Endapo utafika London halafu ukaacha kutembelea Club Afrique iliyoko mitaa ya Canning town utakuwa hujajitendea haki. Hapo bolingo na kampani kama uko bongo. ukizingatia inaendeshwa na mmatumbi mwenzetu Jesse Malongo. Halafu mishikaki yake acha! Mahala pametulia kwa kweli...
ankal akiwa na bosi wa Club Afrique Jesse Malongo usiku wa kuamkia leo
Ankal akiwa na Jesse Malongo na kiongozi wa bendi ya Jambo Stars inayopiga hapo kila Jumpili, Kawelee Mutimwana na ankal Baraka Msiilwa Mwenyekiti Mtendaji wa African Stars Entertainment ya Twanga Pepeta ambaye yuko vekesheni london
ankal, jesse malongo na wadau wa Seven Sisters
DJ akifanza mambo yake. hapo ni yenu kwa kwenda mbele





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ankal,
    Dress code inasema NO HATS, lakini wewe umekula kapelo vilevile. Hii ni VIP treatment au unaonyesha u STARDOM wako.Kula raha zako.

    ReplyDelete
  2. Naomba kuuliza uongozi wa Club Afrique una maana gani kuandaa hiyo shoo siku ya Ijumaa Kuu? Hiyo siku kwa kawaida katika kukumbuka kufa kwake Bwana wetu Yesu Kristo mambo kama haya hayatakiwi.

    Kwani mngesubiri hadi siku ya Pasaka ingekuwaje?

    Mdau, Bloomsbury, London, UK

    ReplyDelete
  3. ADILI NA NDUGUZEMarch 29, 2010

    Ee bwana eh Michuzi. Hapo kweli. Na mimi nikijaaliwa kufika London lazima nifike hapo mahala. Ninakumbuka mwaka 1993 nikiwa London marehemu Mike SIkawa alinipeleka Finsbury Park kwenye basement ambayo Mariam Kilumanga alikuwa akiendesha disco na kutuuzia supu. Pale pamoja na kuwa mlango wa kuingia na kutokea huo huo mmoja ilikuwa mnakutana na Wakenya na Waganda. Lakini naona hiyo ya Malongo ina hadhi haswa.

    ReplyDelete
  4. Idumu ze flanazzzzz!!! Niliimithi ile mbaya

    ReplyDelete
  5. Mdau hapo juu ijumaa kuu ni this coming Friday sijui wewe uko ulimwengu upi. Au ulitaka tu kusema?

    Box kali hata hujui siku zinaendaje...LOL

    ReplyDelete
  6. wadau mi na wazo naomba huyu ankul tumuite ANKO SUGU WA FULANAAAZ,,maana hakomi kuvaa hilo fulana,,au hasomi comment nini?

    ReplyDelete
  7. Haki ya yani ZE FULANAZ hadi UK!! kula bata Ankal u deserve it. Tunashukuru kwa kutuhabarisha news japokuwa uko mbali. Karibu na huku kwa Hu Jintao ukipata mwanya.

    Mdau - Beijing.

    ReplyDelete
  8. Mdau BloomsburyMarch 30, 2010

    We chizi wa 29th March 09.56 pm ndio umechoka kama si joto la Bongo linakula ubongo wako basi ni ujinga wako tu.

    Kwani mimi nimebisha kuwa this coming Friday ndio Ijumaa kuu?

    Halafu watch your mouth, not everybody who comes to the UK comes "kubeba box". Hao wenye shughuli hiyo huwezi kuwakuta Bloomsbury, sawa?

    ReplyDelete
  9. Jamani huyu ndiye kawelee mutimwana wa tancut ochestra na MK group (ngoma za magorofani). Tunammisi sana na jitaa lake la solo. Tutafurahi kama tutapata CD za nyimbo zake za sasa hapa bongo.
    Michuzi tufahamishe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...