Familia ya Mzee na Mama Elton Lusingu wa mjini Arusha Tanzania, wanapenda kutoa shukrani zao za dhati kwa wale wote walioshirikiana na familia wakati wote wa kuuguza na wa msiba wa mke wa kijana wao Marehemu Sophia H. Gerald Lusingu.

Tungependa kutoa shukrani zetu za pekee kwa Ndugu, jamaa na marafiki hasa Watanzania wote nchini Uingereza ambao kwa kushirikiana na kamati iliosimamia shughuli zote za msiba walihakikisha kwamba wametoa msaada wowote uliohitajika, ikiwa ni pamoja na kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Tanzania! Kwa heshima hio hio tungependa pia kuwashukuru viongozi wa taasisi mbalimbali za kidini, serikali na binafsi kwa ushirikiano wao katika kipindi chote hicho.

Mwisho tunawashukuru wote waliotukumbuka katika sala na maombi, tunaamini kwamba mafanikio ya mambo yote yalitokana na maombi na sala zenu. Tunawaombeeni baraka na mafanikio katika shughuli zenu zote.

"BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA"

ASANTENI SANA,
Familia ya Lusingu
Arusha Tanzania na Reading (UK)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. laiza yussufuFebruary 08, 2010

    Shikamoo mzee lusingu. poleni sana wew pamoja na familia yako kwa kuondokewa na mkwe wenu. hakika kwa MOLA ndio marejeo yetu sote.Mungu awape moyo wa subira

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...