TAARIFA ZINASEMA BALOZI WETU NCHINI UINGEREZA, MH. MWANAIDI SINARE MAAJAR, ANAHAMISHIWA UBALOZI WETU HUKO WASHINGTON MAREKANI, KUCHUKUA NAFASI YA BALOZI OMBENI SEFUE AMBAYE HAIJATANGAZWA ATAENDA WAPI.
TAARIFA HIYO ILIYOTOKA MCHANA HUU INASEMA BALOZI RADHIYA MTENGETI-MSUYA ATAKWENDA KUWA BALOZI WETU AFRIKA KUSINI KUCHUKUA NAFASI YA BALOZI MWAMBULUKUTU AMBAYE AMESTAAFU KWA MUJIBU WA SHERIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 57 mpaka sasa

  1. Hongera sana Mhe Balozi na karibu ktk jiji la BO, lakini ombi moja tu Mhe. Balozi, Tawi la CCM la London uliache huko huko. Ukibisha yatakayokupata shauri yako. yakija yakatokea muulize Ankal akupe contacts zangu
    Karibu sana

    ReplyDelete
  2. Hongera dada Majaar. Nakupenda sana kwa simplicity yako, tpfauti na wakubwa wengi tuu ninaowajua. Nakuombea siku moja uje kuwa mbunge na ufanye kazi huku vijijini kwetu. I am confidently sure that tunakuhitaji sana huku Moshi kwa maendeleo.

    JOB MARO - KIDIA - OLD MOSHI KILIMANJARO

    ReplyDelete
  3. du ngoja tupumue sasa

    ReplyDelete
  4. Ameukata basi.

    ReplyDelete
  5. Hapa kwa kweli JK umetuonea sana sisi wakazi wa UK. Kwa nini unamhamisha mama yetu? Ndio, anaenda Washington kujenga Utanzania kama alivyofanya London lakini hapa JK mzee wa haki hujatutendea HAKI. Tukuombea kila kheri mama. Nchi inakuhiji zaidi yetu mama. Kaitumikie. Mwenyezi Mungu aibariki kazi ya mikono yako.

    ReplyDelete
  6. Karibu Marekani mama, wewe ni kati ya mabalozi wachache sana ambao ni watendaji wa kazi hodari. keep up the good job

    ReplyDelete
  7. kama ni mtendaji mzuri ki hivyo angepelekwa India maana huko ndio wanahitaji balozi. Haya sasa Wabongo Marekani jiandaeni kufungua matawi ya sisiemu

    ReplyDelete
  8. Mzee tukumbuke na sisi malaysia

    ReplyDelete
  9. mmmh mambo ya ushemeji ushemeji haya unachaguliwa pa kwenda!

    ReplyDelete
  10. Kizuri kula na nduguyo. ila mama maaja UK tulikupenda sana, baloziu poa.kila la heri madame balozi.

    ReplyDelete
  11. Karibu USA ila nakuomba sana tena sana mambo ya matawi ya CCM yaache huko huko,hapa sisi ni shule na kazi tu na kufuatilia siasa za hapa zinazofanya nchi inaendelea.

    ReplyDelete
  12. Kama walivyosema Wadau, matawi ya CCM muyaachie huko huko..nadhani siyo haki kwa vyama vya upinzani mnatumia pesa za serikali ninyi ni watendaji kufungua matawi ya CCM..Lol..

    ReplyDelete
  13. Waswahili hamuachi kusema, karibu mama balozi tunakusubiri labda kutakuwa na ushirikiano wa watanzania na ubalozi wao hapa washington. Maana niliishasahau hata kama tunaubalozi hapa DC. Tangu Balozi Nyang'anyi alipoondoka basi tena hata nyumba yetu hatuijui ipo wapi. Uongozi wa watanzania DC na Ubalozi sijui kumetokea nini. Angalau wakati wa Kaka Kesi na Balozi Nyang'anyi walfanya kazi nzuri na kutujumuisha wote kwenye matokeo muhimu Uhuru, muungano, picknick hata watoto wetu walikuwa wanajuana. WE NEED CHANGES IN DC!

    ReplyDelete
  14. Nyie wadau wa India na Malaysia hamhitaji Mhe Mama Balozi kwa sababu huko tayari mnayo matawi ya kutosha. Hapa US halipo hata moja kwa hiyo ndipo anapohitajika zaidi. vijana waliotumwa walijaribu kulifungua tukawaambia hapa si mahali pa vyama - tokea hapo hatujawasikia tena. Jamani wabongo wapenda maendeleo walio US tumkaribishe mama kwa mikono miwili atimize wajibu wake wa kiubalozi lakini akijaribu kuingiza siasa za ccm tuunganishe nguvu zetu zote hata kama ni kufika kwa jaji mkuu tufike.

    ReplyDelete
  15. SUGU imekula kwako, ushahidi ushayeya.... wabingo sieeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  16. Karibu Mama R street in D dot C aka Chocolate city uulize sura japo hatuna huo muda wakuchezea

    ReplyDelete
  17. Sefue nasikia anaenda New York alipokuwa Dr Mahiga.
    Hongera sana Radhia kuja Pretoria. Iga mfano wa dada yako Asha Rose Migiro. Utaweza tu. Hongera JK

    ReplyDelete
  18. Matawi ya chama na upendeleo wa kidini ubaki huko huko UK.

    Kama alivyosema huyo anonymous wa kwanza, msipozingatia hilo mtaumbuka mapema kuliko mnavyodhani.

    ReplyDelete
  19. Mama Maajar matawi na magwanda ya CCM tafadhali yaache huko huko kwenye Ubalozi wa UK. tunakuomba Mama kwa heshima na taadhima zoote.

    ReplyDelete
  20. finally! all the best

    ReplyDelete
  21. Mama karibu kiwanja... ila matawi ya CCM hapana.... peperusha bendera ya Taifa. Hongera sana.

    ReplyDelete
  22. duuuh hii issue ya huyu mama kupelekwa marekani nilikuwa nimeiosoma kama wiki 3 zilizopita kule jamiiforums,wao walisema kama rumours naona yamekuwa kweli.

    haya mama karibu marekani labda sasa hivi na sisi tuliokuwa huku marekani tutahudumiwa vizuri hapo ubalozini.

    mabalozi wa mwanzo walikuwa wanatunyanyasa sana tukija hapo ubalozini bila sababu.kisa mtu anataka kujionesha kwamba anafanya kazi ubalozini kwahio anataka umnyenyekee huku anakuzungurusha zungurusha bila sababu.


    tunataka balozi zetu zote duniani zijue kwamba mko hapo kwa jili ya watanzania na mtanzania anapokuja kutaka msaada wenu inabidi mumsaidie haraka hiwezekanavyo na sio kumuongezea matatizo.

    ReplyDelete
  23. Glad to have her in US ila kama walivyosema wengine upuuzi wa CCM auache UK kabisa hatutaki kuuona US.Ametumwa kama balozi wa Tanzania na si CCM.

    ReplyDelete
  24. Vyama vya watanzania kila states vimejaa hapa na tumeishi vizuri tu kwa kusaidiana kwa karibu. Tusichotaka hapa ni kugawanywa katika makundi ya kisiasa wala udini. Mambo ya kufungua matawi ya CCM uyaachie kule UK.

    ReplyDelete
  25. HONGERA SANA Mh. BALOZI. KWA KWELI UBALOZI WETU MAREKANI UNAHITAJI BALOZI WA KUTUVUTA WATANZANIA KARIBU,TUJUANE NA TUFANYE VITU VYA KUELEWEKA KWA AJILI YA TAIFA LETU.ILA MAMA UJUE MAENDELEO YA TZ HAYAJALETWA NA CCM PEKE YAKE BALI KILA CHAMA KINA MCHANGO WAKE.DHANA YA MATAWI ACHANA NAYO KABISA NA MUNGU AKUBARIKI

    ReplyDelete
  26. KARIBU MAMA, LAKINI CHONDE CHONDE CCM IACHE UK. UJE KUTUUNGANISHA LAKINI IWE KITANZANIA, KAMA ALIVYOSEMA MDAU MMOJA HAPO, TUKUTANE KWENYE SIKUKUU ZA KITAIFA NA KUJISHUGHULISHA KITANZANIA. CCM NA MATAWI YAKE YABAKI HUKO HUKO UK!!!!!!!

    ReplyDelete
  27. Tunakuomba CCM isifungashwe. We are just fine as Tanzanian and not wana CCM.Tukitaka CCM tutarudi Tanzania ila huku tumefuata mabo mengine.

    ReplyDelete
  28. Mama nimefurahishwa kuja kwako huku.Cha kwanza kabisa naona urekebishe admistration ya ubalozi hapo DC. Ukipiga simu hapo haman mtu anapokea wala kurudisha message. Yaani hao wafanyakazi wa hapo ni wavivu na wanaringa. Kazi haifanyiki. Yaani ni mambo ya kujuana. Ni aibu sana ubalozi wetu wa hapa DC. Please wafukuze wale wanawake wote wanaopokea sime wanaringz na wanamaneno ya dharau.

    ReplyDelete
  29. US UDINI NDIO KABISAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA

    MIJITU WANAVYONGELEAK AMA NCHIZAO HUKO WALIPO SI MRUDI TANZANIA.

    ReplyDelete
  30. Hongera mama Majaar; wewe ni mmoja wa mabalozi wachapa kazi sana. Ni bahati mbaya sana kwa watu wa UK kwamba unaondoka.

    ReplyDelete
  31. Ano wa Tarehe Tue Mar 16, 08:01:00 PM, Nguvu nyingi, para 5 zote za nini?

    ReplyDelete
  32. Mama karibu sana Marekani, njoo tuunganishe wote katika neno moja Tanzania na sii CCM.

    ReplyDelete
  33. UK = CCM
    US = UTANZANIA

    ReplyDelete
  34. HONGERA SANA MAMA NA KARIBU US,WANA CCM TUPO TUNAKUSUBIRI KWA HAMU TUFUNGUE MATAWI YETU.'KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

    ReplyDelete
  35. HIVI NINYI WATU WA DC MKOJE JAMANI BADALA YA KUSHUKURU KULETWA MAMA AMBAE SISI HAPA UK ANAONDOKA NA BADO TUNA MUHITAJI,MNAANZA KUMUHUKUMU ATA KABLA AJAFIKA,CUF IKO HAPA UK TOKA ENZI HIZO,CHADEMA IKO HAPA NA INAPATA PESA NYINGI YU KUTOKA CONSERVATIVE PARTY,ANAPOKUJA KWENYE MIALIKO YA CCM AU MIKUTANO YA CCM ANAKUJA KAMA MWANA CCM NA KUHIMIZA WATU WAJIUNGE NA CHAMA NA KUTOA USHAURI NI WAJIBU WAKE, WANA CHADEMA/CUF WANAPOKWENDA UBALOZINI KWA MATATIZO YA KISERIKARI WANASHUGHULIKIWA IPASAVYO KAMA WATANZANIA NA HATA WANAPOKUWA NA HAJA YA KUMUONA HUYU MAMA HANA IYANA NI MTU WA WATU NA MCHAPA KAZI, UNAOONDOKA UK BADO TUNAKUITAJI LAKINI TUNAJUA WENZETU WA DC WANAKUITAJI ZAIDI.

    ReplyDelete
  36. HALOOO ETI WENZETU WA DC WANAKUITAJI ZAIDI SISI TUNAMWITAJI ZAIDI ILI ATURUDISHIE ILE PARTY YA NGUVU YA KILA MWAKA YA KIBALOZI.
    MANA NA SISI TUNAAMBULIA KULA PESA ZA WALIPA CODI MANA MAFISADI WANAZIFAIDI SEMBUSE SISI WABEBA MABOXI?
    TUNATAKA MAPARTY MAKUBWA MAKUBWA TUNYWE NA TULE MISOSI.
    TENA JAMANI WAHUSIKA WA MAPARRY KINA FANUELI NA QUIZELA ANZENI MAANDALIZI YA PARTY YA KUMKARIBISHA DIVA MWANAIDI WATU TUPIGE VIDUDU TUMKARIBISHE BALOZI. HIYO ITAKUWA WATZ USA MUBIMBA.

    ReplyDelete
  37. Mama Balozi, karibu sana DC. Hivi karibuni tumeshuhudia juhudi kubwa zikifanywa kuanzisha jumuiya ya Watanzania, DC. Hili ni jambo zuri na natumaini waanzilishi hawakusukumwa na mafanikio yako huko UK katika kutanguliza maslahi ya CCM mbele ya Taifa. Naomba nikutonye kidogo tu kuwa uwe mwangalifu sana na mambo ya UK uyaache huko huko. Hapa US tumeishi kwa amani, utulivu na mshikamano kama watanzania bila kujali itikadi wala dini. Naomba ujio wako uendeleze huu ushirikiano. Karibu tena.

    ReplyDelete
  38. HATA SISI HAPA UK TUMEISHI KWA AMANI NA MSHIKAMANO. KILA MTU KWA HIYARI YAKE ANAWEZA KUWA TA, CCM, CUF, CHADEMA, ATWID, TAWA, MAISHA MEMA, WEMSA, SWAHILI SERVICE, BTS, NAKADHALIKA. HIZO NI JUMUIYA MBALIMBALI WATU WA UK WAMEHIMIZWA KUJIUNGA KWA HIYARI ZAO KWA MASLAHI YAO. KWA NINI ISHU NI CCM TU. WIVU, HUSDA NA KUKOSA HOJA!!!!

    ReplyDelete
  39. jamani nyi watu wa DC tulizeni boli, uk sio CCM 2. tuna mambo mengi....tunapiga hatua nyie naona global warmin inawasubua... get a life guys...

    mkereketwa wa kirefure

    ReplyDelete
  40. I AGREE NA MAJORITY HAPO JUU....CCM HUKU KWETU IS NO NO, ALONG WITH OTHER THINGS THAT COME WITH IT! MAANA WAMEIFANYA UK KAMA MBAGALA VILE GEEH!

    ReplyDelete
  41. chonde chonde uccm huko huko na ufisadi huku hatuutaki uccm na ufisadi acha hukohuko kabisa huku tunatafuta maisha na huendeleza utanzania mambo yenu ya uccm uyaache huko Uk. Sisi huku twapiga box kwa kwenda mbele hata kama hatuna makaratasi lakini tunapata mkate wa leo na wakesho.

    ReplyDelete
  42. I am just curious about JK's criteria for appointments of our officers both home and abroad. I hope they are not motivated by religion.Like an anonimous above said, Mbagala just made its debut in US scene!!!!

    ReplyDelete
  43. Dawa ni Moja tu. Mama akileta story za mbagala kama alivyofanya UK. Dawa ni kutoka nduki tu kila mtu kivyake. Kwanza hapa USA kila mtu ana misheni zake. Uduanzi ubaki huko huko UK!!!

    ReplyDelete
  44. Hivi Balozi Mwanaidi akiishi kwa hela za wavuja jasho wa TZ bila kujali itikadi zao, alifungua matawi mangapi ya Watanzania wengine huko UK ambao ni wana CUF ? Kama hakuwahi kufanya hivyo, huo si ubaguzi ?

    ReplyDelete
  45. Unajua kwanini watu wa UK wameanzisha matawi kibao ya CCM? Ni kwa sababu wamelosti na walikua wanatafuta gia ya kurudia bongo.

    Mwanaidi sisi hapa US hatujalosti. Tunapiga boxi na linalipa. Mambo ya CCM uyaachie ukouko. Ukianzisha U-CCM usishangae ukajikosea umaarufu kirahisi. This is not UK dada... This is the United States of America.

    Welcome to the United States...

    ReplyDelete
  46. Yaleyaleee aliyoyasema GT kule JF yametimia maana mwanzo aliambiwa alete ushahidi sasa mna la kusema?

    no wonder JF iko down

    ReplyDelete
  47. Samahani wadau naomba kuuliza ila msinitukane balozi Amosi Msanjila nae bado yuko UK? au pia alihama?

    Ni mimi mdau kutoka DODOMA.

    ReplyDelete
  48. Mama anakwenda kwa US Blogger sio USA.

    ReplyDelete
  49. Wishing u all the best mama,
    kweli wana D.C wanakuhitaji after reading all those comments(seemingly from them.) Londoners + the rest of the U.K give u permission to leave....
    Mimi ni patriotic and m list interested in politics, but t s so sad that waTanzania waishio kwa Obama feel threatened kwa ujio wa huyu mama!!!!!!!!!!!! Hey guys mbona mnajishtukia??? mara ooooh CCM au ooooh Udini??? yeye anakuja kama balozi wa nchi according to hEr role profile and not otherwise,,, by the way.....
    i hope she sucks all those women, maana wanatuaibisha sisi wanawake kwa ujumla,
    Likewise hakuna ushemeji hapa ni utumishi bora maana hamchelewi kusema hata Asha Migiro nae kapata kiushemeji.... ama yeye si mwa CCM???
    All the best Mama, u deserve more...
    Wanawake tunawakilisha!!!!

    ReplyDelete
  50. NASHANGAZWA NA TUHUMA ZA AJABU ANAZOPEWA MAMA MWANAIDI MAAJAR KUWA NI MDINI NA MTU WA CCM,

    HIVI KARIBUNI SEIF SHARIF HAMAD WA CUF ALIKUJA HAPA LONDON KUHUTUBIA WANA CUF KWANINI HAKUENDA MAREKANI AMBAKO MNAJIPAMBANUA NA UPINZANI?

    NA HII SI MARA YA KWANZA KWA SEIF SHARIF HAMAD KUJA KUHUTUBIA UK.

    MWAKA 2007 TULIKUWA NA MBOWE NA TUKAFANYA NAE MKUTANO WA HADHARA,KWANINI MBOWE HAKUENDA MAREKANI NA BADALA YAKE ALIKUJA UK?
    KAMA NYINYI MLIO MAREKANI NDIO WAPINZANI WAZURI WATU HAO WANGEKUJA HUKO NA KUSEMA KUWA UK NI ENEO LA CCM.

    BALOZI MWANAIDI NI MTU MWENYE UELEWA WA HALI YA JUU.NDIO MAANA KILA MTU ANALIA KWA KUONDOKA KWAKE.

    ANAWAJALI WAGONJWA WAKIWA CUF,CCM AU TLP, ANAMSIKILIZA KILA MTU KAMA NI MKATOLIKI,MFUASI WA KAKOBE AU MUISLAM.

    SIJAWAHI KWENDA OFISINI KWAKE AKASEMA LEO NI SIKU YA KUWAONA CCM AU WAKRISTU PEKE YAO.

    JAMANI MNA TATIZO GANI NYIE WAMAREKANI?

    AU MTANDAO WENU WA JAMII FORUM UMEWAFUNDISHA MUWE WATU WA KUKOSOA KILA KITU?

    HONGERA MAMA MWANAIDI UNATUACHIA UKIWA HAPA UK.
    MDAU MEYA WA LONDON.

    ReplyDelete
  51. Mimi nasema Mama balozi karibu sana. Fanya ya ccm na ya serikali. hakunaaneyelazimishwa kujiunga na chama chochote. ikiwa kuhamasisha ccm ndi kutuunganisha basi naiwe hivyo sana tu.

    lakini lakusikitisha katika mjadala huu ni kwamba mafanikio mengi na makubwa aliyoyafanya balozi Majar kwa manufaa ya nchi yetu katika kipindi kifupi alipokuwa london hayaelezewi hapa. mama amechapa kazi kubwa na tunamshukuru sana. hongera mama Majar. karibu usa.

    ReplyDelete
  52. you can tell hao watu wanaoishambulia CCM lazima ni wa vyama vya upinzani. kazi yao kushutumu na kunyoosha vidole badala ya kukaa chini na kupanga strategies za vyama vyao ili viendelee kama CCM. whenever they get a chance all they do ni kutaka kuikandamiza CCM. they already have jamiiforum ya kutolea madukuduku yao, sasa wanataka kuvamia kila topic.

    Myself am not a member of any political party, but if i decide to join kwa kweli nitaenda CCM where work is being done na matanuzi kwa sana na siyo madongo tuuu 24/7. wivu tu!

    welcome to America mama Maajar...

    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!

    ReplyDelete
  53. Kwa kweli hii Blog imefanyiwa reform ya hali ya juu. Maoni ya wananchi lazima yaheshimiwe na ujumbe hapo uko very clear. Kwa ufupi kabisa:-
    (1) Mama Maajar ni Mchapakazi hodari na ni Msomi (Kweli)
    (2) Mama Maajar ni Mtumishi wa Umma (Kweli)
    (3) Mama Maajar amekuwa akijihusisha na siasa (CCM)kinyume na taratibu na sheria za Utumishi wa Umma (Kweli)
    (4) Mama Maajar anatakiwa kuacha siasa alizokuwa anashabikia huko UK mara moja(Kweli)
    (5) Watanzania Marekani wanategemea zaidi mshikamano wa kitanzania na Mama Maajar na siyo siasa kama za UK(Kweli)

    (6) blog hii ya Jamii inatufaa kwa maoni (kweli)
    (5) Mama Maajar

    ReplyDelete
  54. Karibu mama DC. Na mimi nitafunguwa tawi huku nilipo Seattle la ccm, baada ya miaka mitano nitaenda kugombea ubunge kwetu upaleni.

    Mama yetu naomba u change kabisa hapo ubalozini. Watu hawafanyi kazi na wanakula hela za kodi za wananchi. Unakuta voice mail kila wakati.

    Ubalozi wa WAkenya huko first na wakati wao wako wengi hapa US compare na watanzania. Wanajifanya wkao busy wakati watanzania wengi hawana makaratasi hapa hata hawasumbuki kupiga simu ubalozini. Having said this, nina maana wafanyakazi wa DC ubalozini ni wavivu na ignorant.

    ReplyDelete
  55. HAYA MAMBO TUSUBIRI TUU, MARA UTASIKIA MWAJUMA KATEULIWA KUWA SIJUI NANI, MARA ASHA HUJAA VIZURI MWANAHAWA NA MWAJABU ILIMRADI TUU. WAMAMA WAPEWE KIPAUMBELE

    ReplyDelete
  56. LET ME PUT THIS CLEAR...BY THE WAY I AM A CHRISTIAN...

    WATANZANIA WA DC ACHENI UNAFIKI. KUNA MAKANISA YA KITANZANIA DC YAMEFUNGULIWA KAMA 200 HIVI. LEO HII MNAMSHUTUMU MAMA WA WATU ETI ANALETA U-DINI. SASA HAPO U-DINI UKO UPANDE GANI? MMESHASIKIA HATA SIKU MOJA KUNA MSIKITI WA WATANZANIA UMEFUNGULIWA? KILA MTU ANARUHUSIWA KUIPENDA DINI YAKE JAMANI EEH!

    NA NYIE WATU WA JAMIIFORUM MLIOHAMIA KWA MICHUZI GHAFLA KUIPAKA MATOPE CCM, WHAT'S WRONG WITH YALL? GEEH! MNAWAONEA WIVU VIONGOZI WA CCM KWA VILE WAMESOMA EEH...NENDENI SHULE LABDA HIVYO VYAMA VYENU VITAKUWA NA COMMON SENSE!

    MAMA MAAJAR KARIBU DC ALONG WITH CCM MAANA TUMECHOKA NA MAJUNGU YA JAMIIFORUM ...

    ReplyDelete
  57. Habari Hii nimeiona Dakika Za Uzeeni maana najitayarisha kuelekea mapumziko ya Muda Pale kwa Baba wa Taifa.

    Pongezi Nyingi sana Mama Yetu Mpendwa Mama Maajar.
    Kwa Niaba ya Familia Yangu Tunapenda kukupongeza sana sana na tunakuombea kwa Mwenyezi Mungu akupe nguvu na Afya Njema uchape Kazi kama Ilivyo kawaida yako.IshaalLah

    BABA & MAMA NAJU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...