GLOBU YA JAMII INAPENDA KUTOA ANGALIZO KWA WADAU KWAMBA NI VYEMA MTUMIE KIKAMILIFU HUDUMA KADHAA ZILIZO CHINI YA PICHA YA ANKAL HAPO KULIA ILI KUINJOI LIBENEKE.

*HUDUMA YA 'KUMBUKUMBU' INAKUPATIA POSTI ZA WIKI, MIEZI AMA MIAKA YA NYUMA ENDAPO UNATAKA KUREJEA HUKO KWA MUJIBU WA TAREHE

*HUDUMA YA 'BLOG MBALIMBALI' INAKURAHIHISHIA KUTOKUWA NA HAJA YA KUSAKA UPYA BLOG NYINGINE KIBAO UZITAKAZO KWA KUBOFYA HAPO.

*HUDUMA YA 'VYOMBO VYA HABARI' INAKUPELEKA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI, AMBAPO HUNA HAJA KUTAFUTA KWINGINEKO


*HUDUMA YA 'TAFUTA' INAKUWEZESHA KUPATA POSTI YOYOTE AMBAYO HUIONI KATIKA UKURASA WA MBELE. MFANO, UKITAKA POSTI YA MARTINA CHAMBIRI, BOFYA JUU YA 'TAFUTA' KISHA NDANI YA KIBOXI ANDIKA JINA C HAMBIRI, KISHA BOFYA. AMA UKITAKA HABARI ZA JK, BOFYA HAPO PENYE 'BONYEZA KUTAFUTA' NA NDANI YA KIBOXI KITACHOTOKEA ANDIKA NENO 'JK' KISHA BOFYA TENA 'KUTAFUTA'.


ANGALIZO HILI LINAKUJA BAADA YA KUPATA MASWALI YA NI WAPI ZILIPO HABARI ZILIZOPITA. MFANO MWINGINE MASHABIKI WA SIMBA WANAPENDA KUJUA HABARI ZA TIMU YAO PENDWA AMA YANGA. UNACHOTAKIWA KUFANYA NI KUTUMIA HUDUMA HIYO YA 'BONYEZA HAPA KUTAFUTA' NA KISHA ANDIKA NENO SIMBA AU YANGA AMA JINA LOLOTE ULITAKALO, KISHA BOFYA TAFUTA; UKURASA HUSIKA UTAJITOKEZA.


HII IMETOKANA NA WINGI WA POSTI AMBAZO HAZIWEZI ZOTE KUONEKANA UKURASA WA JUU. HIVYO AIDHA NENDA KWENYE KUMBUKUMBU AMA TUMIA HUDUMA YA 'BONYEZA HAPA KUTAFUTA' ILI UENDELEE NA LIBENEKE BILA KWERE.

ENDAPO HUJAELEWA AMA UMEKWAMA KWA NAMNA YOYOTE ILE,
TUMA UJUMBE KUPITIA issamichuzi@gmail.com UTAHUDUMIWA.
PIA KWA WADAU AMBAO WAMETUMA ANUANI ZAO ILI KUPATA ZE FULANAZZZ BAADA YA KUWA WADAU WA MILIONI 8 HADI 100, NI KWAMBA MCHAKATO WA KUWATUMIA ZE FULANAZZZ UNAENDELEA NA INSHAALLAH MTAZIPATA MUDA SI MREFU UJAO. TUOMBE UZIMA.
WENU MTUMISHI
-MICHUZI





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hapo kwenye blog mbalimbali, ndio penye tatizo. Tokea kuanzishwa kwa blog yako, hapana nyongeza yoyote ya blog mpya. Aidha baadhi ya link za blog hazipo tena hewani ama sinasuasua sana katika kublog.

    Cha kushekesha zaidi ni kwamba blog zote zilizotengenezwa na MK Computer Tweaks, links zake ni sasa sawa sawa, haijalishi kama zi hai ama zimekufa!Hii inatia shaka kama hata wewe binafsi kama unatembelea blog jirani.

    Cha msingi unapaswa ku-update links zote hapo kwenye kona ya blog mbalimbali.

    Natumai utafanyia kazi ushauri huu.

    Mdau Finland

    ReplyDelete
  2. Mimi hapa sijaelewa vizuri Ankal Michuzi, mfano nikitaka kupata news za fan,friend wangu Angela Lubala nitabonyeza wapi...kisha wapi....???!!!!!.

    ReplyDelete
  3. MICHUZI HIVI UNA BIFU GANI NA IPPMEDIA NAONA HAPO UMEWEKA VYOMBO VYOTE VYA HABARI ILA IPPMEDIA NDIO HAKUNA. USIJE UKAJITETEA KUWA ULISAHAU, HII KITU NIMEIONA KWA MIAKA SASA. HIVI KUNA NINI?


    Mzozaji.

    ReplyDelete
  4. Hapo kwenye blog: Wakati unaaza ilikuwapo blog ya Miruko, www.rsmiruko.blogspot.com baadaye iliondolewa, haikuelezwa sababu...unaweza kuirejesha ukipenda

    ReplyDelete
  5. VYOMBO VYA HABARI

    @Mzozaji...pia amesahau magazeti ya MWANANCHI, TANZANIA DAIMA, HABARI LEO..... n

    NAPATA SHAKA KUWA HII NI BLOG YA KISERIKALI ZAIDI..KWAHILI!!!

    ReplyDelete
  6. Ankal,
    Pamoja na pongezi zangu nyingi kwako kutokana na kuendeleza libeneke kwa juhudi kubwa hadi kufikia wadau milioni 8 na ushee,nadhani sasa ni wakati mwafaka kwako kuiboresha blogu hii ya jamii.Tunawashukuru jamaa wa MK kwa kukutengenezea libeneke hili lakini banafsi nadhani kuna haja ya uboreshaji zaidi hasa wa kimwonekano tu.

    Kwa mfano,ingependeza sana kuona eneo maalumu au kiunganishi cha video au mahojiano mbalimbali unayotuletea hapa uwanjani.Au pengine ungeweza kabisa kutumwagia yaliyojiri magazetini hasa kwa vile una 'waandishi wa blogu ya jamii'.

    Pia,kama walivyotanabaisha wadau wengine,baadhi ya viunganishi vya blogu mbalimbali ulivyotuwekea ni 'mfu'.Kwa hili,ankal,naokusihi ujibidiishe kwa vile blogger.com imerahisisha sana shughuli hii ya kuongeza au kupunguza vitu katika blogu,na sidhani kama inahitaji msaada wa MK kufanya hivyo.

    Mwisho,kama bloga mchanga,nakuomba utakapo-update orodha ya blogu mbalimbali usifanya ubaguzi.Pengine unaweza kuwaalika mabloga mbalimbali kukutumia rss feeds zao au links zao ili baadaye wasilalamike kuwa umewabagua.Kadhalika naamini kuwa katika wadau milioni 8 na ushee waliokisha kukutembelea,kuna wengi tu wanaoweza kuliboresha libeneke hili ili liendane na hadhi yake (simaanishi kuwa hadhi yake iko chini bali naamini inaweza kuboreshwa zaidi).

    Wasalam,

    Bloga mwenzio (japo mchanga)

    ReplyDelete
  7. michuzi bado hii issue hujaitatua kabisa. mfano sasa hivi nimekwenda kwenye kumbukumbu na kuchagua mwezi wa march, na sikupata habari zote zilizotokea mwezi huo.

    siku chahce ulijaribu kuweka kumbukumbu za kutafuta kwa wiki ile ilikuwa safi lakini hizi za mwezi bado kazi inahitajika.

    ReplyDelete
  8. Mimi sioni tatizo lolote...

    Mkuu wa Libeneke, hebu iongeze na matondo.blogspot.com katika orodha yako ya blogu mbalimbali.

    Kuna nyimbo za Kikabila juu upande wa kulia Wasukuma na Wanyamwezi wachangamke.

    Siku si nyingi nitaweka hapo nyimbo za Kichaga - na za makabila mengine zitafuata.

    Kazi njema

    ReplyDelete
  9. Ankal, kumbukumbu haziji zote, unatunyima raha wallahi, manake wakati mwengine tunakuwa tunasafiri na hatuna access na internet, umetuzoesha tukirudi tunapata habari zote, lakini sasa hivi - ebooo, imelala kwetu. Please rekebisha manake unatusaidia sana kupata habari ambazo tumezikosa.

    ReplyDelete
  10. Kwenye kumbukumbu ukitaka huwezi kupata specific dates, mfano ukiingia mwezi wowote unapata tu baadhi ya matukio na sio yote alafu hakuna tarehe

    ReplyDelete
  11. habari ya kazi, mimi nilikutumia tangazo uwafahamishe wanajamii kuhusu
    online shopping website
    www.kivuko.com
    mkuu naona umeiweka kapuni kabisa mkubwa
    naomba uwatambulishe wanajamii
    kuhusu website hii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...