Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa David Mwakyusa akiwasili makao makuu ya Taasisi ya Utafiti wa magonjwa ya Binadamu jijini Dar akiongozana na Katibu Mkuu wake Mh. Blandina Nyoni mchana huu kuzindua bodi ya taasisi hiyo. Nyuma toka shoto ni Dk. Mwele Malecela, Mganga Mkuu Kiongozi, Dk. Deo Mtasiwa na mwenyekiti mpya wa bodi hiyo Profesa Samuel Maselle
Profesa David Mwakyusa akiwa na Katibu Mkuu Blandina Nyoni na Mganga Mkuu Kiongozi katika picha ya pamoja na wajumbe wa bdoi mpya ya NMR aliyoizindua leo. Wajumbe wa bodi hiyo mpya ni pamoja na Mbunge wa Mbozi Magharibi Dk. Luka Siyame, Dr Hassan Mshinda, Dr. Edith Ngirwamungu, Jonathan Tangwa, Dr Alaick Abdallah Juma, Profesa Eligius Lyamuya, Dk. Catherine Kuwite, Bi. Elli Pallangyo, Elisa Mjema, Dk Salim Mohamed Abdullah na Dk. Mwele Malecela ndiye katibu wa bodi hiyo
Mgeni rasmi na ujumbe wake wakipozi na wafanyakazi wa makao makuu ya NIMR baada ya uzinduzi wa bodi



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kaka Michuzi,
    naomba urekebishe hiyo habari. Jina la Katibu Mkuu Blandina Nyoni halitakiwi kutanguliwa na 'Mh' "ki-itifaki"Huyo siyo Mheshimiwa hata kidogo. Hivyo vyeo vina watu wake. Nao ni Mabalozi, Wabunge, Mawaziri, Majaji...Makatibu Wakuu sio waheshimiwa labda tu kama ni Mabalozi...tafadhali rekebisha hiyo na kama una utata wasiliana na Wahusika ambao ni Itifaki ktk Wizara ya Mambo ya Nje.
    Hivi vyeo vimekuwa vikitumika kimakosa sana siku za hivi kabribuni,

    ReplyDelete
  2. Asante Michuzi kwa updates, taasisi hii inaitwa "TAASISI YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU"="NATIONAL INSTITUTE FOR MEDICAL RESEARCH(NIMR)"
    Asante

    ReplyDelete
  3. UPO JUUUUUU DA MWELE, UPO JUU!!!UNATUONYESHA MFANO MNOOOOOOO, BIG UP SISTA.

    WADOGO ZAKO

    U.K

    ReplyDelete
  4. CORRECTION

    INAITWA TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU

    ReplyDelete
  5. Da edith, miaka mingi sana hatujawasiliana tangu miaka ya form six.....du...

    ReplyDelete
  6. Dk. Mwele hongera sana, Mwenyezi Mungu azidi kukufunulia baraka. Amina.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...