Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kila mwenyekiti wa chama cha siasa bongoland anataka kuwa Rais. Na kwa hakika kila Mtanzania mwenye akili timamu anaweza kuwa rais. Kuwa mkazi wa Magogoni si kazi ngumu! Kazi ni kuthubutu kufanya maamuzi magumu kwa ajili ya kuliokoa taifa. JKN alithubutu na mojawapo ya maamuzi magumu aliyofanya ni kufanya majaribio ya mfumo wa ujamaa na vikolombwezo vilivyoambatana nao. Kazi ya kubomoa nyumba iliyojengwa kwa mwaka mzima inaweza kufanyika katika muda wa saa moja tu. Haishangazi kwamba ilikuwa ni rahisi kwa waliomrithi JKN kukongoloa hadi jiwe la msingi katika kipindi cha muda mfupi. Anayosema ni kweli, rushwa iko kila jamii, tajiri na maskini, tofauti ni jinsi inavyoshughulikiwa!! Ukomavu katika uongozi ni kuthubutu.

    ReplyDelete
  2. atakwenda ndani atapata viboko 24 10 na 2 ciku anaingia 12 siku atatoka akamwoneshe mkewe....kwikwikwikwiiii duh hapa kaka jerry kazi ipo....eeeeeeeee mungu mwepushie kijana jerry.kama kweli hakutenda haya.
    eemmen

    ReplyDelete
  3. Rushwa ni dhambi kama dhambi nyinginezo. Awamu zote 4 zinatofautiana kwa namna ya kulikabili kwa sababu sheria zimekuwa tofauti. Awamu ya nne kumekuwepo na seriousness on how to deal with it ndiyo maana sheria zimeboreshwa kipindi cha awamu hii.

    Hata hivyo tatizo la msingi ni kuwa dhambi hii imechukuwa sura ya kitaifa. Corruption is part and parcel of our national character. Ni lazima uwepo mchakato kuanzia majumbani mashuleni viwandani makanisani na misikitini kupiga vita rushwa.

    Naipongeza serikali hii yetu kwa namna ambavyo inavyopambana na rushwa. Angalieni vigogo waliopelekwa mahakamani. Ni ushahidi tosha. Angalieni uwajibikaji wa viongozi wa kisiasa Waziri Mkuu na mawaziri 2 walivyojiuzulu. Hiyo ni ishara kuwa hakuna kulindana. Nampongeza Rais JK kwa ujasiri wa kufanya maamuzi hayo magumu. Ninamuomba asikatishwe tamaa na kejeli zinazoelekezwa kwake. Katika mazingira tuliomo anaonekana kulishughulikia tatizo hilo.

    Ukitaka kuelewa juu ya national character hebu angalia ubishi wa baadhi ya wabunge wetu ambao wanaopinga muswada wa fedha za uchaguzi. Badala ya kuangalia maslahi ya kitaifa wameonyesha dhahiri jinsi walivyojaa ubinafsi. Mimi nasema ni aibu aibu aibu.

    Kwa nini Serikali ikazie uzi mpaka ipitishwe. La sivyo Rais awaambie kuwa anaipeleka hoja hii kwa Watanzania kwa kuitisha uchaguzi wa awali ili wananchi waamue kati yake na wao. Ndipo wabunge watakapoiona hasira yetu sisi wapiga kura. Hata wakiamua kugombea kwa tiketi ya CCJ huko ndiko watakutana na jeneza lao la kuwazika kisiasa. Hawana utu hata kidogo baadhi yao.

    ReplyDelete
  4. waao!!!!nice one- funny @ the same time! What a man JKN was huh! RIP papa.

    ReplyDelete
  5. absolutely classic!!

    ReplyDelete
  6. KAKA MICHUZI KWANZA NAPENDA KUJUA, HIVI HAYA MAONI TUNAYOANDIKA HUMU YANAWAFIKIA WAHUSIKA, AU TUNAJIFURAHISHA TU? TAFADHALI NAOMBA JIBU.

    JUU YA WOSIA WA BABA: VIONGOZI WA SASA AU HAWA WENYE VYOMBO VYA HABARI, NADHANI WANAWEKA HIZI HUTUBA ZA BABA WA TAIFA KAMA SEHEMU YA KUJIFURAHISHA TU. MIMI NILIDHANI WANAFANYA KAMA KIOO CHA KUJIANGALIA JUU YA UWAJIBIKAJI WAO. NILICHOJIFUNZA NI KWAMBA, NAONA WALIO WENGI HUU WOSIA WA BABA WA TAIFA WANASIKILIZA 'AS PART OF THEIR LEISURE TIME'; SOMETIMES KAMA KUJILIWAZA NA HATIMAYE KUISHIA KUCHEKA TU. ANCLE, HEBU SIKILIZA HAO WANAOCHEKA. KWA MWENYE BUSARA HAIKUWA SEHEMU YA KUCHEKA, MAANA INAONYESHA NI JINSI GANI MZEE ALIKUSUDIA KUCHUKUWA MAAMUZI MAGUMU ILI KUKOMESHA RUSHWA.

    WASICHEKE KUJIFURAHISHA BALI WACHEKE ILI KUCHUKUWA HATUA.

    ReplyDelete
  7. Kinachonikera kuliko vyote ni matusi ya wagombea eti siku nyingine hatuwaoni lakini uchaguzi ukikaribia ndio wanaonekana na kuanza kutoa rushwa aka takrima.

    Haya ni matusi makubwa sana kwa jamii. Serikali inatakiwa kuwa wakali sana kwa yeyote anayetoa rushwa wakati wa uchaguzi yaani sasa sheria ingekuwa ni kuwachapa viboko 48 hadharani njia panda. 24 siku wanahukumiwa na 24 siku wanatoka jela hadharani ili wapiga kura wote wamuone na kumzomea hata watoto wadogo, pumbafu sana yaani nina hasira sana na watu hao.
    Na inatakiwa kila aliyetoa rushwa ni kufungiwa kabisa milele asigombee wadhifa wowote wala kupewa kazi katika ofisi za umma.

    Badala ya kuongelea mahakama za kadhi, Wabunge wangeongelea kuwepo mahakama maalumu juu ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi. Na ziongozwe na Mahakimu wachache waadilifu waliopitia katika tanuru la mchakato wa viongozi wa Usalama wa Taifa na viongozi wa juu wa dini zetu tu hakuna cha siasa hapo period!

    ReplyDelete
  8. JKN alikuwa ni kichwa wa kipindikile,lakini bado mpaka sasa ni kichwa na ataendelea kuwa kichwa kwa sababu ya Ujinga wa wote ambao hawana nia ya mafanikio ya jamii.Viongozi wamejawa na ubinafsi katika mali za uma maajabu makubwa sana.Pia inasikitisha mno mawaziri wanafanya kazi kwa kuwekwa tu sio kwa kulinganga na professional zao utumbo mtupu.TANZANIA ACHA KUTEMBEA HUKU UNAANGALIA NYUMA KWA KUTEGEMEA KUTOJIKWAA.

    ReplyDelete
  9. Jamani mnamjua anaetengeza hizi Wosia wa baba?
    Anaitwa Dr. Amy Lymo anafanya kazi TBC1. mnaweza kuziona nyingi hizi kazi za wosia wa baba, ingia Youtube then andika amilymo utaziona nyingi tu. na bado anatengeza nyingine.

    Big Up Amy Lymo

    ReplyDelete
  10. when i said ,''funny'' i didnt mean disrespect. Mwalimu's speech were painful truth bitter with humorous touch hence funny. I hope the misunderstanging is put asside.

    ReplyDelete
  11. hivi wadau tuambizane ukweli sasa hivi utamchapa nani umwache nani???????????????????????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...