mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. halmashauri ya mkowa wa Dar hususan wilaya ya ilala imejitahidi kuweka eneo la kati kati ya jiji safi na la kijani kama inavyoonekana. Ila sema wana mtindio wa ubunifu kwani hadi sasa hawajaeleza kwa nini bustani ya mnazi mmoja garden haifunguliwi kwa walipa kodi kujioma nayo hadi kuwepo na sherehe fulani. na vichekesho ni kwamba wakati wa hizo sherehe magari kibao yanaingia hapo ndani na kuua manyasi
sehemu ya mnarani
upande wa kaskazini ambako kuna banda la sherehe limejengwa hapo, wakati upande wa kusini kuna banda lingine ambalo hivi sasa wameliacha kuwa choo cha wazururaji



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. HIZI NDIZO HALMASHAURI ZETU ZA MAJIJI;MANISPAA;MIJI NA WILAYA ZINAZOENDELEA KUDAI KODI ZA HUDUMA ZA JAMII BILA HUDUMA YOYOTE KWA JAMII.AU MIMI SIELEWI MAANA YA HUDUMA KWA JAMII WADAU?

    ReplyDelete
  2. nasikitika kwa blogu maarufu kama yenu mnashindwa kuhariri matumizi ya lugha, Mfano hio kichwa kinachosema ''BUSTANI YA MNAZI MMOJA GARDEN'' ni sahihi kweli kwa kwa blogu inayomilikiwa na mtu makini kama uncle Michuzi? Rekebisheni bwana!

    Mdau wa Njombe!!

    ReplyDelete
  3. Jangwa Dar es Salaam!! Hii ndio sehemu ambayo tungeweza kuweka mandhari mazuri na mji ukapendeza. Lakini ukipita sasa hivi utafikiri upo Kalahari, au kandoni mwa jangwa la sahara. Hakuna raha hata ya kukaa ukapumzisha akili kidogo (meditation).

    Hatujachelewa, maji ya mto Rufiji bado yanaingia baharini kila sekunde. Tuyalete hapa mjini kwa matumizi ya binadamu na kuupendesha huu mji (au jiji).

    Hamjayaona majiji ya wenzenu!! Ukitaka kujua mji wenye matatizo usiulize, wewe toka nje ukiona idadi ya kunguru inazidi indadi ya njiwa, hapo ujue hali ni tete!!

    ReplyDelete
  4. Alex mdau wa njombe, wote walianza hivyo hivyo. Twende taratibu tu hatimaye utazoea. Pole.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa Njombe sikiliza...Hii gLOBu tuachie wenyewe, tuna Lugha zetu wenyewe tunazitumia humu na tunaelewana, wewe kama vipi kaombe kazi TUKI utapewa.. Lugha ya humu ni ya Kilibeneke na wadau tumeridhia. mfano Blog tunaita Globu na maisha yanakwenda, tatizo liko wapi?? Achana na sisi.

    Mdau wa Libeneke
    UKEREWE.

    ReplyDelete
  6. wewe mdau wa Njombe ni mgeni, haya mambo ya libeneke yana Lugha zake...mfano...akiwa na my wife wake ....nk.

    ReplyDelete
  7. Mdau wa Njombe, pengine ankel atataoa ufafanuzi wa kina. Ebu mimi nitoe ya kwangu. Kila jamii ya (au kikundi cha) wazungumzaji wa lugha - ndogo na pana - huwa na mitindo yake ya kutumia lugha husika inayoipambanua kutoka jamii/vikundi vinginevyo vinavyotumia lugha hiyo hiyo. Ukiwa ni mgeni katika jamii hiyo ni kweli utashangaa lakini hatimaye utajikuta unalazimika kurekebisha mtindo wako wa uzungumzaji hili uweze kuelewana na wanajamii wengine.
    Hiki ndicho kinachotokea katika globu hii ya jamii. Kwa mfano unakaribishwa na kauli ya 'karibuni katika libeneke la globu ya jamii' na sio katika 'blogu ya jamii', wanajamii ni 'wadau', 'barabara ya Morogoro' ni 'barabara ya Morogoro Road', 'Chuo Kikuu cha Dar' ni 'Chuo kikuu cha University ya Dar', 'bustani ya Mnazi Mmoja' ni 'bustani ya Mnazi Mmoja Garden', libeneke, msaada tutani, hoja ya haja, nk ni lugha ambayo nje ya globu ya jamii inaweza isiwe na maana au ikaonekana ni kuharibu lugha. Ukweli si kuharibu lugha bali ndio kitambulisho cha kilugha cha jamii ya wazungumzaji wa GLOBU hii.

    ReplyDelete
  8. ALEXANDER, acha ushamba wa Njombe huo. Ugeni wako kwenye Blog ya jamii isikufanye we ni mtaalamu wa Lugha. Sisi wanajamii wa hii blog tuko poa tu na lugha yetu na tunaielewa saana bila ya wasiwasi wowote ule. Kama unakereka na lugha yetu basi anzisha blog yako ya mismihati na spell check. Anko, endeleza lebeneke la lugha za jamii, ni therapy kwa walala hoi. Achana na hao washamba wa lugha.

    ReplyDelete
  9. Mdau wa Njombe karibu kwenye globu ya jamii. Kiswahili chako cha darasani kiweke kando, happa kuna kuna Kiswahili cha ankal.

    ReplyDelete
  10. We Mbwiga wa Njombe, a.k.a Alexander, (Mramwike bee), kabla hujaingia mahali ni vema ukapiga hodi. Ungehoji kwanza ni kwa nini Michuzi anajiita Ankal badala ya "Uncle", akimaanisha mjomba. Au ungejiuliza sababu za Michuzi kuita hili jamvi GLOBU badala ya BLOG.
    Lugha za hapa globuni tuachie wenyewe. Hii inanikumbusha dada Maggie wa London, nae aliingia kichwa kichwa kama wewe!

    ReplyDelete
  11. central park new york

    ReplyDelete
  12. Hapo wakiruhusu tu watu waanze kuingia, ni sawa na msafara wa Mamba, Kenge huwa hawakosi, ndo maana jiji limeamua kupafungia, hadi haja kubwa ndogo zitapatikana na mateja ndo itakuwa maskani,

    ReplyDelete
  13. hivi anayechora majengo mengi ya dar ni mtu huyo huyo mmoja,au..maana yanafanana ati,halafu hayavutii sijui alisomea kule baghdad,maana ni kama iraq kabla ya vita...hapo hayajipitiwa na tetemeko au mtikisiko wa bomu yamechoka hivyo..na kama wamesomea pale UCLAS basi mtaala wao uchunguzwe na ikiwezekana ufutwe majengo gani wanatujengea dar tunakuwa kama tuko beirut bwana...na city mnapitisha maramani ya kale..kataeni waambieni ramani za kale wakajenge kiluvyaaaa

    ReplyDelete
  14. Ahsanteni wana blog kwa kutusadia hii lugha ya globu wengine tumeondoka bongo wakati wa DUKI NAA, DANGA CHEE na MIKUYATI.

    ReplyDelete
  15. ningeshauri Ankal angeweka page moja inayotafsiri lugha za globu ya jamii ili tupoona neno linatutatiza tunaenda kwenye page na kupata tafisri yake, sio wote watakaoelewa maneno ya globu ya jamii , ni vizuri kukawa na page ya kutafsiri. mdau BAGAMOYO

    ReplyDelete
  16. kaka michuzi sasa hii ishu ya "bustani ya mnazi mmoja gardens" au "barabara ya morogoro road"....inakuaje?au wafanya makusudi? lakini asante sana kwa kazi yako nzuri ya kutuelimisha.

    ReplyDelete
  17. TUELEWANE NDUGU ZANGU HAINA HAJA YA KUROPOKA KWA JAZBA KM AKINA MAMA WA USWAZI..

    NIMEJIBU TENA KWA HERUFI KUBWA WOTE MLIO REACT YAONYESHA MNA VICHWA VYEPESI, SAWA NA JIWE LILORUSHWA GIZANI LILIEMPATA KAITIKA..

    HUO NI USHAMBA KURUDIA RUDIA MANENO WKT MAANA NI MOJA..

    MMENISIKITISHA SANA NDUGU YAONYESHA MNACHOSAPOTI NDICHO KILICHOMO NDANI YA PEO ZENU ZA KUFIKIRI..

    MSIRUDIE TENA!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...