Habari ankal,

Ebwana mimi tatizo langu ni hawa Tanesco, ni takribani wiki mbili na siku kadhaa sasa umeme unakatika kuanzia saa moja na dakika kumi na kurudi baada ya saa moja au mawili. Tatizo hili liko huku kwetu Mwenge na maeneo jirani sijui sehemu zingine za jiji hali ikoje.
Hatujui tatizo ni nini maana tulikuwa tumeshaanza kuiona Tanesco kama shirika linaloanza kustaarabika kwa kuongozwa na watu wenye upeo wa juu wanaotambua umuhimu wa wadau wa upande wa pili ambao ni sisi watumiaji au wateja japo kwa kutupatia taarifa za makatizo ya umeme kila inapowezekana.
Natambua kuwa kuna shughuli zao zingine huwa ni za kidharula zaidi hivyo huwa ni vigumu kuzitolea taarifa, sasa swali ni je hii kata umeme ya kila siku majira ya saa moja jioni maeneo ya Mwenge nayo ni dharula au kitu gani? Inasikitisha sana pale unaporudi kutoka kazini halafu unafika nyumbani usikute umeme na joto la Dar lilivyo juu.
Ushauri wangu kwa Tanesco ni kwamba kila kitu kina mwisho, nadhani watakumbuka ukiritimba wa enzi zile za posta na simu, enzi za kuomba line posta halafu unasubiri masaa manne au zaidi.
Sijui wadau wa pande zingine za jiji wanakumbana na hii kero au ni sisi tu huku, au sijui tunaadhibiwa kwa vile Kakobe anapatikana huku na kawatilia ngumu kupitisha waya ingawa yeye si mteja wao kwa vile anajiungurumishia mjenereta masaa 24 siku 365 za mwaka!
Swali je, hivi bodi ya wakurugenzi na mkurugenzi mtendaji wa Tanesco wangekuwa wanachaguliwa kwa kura kama madiwani na wabunge mwezi wa kumi nao wangejitokeza majukwaani kutuomba kura?

Ni hayo tu, nawasilisha!

Mdau
Mwenge Kwa wastaarabu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. "dharula"....... jamani tunavyonga kiswahili siku hizi??? Yaani hata Kenya tuliokuwa tunawacheka siku hizi wanazungumza na kuandika kiswahili fasaha zaidi ya wa-bongo by far.

    the word is DHARURA.....

    ReplyDelete
  2. kheri yenu Dar hata umeme ukikatika mnaambiwa ,huku vijijini hatujawahi kuona hata nguzo ya umeme,karibia nusu karne baada ya uhuru,bora tuhamie Congo au Rwanda,hii nji kweshnei.

    Kama kawaida matatizo ya Tanzania yanaletwa na Watanzania wenyewe,kama alivyowahi kusema mdau.

    ReplyDelete
  3. We anonymous wa feb 26 01:27am uanamatatizo. Badala ya kuangalia content na ukubwa wa tatizo linalowakabili wananchi unajifanya bingwa wa kukosoa lugha, hebu kuwa muwazi kwa kutubandikia matokeo yako ya o-level humu ili tujue kiswahili ulipata nini pamoja na kuwa lugha ya taifa. Acha hizo ndugu yangu, kama hauguswi ni vema ukaa kimya kama. Mimi naungana na mtoa maada maana ni kweli kabisa sikuhizi taarifa ya habari tunaangalizia bar!

    ReplyDelete
  4. anony huyo huyo mkosaji wa lugha feb 26 01:27am kachemka wakati akijidai kukosoa kasema, kasema ....jamani "tunavyonga" badala ya tunavyoongea. Sasa ueledi wako wa lugha uko wapi kumbe pumba tupu! Teh teh teh

    Muathirika wa tatizo tajwa

    ReplyDelete
  5. mimi nilifikiri ni huku Arusha tu tunakumbana na tatizo hilo, hawa Tanesco kwa kweli upo mwisho wao tu, kwani hata ttcl si walikuwaga hivyo tu sasa wako wapi?????


    mdau
    a-town

    ReplyDelete
  6. Ni kweli kabisa TANESCO mmezidi maana hili tatizo ni la kila siku na hatujui tatizo ni nini na kwanini iwe muda ule ule. Kuweni wastaarabu tumechoka.

    ReplyDelete
  7. Ni kweli kabisa hilo Tatizo sio Mwenge tu hata maeneo ya Mbezi beach mpaka Africana ni kero kubwa sana.
    Hebu wahusika walirebishe hilo tatizo mara moja.

    ReplyDelete
  8. Mtoa maoni wa 1, unaelekea kule kule, hapa mada ni kwa nini umeme unakatika mida ya jioni kwa saa limoja, huyu mdau kaweka kero yake ili wanaoguswa wasaidie kutoa maelezo(pengine sisi hatusomi magazeti),.Ingekuwa ni mada ya kiswahili (lugha) hapo ndipo tungeanza kuijadili hii dharula... Tujifunze kuangalia mema zaidi na tuyaige,..
    Mdau samahani ila napenda kukwambia hapa HUJASAIDI kitu, unaweka chenga kwenye mada.
    .Napenda kuungani na mtoa mada kwamba Sio mwenge tu hapa maeneo ya Kimara, Mbezi Luis mpaka kibamba, habari ndio hio hio, hatui ni nini kinaendelea, .. Ukisoma kwenye Website ya TANESCO utakutana na haya..

    VISION
    To be an efficient and commercially focused utility supporting the development of Tanzania

    MISSION
    To generate, transmit and supply electricity in the most effective, competitive and sustainable manner possible.

    TANESCO TEKELEZENI HIZO VISION NA MISSION ZETU,,,,,

    Nawatakia Baraka za MUNGU, Pia MUNGU AWAPE HAJA ZA MIOYO YENU KAMA MKIOMBA SAWASAWA NA MAPENZI YAKE..
    MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  9. hata mbezi tank bovu tatizo ni ilo ilo mzee,ikifika saa moja usiku lazima wakate mpaka saa 2 au 3,tatizo sijui nini?

    watuambie kama kuna mgao tujipange!!!

    ReplyDelete
  10. JAMANI, MTAWATAMBUAJE KUWA WAO NI MUHIMU? NDIYO MAANA WANAFANYA HIVYO KUUZA UMUHIMU WAO, KUMBE HAWAJUI KUWA WAMEPITWA NA WAKATI. BADALA YA KUWA MAKINI, WANAFANYA MICHEZO YA XY{_=..., AH, WABONGO BWANA?
    SIJUWI KWA NINI HAWAPATI KICHEFUCHEFU KILA KUKICHA KULAUMIWA KWA HILI MARA LILE!! LAKINI SISHANGAI, KWA KUWA WENGINE LAWAMA KAMA MASHATI AU MAGAUNI YAO; YAMEWAZOEA.

    LAKINI KAMA MDAU ALIVYOSEMA, HAKUNA MAREFU YASIYOKUWA NA NCHA. ITAFIKIA WAKATI WATATUKUMBUKA WATEJA NA HIZO BONASI ZAO WALIZOKUWA WANAGAWANA KILA MWISHO WA MWAKA KWA.
    LAKINI WAJUWE, AWIKE ASIWIKE, KUTAKUCHA TU. IPO SIKU AU MWAKA ATATOKEA FARAO ASIYEMJUA MUSA NA MABO YAKABADILIKA.

    TANESCO, TAFAKARINI HAYA. JIREKEBISHENI.

    ni mimi mwathirika na tatizo hilo hilo.

    ReplyDelete
  11. Yote yana mwisho haya, hata kijitonyama ikifika mida hiyo lazima ukatike na hakuna hata siku moja hawa jamaa wameongea chochote.... mi huwa najiuliza kila siku hili linchi linaenda mbele au nyuma sielewi kabsa

    ReplyDelete
  12. hata huku kurasini kila siku dakika chache kabla ya saa mbili umeme unakatika hivi hawa tanesco hawajui kwamba ni haki yetu kupewa taarifa?

    ReplyDelete
  13. Kwa kweli TANESCO ni kero kero tupu. Tatizo hili la kukata umeme kila wanapojisikia lipo pia maeneo ya Goms. Kweli kungekuwa na utaratibu wa kuwapigia kura hawa wangetoka kapa kabisa. Hebu wajibikeni kwa wateja kwetu na mtuthamini.

    ReplyDelete
  14. Mdau umeniwahi kweli kweil. Halafu juzi kati wakaurudisha mwingi, tulisikia mishindo tu. Kila saa moja na dakika 10 wanakata.

    Labda kuna mkitu mkubwa unawashwa mahala....! Labda kuna mambo yanafanywa kimya kimya muda huo(siyajui),

    Lazima kuna explanation tu tena nzuri na tamu.

    Na kwa habari nyingine hiki kijua cha wikii hii bongo kimekausha maji mtera, tegemeeni mgawo. Na hiki kijua tungezalisha kijiumeme cha solar angalau sasa tunapigwa na joto,, umeme mgao huoooo. UOZO

    ReplyDelete
  15. jami tatizo letu ni kweli sisi wenyewe, tatizo la umeme,limekuwa nenda ludi. lakini cha kusikitisha ni kwamba yupo mdau uholanzi anao company ya kuzalisha umeme kwenye takataka, ameshakuja mpaka hapa, amesema tatizo ni dogo sana. anaomba kuja kufanya kazi yake hapa bila hata shilingi 1 yeye atakuwa anawauzia tanesco kwa bei poa,na tanesco wanaendelea na customs wao kama kawa. sasa cha kusikitisha baruwa ya kuomba anao mh wizara husika anao copi mh wa dar c.c. .lakini inasemekana wamekataa aje huku. sijui kwa nini? jamani mpeni mwenye uwezo aje amalize shida hizi na giza kila siku.

    ReplyDelete
  16. tunaomba tanesco na mh wa dar ci.c.waangalie upya maombi ya jamaa wa uholanzi aliomba kuja kumaliza tatizo la huku la umeme kwa kutumia techk ya taka. mpaka sasa wamekataa kumwalika. na yeye ni mtaalam na ameshakuja akaliona tatizo la umeme akasema ni dogo sana.

    ReplyDelete
  17. hiyo ni emergency loadshedding due to machine outages, it cant be planned as you dont plan fault, it can only be prevented through preventive maintenance, but then if the machine is ageing then there is nothing we can do but replace it at a hefty price...by the way sometimes its easier to remove a feeder which has 10MG to assit load, so poleni, hopefully kesho na keshokutwa halitatokea, if you are anywhere log into www.tanesco.co.tz and register your complaint , enter your region and see emergency numbers, call them for clarity of situation
    thanks

    ReplyDelete
  18. BIBI UMEME MPAKA TULALAMIKE KWENYE VYOMBO VYA HABARI NDIO M-RESPOND. MLIKUWA WAPI KUTUJULISHA HIYO HABARI. HATA HIVYO BADO MMECHEMSHA!!!!!!!!

    ReplyDelete
  19. TATIZO KAKOBE

    ReplyDelete
  20. solar power wandugu, oneni wenzenu wa Malawi wanatumia sana hiyo,tena wala sio ghali sana. You solve the problem once and for all, kama unakaa kwenye nyumba yako fikiria solar power, kaangalie hata baadhi ya wakazi wa Wilaya ya kyela mbeya wameanza kuitumia hiyo wameona wenzao wamalawi wanavyonufaika. asante.

    ReplyDelete
  21. TANNESCO WASHAKULA RUSHWA HAPO MA MAKAMUNI YA GENERATAS ILIO YANUNULIWA KWA KASI. KALALAGA BAO

    ReplyDelete
  22. Hakika Tanesco ni UOZO Mtupu na aibu kwa taifa na inasikitisha walioko huko ni watanzania wenzetu... Aibu yenu milele... Tatizo si Dar tu - hapa Moshi mjini maeneo MENGI manispaa tatizo hilo lipo na hatujawahi ambiwa kisa ni kipi.... Ifike mahali watu hawa wajisikie aibu hata kwenda ofisini... Hivi huyo injini wa mkoa vipi anakazi gani na anajisikiaje anapolipwa mshahara wake wakati huduma haipo kwa wateja wake...??? Aibu hii mpaka lini?? Hapo juu unatuambia tupige simu ili iweje?? tatizo mnalijua tuwapigie kuwaambia nini?? aibuaibu hii acheni bwana!!

    ReplyDelete
  23. Hapo chuo kikuu kitengo cha sayanzi kina semaje juu ya njia mbadala ya kupata umeme... tuachane na walioshindwa - tanesco!! Tanzania inayo maji, jua ndio kwao, upepo kibao!! je vipi jamani mainjinia wetu mnaendesha makongamano na masemina tu hamna kitu!! au mo weupe maeneo haya... semeni hapa tusikie..

    ReplyDelete
  24. Huku Tanesco huwa hawakati umeme kwa sababu wakikata tunawaachisha kazi.

    Huko wanakata kwa sababu wenyewe hamutaki kuwawajibisha.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  25. it sound more worse "DHARURA"!!!!!!!! it sound nice "dharula" na mimi nadhani hii ndo sahihi "DHARULA" siyo DHARURA, IT IS DEBATABLE, BUT I CONCUR WITH OTHER KWAMBA TUKO JUU YA UMEME SI LUGHA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...