Ankal,
Naitwa Peter Mtemekele (pichani). Mimi ni Mtanzania mlemavu wa Miguu, niliyezaliwa miaka takribani 46 iliyopita. Elimu yangu ni ya kidato cha sita, niliyohitimu katika Shule ya Sekondari Mzumbe mwa 1990.
Kutokana na sababu zisizozuilika sikufanikiwa kupata kazi wala masomo zaidi hadi sasa. Hata hivyo, ninaifahamu vizuri computer (haswa kwa kazi za kiofisi).
Kutokana na kukosekana huko kwa kazi, maisha yangu kwa jumla yamekuwa ni yakubahatisha na yasiyo na “future” nzuri. Ufupi ni kwamba naishi kwa kutegemea zaidi marafiki zangu wa karibu ambao kwa kweli ni lazima nikiri kwamba bila wao pengine kwa sasa hata haya ninayoyaandika yasingekuwepo kwani ni dhahiri kabisa kwamba nisingekuwepo duniani.
Msukumo wa kuyaandika haya unaletwa na ukweli kwamba nina binti yangu anayesoma kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari iitwayo Iwemba katika Kata ya Kidodi Wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro. Ukweli ni kwamba binti huyu anasoma katika mazingira magumu sana kwani ninashindwa kumgharimia mahitaji muhimu ili asome katika mazingira takiwa.
Kama hiyo haitoshi imefika mahala hata mimi mwenyewe nashindwa kumudu mahitaji yangu muhimu kama vile kodi ya chumba nilichopanga, chakula na matibabu pale inapotokea mimi mwenyewe kuumwa ama vitegemezi vyangu.
Niliwahi kutolewa kwenye gazeti la Uwazi Toleo Na. 621 nikiomba jamii yenye mapenzi mema inisaidie kuondokana na kadhia hii na kwa bahati nzuri wapo baadhi ya watu walinipigia simu wakinishauri nifungue Bank Account.
Hivyo nimefungua tayari Akiba Commercial Bank, Kariakoo Branch, Account No. 5803938092. Hata hivyo, nilishauriwa kwanza nitolewe tena kwenye gazeti nikionyesha Bank Account Number. Nikawasiliana na jamaa wa Uwazi ili wanitoe tena wakionyesha namba hiyo, lakini hadi leo wamekuwa wakiniahidi kunitoa tena lakini kutokana na mtiririko wa foleni zamu yangu haijafikia kwa maana hiyo naomba unitoe humu wakati zamu yangu kwa hawa jamaa wa Uwazi itakapofika.
Kwa heshima na taadhima, naleta kwako maelezo haya mafupi ili uweze kunisaidia kunirusha kwenye “Blog ya Jamii”, kama nilivyoeleza hapo awali, ili jamii yenye mapenzi mema iweze kunisaidia kuondokana na kadhia hii.
Mimi computer ninaifahamu hivyo kama nikiwezeshwa kufungua Secretarial Services yangu nitakuwa nimekombolewa vya kutosha ili nisiendelee tena kuwa tegemezi kwa jamii inayonizunguuka, kwani mimi mwenyewe naamini fika kwamba itafika mahala hata hawa wanaonipa misaada midogo midogo wataelemewa na majukumu yao na kushindwa tena kunisaidia; na hapo ndipo itakapokuwa “the end of me” – ukiona mtu mzima analia, ujue maji yamemfika shingoni.
Mungu akutangulie kwa hili.

Peter M. Mtemekele,
P.O. Box 72718,
Dar es Salaam.
Mobile: 0714 999837
pmtemekele@live.com
P.O. Box 72718,
Dar es Salaam.
Mobile: 0714 999837
pmtemekele@live.com
weka email yako nikupe maelezo fulani.
ReplyDeletemr peter pole sana lakini usivunjike moyo. kwani ujue mungu yuponawewe
ReplyDeletedaima kwa maana usingefika hapo
ulipo sasa.kubwa kama msemaji mwenzangu hapo juu mwambie michuzi
akuwekee email itakusaidia sana
kimawasiliano kwetu. ahsante yataisha tu hayo ulionayo
Naomab jamani watu wanaosoma kwa michuzi na wanaajira wamsaidie huyu. Kuwa mlemavu isiwe kigezo. Akipata kazi ataweza kupull up maisha yake.
ReplyDeleteHela za kugawiwa leo hii kesho zitaisha halafu itakuaje tena jamani. Msaidieni hapo apate hata kazi yeyote atakayoiweza
Be blessed
Ankal, Mungu akubariki kwa kuweka maswala nyeti kama haya.
ReplyDeleteMjomba, tusaidie email yako ili tutete kwa faragha.
(US Blogger)
wadau msaidieni huyu, mtafutieni mfadhili aksome zaidi inawezekana sana, jaribu kwenda kanisa katoliki, ubalozi wa USA na CANADA kamakidato cha sita ulifaulu unaweza kupelekwa shule hata kama hukufaulu wanaweza kukusaidia scholarship
ReplyDeleteaisee yani tena umesoma kabisa ivi?
ReplyDeletembona inawezekana ni kweli upate mtaji wa kuanzisha biashsra au usome zaidi uku unaendesha iyo biashara itakuwa vema zaidi,,,
ata ukienda maeneo annon apo juu avotaja uwezo wa kusaidiwa zaidi upo maana una nia kabisa na umesoma tu (umenigusa moyo)
ni kweli email huwa raisi zaidi
Mungu akutie nguvu
kwa mwaka alomaliza jamaa form6 ilikua ni ngumu kwa jamaa kukosa kazi ila kutokana na ulemavu wake akashindwa kupata kazi mpaka leo!!pole sana kaka yangu ila jua tu neema ipo njiani!pamoja
ReplyDeleteMzumbe 1990! Hivi ndio vichwa vyenyewe. Elimu haina mwisho, ila jamani jamaa ana 46yrs, na binti anayemtegemea. Sasa nyie wachangia hoja mnataka aende ughaibuni kusoma, na maisha ya huko ya boksi kweli atayamudu? Mwenyewe ametoa wazo la mtaji nyie mnataka kucomplicate issue.
ReplyDeleteWatu mnachekesha sana email ya nini kama ametoa namba ya simu kama huwezi kumpigia simu au msg unaweza kumwandikia mail na je kama hana mail, kwa nini umpigie umshauri hata afungue hiyo mail unayosema... watu mbona mnakwepa majukumu??
ReplyDeleteXYZ
NDUGU HAKIKA MUNGU ATAKUSAIDIA NIMEWASILIANA NA NDUGU ISSA MICHUZI YA KUMSHUKURU KUWEKA TANGAZO LA NDUGU ILA NIMEJARIBU KUMTUMIA SMS KWENYE NUMBER ALIYOTOA NAONA HADI SASA IKO PENDING NINGALIOMBA NDUGU ISSA KUNIPA NUMBER NYINGINE ILI NITOE SADAKA YANGU PIA ITAKUWA VYEMA KAMA KUNA MTU WA SERIKALI ATAYESOMA HIZI COMMENTS KAMA NAWEZA KUTUMA PC JAPO KUKUU LAKINI ZISIWE NA USHURU PIA NIMESAMBAZA E-MAIL KWA NDUGU HUKU OMAN ILI KUPATA MSAADA HAKIKA SIMU NI BORA KULIKO E-MAIL MAANA SIMU MARA HABARI ZINAMFIKIA HIVYO NDUGU INSHALLAH MUNGU ATALETA KHERI MIMI MWENYEWE NTAJITAHIDI PESA ZIKUFIKIE NA PIA AWAMU YA PILI NTAJITAHIDI KUJUA SHERIA ZA USHURU ILI NIWEZA KUJITAHIDI KWA UWEZO WAKE MUNGU NIKUTUMIA PC NA PRINTER JAPO HII HAITAKUWA AHADI KWA VILE HADI UPATE HABARI ZA USHURU AMA PESA NI MARA MOJA NUMBER YANGU 00971505623298 NIKO HAPA OMAN. NDUGU ZANGU HIZI SADAKA NI MUHIMU NA NI WAJIBU WETU KATIKA KUSAIDIANA. NAIMANA IKIWA KILA BINADAMU ATATOA SADAKA YAKE BASI HAKUTAKUWA NA MTU MWENYE SHIDA DUNIANI. NIA YANGU SIKU ZA MBELE NIKIJALIWA NATAKA KUANZISHA MFUKO WA WAHITAJI ILI KUNUSURU MAISHA YA NDUGU ZETU WENYE MATATIZO CHUKULIA JANA NILIKUWA NASIKIZA HABARI ROHO YA BINADAMU IMETOLEWA KWA KUIBA MAHARAGE JAMANI HUYU BINADAMU HUENDA KAZI HAKUPATA NA CHAKULA HAKUPATA HAKIKA KILA MARA ROHO HUNIUMA SANA KUONA BINADAMU ANAULIWA JAMANI FIKIRIA MAMA YAKE MIMBA MIEZI 9 NA HADI KUMKUZA. NAIMANI MFUKO HUU UTASAIDIA SANA NDUGU ZETU MAANA UTATOA KAZI ILA UTAHITAJI MCHANGO WA KILA MTU JAPO KIDOGO. NAMUOMBA MUNGU NIWEZE KUFANIKISHA HILI JUKUMU AMBALO NAFIKIRI LITATOA UMASIKINI NA KUFUMBUA WATU MACHO MAANA YENYEWE ITAKUWA NI ELIMU YA VITENDO PAMOJA NA PESA TUOMBE KHERI
ReplyDeleteKaka nimejaribu kukupigia lakini simu yako haipatikani, kuna njia nyengine ya kuwasiliana nawe?
ReplyDeleteHili ndio zawa la serikali ya Tanzania kula fedha za misaada ya walemavu kwa kununua magari ya kifahari na kuwa na kasumba ya kuwapa mikopo wahindi ambaoo wananufaisha maisha yaoo na kuchukua morgages ulaya ..NGO's nyingi Tanzania zinachukua misaada ya hawa watu walemavu.
ReplyDeleteNinashukuru nimepata account yako ..naamini nitakuwekea chochote ili ufanikishe malengo yako
mdau wa Oman pc ukileta bongo hazina ushuuru,wewe fanya bidii umtumie tu tena kwa msaada ndio kabisa hawasumbui hata mafisadi wanajua hilo
ReplyDeletePeter,nimejaribu kukupigia,lakini simu yako haopatikani.Naomba kama una namba nyingine ya simu utuwekee ili tuweze kukusaidia.Nimeguswa sana na ada ya mwanao,kwani nafahamu kuwa elimu yake itakusaidia wewe pia.Naomba namba ya mkuu wa shule yake na kiwango cha ada anachohitaji.
ReplyDeleteMdau-DC
Michuzi,Tusaidie kupata taarifa zaidi za shule ya huyo binti tuweze kumsidia asije akakosa masomo.
ReplyDeleteMdau Silver spring MD.