Mheshmiwa,

Naomba kutoa maangalizo kadhaa juu ya mjadala wa diaspora unaoendelea…Kwanza naomba kutanguliza kero ambayo naipata kwa wachangiaji kuandika kidhungu..Ina maana ndo huo ‘Ăślowezi” ama kitu gani??
Binafsi nina mpango wa kwenda kusoma na pengine kuishi nje lakini katika vitu ambavyo sitakuja kutamani ni kuwa Raia wa nchi hiyo nitakayokwenda…Kama kuna faida ama hasara basi nitakuwa radhi kuishi nazo na kama yakinizidi basi nirudi kwetu.
Nitalipa gharama ya Utanzania wangu..Asikudanganye mtu maendeleo yetu yapo na yatatoka hapa nchini na si vinginevyo.Tunapoenda kusoma ama kuishi nje sioni chochote tunachoongeza zaidi ya kubeza hali ya nchi yetu ama kukosoa pasipo kushiriki kwenye kuleta hayo maendeleo.
Freud Principal of Pleasure inasema “Human feelings always want more of what’s easy and sweet”….kwamba ni kawaida ya binadamu kutamani na kutaka zaidi vile ambayo ni rahisi na vitamu..Leo hii tunangángánia suala hili la Uraia wa nchi zaidi ya moja kwa kuwa kuna nchi Fulani ambayo wazawa walijitoa na kujituma kuleta maendelo hatimaye leo tumepaona ni mahala bora pa kuishi hata kutamani kuwepo huko hali ya kuwa kwetu panaendelea kudorora.
Ni kweli “dual citizenship”ipo na pengine ina manufaa lakini lazma tuwe na uzalendo,uzalendo wetu utakuja kila wakati tunapopata ‘pinch’ ya kukosa vitu flani flani kwa kuwa sio Raia wa nchi ile na tutakumbuka kuwa kuna sehemu tunajaliwa na tunahitajika zaidi ya hapa….

Huenda kwa kuwa tunafanya kazi zisizolipa ndio maana tunadhani kwa ‘dual citizenship’itatutoa…laiti tungekuwa kina Drogba(kwa maana ya mshahara) wala hili suala lisingeibuka kwa kuwa ‘pride’ya Utanzania wangu ingekuwa juu….Kama Nyerere angechukua Dual citizenry nchi hii ingepata uhuru??si angelowea tu uingereza halafu basi..
Naamini tuna vipaji na tumejifunza mengi kwa kuishi ughaibuni na kama pametushinda basi ni wakati wa kurejea na kuleta mapinduzi ya kiuchumi kwa kuwa rasilimali zipo huku sio huko…Binadamu atakuwa kiumbe makini iwapo tu ana uwezo wa kutumia mazingira yake kujinufaisha..
Hizo nchi mnazong’áng’ania zimejengwa na watu wenye moyo na kamwe msidhani zimeshushwa toka mbinguni.Tuchukie utumwa kwa vitendo sio maneno kwa kujivunia hadhi yetu.

Najivunia Utanzania wangu niko radhi kupata dhiki Ughaibuni kwa kuwa Mtanzania na faraja nyumbani kwa kuwa Mtanzania halisi.

“You can’t eat your cake and still have it”

Elly(Mdau wa Mayfair)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. mdau ulichokiandika ni kweli tupu,nyumbani ni nyumbani tu mimi nipo huku ughaibuni mwaka wa nne huu sasa ingawa maisha yako level ila kuna freedom flani unaikosa kwa sababu upo kwa watu,hivi fikilia unaenda supermarkets wateja wote weupeee wewe peke yako ndio mweusi tiii watu wote wanakushangaa sasa hapo kuna raha gani ata kama una makaratasi?

    ReplyDelete
  2. Safi sana Elly. Ishu kubwa hapa ni uzalendo. Kama hauko tayari kuvaa jezi ya Tanzania exclusively wewe si Mzalendo.

    Umeona wapi mchezaji akavaa jezi ya Simba na jezi ya Yanga at the same time?

    Au kuwa na kadi ya CCm na kadi ya CUF at the same time? Lazima kila upande utakuona si mwenzao.

    ReplyDelete
  3. Mshkaji una utani kweli. Unadhani kwa nini maprofesa wanakimbilia ubunge? Prof Sarungi, Prof Kapuya, Prof Mwandosya nk. Hivyo hivyo walienda kusoma ughaibuni wakarudi nyumbani kuleta mapinduzi wakashangazwa ikabidi 'ushikwapo shikamana'. Wengine siasa hatuwezi ndio tumekimbilia ughaibuni.

    ReplyDelete
  4. JAMANI ULIANZA VIZUURI BAADAYE UKANIACHA SIJAELEWA BAADA YA WEWE KUNGIZIA VIPARAGRAFU VYENYE LUGHA YA KIGENI KAMA IFUATAVYO...

    Ni kweli “dual citizenship”ipo na pengine ina manufaa lakini lazma tuwe na uzalendo

    Nyerere angechukua Dual citizenry nchi hii ingepata uhuru??

    “You can’t eat your cake and still have it”


    NAOMBA TUTUMIE KISWAHIRI TUU ILI MUWEZE KINISHIRIKISHA NAMIMI MAMBO MNAYOZUNGUMZA, HUWEZI AMINI HAPA PIA NIMETOKA KAPA

    ReplyDelete
  5. Well i somehow agree with you, this is really good, finally we start critical thinking. This is very crucial for our nation.

    ReplyDelete
  6. Go get another break with your stupidity. Another type of prof Mbele, Fredrick and Mdau Uk alike.

    ReplyDelete
  7. rasilimali zipo huko ndizo hizo ambazo wanatoka huku,kuja huko kuchukukua 97% nakutuachia 3%na hatimaye tunaambiwa tulete madawati ya wanetu shule.

    ReplyDelete
  8. There you go again, kuongea kiinglishi na kiingereza na kiswahili na kidhungu HATUTAKI KABISA kwenye mada hii, ni KISWAHILI, but(lakini) I am saying this(ninasema hivi) "YOU CAN'T EAT YOUR CAKE AND STILL HAVE IT" I dont GET It?? can someone help me out on this..


    Ni vibaya kabisa kutumia kidhungu, but Freud Principal of Pleasure inasema “Human feelings always want more of what’s easy and sweet”….

    ReplyDelete
  9. Nimessoma only three lines then I thought...there you go...another Idiot....wala simalizii

    Toka nje ya nchi kwanza then you will understand or widen up your mind.

    Acha wasomi waongelee hili swala OK!
    Sijatoka nje ya TZ lakini naelewa fika what has been said.
    Wewe ulikua umezaliwa enzi za mwalimu? za kupanga foleni ya sukari na unga wa njano kwenye maduka ya ushirika au gari la NMC? unajua kwa nini watanzania hawakujua what was going on and why by then? Inasikitisha kuona watu kama wewe bado wanaexist hapa TZ.

    ReplyDelete
  10. Some pple know nothing over here. You cant say/comment while u're in Tz.. Go and live abroad then comment!!
    It depends on the situation, some people have to seek for citizenship due to several reasons. And its a matter of choice.
    Mdau, USA!!

    ReplyDelete
  11. Tutaitisha kura za maoni kuhusu hili jambo. Kama ilivyo kwa kura za uchaguzi mkuu, wale mlioko nje mtatakiwa kuja kupiga kura zenu TZ maana hakutakuwa na maboksi ya kura kwenye balozi zetu.
    Mlioukana uraia wa Tanzania ili kupata wa nchi nyingine hamtaruhusiwa kupiga kura kwa sababu si watanzania. Hii pia itawahusu wale waliojilipua - waliofulia passport zao.

    ReplyDelete
  12. Ahsante sana brother Elly kwa kutueleza ukweli. (1) Kwa hatua tuliyoko sasa hatuwezi kuugawa uaminifu wetu (no divided loyalty) (2) Tutazame upande wa pili wa sarafu. Wageni wanaotaka uraia wa TZ lazima waukane uraia wao wa awali. (3) Hizo nchi za nje tulikoishi zilijengwa na wenyewe (mara nyingine kwa utumwa na ukoloni) na sisi Watanzania lazima tuijenge nchi yetu. Ukiviona vyaelea vimeundwa!!!(4) Hao wote wanaolilia dual citizenship wanautaka kwa maslahi yao binafsi; wasijitie eti wanautaka ili waijenge nchi yetu. (5)Eti kwa ajili Uganda wana dual nationality na sisi tuwe nayo. Hatuwezi kuiga kila kitu bila kujali maslahi yetu. Uganda kuna mgogoro unaofukuta chinichini kutokana na issue ya ardhi. (6)You are right bro : you can't eat your cake and still have it.

    ReplyDelete
  13. HILI JITU MNALIELEWA LINASEMA NINI JAMANI, MAANA LIMENICHANGANYA LINANONGEA LINACHOKATAZA

    Tarehe Fri Feb 19, 11:05:00 AM, Mtoa Maoni: Anonymous

    There you go again, kuongea kiinglishi na kiingereza na kiswahili na kidhungu HATUTAKI KABISA kwenye mada hii, ni KISWAHILI, but(lakini) I am saying this(ninasema hivi) "YOU CAN'T EAT YOUR CAKE AND STILL HAVE IT" I dont GET It?? can someone help me out on this..


    Ni vibaya kabisa kutumia kidhungu, but Freud Principal of Pleasure inasema “Human feelings always want more of what’s easy and sweet”….

    ReplyDelete
  14. watanzania inabidi kuamka na kuwa na mawazo ya kujenga.si mawazo ya vijiba vya raho.suala na uraia wa nchi 2 halina tatizo kwa mtazamo wangu.TENA LIHARAKISHWE.suala tunalojadili leo wazungu walitoka huko miaka 200 iliyopita.tena hawana noma na watu wenye pass 2, kama nchi zao za afrika zinaruhusu.kwanini watanzania tuwe watu wa kuishi kwa hasara tu??hiki ni kipindi cha maamuzi makini ya maendeleo ambayo yatatekelezwa kwa haraka sana.kwani tumechelewa mnoo.ikiwezekana tufanye kazi masaa 24.ikiwezekana shift 3.barabara bado,umeme tatizo,kilimo tatizo.inauma sanaaa.kwakherini

    ReplyDelete
  15. Nina imani kuwa mtu yeyote anaweza kuchangia mawazo kulingana na mtazamo wake na uzoefu wake ambao watu wengine wanaweza kuhoji na watapewa maelezo kama inabidi, lakini ni dharau na umbumbumbu kwa mtu kusema 'toka nje kwanza ndipo uchangie'! Hiyo 'dual citizenry' wacha jirani zetu wawe nayo, hapa Tz haina haja kwani mpaka sasa hakuna sababu yoyote inayowezesha mtu mwingine kuona haja ya kuwa na dual citizenry zaidi ya watu waliofilisika mawazo, wameshindwa kufikiria njia na namna ya kuendeleza nchi yao. Tunachohitaji hapa ni uzalendo, sidhani kama wa Kenya ambao wamechukua uraia wa nchi kama Qatar, na hata Ulaya kama sasa hivi hawawasaidii ndugu zao wa nyumbani na hata kuwekeza kwao kwa zamani. Tusidanganyane, Tanzania itajengwa na waTanzania wenye uzalendo wa kweli na siyo watu wanaotoka nchini kwa kutoroka halafu wakifika huko wanaanza kusema ooh fanyeni hivi ili muendelee. Philipines inaongoza kwa kuwa na wafanyakazi wa ndani wengi sana katika mashariki ya kati
    na pato lao hulipeleka nyumabani na linachangia san katika fedha za kigeni za nchi hiyo, na watu hao wanpata adha nyingi sana huko Ghuba, kakini hawajakataa uraia wao, sasa kwa nini Tz? Uganda wakifanya mambo yao na sisi tufuate, Rwanda, Kenya na kwingineko, kwani sisis hatuwezi kubuni vya kwetu, mbona mnaonekana kuishiwa sana baada ya kukaa huko enyi diaspora? N bado watataka referendum ifanywe na wao walioko huko nje au waliopata kutoka, wengine ambao ni wengi hapana (Ridiculous). Huyo Nyerere ambaye mnamlaumu anavyo vingi vizuri alivyoitendea nchi hii na wla hakuilemaza mnavyadai diapsoras wengi. Maendeleo hayana njia ya mkato. Diasporas hao wamekuwa diaspora kwa nia njema kabisa ya waTanzania wa nyumbani lakini wanataka kutugeuka. Tunahitaji hoja za msingi na siyo ubabaishaji eti kwa sababu mtu amekaa siku mbili tatu katika nchi za watu.

    ReplyDelete
  16. Huyu jamaa naona ana ufinyu wa mawazo. Watanzania wangapi wanaishi Tanzania hawalipi kodi kazi ufisadi tu , je nao wanajenga nchi? Au watu wakitoka kutafuta maisha nje ndio inakuwa nongwa? Walio nje wanasaidia kupunguza umasikini wa Tanzania maaana wakitumia wazee wa dola 500 huoni hapo kwamba wamesaidia familia? Wewe unaona kwa mtazamo wako kwamba walio Tanzania ndio wanajenga nchi ila hali wengi hawana hata uwezo wa mlo kwa siku moja. Kwa mtazamo wangu kama mtanzania anaishi nje na ana makaratasi bora abakie huko maaana ukirudi tu ujue unakuja kuongeza umasikini hilo moja. Na la pili ujue utakufa mapema maana ata viongozi wetu wanakimbilia nje kutibiwa nafikiri mmenipata. Nyerere ni baba wetu wa taifa na alifanya maamuzi kwa upendo wa watanzania ila yeye ni binadamu kuna maamuzi ambayo alikosea na aliyopatia na pia dunia uzunguka si vema tuwe tunafikiria Nyerere ndio alikuwa sahihi kumbukeni kipindi kila kulikuwa na vita baridi kati ya wajamaa na wabeberu lakini leo ni utandawazi ndio una nafasi. URAIA WA NCHI ZA ZAIDI YA MOJA NI LAZIMA kama tunataka twende na wakati.

    ReplyDelete
  17. Suala usiolijua kwako ni sawa na usiku wa kiza. Kwa taarifa yako wewe Elly suala hili halimfaidishi yule Mtanzania aliyetoka nyumbani na kuja kuganga njaa tuu huku ughaibuni peke yake. Mfano hai ni kwamba mimi mwenyewe nina watoto wawili ambao wamezaliwa na kukulia huku ughaibuni na mama yao ni mzungu kwa sheria ya nchi hii wanangu hawa wanahaki ya kua raia wa hii nchi pamoja na Tanzania. Lakini kuna kipengele kinachosema kwamba kama nchi husika hairuhusu uraia wa nchi mbili basi inabidi waheshimu sheria ya hiyo nchi. Hivyo hapa sheria yetu ndio kikwazo. Vilevile napenda kukufahamisha kwamba hawa watoto tunaozaa huku nje ni Watanzania kiliko hata wewe Mtanzania uliyezaliwa huko nyumbani. Wanasoma kuhusu TANZANIA wanaijua na wana wania kuijenga kuliko hata wewe uliyeko huko bongo. Sasa kwanini iwe shida kwa wanangu kua na Uraia wa nchi yangu ikiwa mimi nimekaa huku miaka yote bila kubadilisha uraia wangu. Hivyo usikurupuke tuu kwakua kwakua ukopekeyako kwenye screen. Hili lina mantiki kubwa kuliko wewe unvyofikiri. Kwahivyokaa chini utafakari kwa mara ya pili unaonekana unaweza kua mwanasiasa mzuri siku zijazo lakini sio leo.

    ReplyDelete
  18. Ni kweli kila mtu ana uhuru wakutoa maoni, ila kuwabania wenzi wako si jambo jema, toa hoja thabiti na sio kuleta kauli ambazo hazina mashiko, yaonyesha ni tamaa yako kubwa kuishi ughaibuni ila hukubahatika na bado unahangaika, unatumia Principle za Freud kujichanganya na yaonyesha hujui Freud ila kwa vitabu vya kuokota na sentensi za uokota!
    Suala la msingi, wawekezaji wengi hapo nyumbani ni wageni , tena wadhungu?!Akija Mzawa mwenye uraia wa Italy au Canada au UK au USA mizengwe mingi , inabidi muinue akili zenu ninyi watu!Omani walichukua watu ambao walikuwa ni vizazi vyao walioishi Africa mashariki(Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Unguja na Pemba, Comoro na kwingineko) ili kujenga nchi yao, angalia leo hii Oman iko wapi kwenye dunia?Tanzania ikichukua suala hili serious tutakuwa mbali, kuna Wa-Omani, wa Qatar wenye mapesa na visima vya mafuta wanataka kuja kujenga nchi, bado wana upendo na nchi zao(Wazawa/Wazalendo)...!Hebu amsheni akili zenu ninyi watu!!!Acheni roho Mbaya!!tutafaidika sisi sote!!EEEEH MWANANCHI!!

    ReplyDelete
  19. Mungu Ibariki Tanzania na Watu Wake Wote. I love my country, I am proud of it. I was born and grew up there, there no other place like home, but I support the dual citizenship proposal 100 percent.

    I have lived abroad for over 10 years now and I clearly understand how important it is to have this proposal made into law.

    Bwana Elly – Mdau wa Mayfair. Ni vizuri kufanya utafiti japo kidogo tu kabla hujajirusha bloguni na kutoa maoni uliyoyatoa. Kwa maoni yako au mtizamo wako unaona kuishi nje ya nchi ama kwa muda au kwa kudumu au kuchukua uraia hakuna maana yoyote kwa vile wewe ni “mtanzania halisi.” Ujumbe huu ni kwako na kwa wote ambao wanadhani watanzania waishio nje au wanaokusudia kuchukua uraia wa nchi wanazoishi, ni wasaliti, si watanzania halisi au hawaisadii nchi, au wanafaidi huku na huku na maoni mengine mengi ambayo yana mtizamo tofauti na upitishwaji wa sheria inayoruhusu uraia wa nchi zaidi ya moja.

    Huu chini ni mfano wa wenzetu wa-Filipino wanaoishi nje wanavyo-support uchumi wao. You can get this information from many sources, but Im making reference to the following sources;

    CIA Factbook 2009 Philippines;
    “The Philippines weathered the 2008-09 global recession better than its regional peers, due to lower dependence on exports and higher levels of domestic consumption, fueled by large remittances from four-to five-million overseas Filipino workers.”

    Wikipedia;
    “An Overseas Filipino is a person of Philippine origin who lives outside of the Philippines. This term applies both to people of Filipino ancestry who are citizens or residents of a different country and to those Filipino citizens abroad on a more temporary status.

    Most overseas Filipino emigrate to other nations to find employment or support their families in the Philippines. As a result of this migration, many countries have a substantial Filipino community.
    Often, these Filipinos are referred to as "Overseas Filipino Workers" or "OFW". The term "Global Filipino" is another term of more recent vintage but less widely used.

    Philippine President Gloria Macapagal-Arroy recently applied the term "Overseas Filipino Investor" or "OFI" for Filipino expatriates who faucontribute to the economy through remittances, buying property and creating businesses.

    Population of Filipinos abroad
    There are about 8.7 to 11 million overseas Filipinos worldwide, equivalent to about 11% of the total population of the Philippines.

    Each year, more than a million Filipinos leave to work abroad through overseas employment agencies and other programs, including government sponsored ones.

    Others emigrate and become permanent residents of other countries. Overseas Filipinos often work as doctors, physical therapists, nurses, accountants, IT professionals, engineers, architects, entertainers, technicians, teachers, military servicemen, students, caregivers, domestic helpers and household maids.


    Economic Impact
    Money sent by OFWs back to the Philippines is a major factor in the country's economy, amounting to more than US$10 billion in 2005. This makes the country the fourth largest recipient of foreign remittances behind India, China, and Mexico. The amount represents 13.5% of the Philippines' GDP, the largest in proportion to the domestic economy among the four countries mentioned.

    Overseas Filipinos sent $15.9 billion worth of remittances to the Philippines in 2008, up from the $14.4 billion in 2007, and $13 billion in 2006.”
    Je bwana Elly na wenzio wengi ambao bado mmelala haya mnayajua?

    Mkuu wa wilaya ya nanihii, samahani kwa kuandika gazeti, nia ni kueleweshana.

    Mdau,
    Mashariki ya mbali

    ReplyDelete
  20. Jamani Watanzania tuache kujikanyagakanyaga! Tunajikinzani wenyewe. Haja ya dual citizenship (nami nitumie kidhungu) ni ZAO HALISI la utandawazi (katika maana pana ya dhana hiyo) ambao tumeuvalia njuga. Ukishindwa kuhusisha utandawazi na dhana ya uraia wa nchi mbili, basi ujitoe kwenye mjadala. Hata dola zetu zinatumikia wananchi (wanaoziingiza madarakani) na watandawazi (wanaoshirikiana nazo kuwekeza na pia kukwapua). Hili alikwepeki ndugu zangu wazalendo!!

    Mlalahoi
    kwa mfuga mafisadi

    ReplyDelete
  21. TUKIENDELEA NA SWALA LA URAIA MBILI NI KWAMBA KUNA WATANZANIA WA KIKE NA WA KIUME AMBAO WAMEOA NA KUOLEWA NA WALIOZAA NAWAGENI NA KUZALIWA NA WEGENI.HAWA WOTE WANA KUWA TAYARI WAMESHAKUWA NA URAIA SEHEMU MBILI.NADHANI WANGELIPATA PASS ZA PANDE ZOTE MBILI INGELIKUWA NI MURWAA ZAIDI.NADHANI MGELIJADILI NA HILI KIDOGO.ILI APATIKANE OBAMA MMOJA TOKA BONGO.KAMA WALIVYO MPATA WAKENYA.
    MDAU

    ReplyDelete
  22. Mimi Bado sioni faida ya Urai wa nchi mbili kwa nchi za africa haswa Tanzania.Kuna pande mbili ambazo lazima tuziangalie. Kwanza :tuna Imgrant wangapi katika nchi yetu ambao wametoka kwenye nchi zinazoruhusu dual citizenship na wanafanya nini hapa nchini kwetu? Kwa sababu hawa ndio watakao kuwa wa kwanza kufaidika na dual citizenship sabubu watapata yafuatayo:
    1.haki ya kupiga kura hapa kwetu 2. kupata passport. haki ya kumiliki ardhi na other rights..hapa ndio panapo nipa shida ikiwa huyu mhamiaji tayari amewekeza na analipa so called double tax bila shaka serikali yetu itapoteza kodi nyingi.3.Nyingine ni the right to practice licensed profession in the Tanzania kama proffessional medical, accoutancy etc. Sisi tunaomba kila siku investor come to our country but ni lazima tukubali kwamba hii itapunguza pato letu.
    Sasa swali linabaki tunawatanzania wangapi wanataka kuja nyumbani na kufaidika na dual citizenship au ndio tutapoteza pato kwa kuwa na dual citizenship ikiwanufaisha wawekezaji mmoja mmoja?
    Angalia Nchi Kama Australia Mwaka 2000 kulikuwa na wahamiaji wengi kukiwa na watoto wengi wageni waliozaliwa hapo..hivyo wao kweli walikuwa na sababu ya kupitisha dual citizenship..baada ya kuona kuna watoto wengi wamezaliwa pale na wazazi wa nchi nyingine.
    Mi nataka niwaulize hawa Watanzania wanaoishi nje nakutaka kupata dual citizenship kuna faida gani kwa nchi yako Tanzania, Utawekeza US OR UK kama raia wa huko kwa faida ya Tanzania? Kumbuka ukiwa na dual citizenship ukija nyumbani hatuwezi kukupa top ranking jobs (Gavernment top jobs like Minister etc) ni lazima ukane urai mmoja. Naungana na wachangiaji waliopita dual citizenship kwa nchi kama Tanzania its more personal relationship.

    ReplyDelete
  23. mimi ni diaspora ninayelikataa swala la dual nationality. Hatulihitaji na ni hatari kwa nchi yetu Tanzania. Kuna watu wanaishi bongo kwa sababu wanataka kuishi bongo. Na kuna wengine wanaishi bongo kwa sababu hawana uwezo wa kuishi nchi nyingine. Sasa hili kundi la pili ndilo linalotoa maoni vichekesho humu, na kujifanya kwamba eti wao wanaipenda bongo kuliko sisi tunaoishi nje ya bongo.

    diaspora mmoja tuu akituma akituma bongo dola 1000 tuu kwa mwaka, basi mchango wake kwenye kujenga taifa ni mkubwa kuliko mchango wa mzee wa richmond (mkubwa waziri aliyefukuzwa) jumlisha na mchango wa mzee wa vijisenti.

    Kuishi bongo haina maana kwamba eti wewe ndiye unayechangia sana kujenga nchi.

    Na ukitaka kujua "the power of diaspora power"; leo hii ziwa nyanza hamtaki kuliita ziwa nyanza na mnaliita ziwa victoria, jina ambalo nyanza amepewa na diaspora wa waingereza.

    Narudia, siitaji pasipoti ya kibongo kuwa m-bongo. Mimi ni m-bongo lakini paspoti yangu ya ki-danish.

    ReplyDelete
  24. Ninyi wabeba boxes acheni upuuzi wenu. Mmezamia nje ya nchi hata kurudi nyumbani mnashindwa? hivi mnataka dual citizenship ili mfanye nini maana wengine mmeoa vikongwe ili mradi tu mpate uraia wa huko. Kuna jamaa wamefiwa na wazazi wao hata nauli ya kurudi bongo wamekosa sasa mwataka nini?

    ReplyDelete
  25. uzalendo my feet.

    ReplyDelete
  26. kama dual citizenship haiwezekani basi kuanzishwe utaratibu kama wa Marekani wa permanent residency.

    wanaofikiri dual citizenship itawafaidisha walioko nje tu wanakosea. ikiwa sheria hii itapitishwa hata walioko Tanzania sasa hivi wakiamua wanaweza kuchukua uraia wa nchi nyingine bila kupoteza uraia wao wa Tanzania.

    pia msifikiri wote wanaopigania dual citizenship hawana uzalendo au wamepoteza uraia wao wa Tanzania.

    baadhi yetu tunaomba serikali ipitishe sheria ya dual citizenship kwasababu hatuko tayari kupoteza uraia wa Tanzania, lakini wakati huohuo tunapata hasara, na kuna haki ambazo tunazikosa, kwa kutokuwa raia wa nchi tunazoishi sasa hivi.

    NDUGU ZANGUNI, NDANI YA TANZANIA SOTE TUTAKUWA NA HAKI SAWA, WALE WENYE DUAL CITIZENSHIP, NA WALE WASIOKUWA NAYO.

    ReplyDelete
  27. Jamani kuna kitu watu wengi wanachangia hii issue wanakosea nikuona kwamba watu wanaishi njee wanajifanya wanajua sio kweli watu wengi wana roho ya kwanini.Watu walienda nje wakajilipua , wakaoa,walidanganya ilikupata uraia wa nchi nyengine walifanya kwa sababu furani kwa manufaa yao au kwa familia yao au kwa tanzania.
    Miaka kumi iliyopita tanzania kurikuwa hakuna ajira maisha yalikuwa magumu watu walitoka na kwenda kutafuta maisha sehemu ambazo zina ajira.
    watanzania inabidi tujifunze kukubali kwamba mambo yanabadirika na kuna ushindani duniani kwa hiyo watu wakuja kucomment kwa kuwa wanaogopa kwamba watu walioishi nje watakuja watachukua kazi yangu ama watoto wangu waliosoma bongo hawatapata kazi nataka niwambie rise ur game usiwe muoga watu wanataka kurudi nyumbani kuinvest ama kushare vitu ambavyo wamejifunza walipokuwa nje, kwakweli kwamba watu wananza kuihamini serikali iliyokuwa madarakani na wanataka kurudi.Mtu mwengine hatabisha kwanini asichukue uraia wa tanzania na haukane wa nje lakini sio rahisi kama mnavyofikiria.

    ReplyDelete
  28. Ni saa kumi usiku (wa manane) there are salivating barbarians at the gate, jumping up and down and ready to pounce . . .

    ReplyDelete
  29. MDAU MTOA HOJA UMEZUNGUMZIA SANA KAZI NA MASLAHI.UMELENGA ZAIDI KWE UCHIMI NA MAENDELEO BILA KUGUSA MAMBO MENGINE.MIMI NINAISHI CANADA KWA MUDA MREFU SASA.NDUGU YANGU AMBAYE NINAISHI NAYE ALIPATA MATATIZI YA MOYO NA AKATAKIWA KUFANYIWA OPEN HEART SURGERY AMBAYO GHARAMA YAKE NI KARIBU NUSU YA BAJETI YA WIZARA YETU YA ULINZI.ALIPASWA KULIPA HIZO PESA ILI ATIBIWE AMA ACHUKUE URAIA WA CANADA ILI ATIBIWE BURE.SASA WAHESHIMIWA MNAOPINGA URAIA WA NCHI MBILI NAOMBA MNIELEZE,URAIA WA TANZANIA UNGEMSAIDIAJE NDUGU YANGU KUPATA MATIBABU?TOFAUTI NA VIONGOZI WETU WANAPOUGUA HUTUMIA KODI ZA WANANCHI KUTIBIWA NJE,SISI HATUNA UWEZO HUO.NAOMBA WADAU MNIELEZE NDUGU YANGU AMEKOSEA NINI KUUKANA UTANZANIA NA KUCHUKUA URAIA WA CANADA ILI AKOE MAISHA YAKE.JE,TUNGEMRUDISHA AKATIBIWE MUHIMBILI AU BUGANDO KWA KUTOKUWA NA UWEZO WA KULIPIA MATIBABU CANADA HUYU MGONJWA ANAYEIPENDA NCHI YAKE,TANZANIA?WADAU MNAPOJADILI SUALA HILI MSIKIMBILIE PESA TU AU MAENDELEO FANYENI UTAFITI PIA KATIKA MAMBO MENGINE.

    ReplyDelete
  30. asante mdau kwa maelezo,kwanza nianze na wanaolalamika kwa maelezo kuchanganwa na kingereza, mi sioni ubaya, si tunataka maendeleo bwana,ina maana tutawasiliana na watu wa nje ya nje ya nchi kwa mfano una biashara yako,sasa sijui tutaongea nao kisawahili.hilo moja.
    la pili ni kuhusu mada yenyewe,swala la kuwa na uraia wa nchi mbili sio baya inategemea kwanini mtu mwenyewe kaamua hivyo labda ana sababu za msingi.cha maana hapa ni kujiuliza kwanini watu wanachukua uraia wa nje.hii ni wazi kwamba sababu kubwa labda ni resources zilzopo kwa wenzetu.cha kusikitisha ni kwamba hata wenzetu hawakua hivi zamani ila walikua na moyo na uzalendo uliosaidia kujenga kwao kukawa hivi.sasa kwanini na sisi tujenge kwetu.najua ni ngumu hasa kutokana na ukweli kwamba tunaangushwa zaidi na viongozi wetu waroho na wabinafsi.Tanzania tuna resources nyingi sana ambazo zikitumika vizuri nchi yetu itafika mbali.
    nasikitika sana watu wanavyoponda kuhusu Tanzania kwa kuwa wapo nje ya nchi,eti oh tokeni kwanza nje ndio muone, hivi mtu huoni aibu kuipondea nchi yako hivyo, ungekua na busara ungechangia katika mabadiliko ya kuleta maendeleo sio kuongea tuuu.sikatai Tanzania kuna mambo yanaudhi saaaaaaaana lakini kukimbia sio solution.
    Mdau Maryland- USA

    ReplyDelete
  31. majadala wa uraia wa nchi mbili au zaidi kulingana na maoni ya huyu bwana ameelekeza kuupinga uaraia kwa dhana kwamba ni MZALENDO na MJENGA NCHI.
    hebu nichambue kwa ufupi chanzo cha umaskini wa tanzania,chanzo cha kupinga uraia wa nchi mbili,na suluhisho la umaskini wa tanzania na faida za urai wa nchi mbili au zaidi.
    CHANZO CHA UMASKINI WA TANZANIA:-
    .................................
    1.Tanzania haikuwekeza katika teknolojia ambayo ndiyo chimbuko la maisha bora na rahisi katika dunia hii popote pale.
    2.Tanzania haiko tayari kuwekeza katika teknolojia hasa kwa kutumia wazawa kwasababu siasa imechukua kipaumbele,na wanasiasa wanageuza mambo yote kuwa miradi ya kujinufaisha binafsi,wakirithishana toka kizazi hadi kizazi,ndugu na marafiki na mlolongo huu hauwezi kuvunjwa kirahisi,maana kabla hujafanya hivyo tayari utazimwa kama mshumaa.
    3.Tanzania imesheheni watu wengi(asilimia kubwa)wasio na elimu,na hakuna mpango wa serikali/wanasiasa unaotoa dalili za matumaini kumfanya mtanzania kuwa na elimu bora.na unapokuwa na watu wasio na elimu bora,nivigumu kuendelea,maana hawaoni haja wala sababu ya kubadili mfumo wa maisha waliyo nayo.
    4. wimbo wa maendeleo yataletwa na mzalendo umedumu miaka mingi,lakini ukweli ni kwamba huwezi kuendelea kama huna jinsi ya kukufanya uendelee,na hii ni pamoja na kuwa na uwezo sawa wa kushiriki katika kupanga,kutekeleza,kutathmini juu ya nini unahitaji na lini unahitaji na kwa jinsi gani unahitaji. hivyo huu wimbo ni wakubembelezea wajinga ili walale waliwe na wachache walio katika mirija ya kula walioshika mpini wa kisu.
    inaendelea chini......(uraia 1)

    ReplyDelete
  32. WANAOPINGA URAIA WA NCHI MBILI:(muendelezo....(uraia 2)
    --------------------------------
    1.KUndi la kwanza ni watoto wa wanasiasa walioweka mizizi,hivyo wanajuwa wakiruhusu watu wenye upeo na uwezo kifedha kushindana nao ndani ya nchi wataharibu vyanzo vyao na mirija ya ulaji,zikiwemo deal chafu wanazotarajia kuendelea kucheza baadaye wakiwa katika himaya.hivyo wao huenda nje kusoma wakirudi wanaingia katika siasa moja kwa moja bila hata kufanyia kazi kazi walizosomea.
    2.kundi la pili ni wale waliokata tamaa,ambao wanamejaa wivu hivyo wakiona mwenzao anajenga njia ya kumuendeleza wanajisikia vibaya wakotayari kuharibu ili wawe sawa.lakini hawa wanachohitaji ni kuelimishwa na kuona kuwa wanahaki na uwezo wa kuendelea pia.ila hawa hutumiwa na kundi la kwanza ili kupiga kelele wasizojua zinalenga kumfaidisha nani.
    FAIDA ZA URAIA WA NCHI MBILI AU ZAIDI:
    ------
    1.humuwezesha mzawa kupata mtaji ugenini kwa kupata nafasi ya kufanya kazi sawa na kupata malipo sawa na raia wa nchi husika,na hivyo kumpa uwezo wa kuwekeza mtaji wake alikozaliwa bila hofu,maana ni rahisi kuwekeza nyumbani ambako gharama sio kubwa.
    2.humpa fursa raia kupata huduma bora kama raia wa nchi husika zikiwemo afya,elimu n.k,na anaweza kutumia fursa hiyo kusaidia ndugu zake kupata elimu nyumbani kwani kama ana watoto na nchi husika inatoa elimu bure kwa watoto wake,yeye hupata fursa angalau ya kusaidia ndugu.
    3.kama anaujuzi ambao unahitajika nyumbani kama expert,akitumiwa hawezi kuwa na njia za kuihujumu nchi yake,badala yake anataka aonyeshe uwezo wake wote na aboreshe ilikusudi yawepo mabadiliko ya kweli badala ya kufanya deal la kifedha zaidi.kama ni barabara anajenga,basi atajenga kwa kiwango anachojuwa kitaifanya sehemu hiyo ipitike majira yote,kwani anajuwa uwezo wa mtanzania wa hali ya chini na adha anayopata.hivyo basi huruma ya damu ya nyumbani inakuwepo sikuzote badala ya kuchukuliana kama businessparterner tu.na kama ni biashara ya product zinazo hitaji ubora kiafya pia hawezi kuwaathiri watu wa nyumbani maana anajuwa kabisa ndugu zake pia wataathirika.
    5.siku zote anakuwa na nia ya kutaka sehemu aliyozaliwa iwe katika moja wapo ya sehemu bora za kujivunia duniani,hivyo basi akipata nafasi ya kufanya maendeleo hatopenda kuona anaitiwa kuwa ametoka sehemu chafuchafu au yenye watu wenye hali duni,kwa misingi hiyo atafanya maendeleo ya dhati na sio deal za kujinufaisha tu binafsi na kuishi masaki na ukoo wake.
    kuna mengi tu ambayo mzawa akipata haki za uzawa na huku anapata haki za uraia wa kigeni huko aliko vinampa faida binafsi.
    SWALI
    -----
    1.je unapinga uraia wa nchi mbilikwakuwa huna uwezo wa kuupata au kwakuwa huupendi?
    - kama huna uwezo kuupata basi wewe wivu ndio unakusumbua,kama huupendi je uraia ulio nao wa nchi moja unakufanya upate maisha bora sawa na anayopata mwenye uraia wa kigeni?
    mdau

    ReplyDelete
  33. Ndugu wananchi, hii ni topic moja nzuri sana. Kwanza kabisa nianze kwa kusema kuwa wote wanaoipinga na wanaoisupport dual citizenship wana sababu. Almost kila sababu inayotajwa kwa kusupport au kutokusupport ina maana kwani inawakilisha mtazamo wa mchangia hoja. Mimi binafsi naisupport hii dual citizenship kwasababu nyingi ambazo sitazitaja ila nawaheshimu pia wanaopinga. Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba mungu bariki hii dual citizenship ipitishwe, ni wangapi tuko tayari kurudi bongo na kuendeleza nchi kwa kuwekeza kama tunavyofikiri. Najiuliza swali hili sana make Tanzania imebadirika mmno. Mambo mengi iliufanikiwe bongo ni almost depending on the coruption. Yaani kila sekta lazima utoe chochote ili kusukuma gurudumu la sivyo mambo hayaendi. Ukweli ni kwamba nusu ya mtaji itaisha kabla hata project haijaanza. Basi kwa sababu hii mimi naona tunge anzia step one, Diaspora tupige kelele mpaka rushwa ikomeshwe ili ikipitishwa dual citizenship mambo yawe mswano.
    Au mnaonaje wadau. Heshima yenu na sikunjema.

    ReplyDelete
  34. SWALA LA URAIA WA NCHI MBILI WALA SI MJADALA HATA KIDOGO UKILINGANISHA NA SWALA LA MUUNGANO WA AFRIKA MASHARIKI KWA SABABU SWALA LA URAIA WA NCHI MBILI LINANUFAISHA WATANZANIA WAISHIO NG'AMABO NA NYUMBANI TOFAUTI NA SWALA LA MUUNGANO WA AFRIKA MASHARIKI AMBALO HALINUFAISHI WATANZANIA ISIPOKUWA WAGENI MADAU UNGEONGELEA MADHARA YA MUUNGANO WA AFRIKA MASHARIKI NA SI MAMBO YA URAIA WA NCHI MBILI AMBALO MUDA WOTE HUWA LINAFAIDA KWA RAIA ZAKE.

    ReplyDelete
  35. Mimi napenda kuiunga mkono mada hii ya uraia wa nchi mbili au zaidi.Kwanza limekuwa ni jambo la kujivunia kwa sasa watanzania wengi waelewa walio nje ya nchi kuithamini na kuijari Tanzania.Tuelewe kwamba uraia wa zaidi ya nchi moja tunaouhitaji ni kwa Watanzania!Wewe uliye Mtanzania ndiye unayenufaika na haki hiyo.Si oni ugumu wala haiingii akilini kulikataa hili wazo.Swala la maendeleo ya nchi huletwa na wenye mapenzi mema na nchi yao walio nje ya nchi au walio ndani.Na si kweli kuwa watanzania walioko Ughaibuni hawaipendi nchi yao! La hasha.Kuna wengi tu walio ndani ya Tanzania ndio wanaoihujumu nchi kwa kiwango kikubwa. Mara nyingi aliye nje huleta ndani hata hicho kidogo anachokipata; huyu wa ndani anakitoa hata hicho kidogo kwa manufaa yake.Pia tukumbuke dunia hii leo ni kama kijiji kimoja.Kama hakuna ubaya kuwa na nyumba Mwalusembe na nyingine Nyalugusu; hivyo hiyo hakuna ubaya kuwa na hati kauraia kengine kaziada lakini bado mimi ni MTANZANIA.Swala kubwa hapa huu uraia uwalenge Watanzania; watoto wote waliozaliwa nche ya nchi au kuzaliwa na mzazi mmoja Mtanzania (Baba/Mama)hawa wote ni raia wa Tanzania.Kwa kumalizia Watanzania wenzangu tulioko nje au ndani mada hii ni muhimu sana; tuijadili kwa makini na busara; si kwa jaziba na matusi."NAWASILISHA"

    ReplyDelete
  36. MIMI NI MTANZANIA KATI YA WATOTO YATIMA AMBAO WAZAZI WALIFARIKI KWA UGONJWA AMBAO JAMII YETU IMADHIRIKA SANA KIASI KIKUBWA ,KAMA TUNAVYOJUA PROGRAM ZA KUSAIDIA WATOTO YATIMA NYUMBANI MIMI NILIFAIDIKA KAMA WATOTO WENGINE,LAKINI LEO HII NINA WATOTO NANIAHESHIMU WAZAZI WANGU WA KIZUNGU NA NDUGU ZANGU WA KIZUNGU WANANIHESHIMU. NCHI HII WAMENISAIDIA KUNISOMESHA KWA HARAMA ZAO NIMEKUWA RAIA WA HAPA NINA KAMPUNI YENYE DHAMANI YA ZA DOLA MILIONI 19 SASA NIMEWEKEZA TANZANIA KATIKA KAMPUNI ZETU ZA BIA TANZANIA DOLA MILION ZAIDI 3.

    NDUGU ZANGUNI ZIDHARAU MLIOKO NYUMBANI LAKINI KAMA UMEISHI NJE KUNA FAIDA NYINGI SANA ZA DUALCITIZENSHIP,SIKU ZOTE NAPENDA NYUMBANI,LAKINI LEO WAZAZI WANGU AMBAO NIWAZUNGU WANATAMANI KUWA NA URAIA WA TANZANIA ,NIAMBIE WATAFAIDIKA NANINI NA URAIA WA TANZANIA KAMA SI ZAIDI TU YA UPENDO WAO KWANGU NA WAJUKUU ZAO WAKITANZANIA AMBAO KILA SUMMER WANAKUJA TANZANIA ILI WAJUE KISWAHILI NA MUNGU KASAIDIA MTOTO WANGU MKUBWA ANAONGEA KISWAHILI FASAHA.

    MIMI NILIKUWA YATIMA LEO MUNGU KANISAIDIA FEDHA NA NINA WATOTO 2,
    RAFIKI YANGU NI MKURUGENZI MHINDI ALIZALIWA TANZANIA NI MILIONEA ANAENDESHA KAMPUNI KUBWA HAPA NORTH AMERIKA YA SIMU WANAOISHI HAPA NORTH AMERICA WANAJUA NAMSEMA NANI.JE SISI SOTE NA WANAE UNAWAKATALIA URAIA WA NYUMBANI NI HAKI YAO.

    SHERIA ZILIZOPITWA NA WAKATI HAZINA MAANA NA SI SUALA LAKUIGA NIUMUHIMU WA DUNIA YA SASA.

    WATANZANIA WANAOISHI NJE WAMECHANGIA FEDHA ZA KIGENI KUPIA WESTERN UNION KWA MWAKA 2007 MILIONI 14 DOLA.INASIKITISHA KUONA HAWA WOTE WANADHAMINIWA HUKU KULIKO HOME.

    ANYWAY HILISUALA TUMELIPIGIA KELELE KAMA UHURU KILA RAISI TOKA MWINYI,MKAPA,MPAKA KIKWETE LITAPITA TU SERIKALI IMEONA UMUHIMU.KWA HIYO TUKANA FANYA LOLOTE JINYONGE AU GET REAL LIFE BWANA elly, INFACT LIKIPITA NATEGEMEA KUANZISHA KAMPUNI TANZANIA NANITAFOCUS WATOTO YATIMA KUWASAIDIA KUTOKANA NA PROFIT, WEWE elly PIGA KELELE HUNA NA ACHA KUSINGIZIA UZALENDO NADHANI NIWIVU NAUJINGA AU UPUMBAVU ELIMIKA BWANA.

    MNYALU-MTANZANIA MILIONEA (NORTH AMERICA).


    GET A LIFE,JIELIMISHE KUONDOA UJINGA.

    ReplyDelete
  37. BARRICK’S £2.4BN FLOAT
    BARRICK Gold, the world’s largest gold miner, is looking to spin off some of its African assets through a float in London expected to value them at around £2.4 billion

    The move came as credit card and identity protection specialist CPP also announced plans to join the main market. It is thought its valuation will be about £450million.
    African Barrick Gold is expected to jump straight into the FTSE 100 index of Britain’s biggest companies. It will be the
    London stock market’s biggest goldminer, comprising around 10 per cent of Canadian-group Barrick’s total assets, including gold miners in Tanzania.

    The company will join the market with around $280million (£113million) in cash, money which will be used to fund expansion in Tanzania and finance deals elsewhere in Africa.
    MIchuzi naomba niwatumie habari nzuri ya wadau walikuwa wanaulizia wapi wanaweza kununua shre za Barrick Gold.

    ReplyDelete
  38. nenda kwanza huko nje halafu ukirudi ndo ungee pumba zako.Watu hawatafuti uraia ili kukana Tz bali kupata oppurtunities ambazo anapata raia halafu kuja kuzitumia nyumbani.Unajua ada ya university wewe ukiwa mgeni?Hili nis swala mabalo halihitaji mjadala kwa nchi kama TZ, issue iko open kuwa nchi ndo itanufaika kuliko individual.

    ReplyDelete
  39. Dual citizen my foot.wengi wenu hat ahuo utanzania mmeukana sasa mkipewa ruhusa ya urai mara mbili si mtakua warundi,wasomali na mengine mengi mliyojizushia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...