malkia wa taarab Bi. Kidude Baraka akitumbuiza usiku huu katika hoteli ya Travertine, Magomeni Mapipa, jijini Dar katika onesho kabambe akishirikiana na Jahazi Modern Taarab, Mwanahawa Ally na Babu Ayubu. Bi. Kidude ambaye yupo Dar kwa vekesheni fupi alikonga nyoyo za mamia ya mashabiki waliofurika ukumbini kwa kibao chake kisichochuja cha MUHOGO WA JANG'OMBE.
Kiongozi wa Jahazi Modern Taarab, Mzee Yusuf, akimtambulisha malkia
hapakuwa na sehemu hata ya kutemea mate
ma'al anisa wa Jahazi walikuwa gado
Babu Ayubu alichangamsha na kibao chake kipya cha 'Jipu' na 'Chaja ya Kobe' ambamo anaigiza sauti ya Bi. Kidude na kuleta raha ya aina yake
Bi. Kidude akiwa na Promota wa onesho John Tall (shoto) na mwenyeji wake, Yasmin Razak

Ankal alikuwepo pia....
Babu Ayubu, anayekunywa soda kwa chupa ya mtoto, akila pozi na malkia
Bi Kidude akiamkiwa na Mwanahawa Ally,
mmoja wa waimbaji mahiri wa taarabu nchini























Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. kaka misoup ulifaidi viono vya kutosha je mama michuzi ulimpeleka au ulimuogopa md wa Jahaz asije akakwibia ahaaaaaaaaaaahaaaaaa

    ReplyDelete
  2. hivi jamani bi Kidude ana umri wa miaka mingapi?she is amazing

    ReplyDelete
  3. Masikini mapafu ya bibi Kidude na hizo Fegi, Ankal unaangalia tuu sidhani kama umemshauri.

    ReplyDelete
  4. kaka michuzi naomba tuweke hiyo nyimbo ya babu ayubu chaja ya kobe ama nifahamishe wapi na weza isikia

    ReplyDelete
  5. Sijui umri wa Bi. Kidude ila kitu ninachokijua ni kuwa katika miaka ya 1930's alikwenda India na Siti binti Saadi kurekodi sahani ya santuri (records za gramaphone) kwa usafiri wa "steamer" baharini. Kwa hivyo, hata kama alikuwa na miaka 16 ina maana sasa atakuwa ana zaidi ya miaka 90. Aluu.

    ReplyDelete
  6. mwanamke kidole juu
    mwanamke nyonga,makalio majaaliwa
    mwanamke fulu kujiachia
    mwanamke taarab
    halooooo

    ReplyDelete
  7. ...an old lady who needs a good rest. Surely, she must be getting a good proportion of the collections - otherwise it is utterly abusing her...

    ReplyDelete
  8. Bi Kidude ana miaka 103, kwa mujibu wa mahojiano nilosikia wiki ilopita kati yake na Miriam Migomba wa TBC1

    ReplyDelete
  9. Haijulikani rasmi umri wa bi kidude,hata yeye mwenyewe hajui sababu hakwenda shule. Na kidude sio jina lake rasmi japo ndio analotumia hata katika paspoti yake. Alipata jina kidude alipokua mtoto mchanga ambapo mjomba wake(kaka wa mama yake) alikua ana penda kumtania dada yake( mama bi kidude) kwamba kutokana na umbo na vile alivyokua anaonekana kama kidude....huyu mtoto au kidude!??? basi kuanzia hapo ikawa kidude,kidude!

    ReplyDelete
  10. Mdau wa Mon Mar 01, 09:59:00 AM,umenikumbusha mbali sana. Yule mwimbaji maarufu Siti binti Saadi aliyekuwa anaimba kwa mahadhi ya kihindi, kumbe alikwenda kurekodi India wakati huo wakipanda "steamer", umenifurahisha kweli kweli. Hivi yule mwimbaji mashuhuri wa Misri Um Kulthum yu hai? Nakumbuka alivyoulizwa ni lini utaacha kuimba, Um alijibu, "Nitaacha kuimba pale nitakapoona kuwa ukumbini hakuna mtu", nadhani huenda hii ndiyo ndoto ya Bi. Kidude

    ReplyDelete
  11. SIGARA ZINAUWA ZINAUWA.KIBIBI HICHO KINAVUTA NA MAPOSE KINAPENDA PICTURE NA GLAMORIUS KINOMA!

    ReplyDelete
  12. Anon wa 07:01, Um Kulthum alifariki dunia miaka mingi iliyopita.

    ReplyDelete
  13. Hichi kibibi sasa kingetafuta radhi za mwenyezi mungu,umri umemtupa mkono anakula bonasi tu,ni vyema akarudi kwa mwenyezi mungu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...