Timu ya SOKA ya Tanzania ya Mjini New Delhi, inatarajiwa kushiriki katika mashindano ya Balozi mbalimbali (INTER EMBASSIES COMPETITION), yatakayoanza IJUMAA hii tarehe 26 February 2010 katika viwanja vya JAYPEE INTIGRATED SPORTS COMPLEX,G-BLOCK, GREAT NOIDA,nchini INDIA.

Wakitoa wosia kabla ya mashindano hayo kwa wachezaji wa Timu hiyo, kwenye ofisi za ubalozi zilizopo CHANAKYAPURI Mjini New Delhi, Afisa Ubalozi anayeshughulikia masuala ya wanafunzi Bw AMON MWAMUNENGE na Meneja wa Timu na Mwambata wa Jeshi Kanali Nassor wamewataka wachezaji hao kuwa na moyo wa kujituma sambamba na kuitangaza Tanzania katika utamaduni wake wa kuwa na Nidhamu, upendo na uungwana uwanjani.

Timu hiyo ya Tanzania Itafungua Dimba kwa kukutana na Timu ya AUSTRIA, mchezo utakaochezwa saa Mbili Usiku, siku hiyo ya Ijumaa. Huku Jumamosi itaingia uwanjani tena kucheza na Timu ya UNICEF,mchezo utakochezwa saa kumi na Mbili Jioni, na Jumapili itakwaana na Timu ya RUSSIA katika mchezo utakaoanza saa TISA JIONI.

Timu ya Tanzania ni miongoni mwa Timu KUMI NA SITA zinashiriki mashindano hayo zilizogawanywa katika makundi MANNE ,Tanzania ikiwemo katika kundi A sambamba na AUSTRIA, RUSSIA na UNICEF, Timu nyingine ni NETHERLANDS, AFRIKA KUSINI,ISRAEL,BANGLADESH,MALAYSIA,BELGIUM,BOTSWANA,CHINA,CHILE na wenyeji INDIA.

Kwa wanajumuia ya watanzania waliopo New Delhi, wote mnakaribishwa kuishangilia Timu hiyo.MUNGU ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

By.Jennifer Sumi.
Mwenyekiti - TASA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. FURSA HII ITUMIKE KUJITANGAZA KWENYE MCHEZO WA KRIKETI MCHEZO WENYE MASHABIKI WENGI INDIA.

    ReplyDelete
  2. HONGERA KWA TAARIFA NZURI NAPENDA KUJUA HUYU JENIFER SUMI NI YULE WA CHANEL TEN AU? NIMEKUMISS DADA

    ReplyDelete
  3. Jamani SOKA india!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. Tunawaomba mtembee kwa Ma groups
    RIP IMRAN

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...