CHAMA CHA MAPINDUZI

TAWI LA UINGEREZA SHEREHE YA KUZALIWA KWA
Chama Cha Mapinduzi (CCM)
MIAKA 33 YA CCM
Wanachama Wote - C C M
Wakereketwa Wote - C C M
Wapenzi Na Wana-Mapinduzi Wote
Tarehe: 06/03/2010

saa: 10 jioni Hadi Saa 5 usiku

WAPI:
UKUMBI WA: THE WAREHOUSE
1 CUMBERLAND ROAD
READING
RG1 3LB

Mgeni Rasmi
Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania Bara:

Mhe Pius Msekwa

Watanzania ambao wangependa kujiandikisha, mnaombwa kuleta picha zenu za passport size mbili na paundi kumi na tano (paundi tatu kwa kadi, halafu paundi kumi na mbili kwa ada ya uanachama ya mwaka mzima).

Kwa ufafanuzi zaidi, tafadhali wasiliana na:
Moses Katega - 07727475313
Victor Mgoya – 07501083328
Maira Migire – 07799212095
Wote Mnakaribishwa – Kutakuwa na Vinywaji, Vitafunio, na Muziki Baada ya Shughuli Zote.

Kiingilio – BURE!!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Sasa wapinzani nao wakianza matawi yao huku ulaya na usa. Sijui mtatutumia FFU huku huku? ama ndiyo uninja wa usalama utahamia huku?

    ReplyDelete
  2. Nashangaaa viongozi wa CCM kila siku wao ni LONDON tu, matawi ya CCM Russia na msumbiji mbona hawaendi?
    nakumbuka Uganda nako kuna TAWI la wana ccm lakini safari ni Uingereza tu,

    nadhani tawi la UK ni cover ya watu kula pesa za CCM TU.by the way hao viongozi wa ccm UK ni waganga njaa wanatafuta njia ya kurudia Tz tu.

    ReplyDelete
  3. Du!!!CCM UK mmeshaanza tena, hamchoki tu!!

    ReplyDelete
  4. kusema kweli hiyo alama ya nyundo na jembe inanitia kichefuchefu sana yani kila nikiangalia najiskia uvivu kurudi huko nyumbani.

    ReplyDelete
  5. CCM inabidi kuikubali tu, wakati wapinzani hawajamaliza hata Tanzania. CCM wako mpaka Ulaya.

    Tutakuja kula na kunywa bure.

    Idumu CCM.

    ReplyDelete
  6. sasa wa-tz wa nje wanasema eti wala vumbi ccm ni ya nini wakati huohuo wanafungua branch Uk,NL Na Pengine sasa tuwaeleweje nyie wabeba boksi mbona vigegeu

    ReplyDelete
  7. Mdau umesahau kuwakaribisha wafuatao:
    Wafurukutwa wote,
    Wakerwa wote wa chama.

    Mwisho ni ushauri; Huwa vinaitwa vitafunwa na sio vitafunio. Vitafunio ni meno.

    Mdau Waluwalu

    ReplyDelete
  8. I have come to the conclusion that politics are too serious a matter to be left to the politicians.

    Charles De Gaulle
    French general & politician (1890 - 1970)

    I will be there...

    Kidumu Chama Cha Mapinduzi.

    Mkereketwa,
    Milton Keynes.

    ReplyDelete
  9. Wakati sasa umefika CCM Uingereza ifanye sherehe za kusherehereka miaka yake ya kuzaliwa.

    ReplyDelete
  10. Kidumu Chama Cha Mapinduzi

    Ni raha ilioje kuona Chama Kiongozi Tanzania kikifikia Watanzania mpaka Uingereza.

    Endelezeni Uzalendo huo huo.

    ReplyDelete
  11. Aisee Babangu...hawa CCM wamejenga Barabara ya Lami kwenda Tarakea kwa Mzee wangu Shirima, mwaka huu lazima nije kula na kunywa nao kwa furaha. Mimi na Mdogo wangu Isdori sasa tunaenda Tarakea na Corolla.

    Kutakuwa na Mbege jamani?

    ReplyDelete
  12. anonymous wa 9:43 pm
    nakushukuru sana kwa kutusahishisha kuhusu neno hil ya "vitafunio-to vitafunwa" kwa kweli wengi wetu tulishazoea sana kutumia neno hili bila kufikiria kama ulivyofikiria outside the box.
    shukran sana na ubarikiwe daima.
    i like such people like you wenye kuwaelimisha wenzao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...