Baadhi ya ombaomba wakiondoka baada ya kunyimwa kutumia ukumbi wa Idara ya Habari kutoa malalamiko yao kuwa wananyanyapaliwa na jamii kufuatia kisa cha mazingara cha daraja la Salender bridge majuzi
Walemavu wa viungo Bw. Khamis Said (shoto) na Bw.Peter Mayowela mkazi wa Kigamboni wakiwa na huzuni baada ya kuzuiwa kutoa taarifa zao katika Ukumbi wa habari maelezo jijini Dar leo walikofika kutoa malalamiko yao ya kunyanyapaliwa na jamii.

Baadhi ya walemavu wa viungo jijini Dar-es-Salaam wameiomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua hatua za kisheria na kukifungia chombo kimoja wapo cha habari nchini kwa kutoa taarifa zisizo na ukweli ndani yake ambazo zimepelekea kunyanyapaliwa katika sehemu mbali mbali za huduma za kijamii.

Wakizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbu wa habari na maelezo leo, baada ya kunyimwa fursa ya kufanya hivyo ndani, walemavu hao wamesema hivi karibuni Radio moja ilitoa taarifa kuwa katika maeneo ya darala la Salender bridge kuna mwanamke ambaye mkono wake uliota manyoya baada ya kutoa msaada kwa omba omba waliokuwa mahali pale.

Taarifa hizi kwa mujibu wa watu mbali mbali na vyombo mbali mbali zimeonekana kuwa tukio hilo lilitokea ambapo mwanamke huyo alilazimika kumbusu omba omba ili arudi katika hali yake ya kawaida, kitendo ambacho kilipelekea omba omba na mwanamke huyo kutoweka kimazingara.

Omba omba hao wamesema walifika eneo la tukio na kukitaka chombo hicho kudhibitisha taarifa hizo, lakini ikashindikana na hivyo wakaamua kufika ukumbi wa Idara ya habari (MAELEZO) kutoa tamko la kuwa taarifa si sahihi na kwamba zimewafanya walemavu wa viungo na omba omba kuitwa MIZUMU na jamii nzima - pamoja na kunyanyapaliwa hata kwenye vyombo vya usafiri,migahawani na sehemu mbali mbali za huduma ya jamii.

Ombaomba mmoja aliyejitambulisha kama Bi.Rehema alisema mpaka sasa tayari kuna walemavu 3 anaowafahamu ambao wamepewa NOTISI za masaa 24 kuhama kwenye nyumba walizopanga kwa kile kilichoitwa hofu ya wenye nyumba kufanyiwa mazingara.

Ameiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ijaribu kuliangalia swala hilo kwa makini kwani maisha yao hivi sasa yamekuwa ni yenye huzuni na masikitiko na wakati mwingine kujiona hawafai kuishi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. florian rweyemamuFebruary 24, 2010

    Mmmh!! sasa tusemeje? ni kweli vyombo vya habari vinapaswa kuitwa mhimili wa nne wa nchi?? au bado havijakomaa kuvishwa taji hili?. Mhimili mingine ya nchi ni mahakama, bunge na dola ( serikali). Kazi ya vyombo vya habari ni kuelimisha, kuburudisha, na kutoa habari. Vyombo vya habari vinapaswa kufahamu kuwa katika hiyo harakati ya kutimiza hayo malengo yake haviipotoshi jamii na kuidanganya. Vyombo vya habari ni muhimu sana hasa katika nchi hizi maskini ambazo uelewa wa wananchi ni mdogo sana.Leo yametokea haya ya manyoya ya salender bridge, hatujui kesho vyombo vya habari vitakuja na stori ipi itakayowachanganya watu. Tukumbuke kuwa waliochochea mauaji ya Rwanda ni vyombo vya habari.

    ReplyDelete
  2. Nadhani ni muhimu uchunguzi ufanyike ili kubaini kama kweli hilo tukio la la manyoya Selander Bridge ni kweli lilitokea au ni uzushi tu. Na kama lilitokea wahusika wachukuliwe hatua zinazostahili na kama halikutokea pia waliolianzisha wachukuliwe hatu pia. Na ikumbukwe pia kuwa hata kama jambo hilo lilitokea kweli haina maana kuwa jamii yote ya walemavu wanajihusisha na imani za kishirikina.

    ReplyDelete
  3. Hao walemavu walioandamana kwenda ukumbi wa habari maelezo wanajinyanyapaa wenyewe. Omba omba wote sio walemavu na walemavu wote sio omba omba.

    ReplyDelete
  4. hii kali kweli kweli!

    ReplyDelete
  5. sipati connection kati ya OMBAOMBA na WALEMAVU. kuna walemavu wengi tu ambao sio ombaomba na wanajitegemea wenyewe,na kuna OMBAOMBA wengi tu ambao sio walemavu lakini wanaishi kwa kundekeza kuomba,sasa hapa connection ya walemavu kuwa ombaomba iko wapi na ni kwa misingi ipi walemavu wanaandamana?huku ni kujibadili jina badala ya kuitwa walemavu wanajibandika jina la ombaomba.hao wanafaa washitakiwe na chama cha walemavu kwa kuwaaibisha watu wenye ulemavu flani na sio ombaomba.
    haya mambo ya vijituko yanaripotiwa sehemu nyingi tu hata kama hakuna proof,hivyo wanaolalamika pia kuwa vyombo vya habari washitakiwe sioni logic na misingi ya kuwashitaki,kwani hapa hakuna element yeyote inayo mzuru mtu au kuchochea mtu flani kuathiriwa. kwani hamjasikia habari za UFO hadi leo hii nani alishawahi kuprove pamoja na wanasayansi kufuatilia,imebaki kama ilivyo walichokiona kimebaki siri,na wasio kiona imebaki story that is all. so mambo ya kufuatilia ujingaujinga usio na mbele wala nyuma kuihusisha serikali sasa ni utoto. je ikiwa mtoa story ni psychiatric patient na yot kweli aliyaona akiwa ktk hali yake hiyo na anaamini hivyo na sauti alisikia wewe utaseamaje kama hujampeleka hospitalini agundulike kuwa ni mgonjwa. na kama kweli yalitokea na hakuna anayetaka kujiingiza kuthibitisha. vitu vingine vinapaswa kuangaliwa na kuwa ignored,sio kila kitu lazima serikali.
    wammbieni hao ombaomba waache ushamba,kama wanahitaji kukwamuliwa waache kuomba waseme ili wajitegemee,sio kulalamika kwamba sasa wao lazima waombe na kazi yao nikuomba hivyo isiingiliwe au kuathiriwa.kwanikuombaomba ni haki?au ni hali tu ya mpito inayomfanya awe muhitaji kwa muda flani wakati hana uwezo wa kujikimu,lakini inaweza kubadilika kesho akawa ni bonge la tajiri na sio ombamba tena.
    MZUSHI

    ReplyDelete
  6. mmmh kaazi kweli kweli bongo oyeeeee!!!!

    ankal unafaa kupewa nishani maana hizi habari za humu huwa sipendi nizikose sometimes narudi kazini usiku sana nakuwa nimechokaaaa

    lakini siwezi kulala bila kuwasha computer yangu na kuingia kwenye blog ya jamii kupata mapya ya kila siku

    big up ankal.

    ReplyDelete
  7. HIVI UKUMBI WA MAELEZO NI KWA AJILI YA WANASIASA TU? AU MLIOGOPA WATAUCHAFUA, NAO WANAHITAJI KUSIKILIZWA ACHENI KUWANYANYAPAA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...