Ankal,
mimi ni mdau nipo hapa New Mexico inchini Marekani. Sasa kama kawaida ya wabongo wengi tuliopo nje huwa tunafurahi sana tunapokuja nyumbani na kujikumbusha vitu ambavyo huwa tulikuwa tukivifanya zamani au tunaviendeleza hadi leo.
Swali langu ni hili, kwanini wanywaji hasa kinyaji cha bia wakipewa glassi ya kunywea bia lazima kwanza waisuuze na bia kidogo kabla ya kumimina bia yote kwenye glassi? Wadau naomba tusaidiane katika kujua sababu hasa ni nini ya kusuuza glassi kwa bia?
Mdau Lemmy.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Ni unakuwa unatambika kwa mizimu ya mababu zetu,,si unajua tangu enzi mababu walikuwa wakitambika kwa kumwaga pombe kwenye ardhi?So hiyo pombe yote inaenda kwa mizimu..Habari ndo hiyo

    ReplyDelete
  2. hii ni inatokana ya kua kwanza nikuondoa sabuni kama ilisahaulika wakati wa kuosha na pili kama hiyo glass ilitumika kunywea wisky na haikuoshwa vizuri. vyote nilivyo sema hapo juu huwa vinakata bia yaani ukimimina bia povu linaisha haraka na inakua kama ime flet wengine tuna ita kilemba na raha ya bia povu liwepo.
    Mdau
    Bongo forever.

    ReplyDelete
  3. Duuu wewe kweli Mtz.. Kwa matazamo wangu ni huruka tu hamna chochote kinachosababisha kufanya hivyo. Ila kutokana na mazoea hapo zamani gilasi zilikuwa huwezi kuzichemsha kwenye maji moto hivyo walikuwa wanaosha kwa bia kujiridhisha kuwa sasa hii safi kwa kunywea hiyo bia. lakini kwa sasa mimi sioni mantiki ya kufanya hivyo kwani gilasi zinachemshwa kwa maji moto wote wanaofanya hivyo ni sawa na wale wote wanoweka toothstick kinywani kwa muda mrefu... ni ulimbukeni tu...

    ReplyDelete
  4. Sababu kubwa ni kwamba wanywaji wengi wa bia wanadhani na kuamini kwamba uoshwaji wa glasi kwenye baa nyingi si wa kuaminika sana na kwamba kusuuza na bia na siku hizi kusugua/kufuta glasi na tissue paper ni njia itakayomhakikishia mnywaji usafi wa bia atakayoinywa...lakini ajabu ni kwamba mtu akiletewa soda , maji, pombe kali kama konyagi zoezi la usuuzaji huwa halifanyiki, hilo kwangu ni swali!!

    ReplyDelete
  5. ni kutoa mate ya mtu aliyetumia before. si mnajua wanwaji wa bia lazima warudishe na mate!

    ReplyDelete
  6. Naungana na mdau hapo juu.

    Tabia hii inatokana na ukweli kwamba baa nyingi za bongo hawahifadhi glasi zao vizuri. Mtumiaji anatumia bia kuondoa mavumbi na uchafu mwingine uliomo ndani ya glasi kabla ya kuanza kuitumia.

    ReplyDelete
  7. Ni kwa sababu baadhi ya Ma-bar maid wanatumia hizo glass kwa kuchambia wanapokwenda haja ndogo, HIVYO CHEMBE CHEMBE ZA MKOJO WA KIKE ukichanganyika na bia unalewa hata nusu glass na jamaa wanaweza kukudhuru wakati wowote.
    Ankal, wewe hayakuhusu, endelea kunywa juice na maji ya chupa kama ulivyozowea kuzugazuga.

    ReplyDelete
  8. Ni majigambo tu hakuna lolote, mi naishi hapa wash dc kwa muda mrefu sana....kama uchafu hata glass za hapa ni chafu tu.
    Sasa hivi kale ka club ka wakenya (safari) ambako wabongo tunapenda kwenda kamefungwa kwa sababu ya uchafu... panya, mende na kila aina ya uchafu ipo pale.
    Sasa mtu akienda bongo analeta nyodo nyingi ni ushenzi tu.

    BOX MTU.

    ReplyDelete
  9. Wewe mdau unaejiita lemmy inaonyesha siyo mnywaji wala nini ila ulimbukeni maana hueleweki unataka jibu gani hapo, nafikiri ulikua unataka watu wajue uko mexico. watu wa huko ni kama wabongo wanasuuza na bia kabla ya kunywa?

    ReplyDelete
  10. si unajua tena mambo ya sekyurite kila mbongo ni mwanajeshi sasa hapo huwa wanaondoa kitu chochote kama wametegeshewa cocaine na aina yoyote ya madawa ili kumlewesha then wamdhuru

    ReplyDelete
  11. Kuwa new Mexico kuna uhusiano gani na swali ulilouliza?

    ReplyDelete
  12. Jamani i must admit hyu mdau aliyeleta hii mada ni kiboko khaaa!!!

    nimeshindwa kujizuia nimecheka sana

    alafu huyu :Thu Feb 18, 09:46:00 AM
    ndo kaja kunimaliza kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa hiki kitu chaweza kuwa kweli yalahhhhhhhh

    villager

    ReplyDelete
  13. Ankali
    Mimi nina uzoefu wa kula bia kwa miaka 20 sasa. Najua hii tabia ni kutokana na uchafu wa glas ila siku hizi imekuwa kama fasheni. Ila Ankali mimi huwa nakata laga zangu hapo Mlimani City na sioni hii tabia ya kumwaga kapombe kama ipo sana. labda kwa sababu wao ni wasafi kidogo. Pia baa nyingine kama huko ufukweni hii tabia haitumiki.ila kama unakata pombe huko kigogo, sinza uswahili, kinondoni, migomigo lazima usafishe glass kwa bia kidogo...

    ReplyDelete
  14. Mdau wa kwanza amejibu.

    ReplyDelete
  15. Huwa nafanya hivyo pia kwa sababu siamini kuwazimeoshwa vizuri na pia angalia kwa makini gkass nyingi huwa zinakuwa na ramani ya maji yaliyo kauka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...