Hayati Sharoffa Abdarahmani Abdallah

Familia ya Maj. General Muhiddin Kimario ya Moshi Mjini, inapenda kutoa shukrani za dhati katika wakati mgumu kwenye maisha yetu baada ya kifo cha mama yetu mpendwa “ Shariffa Abdarahmani Abdallah” kilichotokea Hospital ya Muhimbili Dar es Salaam tarehe 21 Januari 2010 na Kuzikwa Moshi Mjini tarehe 22 Januari 2010.

Shukrani za pekee ziwaendee dr. kisanga pamoja na madaktari na wauguzi waliotupokea siku ya jumapili tarehe 17 jan 2010 kwa juhudi zao za kujaribu kuokoa maisha ya marehemu… Lakini alilolipanga Mungu hakuna wa kulipangua.
Kwa kuwa sio rahisi kutaja mmoja mmoja tungependa shukrani zetu za dhati ziwaendee majirani wa marehemu wa Ilala Flats na Kinondoni, Wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania na Unit Trust of Tanzania (UTT), Ndugu, Jamaa, na Marafiki wa Dar es salaam, Moshi, Mombasa, Dodoma, Tanga, Arusha, Atlanta na North Carolina kwa kushiriki na kutufariji kwa njia moja ama nyingine. Ahsanteni sana

Familia inapenda kuwajulisha kuwa tarehe 26 Februari 2010, Moshi Mjini, Swahili Street baada ya salat ya Ijumaa kutakuwa na kisomo cha kumuombea marehemu.

“Wote Mnakaribishwa”
"INNA LILLAHI WAINA ILLAIHI RAJIUUN"

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Michuzi
    Mpe pole sana Maj. Generali Muhidini Kimario huko Moshi.Napenda kuwapa mkono wote na kumuombea marehemu.Sitakuwepo kwenye kisomo cha Swahili Street, ila namuomba wajulishe jamaa kuwa huu ni msiba wetu sote
    Ibrahim

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wafiwa.

    Mungu ailaze roho ya marehemu peponi Ameen!

    ReplyDelete
  3. Poleni wafiwa, yote ni mapenzi ya Mungu...

    ReplyDelete
  4. POLE RAHMA, SHAMIM, NA RUKIA NA WAFIWA WOTE

    ReplyDelete
  5. Inna LiLLAh wa INNA Ilaihi Raajiuu'n , huyu mama Kimario niliHiji nae in 2004. YAani imenigusa sana alikuwa mcheshi sana huyu mama na alipenda sana kunitania wakati tupo HAjj pamoja, Mola amswameh dhambi zake, amng'rishie KAburi lake kwa Nuru ya Quraan na amuweke mahali pema peponi Amin Amin Thumma AMin... Dah!!!

    ReplyDelete
  6. pole sana da fatuma kimario, kazi yake mwenyezi mungu haina makosa.

    hellen

    ReplyDelete
  7. Fatuma poleni sana ndio kazi ya mungu na wote tu wasafiri. Nitajitahidi kufika kwenye kisomo inshallah ili niweze kuwapa pole inshallah.

    WENU MKUFUNZI

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...