Wakili mashuhuri wa kujitegemea Mh. Deniol Msemwa (pichani), leo ametangaza nia yake ya kugombea ubunge kiti cha Njombe Kusini ambacho kwa sasa Mbunge wake ni Mh. Anna Makinda ambaye pia ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano.
Akiwa kaongozana na kaka yake ambaye pia ni wakili mashuhuri, Mh. Jerime Msemwa, na mshauri wake wa siasa na mtangazaji mkongwe Enock Ngombale, Mh. Msemwa amesema ameamua kugombea kiti hicho kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano. Hakuwa tayari kuongelea atafanya nini endapo kama atashinda, akisisitiza kwamba hayo atayanadi muda wa kampeni utapowadia
Mgombea mtarajiwa wa ubunge jimbo la Njombe Mh. Deniol Msemwa akiwa na mshauri wake Bw. Enoch Ngombale (pili shoto) na kaka yake Wakili Jerome Msemwa, wakati wa mkutano wake na wanahabari leo ukumbi wa MAELEZO jijini Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Jamani mbona mwatuchanganya na kutu-mix? habari hii haijakamilika. Huyu anayetaka kugombea atagombea kwa tiketi ya chama gani? Au ni mgombea binafsi?maana sijaona jina la chama zaidi ya maneno mashuuri na mshauri ndo yametawala hapo.

    Kaazi kweli kweli, usitubanie comments zetu.

    Mdau Waluwalu!

    ReplyDelete
  2. I hope ameshamwona Sheikh Yahya kabla ya Tangazo hili. Msimu huu ni msimu wa waganga

    ReplyDelete
  3. MAELEZO HAYA NDIYO MUHIMU KWENU, WALEMAVU MLIWANYIMA UKUMBI WANASIASA UCHWARA MNAWAPA UKUMBI.

    ReplyDelete
  4. Kama kweli mtu ana uchungu na nchi angeenda kugombea kwenye jimbo la mwanasiasa asiyekuwa na manufaa kwa jamii. Sasa unaenda kugombea jimbo la Anna Makinda; mmoja wa wanasiasa wachache ambao mchango wao kwa taifa unaonekana. Kawabane wanaolala bungeni.

    Grrrrrrr!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...