja yangu na moja ya mamisapu.
    mlalahoi
    Anwani: Mbuyuni karibu na kwa mfuga mafisadi, Kinyerezi.

    ReplyDelete
  3. ankal michuzi aasikwambie mtu ,wadau tuko makiniyaani hatutestiki.nafikiri umeona mwenyewe reaction.
    itakuwa poa sana kama nami huku nikipata t-shirt moja niwakilishe globu ya jamii kwani nimeibuka kwa kasi au ni wapi naweza nunua??
    sipo kabisa katika hizo nchi ulizotaja nitakujulisha punde.TUWASILIANE

    ReplyDelete
  4. aminia babake. imetulia. uc'nsahau kaka nilishakuomba tangu jana. ha'fu vipi leo naona kimya!! mtandao una kwikwi nini?? leo kimya kimtindo au taswirazzzz ziko bize!!! teh teh teh. uckonde mwana hata ukikosa leo sio hatari wala nini manake cku 2-3 hizi haikuwa haba bado nakomaa nazo c unajua tena.
    Mdauwapajazzznatitizzz

    ReplyDelete
  5. Ankal tunaomba email yako, tuna matukio mengi tunashindwa kukutumia hayo matukio email yako tunaomba

    ReplyDelete
  6. KAKA MICHUZI asante kwa kazi yako nzuri ya kutuhabarisha, naamini unaweka historia kama mtanzania wa kwanza kuwa na blog yenye kuheshimika kupendwa na kuwafikia wadau wengi nje na ndani ya nchi.

    PENDEKEZO kwako kaka, VITU ulivyokusudia kugawa BURE vitumie kuanzisha online store AU kupitia outlet nyingine kama supermarket maarufu mijini na kuviuza kwa bei poa kabisa, nusu dola hadi dolla 5 na mapato yote utakayopata yapeleke kwenye CHARITY mbali mbali kama watoto YATIMA waathirika wa majanga makuu n.k. kufanya hivyo michuzi blog nayo itakuwa inawanufaisha wasiojiweza na utakuwa umetushirikisha wadau wa blog yako kutoa kwa jamii yetu huku tukiendeleza libeneke. Nawakilisha.
    Mdau Meli USA.

    ReplyDelete
  7. Ankal tutakosa wengi

    ReplyDelete
  8. SAHIHISHO: Huyo atakuwa mdau wa milioni nane (8) siyo saba kama ulivyoandika..we vipi??? hutaki maendeleo ya blogu yetu??
    PENDEKEZO: Kwani haziwezi kutengenezwa t-shirt za form six zenye strips kama ile ya ankal iwe na brand kama hizo zilizochapishwa?
    HONGERA/SHUKURANI:Ziwafikie wote waliobuni na kutoa wazo la T-shirts, mbarikiwe sana na hasa wewe ankal....
    OMBI/MZINGA: Na mimi nitaomba tu-tshirt tuwili tu(nasema tuwili ili msione ni mzigo mkubwa) kamoja kangu na kengine ka shemeji/wifi yenu (ni mkali sana nisipomletea zawadi) hiyo ya shemeji/wifi yenu naweza hata kuinunua kwa bei kubwa sanaili ipatikane na ili kujihakikishia mambo fulani , nadhani mnanielewa

    ReplyDelete
  9. Misupu nadhani ulikuwa unamaanisha mdau wa milioni 8. MDAU WA MILIONI SABA KESHAGONGA LONG TYM KITAMBO. Ni angalizo tu Kaka.

    Mdau chiggs, deslam

    ReplyDelete
  10. NAOMBA YANGU NYUMA IWE NA MAANDISHI HAYA

    MICHUZI BLOG ON TOUR 2010
    UKEREWE
    UFINI
    NEWALA
    WICHITA
    MASWA
    READING
    KILIMA NYE**
    UWANJA WA TAIFA

    ReplyDelete
  11. KAKA MICHUZI MI LABDA NINA WAZO KIDOGO LA KUKUPA HIZO T-SHIRT USITOE BURE BORA ZIUZWE TENA BEI GHALI HELA ITAKAYOPATIKANA ANZISHA MFUKO WA KUWASAIDIA WASIOJIWEZA!!!

    KUHUSU MDAU ANAYETAKA E-MAIL YA MITHUPU NI issamichuzi@gmail.com

    Nkya
    a-town

    ReplyDelete
  12. Bro' MICHUZI,hakikisha nakua mdau wa kwanza kwa hapa ZENJI,nipo online kwa 0713-238684,fanya bidii niwakilishe brand hio.

    ReplyDelete
  13. mweee ninavotamani iyo t-sheti jamani ni wengi tu tutakosa na tutalalamika sana tu ankal

    au vigezo gani vitatumika unaposema utawada wadau wachache?wadau wachache ni km vile wanaofanya nn umu bloguni...

    mwanza yaweje?

    ReplyDelete
  14. Na sisi wa Mtwara usitusahau kwa t-shirt za blog ya jamii

    ReplyDelete
  15. hongera kaka michuzi kwa kazi yako nzuri ok na nimefurahishwa sana lugha yako uliotumia mwanzo na kuona watu hawakufurahishwa nayo ukaandika upya vizuri sana hongera humu ni kubadilishana mawazo na mambo mengi sana huwa napapenda hapa mpaka nikaifanya kuwa home page kwenye laptop yangu ok god bless all!!!peace an love!!!!thanx

    ReplyDelete
  16. Waaaaaaaaawz
    seriously hongera kaka michuzi kwa grty job hizi fulana ni hotie also do have a namba ya huyo kaka wa kati nimemind hizi got a qiut smile!!!!!teh teh teh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...