Ankal,
Jana nilikuwa kwa dogo wangu mmoja ambaye anapenda sana kucheza mpira wa miguu na yeye ndiye wanaye mwamini awatunzie mipira ya kuchezea mtaani kwao.
Jana nilikuwa kwa dogo wangu mmoja ambaye anapenda sana kucheza mpira wa miguu na yeye ndiye wanaye mwamini awatunzie mipira ya kuchezea mtaani kwao.
Sasa jana alikuwa akiijaza upepo mipira hiyo ilikuwa kama sita hivi baada ya kujaa aliiweka juu ya kitu na wala sio sakafuni nikamuuliza kwanini akasema ukiiweka sakafuni ikifika asubuhi unakuta imepungua upepo.
Je kwanini ukiweka mpira sakafuni unapungua upepo????
Ni mipira ya Kichina? Teh teh!
ReplyDeleteHaupungui, kwa maana ya kutoka, ila kwa vile sakafuni ni baridi kuliko 'juu', upepo una 'condense', hivyo ujazo wake ndio unapungua.
sayansi ya hii kitu ni kama ifuatavyo.
ReplyDelete1. Ukijaza mpira upepo, unaongeza shinikizo la hewa ndani ya mpira.
2. Ongezeka la shinikizo la hewa ndani ya mpira linaongeza nishati (energy) katika molekyuli (chembechembe ndogo zinazofanya hewa).
3. Nishati ya chembechembe hizo huongezeka sambamba na jotoridi la tungamo(volume) ambamo chembechembe hizo zimo.
Ukiweka mpira sakafuni yafuatayo yatatokea.
1. Kama umechunguza, sakafu huwa yabaridi mara kwa mara hususani usiku.
2. Ukiweka mpira sakafuni, nishati itasambaa kutoka kwenye mpira kuelekea sakafuni mpaka jotoridi la ndani ya mpira litakapolingana na la sehemu ya sakafu inayogusana na mpira (Kanuni ya Fizikia hii baba, kitu inaitwa thermodynamics kwa lugha za ughaibuni)
3. Basi kupungua kwa jotoridi la mpira, kutasababisha kupungua kwa nishati ya chembechembe za hewa ndani ya mpira.
4. Kupungua kwa nishati ya chembechembe za hewa ndani ya mpira kutapunguza shinikizo la hewa ndani ya mpira.
5. Kupungua kwa shinikizo la hewa ndani ya mpira ndio kuisha upepo kwenyewe
hapo itakuwa hiyo mipira ina pancha ndogo na kama haina pancha basi valve ya mipira hiyo imeharibika kwa hiyo ina toa upepo na kama mipira haina pancha na valve ni nzima hazina ubovu basi kwa sheria za kifizikia, pV=nRT, p=mkandamizo (pressure), V=ujazo(volume), n=namba ya mole za hewa, R=konstant ya kewa, na T= halijoto(temperature).kwa ufupi pressure hupungua kama baridi inaongezeka, kwa hiyo kama hiyo sakafu ni baridi ya sakafu inaweza kupunguza pressure ya hewa ndani ya mpira na hiyo kuonekana mpira umepoteza upepo...
ReplyDeleteSakafu wakati wa usiku inakuwa ya baridi, ukiweka mpira mpira nao utapoteza joto na matokeo yake hewa ndani ya mpira itanywea..ndo mana inapungua upepo
ReplyDeleteNIKWELI KABISA MPIRA UKIWEKA KWENYE SAKAFU UNAPUNDUA UPEPO, HII NIKUTOKANA NA GRAVITATIONAL FORCE(nguvu za mvutano ulio ktk ta dunia) HIVYO HUSABABISHA UPEPO KUTOKA KTK MPIRA.
ReplyDeleteNi kwamba imeshakubalika kuwa ikiwekwa sakafuni upepo unapungua na sasa ni sababu inatafutwa? Au unataka kujua kama ni kweli ikiwekwa sakafuni upepo unapungua na kama ni kweli kwa nini?
ReplyDeletepole saana ndugu mtoto mdogo anakuzidi uelewa adi unataka wa2 wakusaidie haya ndo matatzo ya kukalili darasan wakat unatakiwa uelewe tutoleee upuzi wako we culikimbia shule
ReplyDeleteVIENA
Nataka kurudi shule acha utani
ReplyDeleteSomo la fizikia ni kama ujinga flani,kwani vitu unavyoviona au unakumbana navyo katika shughuli za kila siku,lakini karibu vyote wanasayansi wazungu walishavumbua,
ReplyDeleteMfano-mwingine wa kinyinga kwanini ukitupa kitu juu kinarudi chini?
Si shangai sana kwa wewe uliyeuliza swali la kizushi japo wengi wamejifunza,kwa maelezo zaidi soma Boyles na Charles Law
rgds
kisenga
Anonymous #2 umenikuna sana. 101%
ReplyDeleteMdau kutoka Ottawa
Mtoa coment wa 23 feb saa 01:25:00 mbona unampakazia mwezio nyie ndo mnofanya watu wengine wasiulizie. Kama unajua jibu au changia sio kupakazia. Tubadilike tuachene na tabia za kuzarau maswali ya mtu mwengine.
ReplyDeleteme niko hoi kwa kicheko apa hahahaa kwi kwi kwa msisitizo dah!!
ReplyDeleteannon #2 juu wee mwisho yani kama ticha wa jografia enzi zileeee
niko hoi,maana nilikua sijui pia
mtoa maoni na 2 safi safi sana,japo hujasema straight kuwa ni Boyles na Charles law,bt mchango wako safi
ReplyDeleteKwa wale wanaocomment negatively -jueni kuwa utaendelea kutojua na utawaambukiza na watoto zenu,
mtoa maoni namba tano acha uongo hapa gravitational force hai-apply, ila sio kosa lako inaonekana physics yako iliishia form four tu.
ReplyDeleteDuh!Anyn wa pili kiboko.Manake hiyo fizikia kaiweka kiswahili,jotorodi nishti. Pow....safi sana anony #2.
ReplyDeleteSisi watu wa Ughaibuni hata sijui tusemeje. Huku tunakokaa North East- kwa Obama, baridi na Ice Cream(Snow) kila siku (Nov-April).Mie mwanangu mipira yake kila siku iko sakafuni au nyuma ya gari. Huwa anakwenda kucheza mpira kwenye In-door Stadium on weekends. Last time tulijaza hii mipira ilikuwa May 2009 na mpaka leo iko safi tu. Pia kutokana na hali ya baridi ya huku basi Matairi ya magari yangekuwa Flat kila siku. Last time nilicheki air pressure ya matairi ya gari yangu I think is about 4yrs ago. Sasa waosha vinywa nayo hii imekaaje?
ReplyDeletewe mdau wa ottawa umekunwa wapi??
ReplyDeletemdau vancouver kwenye olympic
we mdau hapo juu hii mambo hahusiani na jiografia kamwe hapa ni ishu za fizikia ndo zinahusika kiinglishi chake physics!!
ReplyDeleteMchangia Hoja namba mbili kanipa raha sana, inaelekea jamaa katulia kwenye hiyo fizikia. Ila kosa hajatoa chanzo cha information (Reference) ningependa kwenda kuchimba kwa zaidi
ReplyDeleteAustralia
fizikia niliachia form 2,,,
ReplyDeletekazi kweli madesa aya
Mdau wa pili na aliyetaja Char les law ni vyema sana, keep the blog up.
ReplyDeleteA modern statement of Charles' law is:
At constant pressure, the volume of a given mass of an ideal gas increases or decreases by the same factor as its temperature on the absolute temperature scale (i.e. the gas expands as the temperature increases).[2]
which can be written as:
where V is the volume of the gas; and T is the absolute temperature. The law can also be usefully expressed as follows:
The equation shows that, as absolute temperature increases, the volume of the gas also increases in proportion.
WENU MKUFUNZI