Mkuu wa Mkoa wa Mara Enos Mfuru, akipokea sehemu ya msaada wa madawati kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano benki ya NMB Shy-Rose Bhanji, ikiwa ni msaada wa benki ya NMB, kwa ajili ya kusaidia baadhi ya shule za msingi mkoani Mara, kufuatia tatizo kubwa la madawati kwa shule za Msingi Mkoani humo. Katikati ni Meneja wa NMB tawi la Musoma Joseph Mwagilo. Msaada huo ulikabidhiwa mjini Musoma.
Mkuu wa Mkoa wa Mara akimshukuru Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano NMB kwa niaba ya Uongozi wa NMB kwa msaada wa madawati

Maafisa wa NMB wakiwa wameketi na Mkuu wa Mkoa wa Mara (katikati) katika moja ya madawati katika hafla ya makabidhiano.
Mkuu wa Mkoa wa Mara akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano NMB Shy-Rose Bhanji, Meneja wa NMB tawi la Musoma Joseph Mwagilo na Meya wa Manispaa ya Musoma Mjini katika hafla ya makabidhiano mjini Musoma, Mkoani Mara.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. HII NI BENKI YA KWELI, LAZIMA TUKUBALI WADAU

    ReplyDelete
  2. Benki ya inakuwa ya ukweli kwa kutoa huduma bora na nafuu kwa wateja wake. Na kamwe sio kujihusisha na huduma za jamii ambazo zilitakiwa kufanya na serikali.

    ReplyDelete
  3. mimi ni mkazi wa hapa msoma nimefarijika sana kuona benki ya nmb imetupa msaada wa madawati kwa shule zetu za msingi na kikubwa zaidi benki hii imefanya jambo jema sana kukabidhi madawati na si fedha taslim. naendelea kusisitiza muenderee kutoa misaada ya kutokana na maombi na si fedha taslim. asanteni sana nmb kwa kutujari

    ReplyDelete
  4. nmb safi sana mnajitahidi kwa kusaidia maeneo mbalimbali, faida mnapata lakini tunaona japo asilimia flani inarudi kwa jamii...inapendeza

    ReplyDelete
  5. jitihada mnazofanya nmb ni kubwa na zinaonekana- endelezeni libeneke la misaada kwa jamii

    ReplyDelete
  6. safiiiiiiiii

    ReplyDelete
  7. Sumuni unatuswasha. Mimi pia niko hapa hapa "msoma" hatuonani...

    ReplyDelete
  8. Jamani kifua nimependa

    ReplyDelete
  9. For a better view ulitakiwa uwepo Mwanza maeneo ya Miti Mirefu in the eighties and ninties...

    ReplyDelete
  10. mnastahili hongera sana nmb kwa misaada kwa jamii kiukweli mnajitahidi sana, kila kona mpo!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...