Na Fredrick Mboma (pichani)

Kwa mara nyingine naona mjadala wa multiple citizenship unaibuka. Napenda kuuita “multiple citizenship” badala ya “dual citizenship” maana endapo hoja ya “dual citizenship” itashinda hakutakuwa na ugumu wa watu kuwa na uraia wa nchi hata kumi.

This time around waziri wetu wa mambo ya nje ameushikia bango. Pia mdau maaruf wa globu ya jamii, ndugu Mashaka naye ameunga mkono hoja hiyo. Kuna wengi ambao hawaafiki hoja hiyo. Waliowahi kujitokeza hapa kwenye globu ya jamii ni pamoja na Prof. Mbele na wanafunzi wa UDSM.

Kuna point moja ambayo inaongelewa ili kuunga mkono hoja ya multiple citizenship. Point hiyo ni pesa ambazo hutumwa Tanzania na Watanzania walioko nje. Wenzetu wanadai kwamba multiple citizenship iruhusiwe eti kwa kuwa madiaspora wanatuma pesa kuja Tanzania.

Lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa utumaji wa pesa unategemea mahusiano kati ya mtu na mtu. Kuna kipindi nilikuwa diaspora. Nilipata ajira nje ya nchi kwa muda wa mwaka mmoja. Katika kipindi hicho nilikuwa natuma pesa kwa mpenzi wangu, wazazi wangu na wadogo zangu. Pia nilikuwa natuma pesa kwa washirika wangu wa kibiashara. Hao ni watu muhimu kwangu na kusema ukweli ningewatumia tu hizo pesa hata kama ningechukua uraia wa nchi nilikokuwa nafanya kazi.

Sasa sitaki kusema kwamba kesi yangu ndio ya kila mtu, lakini kama kweli kuna mtu atakayekataa kutuma pesa kwa ndugu zake walioko Tanzania eti kwa sababu yeye amechukua uraia wa nchi nyingine naomba ajitokeze.
Kingine kilichojificha hapa katika hoja ya remittances ni kwamba kwa kukosa uraia wa nchi za kigeni wenzetu hawa wa diaspora watashindwa kupata kazi zenye mishahara mikubwa. Hivyo basi wakikosa kazi zenye mishahara mikubwa watakuwa na hela kidogo tu za kutuma kwa ndugu zao walioko Tanzania.

Hapa ndio mjadala unakuwa mtamu. Kwanza kabisa kuna Watanzania ambao wanafanya kazi nje ya nchi na hawana uraia wa nchi hizo. Je hawa walipataje kazi? Pili, huhitaji ruksa ya Tanzania ili kuchukua uraia wa nchi nyingine. Kama unaona kuna mafao zaidi kuchukua uraia wa nchi ya kigeni kuliko kubaki na uraia wa Tanzania nenda kachukue. Nani kakuzuia?

Ndugu zako, marafiki zako na watu wako wengine wa muhimu unaowatumiaga pesa za remittance hawataathirika maana wanajua utaendelea kuwatumia tu hata baada ya kubadili uraia. Kwa lugha nyingine remittances zitaendelea kuwepo hata ukiwa raia wa kigeni.

Kwa leo naomba niishie hapo. Kuna mengi ya kuongelea katika mjadala huu ila leo nilitaka kugusia remittances pekee.

Mungu Ibariki Tanzania
Wabariki na ndugu zetu wanaochakarika nje ya nchi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 69 mpaka sasa

  1. mkuu, ushauri mmoja. ukiwa unaandika, amua ni ligha gani utumie!

    Naomna mjanja sana, john mashaka ameshawapumbuwaza watu akili, sasa hivi wanamuona kama vile nabii wao na mesiah, ukimpinga tu, wafuasi wake watakumwagikia kaa nyuki

    naona umejaribu kuepuka kumpinga. ukiwa mwanamme wa shoka, tena mwenye upeo inabidi upingane na shoka. unaona us blogger alivyopata umaarufu kwa kupingana na mashaka?

    wabeba boxi hii shuguli tutalivalia njuga hadi lifike, uraia wa nchi mbili

    ReplyDelete
  2. duh hii inaonesha kiasi gani kuna watanzania waliolala akili zao,kuna mambo mengi sana yana faida kwa uraia wa nchi mbili,tatizo la watanzania ni waoga kuanza,tunasubiri kila nchi wakipitisha ndo na sisi tufanye,kenya na uganga wako kwenye hatuwa mwisho za kupitisha sheria,na uhakika asilimia 100 hautapa paka zikwazo maana hana ndugu zetu walifunguka macho siku nyingi,muda si mrefu tutasikia na rwanda nao wanaaanza.tuangalie nchi zinazokuja juu kwa uchumi africa,utagundua uraia wa nchi mbili umechangia kwa kiasi kikubwa.saa hivi ghana nchi inayoheshimia kuliko nchi yoyote africa.wanachi wake wengi wamerudi ghana kuwekeza na kuishi kutokana na uraia wa nchi mbili,ukisikiliza speech ya obama ghana utanielewa vizuri,ukiangalia taifa kama israel ni uraia wa nchi mbili umeweza kuwafanya wawe ni super power kwenye ukanda wa middle east,ni nchi ilioanzishwa tena muda usozidi miaka 50 lakini imeweza kujidhatiti na kuwa tishio hata kwa nchi zote za kiarabu.uraia wa nchi mbili kwanza ni security kwa mali za wengi,wahindi wengi wa tz waliokimbilia canada na uk wanatamani kurudi TZ,maana wanajua wanauwezo wa kuinvest na kupata faida,lakini systerm ya nchi za kiafrica bado mbovu,wanaogopa kubaki na uraia wa tz peke yake,hivyo hivyo wazalendo,tunatamani kurudi nyumbani kuishi,lakini kama tukiwa na uraia wa nchi mbili ni very easy biashara ikienda vibaya(kuibiwa,kufilisika,kudhulumiwa) unauwezo wa kurudi ulaya kuchuma tena.kuna mambo mengi sana ni ya muhimu kuhusu uraia wa nchi mbili,ona leo waghana walivyojazana kwenye NGOs za kimataifa.kwa sababu pia uraia wa nchi mbili unawafanya wengi waweze kuwasomesha ndugu zao nje ya nchi.

    ReplyDelete
  3. awee ndugu usiotaka uraia wa nchi mbili unaajenda gani ya siri,uraia wa nchi mbili ungekuwa wa matatizo basi wazungu wangekuwa wakwanza kuupinga,lakini wanajua faida zake ndo maana hawawezi hata siku moja kuupinga.waafrica sisi ndo zetu kila chenye maaana ndo kibaya kwetu.ona east africa comunity ilivyovyunjwa.na watu walidiriki kusema ni kupoteza mda.ona leo european union wanavyosaidiana.kila kukicha wanaziongeza nchi za easrt europe.sisi saa hivi ndo tumeshtuka tena.

    ReplyDelete
  4. kweli wabongo tumelogwa.unapinga uraia wa nchi mbili.kudaadeki

    ReplyDelete
  5. huyu jamaa mwanga,huwezi kuupinga hivi hivi.hawa ndo wanaodanganya wenzao ulaya shida tupu.msijaribu kwenda.wakati huku watu twazidi kula bata.

    ReplyDelete
  6. du kaazi kwelikweli maana hata sielewi alichoandika.!!!!!

    ReplyDelete
  7. Anonymous February, 15: 02:52PM jaribu kuelewa tofauti ya uraia wa nchi mbili na Muunganoa wa mataifa. East African Community na European Union inahusiana vipi na dual citizenship?
    Kama unaona uraia wa Tz huupendi, chukua uraia wa nchi unayoitaka hakuna atakayekusumbua. Acheni kuiga mambo

    ReplyDelete
  8. Mshikaji nafikiri ume miss the the point ya waziri wa mambo ya ndani. remmitance unayozungumzia ni minor issue lakini ina contribute kwa watanzania wenye mchango wa kutuma pesa.

    Unachotakiwa uelewe, kuwa kuna sisi wengine ambao tuna uwezo wa kujenga nyumba zaidi ya moja na kufungua biashara zaidi ya moja. Tumechukua uraia wa nchi za kigeni kwa sababu wakati tuko huko tunataka ku enjoy full benefits za citizen wa huku ambazo imetuwezesha kungua milango otherwise isingewezekana.
    Sasa kama hatuna haki za ku own land, houses, na business tunaishia kufanya kama wewe ulivyokuwa unafanya kutumia pesa familia. Lakini tungekuwa tuna haki tungeweza kuleta investment ambazo zingeleta ajira na kusadia sio tu familia zetu but also society at large.
    Vilevile, TZ inaweza kupunguza kuajiri western experts kwa kuajiri waTZ amabao western trained and experienced working in their field from the west. Kwasasa, since hatuna haki za huko kwa nini nije nyumbani alafu nipate huduma kama mgeni?
    Kumbuka hili, uraiya wa uingereza au marekani ni on paper tu na hautufanyi sisi kuwa wamerakani au waingereza, kuitamaduni au kiasilia. Sisi bado ni Wachaga, wameraki au Wahaya wa uingereza. Vilevile kumbuka Kabila zetu hazituhukumu kuhold passport ya Britishs au Americans, ila serekali ya Tanzania tu ndio unakutoa haki.In other words, as far as Bukoba concerns, mimi sihitaji uraia wa Tanzania kuprove anything, that is my ancestors land and I will fight to death to defend it regardless which passport I hold.
    To sum up, TZ inatakiwa iposition itself to benefits from wa TZ ambao wameweza kwenda nje kujifunza na kuchuma kichumi. TZ haiwezi kunitoa asilia yangu mimi hata kama haitanipa uraia wa TZ. Itakacho fanya ni kuwa irrelevant na insignificant kwangu kwa sababu wanaasilia wangu hawanikani kwa kuwa na urai wa nchi nyingine. Kumbuka hili, TZ imetengenzwa less that 50 years ago largely by British. Asilia yangu ina exist vijijini kwetu thousands of years kabla ya wakoloni hata kujua kuna bara lingine zaidi kwao huko Europe.

    ReplyDelete
  9. ACHENI KULETA LONGO LONGO ETI HAMUELEWI ALICHOANDIKa, MNAJIFANYA KISWAHILI HAMKIJUI KWA KUWA MNAISHI NJE?

    ALICHOSEMA HAPO NI KUWA TOENI SABABU ZA MSINGI SIO HIZO LONGO LONGO ZENU ZA REMITTANCES ZA £10, £20, £100 MNAZOTUMA MARA MOJA KWA MWAKA.

    MWAGENI SABABU ZA MSINGI HAPA ILI TUWAELEWE MNACHOKITAKA HASA NI NINI? SIO MNATAKA VYEO KWA KUSINGIZIA URAIA WA NCHI MBILI? TIMESHAWASTUKIA HAMNA LOLOTE MNATAKA KUWA KAMA POPO!

    ReplyDelete
  10. ndugu yangu sisi wenye passport za nje tukija bongo kujenga tunasumbuliwa sana,kuanzia mabalozi manispaa wote wanataka cha juu kwenye nyumba tulizo jenga,wanatisha wataripoti kuwa sio raia na umejenga.inabidi turisk kwa kuweka majina yandugu zetu kwenye nyumba.

    ReplyDelete
  11. Mimi naona hili swala aliloliongelea Frederick, ingebakia kwenye comment, kwa sababu moja kuu, kama angekua anamadhumuni ya kuongelea swala zima la uraia wa nchi mbili(kiuchambuzi), angejaribu kuchanganua zile faida/hasara wanazozipata wa raia wa nchi mbili, kama INDIA, Mexico nk, rather than indulging in purely a commentary rather than DISCUSSION on its MERIT... on just a single point, which already proven to be otherwise, from his percepctive, ndio maana tunaona CRDB, kufungua account za nje kwa watanzania nk, sasa kama ingekua hiyo CRDB, ingeondolewa vikwazo vya kwambwa lazima niwe raia wa Tazanzia au DUAL for that matter ili niweze kufungua account hiyo hiyo, JE HAPO huoni faida yake ? kwa kukusaidia Money invested in CRDB by DIASPORA(OF DUAL NOT JUST SINGLE CITIZENSHI), could be available back home kama mikopo ya kibiashara nk, kwa kuwasaidia watanzania wenyewe ??? Mengine mengi tu na faida zake lakini sina muda wa kuyachambua kwa sasa ??

    Swala langu, mimi nimfanya biashara ambae ninapeleka bidhaa mara kwa mara nchini Tanzania, na naweza kusema ni INVESTOR, ijapokua ni mdogo, hivi sasa nimeweza kuwapatia ajira watu wasiopungua kumi, huko huko Tanzania,

    Je Tanzania itanisaidiaje kuhusiana na Bureaucrats na mazingira mengine ya kibiashara ambayo ninayokumbwa nayo kama raia wa nchi nyingine, hali ya kuwa mimi ni mzawa na mzaliwa wa nchi(DOMICILE), na nimechagua kuwa raia wa nchi nyengine, kwa sababu ya nchi hii kunipatia urahisi ambao nchi yangu haunipatii, na wameweza kuona umuhimu wangu kijamii ...

    ReplyDelete
  12. Kufanya biashara/kazi nchi za nje unafanya hata bila dual citizenship nyie wabongo mnao ng'ang'ania uraia wa nchi mbili ndio mna agenda ya siri.

    Mbona Permanent residency zipo, kwanini msichukue Permanent residency na kubakia na uraia wa Tanzania au citizenship ya hizo nchi na kusahau about Tanzanian citizenship? Simple

    Mnaitosa Tanzania alafu mnajifanya Tanzania haiwezi kusimama bila nyinyi.....mnaota sana.

    Mdau Nje ya nchi

    ReplyDelete
  13. Umejitahidi sana kutoa pointi, tatizo hapa ni kwamba kama huna jina kubwa kama Mashaka ama Shayo ama US Blogger inakuwa si rahisi kuungwa mkono.

    ReplyDelete
  14. Mimi nahisi kabla huja andika kuhusu DUAL CITIZENSHIP chunguza kwa kina, kisha utafakari halafu ndio uandike... Sikulaumu ulivyoandika kwasababu sijui uwezo wako wa kuchumbua na kutafakari jambo. Labda kwa kukusaidia tu tafadhali kaa pembeni usikilize kwa makini na kuelewa vizuri nini maana ya Dual Citizenship hapo ndipo utaelewa lipi limezidi lipi faida au hasara...

    ReplyDelete
  15. Kwa wale wanajua kimombo tu, soma faida za urai wa nchi mbili, kwa mfano wa Ghana kupitia link hii

    http://www.modernghana.com/news/209842/1/the-benefits-of-dual-citizenship-to-the-socio-econ.html

    ReplyDelete
  16. Tanzania itajengwa na wenye moyo. Wanaodai uraia wa nchi mbili wanatoa sababu za kitoto kabisa. Kwani wawekezaji wanaokuja TZ wanadai uraia wa bongo ili wanufaike na sheria na taratibu kama waTZ waliopo nchini? Kama unataka kuwekeza tz wekeza kama walivyowengine si lazima uwe raia, kama ulichoma moto passport yako kazi kwako.

    ReplyDelete
  17. Ankali Michuzi,
    Naomba kwanza nimpongeze huyu jamaa na maoni yake. Kwa kweli huyu jamaa anafahamu fika what is talking. Tunahitaji watu kama hawa waweze ishauri makini kwa serikali na nchi.
    Nakubaliana naye kwa aslimia 100 kuwa si lazima kukamata ma-uraia ya nchi kibao eti ndo unaweza changia nchi yako. Kuna mifano mingi na tatifi zimeonesha hilo. Huyu Mhe. Membe anatakiwa akileta hiyo hoja atuletee na scientifc evidence{matokeo ya utafiti]
    Diaspora halisi wapo na hawahitaji hata uraia wa nchi hizo za kigeni kuchangia maendeleo ya nchi yao. Wamekuiwa wakituma michango yao ya pesa na kijamii kuisadia nchi yao. Nina maana wale watanzania wanaofanya shughuli zao nje ya nchi kihalali na always kwa kwa sababu za mahusiano yao ya nyumbani wamekuwa wakituma pesa,maarifa nk.
    Kwanza kuna maswali nataka niwaulize wananchi/wadau
    (1) Kuna "diaspora wangapi" wa Tanzania huko nje,
    (2) wanafanya nini na makisio ya kipato chao ni kiasi gani,?na wanatuma nyumbani 'remittance' ya kiasi gani,
    (3) je kuna mahusiano yeyote ya uraia wao na utumaji pesa nyumbani?Kama yapo ni yapi na kwanini yanaathiri utumaji pesa au mchango wao wa maendeleo Tanzania.

    Kaka michuzi mimi kama huyo jamaa nimekaa nje sana tu na bado sioni applicability ya hiyo kitu kwa Tanzania kwa sasa.Ni vyema kukawa na 'scientifi kufanya maamuzi ya kishabiki.
    Hongera Mdau Fredrick Mboma kwa scientific and fact.

    ReplyDelete
  18. JAMANI WATANZANIA NI NANI ALIYETULOGA? INAMAANA NYERERE ALIKUFA NA AKILI ZA WATANZANIA WOTE?

    TUFANYE UCHUNGUZI MDOGO TU, KUNA MAMBO NA MIPANGO MINGI SANA INABUNIWA NA WATANZANIA LAKINI UTEKELEZAJI WAKE NI ZERO, SABABU WANAZOTOA, UTAAMBIWA SERA, KATIBA, ILANI NA DIRA HAIRUHUSU;

    SUALA LA URAI WA NCHI MBILI WATU WANAANGALIA UPANDE WA MASLAHI TU BASI; HEBU FIKIRI WEWE UMEENDA NA MKE/MUME NJE MKAPATA MTOTO YULE MTOTO KWA SHERIA YA SASA SI MTANZANIA HANA SIFA YA KUWA MTANZANIA. SASA KWA WATOTO WANANYIMWA HAKI YA URAIA KWENYE ARDHI ZA MAMA NA BABA ZAO.

    MTOA HOJA ANA MAWAZO MGANDO, AFANYE TENA UTAFITI; NA WATU WOTE WENYE NIA NJEMA WANAMUUNGA MKONO WAZIRI WA MAMBO YA NJE.

    ReplyDelete
  19. WAZUNGU, WAARABU, WAPAKISTAN, WATURUKI WALIOJENGA NA KUENDESHA FEZA SCHOOLS, NA INVESTORS WENGINE WOOTE AMBAO WANAPEWA UPENDELEO KIBAO KUPITIA TIC, JE HAWA NI RAIA WA TANZANIA? SI WANAITWA FOREIGN INVESTORS? SASA KAMA HAKUNA FAIDA KWENYE HIZO INVESTMENT ZAO MPAKA WAWE RAIA WA TZ PIA, MBONA HAWAJAKIMBIA? NYIE MNA LENU TUSHAWASTUKIA, KWANZA NI WANGAPI NI RAIA WA HIZO NCHI? WANGAPI WANA GREEN CARD TU HUKO US, NA WANGAPI NI ASYLUM SEEKERS? MAANA MSIPIGE KELELE BURE WAKATI PASSPORT ZA TZ MMEISHAZICHANA, HALAFU HATA HAYO MAKARATASI MAMJAPATA BADO.

    SWALI LINGINE, JE MKIAMBIWA KULIPA KODI YA MAPATO NA KUFUATA SHERIA NYINGINE ZA TZ, MKO TAYARI? SI MNATAKA URAIA WA PANDE MBILI, MUANGALIE NA MAMBO MENGINE PIA KWA SABABU ISIJE JAMAA ANAWAUZA HUKU SERIKALI INATAKA KUPATA KUONGEZA MAPATO, MI NAONA HIYO DUAL INA FAIDA SANA KWA SERIKALI KWA SABABU ITAWADAI HAWA JAMAA TAX RETURNS KILA MWAKA.

    ReplyDelete
  20. NYIE VIBARAKA NA WAFUASI WA JOHN MASHAKA MSITUPIGIE KELELE. NENDENI MKAMUABUDU NABII WENU, BONGO MLISHAITENMA SAS MNTKA NINI? NABII WENU SASA AWAOKOE

    ReplyDelete
  21. yale yale ya Siasa, kwani woga ni wanini?, kwa nini tunaogopa Competition.. mashindano ni Afya kwa jamii, waachieni watanzania wawe na dual/Multiple citizenship, kwani itajenga mazingira ya upendo na uzalendo zaidi, ya nchi yetu, mimi naona si tatizo....

    ALLOW FREE MOVEMENT FOR ALL CITIZENS, NEVER MIND A PIECE OF DOCUMENT,


    kama tunafikira hizo, basi Mchaga abakie uchagani, na mnyamwezi abakie unyamwezini, mazingira ni yale yale, sema hii ya nchi kwa nchi, na kama tutaona faida ya FREE MOVEMENT kwa watu wa makabila so do MULTIPLE citizeship, kwani tatizo nini au faida ni nini, kama mazingira ya KIUCHUMI, NA MAENDELEO, we all see winning winning situation..

    ReplyDelete
  22. Maono yangu ni haya:
    A: Dual citizen inatolewa kwa Mtanzania anayetomba pasi ya nchi nyingine na sio mgeni anayetaka kuongeza uraia wa kitanzania.
    B: Swala sio kutuma pesa tu. Nchi nyingi zina sheria tofauti na hata yule aliyeku say UK atakutwa na sheria tofauti kulingoni Sweden. Kuna nchi miliki za mali, mikopo,pension na hata haki za watoto uliozaa na mke mgeni, zinaligana na status yako. Kwa maana nyingine, nondo ya crown pale tulipokuwa inaweza saidia kuongeza hali zetu kiuchumi pale tulipo hence investments/misaada bongo.
    Pia PP zetu ziliibiwa sana hapo nyuma, hivyo safari hata ndani ya EU/UK sometimes ni matatizo tu.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  23. Acheni kutuyeyusha bana,nyie kama mnaona huko nje ndio deal sana si bakini zenu tu? Msitake kutupelekesha na kutulazimisha tujue uwepo wenu nje ya nchi. Kama hamuwezi kukaa nje tieni tim bongo mtulie,kama vipi bakini huko. Tuondoleeni pumba zenu hapa.
    Tatizo la mbongo akishaenda nje basi anataka tz nzima ijue sasa yupo nje na kumsikiliza na kumnyenyekea kama nini sijui. Hatutaki ng'o!

    ReplyDelete
  24. Hili somo unapoliangalia kwa wote, DIASPORA wa nchi yoyote, ukuiingiza Tanzania ina FAIDA nyingi tu, toka ktk nyanza za elimu, uchumi na enrichment ya elimu na watu,

    ELIMU,


    kwa mfano wapo wasomi wengi nchi za watu, ambao ni watanzania, sasa kama hawa wakiweza kupata access ya kuja Tanzania kuinvest elimu yao, bila ya VIFICHO, vya kuwa na uraia wa nchi ya makazi, huoni kwamba hili litawawezesha hao wasomi kuchangia kwa kiasi kikubwa bila ya kuwa na kitanzi shingoni, knowing that it is against the law if he/she engage in any work in TANZANIA, kwa hiyo hawezi kutoa maarifa au mwelekeo wa aina yoyote ikiwa ni physical presence au in views, wakati yuko Tanzania.

    KIBIASHARA,

    kama ilivyoongelewa na wachangiaji wengine hapo juu, hii pia itahamasisha wafanyakazi wa nje ikiwa wadogo au wakubwa kupata hamasa ya kujua kwamba Tanzania daima itawaenzi ktk uwekezaji, mathalani hivi sasa wengi wako underground, kwa kuhofiwa kuhukumiwa kama traitor wa nchi, hatima yake, wachina wanawekeza Tanzania hata kwenye dala dala na kupata priviledge ya hali ya juu kuliko ya yule MTANZANIA mwenyewe ? Je hii inakaa wima? kwa miono yenu ?

    Ni mimi MTANZANIA HALISI, it happen to posses a piece of cardboard la nchi nyengine, kwa manufaa yangu, na NCHI YANGU TANZANIA..

    ReplyDelete
  25. prof. chiumeFebruary 15, 2010

    DUNIANI UKIWA MBUMBUMBU BASI KILA KITU KINA KUPITA PEMBENI KAMA JUHA TU LISILOJUA KAMA LIKO UCHI BALABALANI SASA WEWE UNAFIKIRI MEMBE AMA MASHAKA WANA AJENDA YA SIRI KUSAPOTI URAIA WA INCHI MBILI? WATU WANAONGELEA INVESTMENT KUBWA WEWE UNAONGELEA POINT ZA KUBEBA BOX. KWA TAARIFA YAKO KAMA SIYO RAIA WA BONGO HUWEZI KUMILIKI ARDHI HUWEZI KUFUNGUA BUSINESS KUBWA BILA KUWA NA PARTNER RAIA HUWEZI KUGOMBEA MADARAKA KAMA UBUNGE UWAZIRI N.K SASA UNACHOFIKIRIA WEWE NI PESA NA BOX TU HUJUI PIA KUNA ELIMU? WATANZANIA WASHIO UHAMISHONI WANASADIKIKA WANA AKILI NYINGI NA UPEO WA HALI YA JUU KULIKO WEWE AMBAYE HATA MALAWI HUJA FIKA AND YET YOU ARE CRITICISING THEM, INASIKITISHA SANA SIJUI UMEKULUPUKA NA KUANZA KUROPOKA MAJUNGU. MWULIZE KAKA MICHUZI ATAKUELEZA KINAGAUBAGA YEYE AMEBAHATIKA KUJA HUKU. ACHA USHAMBA WA KULIZIKA NA WALI. KUNA MAMBO MENGI YA WEWE KUFIKIRI KABLA YA KULOPOKA KWENYE MINUSO YA HARUSI. NITAKUTAFUTIA URAIA WA CHINA UJIONEE UTAMU WA MAISHA, HAYA NDUGU ZETU WAMEJIPELEKA KWENYE UHUJUMU UCHUMI SASA KILA KITU GHARAMA. BOX LINAUWA BE CAREFUL USIKURUPUKE UKI EXPECT UTAKUWA POA. ASANTE MICHUZI NINA WAKILISHA......!

    ReplyDelete
  26. huyu jamaa hata sijamwelewa anongelea nini na yupo upande gani maana anajifunga yeye mwenyewe halafu point hazina mapangilio wala mtiririko

    hizi ndio post za kuweka kwapani

    ReplyDelete
  27. Kweli ufinyu wa mawazo bado ni tatizo kubwa Tanzania.Watu wana viroho vya kwa nini badala ya kuangalia the big picture. Watu wanaposikia kuna watu wanaiishi nje wanachofikiria ni vijisenti wanavyotuma nyumbani ambavyo kwa ujinga wa wengi badala ya kufungua genge wanaenda kutanulia kiwanja. Tunapozungumzia fedha za watanzania wanaoishi nje hatuzungumzii vijisenti,tunaongelea uwekezaji wa kibiashara kunufaisha watanzania ndani ya nchi kiajira na kwa mapato ya kodi na sisi wenyewe kupata faida.Kuchukua uraia wa nchi nyngine haimaanishi hatutaki utanzania we are just looking for a better life,kila binadamu mwenye utimamu wa akili anapenda maisha bora.Kwa nyinyi mnaosema huitaji uraia wa nchi nyingine ili kuweza kufanya kazi kwenye hiyo nchi,mpo sahihi.Ila kuna ngazi fulani hutaruhusiwa kufika,si jeshini tu hata kwenye kazi kama engeneering au kwenye kazi za serikali za nchi husika.Kwa hiyo kama umeridhika kubeba boksi basi usichukue uraia lakini kama unataka kuboresha maisha yako ....
    Naomba mnaotoa hizi hoja mtumie fikra kutoka kichwani zaidi badala ya ma..... na wale mnaosema bongo inaendelea naomba muende vijijini mkaone watu wanaishije. Na swali la kizushi hivi kwa mtoa mada hivi unamaji ya bomba? wakati nchi kama Norway wanaongeza kifungu cha sheria kwenye katiba yao kinachosema high speed internet ni haki ya kila raia bongo umeme haujafikia asilimia 40 ya raia wake.
    NB;Kikwete maza bado anadai mafao yake.

    ReplyDelete
  28. Hebu acheni fikra finyu kwani uraia wa nchi mbili ndio nini. Wewe kama unataka kuwa na uraia hata wa nchi 100 ruksa hakuna atakayekuzuia, tuachieni bongo yetu nyie endeleeni kubeba mabox na kufanya kazi dhalimu huko ulaya na marekani. Tuliishi nje tukaona ya huko tumerudi nyumbani kujenga taifa. Mdau kila unapokuwa na jipya la kujadili njoo usikatishwe tamaa na hawa wavimba macho wanaojifanya eti wanakula bata ulaya wakati mnafanya kazi kwenye majokofu ya nyama.

    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  29. Mtoa maoni wa Tarehe Mon Feb 15, 02:52:00 PM

    Acha fikira za kikoloni wewe kwani kila wazungu wanachofanya ni sahihi? Nani amekuambia Tanzania inataka uraia wa nchi mbili kwa kuiga wazungu?

    watu kama nyie ndio mnoishia kutaka ndoa za jinsia moja, kisa wazungu wanafanya hivyo.

    ReplyDelete
  30. Nakubaliana na watu watakao tetea hoja ya kuweza kufanya biashara. Lakini bado kuna wafanyabiashara wengi duniani wanafanya biashara ktk nchi nyingine bila kuwa na uraia wa pale. Kwa mimi ingekuwa ni swala la kuishauri serikali kuangalia namna ya kuwezesha investor kuja na kufanya biashara. Naelewa wengi mliko nje mnataka kwa aliji ya kuweza kuja nyumbani bila kuomba viza. Maana hata hivyo bado wengi ya watanzania walioko nje hawajawa na mitaji ya kuweza kufanya biashara katika nchi mbili. Watakoo faidi zaidi ni wahindi watakuja kuiba tu na kukimbilia canada na nchi kama hizo na nyie mkabakia hamna kitu. Nina uhakika watanzania mlioko nje mkijitahidi kuwa na umoja kifedha mtaweza kufanya mengi. Lakini bado hakuna hoja kubwa sana kwa sasa.
    Kuingia na kutoka inasumbua, ukimbizi mbaya!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  31. Frederick Mboma,Ulichokiandika
    hakieleweki!?
    Kabala ujaandika ungefanya utafiti wa kina kwanza,kuhusu faida na hasara za uraia wa nchi nyingi.
    (b)Pia ungetafiti mataifa jirani yaliyo tuzunguka kama vile,Uganda,Kenya,Rwanda,Burundi hata Kongo(DRC) nchi ambazo kwa namna moja au nyingine tunashea au kushirikiana nazo ktk masoko ya kibiashara au ajira,penginepo hata katika tunachokiita jumuiya nk.ungetafiti nchi hizo zimekuaje zianze kuwaruhusu wanchi wake kuwa na uraia wa nchi nyingi? lazima itakuwa kwa maslahi ya nchi zao.
    (B) Frederick maandiko yako yanaonyesha kwa kiasi kikubwa kuwa
    itakuwa labda msoni lakini ujaelimika!!?? yaani kwa kiasi kikubwa umepitwa na wakati pamoja na mambo mengi sana ya karne hii?!
    Mahandishi yako yameonyesha kwa kiasi fulani kuwa umelewa ulevi wa kisiasa chakali! kuliko mtazamo wa kiuchumi kuonyesha wapi! dunia inakwenda na faida gani? zinazopatikana katika uraia wa nchi nyingi?
    (D) Labda nikuelimishe kidogo,
    kwa kuwa dunia kwa sasa ni kijiji,na kuzingatia kukua kwa upinzani wa kibiashara na kiuchumi
    TANZANIA haina jinsi lazima iwaruhusu raia wake kuwa na uhuru wa uraia wa nchi mbili,vinginevyo
    Tanzania itafikia hatua ya kuletewa wataalamu waafrika wenzao wenye uraia wa nchi fulani za EU,USA,n.k waje kufanya kazi kama TX? na tanzania itakuwa haina uwezo wa kuwakataa? mfano IMF,au World Bank au EU ambao ndio wafadhili wakubwa wa Tanzania,wafadhali hao watakapo pendekeza kuwa wanataka miradi yote wanayoifadhili isimamiwe pia na japo kuwa wataalam raia wa EU,USA n.k basi hakuna shaka mkenya,mrundi,mganda mwenye uraia wa EU,au USA akaomba nafasi hizo na kuletwa Tanzania kama TX na pia kulipwa mshaara kwa US dola,Euro sio fedha za madafu
    Sasa kama Tanzania itakuwa imewaruhusu raia wake kuwa na uraia wa nchi nyingi ..watanzania wataweza kuleta ushindani katika soko la ajira kama nililolitaja .
    Lakini kwa wewe mtazamo wako ni
    KUNYWA MAJI YA BENDERA MPAKA YAKAKULEVYA hatuwezi kukuelimisha
    kwani ni sawa na kumpigia gita Mbuzi

    ReplyDelete
  32. Mdau mtoa hoja umeongea vizuri,lakini katika haja yako ya kwanza ni vizuri kuwaelisha wadau kuwa:1.Pesa zinapotumwa kwa ndugu na jamaa kutoka nje haziwafaidishi tu wale wanaozipokea,bali zinachangia kuliingizia taifa pesa za kigeni na hivyo kukuza uchumi wa Tanzania.2.Nikweli kuwa wapo watu wengi wanaofanya kazi nje wakiwa raia wa Tanzania na siyo vinginevyo.Watu hawa hawezi kuwa ma CEOs,directors au ma presidents wa makampuni wanayoyafanyia kazi.Kutokana na katiba za hawa wenzetu nilazima nafasi fulani zishikwe na raia wa nchi zao.3.Sidhani kama watanzania waoishi nje wanahitaji vyeo wakirudi nyumbani,kama wapo ni wachache sana.Wengi wanaporudi nyumbani hupenda kujiajiri wenyewe na kusaidia ajira kwa watanzania.Sasa wanapokuwa siyo raia wa Tanzania,pale mahusiano kati ya Tanzania na nchi ambazo hawa watu ni raia wake yanapoharibika,serikali ya Tanzania inahaki ya kuwafukuza nchini hawa watu.Hivyo wataondoka na kuacha vitega uchumi vyao kama viwanda ,mabenki nk.Tatizo ninaloliona mimi ni kuwa wengi tulio soma na kufanya kazi nyumbani tunawasiwasi sana na ajira zetu.Tunadhani kuwa dua citizenship itafanya wenzetu hawa warudi kuja kuchukua ajira zetu.Ndiyo maana wengiwetu tunatumia chuki kujadili suala hili badala ya ku-reason.Tungejadili faida na hasara za hili swala halafu tuache watu wafikie conclusion.Wakati Nyerere anaondoka madarakani wengi wetu tulikuwa na wasiwasi kuwa nchi ingeangamia kwasababu si rahisi kumpata Nyerere mwingine.Pia tukumbuke watu walivyokuwa na uoga kipindi kile cha mjadala wa chama kimoja na vyama vingi.Iliwahi kutolewa mifano ya kutisha na wana CCM kuwa Tanzania tukiruhusu mfumo wa vyama vingi kutakuwa na machafuko kama yale ya Rwanda,Burundi au Somalia.Lakini mabadiliko yote hayo yalitokea bila kuwepo mwisho wa dunia.Kwahiyo ndugu zangu wadau tutake tusitake dual citizenship itakuja pale muda utakapowadia.Watu wataelimishwa vizuri na wataelewa ingawa tofauti zitaendelea kuwepo.Mabadiliko yaliyotokea na yatakayotokea tutayakubali kutoka na umaskini wa taifa letu.Kama tunaishi kwa kutegemea misaada kutoka nje kuna siku zitafika tutaruhusu mpaka ndoa za jinsia moja.Hatuna jeuri kwasababu ya umaskini.

    ReplyDelete
  33. Fredirick alijaribu kuzamia nje akafanya kazi ndog ndogo kihuni kihuni (kinyume na sheria) ndiyo maana akarudi Tz baada ya mwaka mmoja tu. Wenye akili zao wanajua umuhimu wa uraia wa nchi mbili na hamna haja ya kujieleza hapa, anayetaka elimu asome uchumi na siasa.
    Watanzania wanaoishi nje ya nchi wanasaidia sana nchi kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hii sera isipopita nchi ndiyo itakayopata hasara, wadau walioko nje wataendelea kutesa pamoja na familia zao.
    Msafiri Al-Khamis

    ReplyDelete
  34. silly boy inee?
    uk

    ReplyDelete
  35. Wakati wa Mkapa, kulikuwa na mjadala huu wa dual citizenship kutoka kwa wabongo walio nje. Liliulizwa swali kwa wale watanzani walio nje. Kama Mzungu anaweza kufungasha virago akaja kujaribu bongo niki kinakushinda wewe. Sawa wee chukua urai wa ulipo ili upata benefits zote za huko, lakini ukija nyumbani kwanini lazima uwe na citizenship ili uezeke. Hawa wa South, wachina wa kimachinga na wengineo mbona hawana na bado wanakuja?

    Pale tutapoweza kulijubi hili swali vizuri naona itarahisha sana kuwa convince the public in general.

    ReplyDelete
  36. Mdau Fredrick Mboma,

    Ninavyokufahamu wewe una elimu, lakini kwenye hii mada kwa kweli umeniangusha. Hizi hoja zako wakisoma wasio bahatika kwenda shule kama wewe wanaweza kusema umuhimu wa elimu unatiwa chumvi..!!

    Nashindwa kabisa kuamini, unapinga hoja ya Uraia wa Nchi 2 kwa kigezo cha hela ya mboga £10/$20 etc ambazo tunawatumia Watanzania wenzetu wasio na kazi hapo nyumbani…??!!!

    Kweli haya ndiyo uliyojinza ulipokuwa DRC??

    Shukhrani kwa wadau hapo juu "Mon Feb 15, 02:49:00 PM" na "Mon Feb 15, 03:15:00 PM" kwa kujaribu kukuelewesha. Sioni haja ya kurudia sababu najua hoja ikifika Bungeni utasikia mengine mengi ambayo yamefanyiwa utafiti makini. Kutakuwa na hoja nzito kuliko hizi za kwako na ile Prof Shivji aliyesema walioka nje ya Tanzania ni watoto wa Vigogo.!!

    Nina imani utasikiliza na kuelewa kwa faida yako na Watanzania wengine.

    Nimalizie kwa kunukuu hotuba ya [then] Sen Barack Obama alipokuwa anahutubia mkutano wa chama chake cha Democrats mwaka cha 2004 jijini Boston "I believe that we have a righteous wind at our backs and that as we stand on the crossroads of history, we can make the right choices, and meet the challenges that face us." Uraia wa Nchi 2 ni uamuzi muhimu kwa Tanzania. Nina imani tutasimama upande sahihi wa historia.

    Network Engineer (NE),
    Reading, UK

    ReplyDelete
  37. Uraia wa nchi mbili naupenda lakini kila nikiangalia tunavyopakuliwa madini yetu naona hatujakomaa vya kutosha kutunga sheria ya uraia wa nchi mbili au zaidi itakayotusaidia.
    Mfano wa faida za uraia wa nchi mbili ni kama hivi: mwanasoka wa kibongo akipata nafasi kucheza soka ya kulipwa kwenye nchi kama Hispania anatumia moja ya nafasi ambazo nchi ile inazo za kusajili wachezaji wa kimataifa. Kiwango kikishuka (majeruhi yanaweza kusababisha) inabidi atafute timu nyingine ambayo iko tayari kumsajili kwa kutumia nafasi yake ya kusajili kimataifa. Ni vigumu. Kumbe kama amechukua uraia wa nchi ya mataifa ya Ulaya anaweza kupata timu kwa urahisi zaidi kwa sababu hachukui nafasi adimu. Kiwango kinapanda kwa kucheza.

    ReplyDelete
  38. mbona serikali iko radhi kuwapa uraia wakimbizi wa Kinyarwanda na Kirundi? watoe uraia tu Watanzania waliopoteza uraia kwa sababu moja au nyingine. binafsi sioni hasara yoyote ile itakayopatikana kwa kuwepo kwa dual citizenship.

    ReplyDelete
  39. tatizo asilimia kubwa ya wasomaji wa blog hii ni wale wale waliukana uraia wa Tanzania huku wanauhitaji. Ni kitu gani ambacho hakieleweki alichoandika jamaa. Eti faida ya uraia wa nchi mbili ni ku invest nyumbani? acheni hizo nani kawazuia ku invest bongo hata kama mlishaukana uraia? kwani investors wote walio bongo ni wa Tanzania? acheni longo longo kama jamaa livyosema hapo juu. Toeni sababu za kwanini dual citizenship ipitishwe na sio kisema eti sijui kenya wanapitisha. acheni longo longo mmeshaukana uraia sasa mnataka nini. Kama ni hela haziangalii uraia acheni kutuzingua

    ReplyDelete
  40. Ndio hii issue naona ni kubwa make inaleta changamoto kubwa. Kwa kifupi ni kwamba dual citizenship inaasilimia kubwa ya faida kwa Tanzania nikimaanisha kuwa na mengi mazuri ya kunufaisha nchi. Na kama kunamatatizo yanayoweza kutokea kutokana na hili basi sijui ni yapi make hata sifikirii lolote. Lakini vile vile sioni kuwa kama umechukua uraia wa nchi nyingine kuna tatizo kuwekeza nyumbani ukilinganisha system ya nchi yetu ilivyo. Usipoenda bongo kwa kujitangaza kuwa umetoka nje na vilevile umechukua uraia wa nchi nyingine nani atajua business yako. Hapa tatizo wabongo wengi tukienda nyumbani tunataka kutangaza o mie natoka nje, o mie siraia tena ni raia wa nchi fulani. Keep your business to yourself. Tanzania as a country doesn't know when you leave or comeback. Ukizingatia hili unaweza ukainvest bongo na mambo yakaenda kama kawa. Mbona kuna watu na wanafahamika kuwa wamezaliwa nchi za nje tena wako kwenye nafasi za kufahamika na public na wanatesa bongo kama kawaida. Unataka kuniambia wameukana uraia wa nchi walizozaliwa. Wakati hii issue inaendelea kujadiliwa nendeni mkainvest bongo as long as you keep your business to yourself. Simple.

    ReplyDelete
  41. Wewe uliyoongea hivyo ni very ignorant, na sijui ni nchi gani uliwahi kusafiri labda burundi sababu kwa sisi ambao tunaishi nchi za nje toka watoto tunaelewa umuhimu wa urahia wa nchi mbili, your very very ignorant, i mean ur very ignorant nashindwa hata jinsi ya kueleze.Ukiwahi sikumoja kusafiri uje labda maarekani au londoni utajua jinsi watu wanavyofanya kazi lakini since hujawahi siwezi nikajisumbua kuelezea, ni vizuri ukae kimya muda mwingine kama ujui kitu watu wata kuona una busara kuliko ufungue mdomo wako watu wakujue jinsi gani ulivyopumba. Tarafali acha kabisa kuongelea vitu ambavyo huvijui maisha ya mbagala tofauti sana na nje.

    ReplyDelete
  42. Na nyie wote mnaochangia eti hamtaki dual citizenship kumbukeni wivu ni kidonda mnajua kabisa mnataka na wala tusibishane kuhusu hilo sema hamuwezi tu kupata wenyewe mnajifanya mmeridhika na bongo upuuzi mtupu, unajua nini maybe wewe hujapata uwezi kujua kitukuu chako!

    ReplyDelete
  43. bwana mbona nakuhurumia kuwa na ujasiri wa kutuletea upupu wako hapa. wakina john mashaka wanaandika wakishafanya utafiti wa kutosha hawakurupuki, na pointi wanakuwa nazo hata mimi mpinzani, nawapinga ili mradi ila njua pointi wanazo. kwa hiyo mkuu, tafadhali rudishe upupu wako jikoni, umeniangusha sana. au ulifundishwa na profesa mbele?

    ReplyDelete
  44. Do your homework before you speak son, don't embarrass yourself. Look at a bigger picture, investments and not petty cash for subsistance. Ukiwa ni raia wa marekani you get access to almost unlimited funds to invest it anywhere in the world just so you know. I really cant't help you because I feel like you wont understand me, we obviously speak at different levels. Ushauri wa bure, usiandike things you only know one side of the story, obviously the other side is usiku wa giza kwako. Mungu akujalie werevu zaidi.

    ReplyDelete
  45. cha ajabu wanaopinga hata hawajui kwanini wanapinga hii dual citz,haya mawazo ya kizamani na kubanana bila sababu ya maana lazima yaishe...waache watu wawe na freedom wanayotaka,sielewi kabisa hawa mawazo mgando nia yao nini zaidi ya sababu za kipuuzi tuu,mtake msitake dual citz inakuja na hakuna kitu mtafanya zaidi ya makelele yenu yasiyo na faida

    ReplyDelete
  46. TUNASHINDWA KU-INVEST BILA VITISHO NA KODI LUKUKI AMBAZO HUPOZWA KWA RUSHWA NZITO.

    HATUTAKII HII.

    JAMAA WA UHAMIAJI NAO WATUNYEMELEA.


    CHAGUENI KATI YA HELA ZA MATUMIZI (URAIA MMOJA) AU HELA ZA UWEKEZAJI (URAIA MWENGI)

    ReplyDelete
  47. baada ya kusoma paragraph ya mwazo tu nimeamua kusita kusoma zaidi kwani inaonyesha kabisa mwandishi hajui lolote juu ya suli zima la uraia wa nchi mbili na upatikanaji wake.

    ReplyDelete
  48. SIKU ZOTE NI NGUMU MNO KUMWAMBIA MJINGA MAANA NA HAKUNA KITU KIBAYA KAMA UKIWA MASKINI WA MAWAZO.

    YAANI UNATOKA TU HUKO UNAKUJA KUANDIKA UPUMBAVU KAMA HUU ETI HAWA NDIYO WASOMI WA WETU WA TANZANIA NA HIZI NDIYO ARTICLES ZAO. YAANI ANAHISI KAONGEA POINT KWELIKWELI, INASIKITISHA MNO.

    HUYO MASHAKA NDIYO NANI? NINA MAANA ANANYADHIFA GANI YA KUWEZA KUWASEMEA WATANZANIA WOTE WALIO NJE?.NA HAO WANAFUNZI WA UDSM WANANYADHIFA AU UWEZO GANI WA AJABU (KIPEKEE) WA KUWEZA KUWASEMEA WATANZANIA MILLIONI 40.

    1.TAFADHARI KIJANA NENDA KATAFUTE UMAARUFU KUPITIA BONGO FLAVA SIYO HAPA SAWA.

    2. NANI ANATAKA KUONA PICHA YAKO KWANINI USITUME UJUMBE TU PICHA YAKO SISI INATUHUSU NINI?

    3.NENDA KASOME YENYE MAANA HALAFU NDIYO UJE NAYO HAPA SAWA. HUYO PROF.MBELE MWENYE AMESHAJISHUSHA THAMANI KWA MAANA HIYO CHOCHOTE ATAKACHOONGEA NYIE HUKU WA UDSM NDIYO MTAMSIKILIZA SAWA.

    4.SOMA KWANZA UFAHAMU FAIDA ZA URAIA WA NCHI MBILI NA HASARA ZAKE, FAIDA ZA URAIA MMOJA NA HASARA ZAKE. SOMA UCHUMI WA TANZANIA KWANZA, HALAFU FANYA UTAFITI WA WATANZANIA WANAOISHI NJE UJUE UWEZO WAO.UKISHAMALIZA HAPO ANGALIA FAIDA NA HASARA ZAKE NDIYO UJE HAPA NA MIFANO HALISI SAWA.

    SIYO ULIKAA NJE SISI INATUSAIDIA NINI? USIWE MPUMBAVU MDOGO WANGU. KUNA MAMBO YANAWEZA KUKUPA UMAARUFU YAKAWA HATA YA KIPUMBAVU LAKINI JARIBU KUFIKIRI JAMII ITAKUCHULIAJE?

    KWANGU MIMI WEWE UNATULETEA MAZUNGUMZO YA KIJIWENI YA KAMA PROF. HAPA HALAFU UTEGEMEE KUPATA UMAARUFU SAWA.

    NEXT TIME CHAGUA LUGHA MOJA KAMA KISWAHILI KIWE KISWAHILI NA SIYO KUTULETEA UBISHOO WA MIAKA YA 80 HAPA.

    MDAU BUCKINGHAMSHIRE, UNITED KINGDOM

    ReplyDelete
  49. Kweli inasikitisha kuona kwamba mpaka leo hii watu bado wana muonekano mfupi wa maisha na dunia kama huu. Tutajadiliana hapa mpaka kesho kutwa, ukweli ni kwamba kwa manufaa ya watanzania wote, ni lazima Tanzania iruhusu dual citizenship. Swali ni lini hili jambo litapitishwa, sio kama litapitishwa...the sooner the better.

    Wewe mdau ulitoa hii mada, upeo wako katika hili jambo ni mdogo sanaaaa, kuna wadau kadhaa hapo juu wamejaribu kukuelewesha, fuatilia walivyosema. Na mara nyingine tafakari na fikiria kwa makini kabla ya kutoa mada yenye vigezo vibovu kama hivyo ulivyovitoa.

    Watanzania mjue kwamba dual citizenship inakuja, mtake msitake, itakuja tuu.

    ReplyDelete
  50. Bwana mdogo umechemka na bora kama usingeweka picha yako. When I see your face and what you have written I capitalize the BOGUS and that's exactly you.

    ReplyDelete
  51. wadau kabla hamja comment on this issue , lazima muwe na upeo wa kutosha sana.
    Nimeona mada ya mdau inayozungumzia swala la kutuma hela TANZANIA hata hivyo upeo wake ukawa mdogo kuchangia benefit za kutuma hela, ati ni kwa ajili ya marafi, ndugu , familia , n.k,Kaka kutuma fedha nyumbani inabenefit zaidi nchi ndg, wewe una habari kuwa tunaisaidia serikali ya TANZANIA kwa kukwepa kuwapa wananchi BENEFITS such as job seeker allowance,or unemployed benefits,housing benefits ati sisi ni nchi maskini,shughuli zote hizo ni kuwa nchi iwe responsible kusaidia WANANCHI WAKE, no excuse,nchi za AFRICA ZINA UTAJIRI MKUBWA WA RESOURCES.TUKIJA KWENYE SWALA LA MULTI-CITIZEN, NCHI ITABEFIT NA WATANZANIA WALIOKO NJE KUINVEST TANZANIA,KWANI SASA HIVI TUMEBANWA,SISI TANZANIAN DOCTORS HAPA UK TUNATAMANI TUFUNGUE KITUO CHA AFYA (MOBILE CLINIC)NYUMBANI BUT THE SITUATION DOESNT ALLOW. PLEASE MAKE CONSIDERATION.

    ReplyDelete
  52. YAANI HAWA WATU, MASHAKA AKIWEKA KITU LAZIMA MTU AJIBU, NA WAKIJIBU, INAKUWA NOGNWA, NAPENDA SANA GLOBU YA MICHUZI. JAMAA KAPONDWA ILE NI MBAYA, USHAKUWA MAARUFU KWA PUMBA, YAANI HATA MADEMU ULIOKUWA UKIWAFUKUZIA WASHAJUA KWAMBA KICHWANI HAZIMO YAANI WEWE SIYO MJANJA. BWANA HIZI ANGA WAACHIE WATAALAMU WAKINA MASHAKA AISEE, HAPA UMECHEMSHA KWELI KWELI, NA HII NDO DAWA YAKE NEXT TAIMU FANYA UTAFITI SIYO KUKURUPUKA NA IDEAS ZAKO ZA KUBEBA BOXI ZILIZOKATIZWA. NAIPENDA KWELI GLOBU YA MICHUZI, INATOA STRESS KWELI, SASA KIBAYA ZAIDI JAMAA KAWEKA PICHA NA TABASAMU UTADANIA ANASUBIRIA TUZO LA BONGO FLEVA STAR WA 2010

    ReplyDelete
  53. Nchi zilizo kwenye hali mbaya kama bongo ni nyiiiiingi mno, na baadhi actually nyingi zina wasomi xxxx kuzidi wabongo. Bado hizo nchi hazina dual citizenship.

    Its ignorant to think yule anayepinga hili swala ni ingorant hana wepevu. Ana sababu zake kama wale wa nchi nyingineo wanasababu zao.

    Weka heshima mbele na usijione unajua kuliko mwenzako. Kuna strong supporting arguments for/against this.

    Huu mjadala hapa umeshakosa opportunity nzuri kwa kuwa wajuaji wameshaukimbilia. Very sad.

    ReplyDelete
  54. Jamaa huyu kweli ana akili kweli? amewahi hata kufika nje? kaona wapi kuwa mtu kupata kazi nje ya nchi ni lazima uwe raia wa nchi?

    ReplyDelete
  55. Leopold Senghor of Senegal was correct when he said: “To build a nation, to create a new civilization which can lay claim to existence because it is humane, we shall try to employ not only enlightened reason but also dynamic imagination.”

    ReplyDelete
  56. Katika hotuba yake JK alipokutana na watanzania DC alisema kwa wale walioko nyumbani wana wivu
    Na ndio matatizo ya wivu wa kitanzania sio wa kutakia maendeleo mwenzako akijaribu kuneda mbele wewe utajaribu kuvuta au hata kumloga ili nayeye akose.
    Mfano mdogo tu ni mtu kama Obama mliyemshangilia watu tulikuwa tunajiuliza kulikoni.
    Wataalamu kibao wako nje saa nyingine wanalazimika kuchukua uraia wa nchi nyingine ili kuweza kujisaidia na maisha yao na nduzu zao. Watoto wanaozaliwa kwa watanzania waliopo nje pia bado ni hazina ya Taifa kama ni kwenye utaalamu, michezo nk. Mnataka foreign investors kama hatuwezi ku-invest kwenye damu yetu wenyewe kuna tatizo.
    taifa kubwa kama la Marekani linakubali dual citizenship na watapigania watu wao hata kama wapo wapi. Mtanzania anakufa India kinyama hakuna hata anayejali.
    Kesi ya mwisho ilikuwa ni Mama wa Brazil, baba mmarekani mechi ilichezwa mpaka mtoto akarudishwa. Nikirudia maneno ya Rais wetu Tuacheni wivu usiokuwa na manufaa wa kuvutana mashati

    ReplyDelete
  57. Mshikaji nafiri hujaelewa point nzima ya uraia wa nchi mbili. Watu wanachotoka sio kutuma pesa, hilo si tatizo. Watu wanataka wa-invest kama WANTANZANIA NA SIO KAMA WAGENI kutokana na utaratibu wa sasa, au hata kama una utaalamu adimu pindi ikiwapata uraia wa nchi ya pili Tanzania unakuwa mgeni kwa hiyo inakuwa vigumu kusaidia au kupewa uongozi katika hiyo nyanja.

    Mshikaji usiwe na roho ya korosho kama JK alivyotueleza kuwa mnapinga tu kwa sababu ya wivu (JK na watanzani Los Angelos -USA}.

    ReplyDelete
  58. Kijana, umefanya kazi nchi za nje mwaka mmoja na unaleta hoja nzito kama hii. Kwa nini usiwasiliane na watu kama sisi tuliofanya kazi nchi mbali mbali dunia nzima tukuambie jinsi hali ilivyo kabla ya kuropoka. Nakupa data mbili tu kwa leo, mimi ni Mtanzania mwenye kuipenda nchi yake lakini nimechoka kufadhaishwa na kunyanyaswa katika airport zote nilizokwenda dunia nzima.Wanaiangalia passport yangu kama taka taka. Pili, mimi ni Engineer mwenye uzoefu wa miaka kadhaa sio Tanzania tu bali nchi nyingi, lakini nikiomba kazi nchi yeyote nyingine wananipa offer yenye mshahara ambao haulingani na uzoefu na elimu yangu kwa ajili eti mi ni Mtanzania. Wenzangu ambao wana uraia wa kimarekani au uingereza wanapigwa ofa za nguvu. Sasa wewe unakuja hapa na unatuambia huu uraia wa nchi mbili haufai...wewe ni nani? na una ajenda gani? kama umeridhika basi tuachie vijana tuendelee kuchakarika...
    Asante na endelea kufanya shughuli nyingine tafadhali sana. Ankal naoma mwekee hii huyu kijana aelimike! Asante!

    ReplyDelete
  59. wanaotukana na kubeza wenzao humu katika kutoa hoja wengi ni waishio kinyemela nchi za nje au wanandugu aishie si kiuhalali nchi za nje sasa wanataka kutumia dual citizenship kupata uhalali wa kuishi nje ya nchi na TZ, kisingizio eti wanataka kuinvesti,kama mtu una mahela unakataliwa kuinvesti TZ taabu ya nini kainvesti Kenya watu wakuonee wivu kma utakuwepo

    ReplyDelete
  60. Inadhihirisha tu kuwa upeo wako wa kufikiri ni mdogo. Na hiyo nchi uliyokwenda kuishi mwaka mmoja ni Burundi au Rwanda?

    ReplyDelete
  61. WAOPINGA URAI WA INCHI MBILI NI WAJOMBA(hawaendi na wakati) NA HAWAJIAMINI.

    ReplyDelete
  62. linaloonekana hapa;
    1.Kuna watu wengi wametoka hapa wameeda nje wakakurupukia uraia wa nchi hizo wakidhani ni pazuri, wameona sasa sio dili tena kwa maisha hayo, sasa watamani kurudi nyumbani, mnajuta mmekosea. mlikuwa watoto sasa mmekua (kweli titi la mama ni tamu hata likiwa la mbwa).

    2. Pia utaona kundi linalolumba ni la aina gani, maana hoja zao ni jaziba na pengine matusi kama (pumbavu, huna akili n.k) hawa ndio wanaotaka urahia wa nchi nyingi???

    3. Kiwekeza hakuhitaji uraia wapo watu wengi tu wamewekeza bila kuchukua uraia tunawaona. Kama peesa zenu hazijatosha endeleeni kutafuta tu.

    4. Kuna kundi lina msukumo huko hasa wengi wakiwa wahindi wanataka kuja kufusadi tu. Nyie hamjui hayo.

    hoja ya uraia wa nchi nyingi si wa kikawaida tu kama mnavyofikiri eti kurudi nyumba kuwekeza, mie naona hakuna mwekezaji katika nyie.

    5. Sasa nyie mlioko nje mmesoma lakini mnabeba mabox mkija nmataka senior positions kwa uzoefu gani "wa kuweka samaki kwenye barafu.

    Tunayo mengi ya kuwafundisha msiyoyajua. Hoja ya dunia kama kijiji haiji kwasababu mpo ulaya. Exploition ya hiyo hamuijui kikweli maana.
    naomba muudhurie madarasa zaidi

    ReplyDelete
  63. Kwani nchi nyingine ikiamua kuruhusu dual citizenship ndio na sisi kurup tufuate mkombo? Je mnajua sababu zao? Watu wengine mnachekesha kweli.

    Uraia wa Tanzania ni wa thamani, msiuchezee.

    ReplyDelete
  64. TOENI HOJA ZA NGUVU sio mnamnyooshea midole yenu mtoa mada

    ivi hamuelewi?toeni hoja ya msingi kwanini uraia wa nchi 2,andika hapa point zako alaaaaaa

    ReplyDelete
  65. Kwa faida ya wasomaji. Mtoto aliyezaliwa nje ya ya Tanzania na wazazi Watanzania ni Mtanzania na raia wa nchi aliyozaliwa na ana haki zote za Mtanzania. Kwa maneno mengine mtoto huyo anakuwa na uraia wa nchi mbili, ila kwa sheria ya Tanzania atakapofikisha umri wa miaka kumi na nane anatakiwa kukana uraia mmoja na kubaki na mmoja wa chaguo lake.

    ReplyDelete
  66. DAH INASIKITISHA SANA KUONA WATU KAMA HAWA WENYE MAWAZO FINYU WANAPEWA UMKUMBI MKUBWA WAKUANDIKA MAPUPU. HUYO JAMAA SIONI CHA MAANA ALICHOANDIKA HAPO JUU. NA HII NIKUWA WANASHINDWA KUENDA KUFUANYA RESEARCH YA CHINI SANA ILI WAFAHAMU NINI KWANINI WATU WANAPENDELEA DUAL CITIZENSHIP.KWNYE NCHI AMBAYO RUSHWA NI NGUZO YA MAISHA NI VIGUMU KWA INVESTORS KUTIA MIKONO YA KIZANI. NA SIO SABABU MOJA TU KUNA SABABU NYINGI NA NASHINDWA KWANINI WANASHINDWA KUZIONA..BWANA FRDRICK MBONA LABDA UKAFANYE RESEARCH KWANINI IMMAGRATIONS FROM ONE COUNTRY TO ANOTHER ILIKUWA KWA KASI MIAKA YA NYUMA HADI SASA.NINI CHANZO CHAKE..NAJUWA UTASEMA VITA...ANGALIA SABABU ZINGINE..KAMA NI MWANAFUNZI WA BIASHARA NA UCHUMI NAAMINI UTAPATA JIBU ZURI SANA..

    ReplyDelete
  67. Wadau Nielimisheni kidogo..
    1. Nini faida ya DUAL / MULTIPLE CITIZENSHIP.

    2. Kuna hasara gani za Dual / Multiple Citizenship.

    3. DUAL/Multiple Citizenship zinaathiri vipi kutuma hela nyumbani?

    Ni hayo tu wadau.. wengine mada imetupita kando kidogo.

    ReplyDelete
  68. A person who holds dual citizenship is considered to be a citizen in two countries. For example, a child may be born in one country to parents who hold citizenship in another. The place of birth can enable someone to hold citizenship automatically in the first country, and the parent's citizenship can also be passed along to the child. In other cases, a person may hold citizenship in one country and apply to become a naturalized citizen of another. In many cases, the second country will allow the first citizenship to be retained. As citizenship laws broaden and the world becomes more connected, holding dual citizenship is becoming more common and offers benefits to those who are able to take advantage of it Passport and Travel Citizens with dual citizenship may carry passports from both countries. Using the appropriate visa in each of the countries enables the holders to pass the border more easily, without the need for long-stay visas or customs complications. If one of the passports is from a country that belongs to the European Union, a passport for one effectively opens up travel and the potential to reside in any country throughout the EU without the need for visas or residency requirements.
    Career and Work
    Countries reserve jobs for their citizens and require special work visas for those who are visitors. At the very least, applying for a work visa without citizenship can be a problem, and success is not guaranteed. Dual citizenship doubles the opportunities to work legally in either country (or countries if the passport held is from an EU country) without the bureaucracy of long-term work visas.
    Safety
    In a post 9/11 age, some Americans who hold dual citizenship feel more secure when traveling. They can use whichever passport makes them less of a target. When dealing with local police of either country, they can claim citizenship.
    Connections to Native Land
    Some individuals choose to reside and be a naturalized citizen in one country. However, they may not want to totally resign their connections to the land of their birth and family. With dual citizenship, they can usually retain their rights in both countries to vote, own property and obtain government health care if applicable.
    Property Ownership
    Some countries restrict property ownership based on citizenship. For example, a country may regulate the ability of foreigners to own land near a border or coastline. In such countries, a person who plans to live there full or part time may find that being a naturalized citizen (even if they are also a citizen of another country) enables them to own property, and travel back and forth more easily.
    Improved Acceptance
    In the past, laws in some countries forbade a naturalized citizen from retaining the original citizenship of his native land. Now, dual citizenship is increasingly allowed. Several countries have adapted their laws to encourage citizenship by offering it to former citizens, their children, and even grandchildren and great-grandchildren who wish to carry more than one passport.
    Access to Retirement Programs
    Several countries are making it possible for people to gain citizenship more easily for retirement in other countries that may be more affordable, such as in Latin America. Countries such as Panama, Belize and Mexico want to encourage people to settle there. In other cases, people with a parent, grandparent or great-grandparent in a country such as Italy or Ireland may be eligible to apply for citizenship there. As mentioned above, this opens up the entire European Union for residence and work.
    ABOVE IS ADVANTAGES OF DUAL CITIZENSHIP.

    THERE IS MORE THAN THAT AND IF YOU THINK THOSE COUNTRIES WHO CHOOSE TO DO SO ARE STUPID THEN YOUR IDIOT.

    MJUSI

    ReplyDelete
  69. Humu ndani ukisoma maoni ya watu ndio utajua ni jinsi gani watu wengi wanabidi kuelimishwa wanapochangia maoni.Hili swala ni la kitaifa na sio la mtu mmoja au watu ambao wapo nje.

    Swala la uraia wa nchi mbili halina sababu yoyote ya watu kurushiana matusi,malumbano au kuleta chuki ni swala kujua ni nini fida yake na nini hasara zake.

    Kama faida ni nyingi kuliko hasara basi serikali iangalia pale ambapo kuna mapungufu irekebishe na kama ni hatari kwa nchi basi Serikali isiruhusu mpaka itakapokuwa na uhakika.

    Kinachonishangaza zaidi ni kwa Watanzania wengine kuwakana wenzao wa nje wakati Muungano wa Afrika mashariki unampa haki mkenye na Muganda kuliko Mtanzania ambaye amechukua uraia wa nje na watanzania wakiwemo wanasiasa na wasomi wanashindwa kuliona hilo.

    Hapa ndipo pananipa wasiwasi mimi, kama kuna watanzania ambao ni raia wa Nchi nyingine na wanaweza kuziba mapengo ya kazi za kitaaluma Tanzania.
    je ni lipi bora watanzania wenye uraia wa nchi nyingine kuziba mapengo yale au wenzetu wa jirani (Kenya au Uganda)?

    Je nilipi bora raia wa nchi nyingine ambao hawana uhusiano na nchi yetu kufanya kazi za kitaaluma na kulipwa mapesa kibao au watanzania ambao ni wazawa ila wanauraia wa nchi nyingine kufanya kazi hizo? Kumbukeni tuna "attract capital Flight" na kama kazi hizo wangepewa watanzania wenye utaalamu ambao zambi zao ni kuwa na uraia wa nchi nyingine tu basi hizo hela (Capital) zingebakia nchini na uchumi wetu kuendelea zaidi.

    Tunakasumba ya kuamini kwamba mambo yote wanayofanya wataalamu wa kigeni(hasa Wazungu), watanzania hatuwezi.

    Tunakasumba ya kukomoana na kufikiri wale wote ambao wamekimbia tanzania ni watu wabaya.Kama tutaacha kasumba hizo hili swala hili linaweza kujadiliwa kutumia common sense zaidi kuliko jazba au chuki.


    Mungu wabariki watanzania wote wawe na busara wanapoamua mambo muhimu ya nchi.

    Inshallah

    (Hamoud alias JAX)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...