Na Mwandishi Maalum, New York
Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kushiriki operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa, licha ya kwamba operesheni hizo hivi sasa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Msisitizo huo umetolewa na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Augustine Mahiga wakati alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Kamati Maalumu inayohusika na Operesheni za Ulinzi wa Amani maarufu kama C-34

Mkutano wa Kamati hiyo unafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na wajumbe wake ni kutoka nchi wanachama wa UN wanaochangia operesheni za ulinzi kwa kutoa wanajeshi na polisi.

Balozi Mahiga amewaeleza wajumbe wa mkutano huo, kwamba Tanzania ambayo ni mgeni katika ushiriki wa operesheni hizo, kwa maana ya kuchangia wanajeshi na polisi, inajiunga katika jukumu hilo katika kipindi ambacho ulinzi wa amani hivi sasa unakabiliwa na changamoto nyingi na kubwa.

Kwa mfano anataja baadhi ya changamoto hizo, kuwa ni kubadilika kwa uasilia wa mwenenzo mzima wa vita kutoka ule wa mapigano kati ya taifa moja na jingine na kuwa vile vinavyopiganwa na makundi yanayohasimiana ndani ya nchi husika tena yakishindana kwa silaha nzito na kali.

“ Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa hivi sasa wanakabiliwa na changamoto tofauti kabisa na zilizo nje ya misingi na majukumu yanayojulikana na ambayo tayari yameainishwa katika mfumo mzima wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa” akasisitiza.

Na kuongeza .“ na sisi Tanzania tunaingia katika jukumu hili tukiwa ni wageni, bado tu wapya katika uchangiaji wa wanajeshi na polisi wetu na kwa kweli ushiriki wetu ni mdogo, kwa sasa tupo katika misheni tano tukiwa na idadi ndogo ya walinzi wa amani. Na tunaingia katika kipindi ambacho Umoja wa Mataifa na taasisi zake zimo katika majadiliano ya kina kuhusu changamoto na mwenendo mzima wa operesheni hizi za ulinzi wa Amani” anaeleza Mahiga

Akasema kuwa Tanzania iko tayari kukabiliana na changamoto hizo na kueleza kuwa ni hivi karibuni tu Tanzania imekamilisha zoezi la kupeleka kwa mara ya kwanza Bataliani yenye wanajeshi 875 katika misheni ya kulinda amani huko Darfur nchini Sudan chini ya mwamvuli wa jeshi la mseto la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (UNAMID).

Balozi Mahiga akatumia fursa hiyo kutoa shukrani za serikali ya Tanzania kwa Umoja wa Mataifa na wahisani wengine waliofanikisha maandalizi ya ushiriki wa Tanzania huko Darfur.

Kundi la mwisho la wanajeshi 600 wa TANZBATT-1 waliondoka nchini kati ya tarehe kumi na moja na kumi na tatu mwezi wa huu wa pili kwenda Darfur ambako wamejiunga na wenzao ma- injinia na maafisa 275 waliokuwa wametangulia kuaanda kambi ya kufikia wanajeshi hao

Pamoja na ushiriki wa Tanzania huko Darfur, Balozi Mahiga pia alibainisha kuwa Tanzania inaendelea na maandalizi ya kupelekea wanajeshi wake 200 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Misheni ya MONUC ambako watakwenda kutoka mafunzo kwa wanajeshi wa nchi hiyo.

Katika hatua nyingie, Tanzania imesisitiza umuhimu wa Umoja wa Mataifa wa kuendelea kuijengea uwezo Umoja wa Afrika, ili umoja huo uweze kujizatiti katika kuzuia machafuko, kuyatafutia ufumbuzi machafuko na ujenzi wa amani.

Akasema kuwa kwa ujumla umoja wa Afrika unaridhishwa na mwenendo wa ushirikiano uliopo kati yake ya Umoja wa Mataifa. Lakini anasema Tanzania inaamini kwamba kuna kila sababu ya kuongeza kasi ya ushirikiano huo, kwa kile alichosema ikiwa Afrika itawezeshwa kukabiliana na migogoro siyo tu itapunguza gharama za operesheni hizo. Lakini pia itapunguza urasimu na mlolongo mrefu wa maandalizi ya misheni za ulinzi. Na Mwandishi Maalum

New York-Tanzania imesisitiza kuwa itaendelea kushiriki operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa, licha ya kwamba operesheni hizo hivi sasa zinakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Msisitizo huo umetolewa na Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Augustine Mahiga wakati alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Kamati Maalumu inayohusika na Operesheni za Ulinzi wa Amani maarufu kama C-34

Mkutano wa Kamati hiyo unafanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na wajumbe wake ni kutoka nchi wanachama wa UN wanaochangia operesheni za ulinzi kwa kutoa wanajeshi na polisi.

Balozi Mahiga amewaeleza wajumbe wa mkutano huo, kwamba Tanzania ambayo ni mgeni katika ushiriki wa operesheni hizo, kwa maana ya kuchangia wanajeshi na polisi, inajiunga katika jukumu hilo katika kipindi ambacho ulinzi wa amani hivi sasa unakabiliwa na changamoto nyingi na kubwa.

Kwa mfano anataja baadhi ya changamoto hizo, kuwa ni kubadilika kwa uasilia wa mwenenzo mzima wa vita kutoka ule wa mapigano kati ya taifa moja na jingine na kuwa vile vinavyopiganwa na makundi yanayohasimiana ndani ya nchi husika tena yakishindana kwa silaha nzito na kali.

“ Walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa hivi sasa wanakabiliwa na changamoto tofauti kabisa na zilizo nje ya misingi na majukumu yanayojulikana na ambayo tayari yameainishwa katika mfumo mzima wa operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa” akasisitiza.

Na kuongeza .“ na sisi Tanzania tunaingia katika jukumu hili tukiwa ni wageni, bado tu wapya katika uchangiaji wa wanajeshi na polisi wetu na kwa kweli ushiriki wetu ni mdogo, kwa sasa tupo katika misheni tano tukiwa na idadi ndogo ya walinzi wa amani. Na tunaingia katika kipindi ambacho Umoja wa Mataifa na taasisi zake zimo katika majadiliano ya kina kuhusu changamoto na mwenendo mzima wa operesheni hizi za ulinzi wa Amani” anaeleza Mahiga

Akasema kuwa Tanzania iko tayari kukabiliana na changamoto hizo na kueleza kuwa ni hivi karibuni tu Tanzania imekamilisha zoezi la kupeleka kwa mara ya kwanza Bataliani yenye wanajeshi 875 katika misheni ya kulinda amani huko Darfur nchini Sudan chini ya mwamvuli wa jeshi la mseto la Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (UNAMID).

Balozi Mahiga akatumia fursa hiyo kutoa shukrani za serikali ya Tanzania kwa Umoja wa Mataifa na wahisani wengine waliofanikisha maandalizi ya ushiriki wa Tanzania huko Darfur.

Kundi la mwisho la wanajeshi 600 wa TANZBATT-1 waliondoka nchini kati ya tarehe kumi na moja na kumi na tatu mwezi wa huu wa pili kwenda Darfur ambako wamejiunga na wenzao ma- injinia na maafisa 275 waliokuwa wametangulia kuaanda kambi ya kufikia wanajeshi hao

Pamoja na ushiriki wa Tanzania huko Darfur, Balozi Mahiga pia alibainisha kuwa Tanzania inaendelea na maandalizi ya kupelekea wanajeshi wake 200 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Misheni ya MONUC ambako watakwenda kutoka mafunzo kwa wanajeshi wa nchi hiyo.

Katika hatua nyingie, Tanzania imesisitiza umuhimu wa Umoja wa Mataifa wa kuendelea kuijengea uwezo Umoja wa Afrika, ili umoja huo uweze kujizatiti katika kuzuia machafuko, kuyatafutia ufumbuzi machafuko na ujenzi wa amani.

Akasema kuwa kwa ujumla umoja wa Afrika unaridhishwa na mwenendo wa ushirikiano uliopo kati yake ya Umoja wa Mataifa. Lakini anasema Tanzania inaamini kwamba kuna kila sababu ya kuongeza kasi ya ushirikiano huo, kwa kile alichosema ikiwa Afrika itawezeshwa kukabiliana na migogoro siyo tu itapunguza gharama za operesheni hizo. Lakini pia itapunguza urasimu na mlolongo mrefu wa maandalizi ya misheni za ulinzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. OK SAWA,SASA NA MISHAHARA YAO WANALIPA NANI MAANA ULAYA WIKI 350 ILA DANGER ZONE NI 500 HADI 700 INATEGEMEA UJUZI JE NA HAO WATANZANIA WANALIPWA KULINGANA NA VIWANGO HIVYO AU HELA INAFIKIA SERIKALI KWANZA?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...