Mtuhumiwa wa utapeli, Ashrafu Kingu,(kati) akiwa amedhibitiwa na askari kanzu wa uwanja wa ndege. Kulia nyuma ni Bi. Hilda aliyetaka kulizwa madawa feki wanayotumia watuhumiwa kulaghai watu



Walinzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam, kwa kushirikiana na askari kanzu mnamo Februari 3, mwaka huu walifanikiwa kuzima jaribio la utapeli mkubwa wa mamilioni ya fedha uliokuwa ufanyike uwanjani hapo.

Katika sekeseke hilo, Polisi walifanikiwa kumnasa mtu mmoja aitwaye Ashrafu Kingu ambaye inadaiwa ni tapeli mzoefu kutoka katika genge moja lenye mtandao mkubwa wa shughuli hiyo uliosambaa nchini kote na hata nje ya nchi.

mpango huo kabambe ulikuwa wa kumtapeli mfanyakazi mmoja wa uwanja huo, Bi.Hilda Kusoka, kiasi cha zaidi ya Sh. Milioni 20 kwa kumpa dili la bidhaa feki ambazo walidai ni dawa za mazao zinazotolewa kinyume cha sheria kutoka katika kiwanda cha dawa cha Shellys Pharmaceuticals Ltd , kilichopo Mwenge jijini Dar. Gia yao ni kuwa madawa hayo ni dili huko Kigoma kwenye maghala ya chakula cha misaada ya FAO.

Kwa mujibu wa Bi.Hilda , alidai kuwa mpango mzima wa utapeli huo ulifanywa na kaka yake wa tumbo moja mkazi wa Masaki, jijini Dar es Salaam ambaye ni memba wa mtandao huo wa matapeli.


habari kamili
BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. HAYA NDIYO ANASEMA PROF MBELE HAPO CHINI.

    HUYU TAPELI NI MJINGA KWANI HUU UTAPELI WA DAWA WATU WENGI SANA WAMESHAUSIKIA HIVYO NI RAHISI TU KUKAMATWA.

    ReplyDelete
  2. DAH!!
    AFADHALI HAWA JAMAA WAMEKAMATWA, WALISHA MLIZA MY BEST FRIEND HIVI HIVI.

    ReplyDelete
  3. MTU KAMA BADO UNATEPELIWA KWA STAILI HII, BASI WEWE NI MPUUZI...NI NANI ASIYEJUA UTAPELI WA AINA HII???

    ReplyDelete
  4. Veri enterestingi ha owni braza, naye anahusika kweli kiboko!!

    ReplyDelete
  5. Kweli jamani hapa ni pagumu! Sasa kwa huyu jamaa wa kutapeli imeeleweka. Na itabidi ashughulikiwe. Sasa swali linakuja, huyu mama amefanya makusudi ili kumpata mdogo wake ambaye anijihusisha na huu utapeli au na yeye alitaka utajiri wa HARAKA? kama alitaka kumpata huyo tapeli ndugu yake basi HONGERA MAMA. Na kama ulitaka utajiri wa haraka basi naomba hiyo biashara uache KABISA, kwani tunarudi huko huko. Kwa nini hizo milion 10 usiziweke kwenye shughuli ya harali ili utakachopata ni harali yako na utalala siyo usingizi wa wasiwasi ukiofia labda kukamatwa!

    ReplyDelete
  6. huyo mfanyakazi wa uwanja wa ndege hizo milioni 20 kazitolea wapi nae kama sio kesi ya mwizi kumuibia mwizi mwenzie hii?

    ReplyDelete
  7. Mhh wabongo tunahela kweli kweli, yaani ana milioni 20? Ilikuwa bado kidogo tu (kiasi cha shilingi milioni 5) afikishe kiasi alichokitangaza Waziri mkuu kuwa anacho pale alipokuwa anataja mali zake.

    Bongo tambarare!

    ReplyDelete
  8. Anon wa 06.52 huu utapeli wa aina hii hapa sasa karibu kila mtu amesha ufahamu hivyo si lazima huyo dada awe alitaka kutoa hizo pesa. Huenda lengo ni kuwa kamatisha hao matapeli pamoja na huyo kaka yake.

    ReplyDelete
  9. yani kweli mtu unamtapeli dada yako mwenyewe!kweli pesa yawezafanya mtu afanye mambo ya ajabu.mh!!

    ReplyDelete
  10. Kaka Michuzi kwakweli naishukuru sana blog ya jamii maana kama sio hii basi jana nami ningelizwa na hawa Matapeli. Nilipigiwa simu jana asubuhi saa 2.30 nikiambiwa nimpigie simu Dr. Ashrafu na maelezo meengi ila kwakuwa niliishasoma tena habari hii ya utapeli wa aina hii hapa basi nikanusurika.Tafadhali usichoke kuwaelimisha watu.Hongera kaka kwa kazi yako nzuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...