Baadhi ya wanafunzi wa Tanzania walio masomoni Misri
Leo Ni Mwezi 12 Rabi Al-awwal(Mfungo sita)1431Hijria sawa na Tarehe 26-2-2010 Ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad(S.A.W)
Kwa niaba ya wadau wa Globu hii ya jamii waliopo Misri na mikoa yake yote wakiongozwa na Al-akhiy Ghalib N Monero Tunawatakia kila la kheri katika kukumbuka uzawa wake Bwana Mtume Muhammad(S.A.W) na kupitia siku hii na siku zote kwa ujumla tukumbushane mema na na tukatazane mabaya ili tupate radhi zake M/Mungu.
Illahi tupe mahaba ya kumpenda Nabia
Thuma na Aqarabah na Swahaba wote pia.
Tufungulie ya ijaba ya Akhera na Dunia
Uturuzuku Jalia mahaba ya Mtume wetu.
Fungamano la moyoni mola wetu ya Wadudu.
Mwengine hatumuoni ila wewe ya wahidu.
Tumiminie Nyoyoni mahaba ya kukuabudu.
Mola wetu ya Wahidu tunusuru ya Allahu.
Yaaillah Dua zetu kwako hazitunufaishi.
Wala kukuasi kwetu kabisa hakukudhulishi.
Tufutie dhambi zetu rehema zako hazishi.
katika mema tuishi tusamehe mola wetu.
Linukishe vyema Yaa illah Mola Raufu.
Kaburi la Bwana lizidishie harufu.
Kila kinukasho uzuri na utukufu .
hizo ni rehema na Salamu na Amani Kwa Tumwa karima.
Na Ghalib Nassor Cairo.
Thuma na Aqarabah na Swahaba wote pia.
Tufungulie ya ijaba ya Akhera na Dunia
Uturuzuku Jalia mahaba ya Mtume wetu.
Fungamano la moyoni mola wetu ya Wadudu.
Mwengine hatumuoni ila wewe ya wahidu.
Tumiminie Nyoyoni mahaba ya kukuabudu.
Mola wetu ya Wahidu tunusuru ya Allahu.
Yaaillah Dua zetu kwako hazitunufaishi.
Wala kukuasi kwetu kabisa hakukudhulishi.
Tufutie dhambi zetu rehema zako hazishi.
katika mema tuishi tusamehe mola wetu.
Linukishe vyema Yaa illah Mola Raufu.
Kaburi la Bwana lizidishie harufu.
Kila kinukasho uzuri na utukufu .
hizo ni rehema na Salamu na Amani Kwa Tumwa karima.
Na Ghalib Nassor Cairo.
Sadakta maneno murua kabisa. Twawatakieni heri na fanaka waislamu wote duniani katika sikukuu ya Meilaad tunapomkumbuka kipenzi cha Mwenyezi Mungu. SAW. Aslaam alei kum Warahmatullahi.
ReplyDeletemashallah,mwenyezi mungu awazidishie,na mkimaliza chuo mrudi nyumbani mkazishike idara za kiislam,maana bila wasomi waislam tutazidi kuwa nyuma,mkawaondowe watu wanaogombania misikiti na kuuza viwanja vya bakwata.bakwata inatakiwa iongozwe na wasomi sasa.si mnaona uganda waislam walivyo delep kwenye big project,ni kipindi na sisi kuanza kujenga vyou vya kisasa,mahospitali na viwanda.tusiishie kujenga shule zinazotoa division 4 na zero.
ReplyDeleteNawatakiwa waislamu wote popote pale walipo duniani Maulid njema, tufuate mafundisho tulofundishwa na Mtume wetu Muhammad (SAW). Vile vile nawatakiwa Aljumaa Karim.
ReplyDeleteamina rabbi amina.
ReplyDeleteAsanteni kwa salam za Maulid.Ila wazee nimepitia ubeti wote wa salam ya maulidi sijaona hata sentence mlioteleza "mkasema mpunga utakuwepo kwa mmoja wenu tuje".Samala tupu hazitoshi.
ReplyDeleteasanteni kwa dua zenu
ReplyDeleteJazakalaah Khairun.
(US Blogger)
jamani mbona mimi naona hapo ni uk na sio misri? kwani kunasura mbili hapo nazijuwa zipohapa uk,nahizo nyumba nyuma looks like milton keynes
ReplyDelete