Habari za kazi mkuu wa blog ya jamii. Ni matumaini kuwa wikiendi imeenda sawa kwa upande wako. Hapa Mwanza nimekuta ajali moja mbaya sana ambayo ni asilimia mia uzembe na tusimsingizie Mungu. Kipanya kinachosafirisha abiria kati ya Airport na Buhongwa kimegogana uso kwa uso na gari la samaki aina ya isuzu zile ndogo za kama tani 3 hivi.
Ilikuwa hivi: daldala ilitokea Buhongwa na gari la samaki lilitokea mjini kati. Kwenye mlima wa Nyegezi kabla ya kufika Nyegezi kona ukitokea mjini, daladala lilikuwa nyuma ya gari ndogo aina ya saloon na nyuma yake ikija pickup ndogo ya tani moja. Dereva wa daldala akalazimisha kuipita saloon bila kuzingatia kama ni kwenye kona ndogo. Kabla hajamalizia ndipo akakutana na hiyo isuzu na kugongana uso kwa uso.
Dereva wa pickup alijaribu kukanyagia breki lakini hakuweza kusimama na hivyo kuigonga daladala kwa nyuma japo kwa mshindo mdogo tu.
Habari alizotoa shuhuda mmoja ni kwamba dereva wa daladala amekatika mguu na anatapika damu na hali yake ni mbaya sana, wakati Yule wa isuzu naye hali yake nayo ni mbaya vilevile. Hakuweza kunidokezea kama kuna majeruhi wengine na wameathirika kiasi gani. Ila kama unavyoona picha inasikitisha.
Tunajifunza mambo kadhaa hapa:
· Tusidharau sheria- kwa nini ametaka kupita gari nyingine wakati si sehemu salama
· Tuzingatie sheria – angalau mita tano kutoka kwenye gari iliyoko mbele yako (mwenye pickup hakuzingatia hilo)
· Bumps barabarani ni kielelezo cha mfumo wa usalama barabarani kushindwa-elimu na kutekelezwa kwa sheria kutafanya kazi zaidi kuliko matuta ya barabarani na vidhibiti mwendo. Mfano wa mtoto aliyefunzwa vizuri huwa na tabia nzuri kuliko mtoto aliyefunzwa kwa viboko
· Tuangalie mfumo wa jeshi la polisi upya na kama namna gani ni wakati muafaka wa kulivunja na kuanza upya. Bahati mbaya ni mfumo mzima wan chi na siyo jeshi tu.
kama daladala yenyewe ilivyoandikwa "Mungu Ni Mkubwa".kwani kwa muonekano wa hiyo gari,ni zali la Mola huyo dereva kupona.
ReplyDeletemadereva wengi wazembe na hawajari maisha yao na hata ya wengine.
hicho kipanya kimeandikwa Mungu mkubwa!!!
ReplyDeleteHUYO MHESHIMIWA ALIYELETA HIYO ARTICLE HAPO, AMESEMA AJALI NI YA UZEMBE NA SIYO YA MUNGU..SWALI LANGU KWAKE JE TANGU LINI MUNGU AKALETA AJALI? UNAWEZA KUFAFANUA JE AJALI ZINAZOLETWA NA MUNGU ZIKOJE? NADHANI TUNAHITAJI ELIMU KUWAELIMISHA WATANZANIA ILI TUWEZE KUWA NA REASONING CAPACITY KUBWA TUACHE KILA SIKU KUMSINGIZIA MUNGU.HUKO TANZANIA MTU AKIFA KWA KIPINDUPINDU AU AMEIBA AKAUAWA UTASIKIA " AAH NI KAZI YA MUNGU!! JAMANI HUYO MUNGU MBONA MNASINGIZIA NAMNA HIYO? LET'S BE MATURE NA KILA MMOJA AWE NA RESPONSIBILITY NA MAISHA YAKE NA TUWE WAKALI TUNAPOONA HAO MADEREVA WAHUNI WANACHEZEA MAISHA YETU WATANZANIA.
ReplyDeleteHaya yote ni makosa ya serakali maana wamekaa kusema hichi ama chile vitu sikuwa na msingi wowote mapolisi wa tirafiki wanachangia kiasi kikubwa, kwanza magari au mabusi mengi ni mabovu au yanaendesha bila utaratibu wa usalama mbio or kupitia njia za mkataokato .je kwa nini yapo barabara, pili tirafiki hakikamata gari uwa wanataka kitu kidogo dogo, tatu manispaaa au watu wa halimashauri wa mji wanatakiwa wanatizama kuna mikakati gani ya kuepusha ajali maana kila mji au barabara zina matatizo tofauti, tatu mwisho serekali wawe na mikakati ya kutizama barabara kuu kama ya kwenda kanda arusha na pia kampuni inayopewa mkataba wa kutengeneza barabara wawe wauwezo sio kumpa mtu ambaye atatoa rushwa maana barabara ikiwa baya hata wewe mkubwa utapita hapo mna utapishana na magari mabovu na barabara hizi ninaona ajali zimedizi je kwa nini wasitengeneze two ways yaani katikati za barabara hizi kuwe na ukuta au garden inayo upana kidogo wa kutenga barabara ya kwenda upande kulia na ya kurudi upande kushoto maana ajali nyingi ni magari yanataka kupita mbio na hapo ndio wanakutana na gari ya upandi wapi kama barabara ni upande mmoja gari likipita mbio itakuwa na kazi kubwa kugongana na gari ya upande wa pili maana mpaka ifuke ukuta au ipande garden..hakuna sababu ya kusema eti serakali yetu aina pesa maana kuna viongozi wa ngumba tatu tatu huku nje je pesa wamepata wapi kama sio rushwa, tujengeni nchi yetu kama hakuna umeme au maji ni kwetu sababu ukiwa na machine ya kukulete umeme bado jirani yako yupo kizani au barabara ni mmoja hata kama una kubwa. umoja ni nguvu...ila tuwape nafasi viongozi nao wafanye kazi zao sio vyama vya upinzani kulalamika kila siku wakati manakula sahani mmoja na baadhi ya wala rushwa... KK amefanya kazi kubwa ila watu walio chini yake ndio wanaomuharibi mambo...asante michu kwa kuweka hii
ReplyDelete