Ankal!
Hebu wawekee hii taswira ili wahandisi wetu (kama wapo) wapate aidia ya nini kifanyike kupunguza, kama si kuondoa kabisa foleni, jijini dar. waambiw hao wahandisi wasifikirie daraja la manzese tu bali pia hata flyovers kama hizi hapo. Mfano moja itapita jangwani kuchogea ilala na kariakoo na huku kariakoo na kwegineko iwe pale daraja la salenda briji 'mamnyoya' kwenda kinondoni na barabara ya old bagamoyo rodi. wadau wengine mnakaribishwa kuchangia. Ni wazo tu wadau, msintoe roho bure mtoto wa mwenzenu....
Mdau wa Lagos

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. mi nachoweza kusema,hatuna uwezo huo wa kujenga katika namna hiyo,pili mainjinia wetu hawawezi kujenga kitu cha namna hiyo,kwa sababu elimu hairuhusu.
    Hivi vitu havijengwi kirahisi,eti mtu kaenda chuo na kapata dgree,its more than that,it needs a century experience.

    ReplyDelete
  2. Huu ni utani kwa nchi masikini kama Tanzania. Dawa ni kutotoa vibalivya kuanzisha huduma muhimu mjini kati kati. Kwa nini huduma hizo zisiwekwe nje ya mji ili watu wagawane wengine wanaenda nje ya mji na wengine waliobaki ndio wanaenda mjini. Mipango miji wakatae PPF, NPF kuzidisha mijengo mikubwa mjini kati kati. Nje ya mji kukijengwa na huduma nyingine zitahakia huko na misururu itapungua.

    ReplyDelete
  3. Mimi ni miongoni mwa wadau wasioafikiana na wazo la kukabiliana na foleni kwa njia ya 'flyovers' kwa sababu kubwa kadhaa:
    1. Madereva wetu watageuza barabara zinazopita chini ya madaraja kuwa eapoti kila siku. Wakishafanya hivyo foleni itaongezeka badala ya kupungua.
    2. Kupanua barabara na kujenga maflyover ni kuhangaika na symptoms bila kujua chanzo hasa cha ugonjwa ni nini. Uzoefu wa mataifa ya magharibi ni kuwa kila ukipanua barabara baada ya miaka mitano zinakuwa hazitoshi unapanua tena. Panahitajika 'smart growth'.
    3. Kwa uzoefu wa utamaduni wetu wa matengenezo, kila siku madaraja yatakuwa yanatuangukia mjini.
    4. Gharama za ujenzi wa maflyover zinaweza kusaidia kuboresha barabara nyingi sana za kiwango cha vumbi huko kijijini na hivyo kumwezesha mkulima kufikisha mazao yake sokoni, tofauti na kumpunguzia foleni ashkum si matusi fisadi.

    ReplyDelete
  4. Waje India wajifunze ma-flyover very simple na gharama zake ni rahisi tatizo ni politics ni nyingi kuliko, mambo ya maana, India magari megi pikipiki,autorickshore(bajaji),baisikele mikokoteni, ng'ombe, nyati,mbwa pamoja na waenda kwa miguu na wote wanatumia barabara, lakini foleni inakwenda kwasababu ya ma-flyover,haya lakini Bongo miaka inaenda watakuja wengine mambo yatakua vilevile na watamaliza muda wao wataondoka ????????????

    ReplyDelete
  5. mdau wa 12:03 KULA TANO...ni kweli nchi yetu haiitaji hayo mavitu kwani tuna matatizo lukuki ya kuyapa kipaumbele.wanaotusaidia kwenye budget yetu watatushangaa tukijenga hayo mavitu badala ya kutokomeza Malaria"ZInduka" na kutekeleza kilimo kwanza.....ndio hio.
    mdau wa kwa mfuga mbwa.

    ReplyDelete
  6. mimi nakubaliana na huyu jamaa alotuma picha hiyo kwani kila kitu kinawezekana kama hatuna wataalam hapo bongo si wachukuwe kutoka nje! mbona umejengwa uwanja wa kisasa wa kabumbu wa Taifa?? na wataalamu si wametoka nje! kila kitu ni FEDHA tuuu!!!nakumbuka nilikuja kimatembezi hapo nyumbani kutoka Ilala kwenda kariakoo na hasa mida ya kuanzia saa 3asubuhi mpaka saa 12 jioni ni bora uwende kwa miguu utafika mapema kuliko kwenda na gari si mchezo foleni ya nguvu!!!.mdau Leicester.vaill

    ReplyDelete
  7. Politics inaingilia mno wataalam huko uswahilini.Wakati wa proposal ya kujenga uwanja wa taifa (huu mpya)watu wenye akili zao wakashauri uwanja upelekwe Mlandizi na wakatoa sababu za msingi(kupanua mji,kuendeleza maeneo ya pembezoni, kupunhuza foleni, kukuza michezo pembezoni, n.k)Wakaingilia wanasiasa wasiojua chochote wala lolote wakapinga kwa nguvu zoote.
    Sasa huo ni mfano tu wa jinsi viongozi walivyo mananga huko TZ.
    Kwa viongozi mlionao huko (hawana tofauti na KAGAME)foleni zitaendelea mpaka yesu arudi.Flyovers sio solution.Huduma za jamii zipelekwe nje ya mji au mikoani.Si lazima mawizara yote yawe Dar!Si lazima watoa leseni wawe Dar.Mtu anatafuta leseni ya kuwindia kigoma, lakini leseni zinatolewa Dar tu!! hii nini maana yake?

    ReplyDelete
  8. So far Dar hakuna Feeder road za kutosha, je Gari zikitoka kwenye Flyovers zitakua zinaingia kwenye barabara gani?Kunaitajika utengezwaji wa Feeder road za kutosha kabla ya kufikiria Flyovers.Hakuna haja ya mdau wa hapo kwenda kariakoo kupitia Uhuru road, wakati tuna space za kutosha za kuchonga barabara ndogo kutoka Ilala mchikichini kwenda Kariakoo.Pili Tuiunganishe mikoa yetu yote kwa Tarmac road ndio tufikirie Flyovers...tuache ubinafsi wa kufikiria kila kitu Dar es salaam.

    ReplyDelete
  9. mnacheza nyie, kandarasi kazaliwa mtwara kakulia mtwara shule kaenda mtwara, chuo kikuu ndio kaja UD.. akili ya kudesign barabara kama hii atatoa wapi?

    ReplyDelete
  10. Naungana na mdau wa pili hapo juu, karibu wizara zote zipo city centre. Kwa nini wasitawanye hizo huduma na kujenga miji midogo midogo ili kusudi kama mtu anahitaji kitu sio lazima afike posta au kkoo.

    Njia nyingine ambayo ni simple na pengine gharama zake ni ndogo ni njia ya reli. Kuna reli toka ubungo maziwa inapitia mpk tabata hii ikiboreshwa itasaidia sana funga behewa kama 3 au 4 zikiwa zinapishana tren(huku ng'ambo tunaziita tram)kama mbili hivi tatizo kwisha. Kwa watu wanaotoka tegeta,mwenge, sinza au kimara wengi watakuwa na option ya kupandia hilo tram hapo ubungo maziwa kwa kweli itasaidia sana kupunguza foleni (i mean daladala za maeneo hayo niliyoyataja zitakuwa zinaishia ubungo na hakuna haja ya kufika posta au kkoo),sema hili jiji hakuna watu wabunifu wa kuumiza vichwa kila siku kamati zisizokuwa na mpango wowote isipokuwa kujaza matumbo yao. Mimi naamini kabisa kuna mabehewa na vichwa vya treni ambayo yanahitaji ukarabati kidogo kuweza kufanya kazi,halafu gharama za mafuta hata jiji linaweza kuchangia pia kwa sababu hawa wanapokea kodi kutoka vyanzo mbalimbali na hivyo iwe km mchango kwa jamii. Pia inawezekana kabisa kujenga reli katikati ya eneo ililopo kati ya barabara (badala ya kupanda maua. Naamini pia hii nayo itapunguza foleni badala ya huo mradi wao wa magari yaendayo kasi, lakini mbali na hilo jiji liboreshe barabara za mitaani sio lazima wote waendao posta au kkoo lazima wapitie morogoro road.Ninayo mengi ila inatosha, sina uhakika kama hawa viongozi wa jiji huwa wanasoma hata hizi comments.
    Kinachoboa hivi hawa viongozi wakiwa wanakuja huku hawawezi kujifunza kwa wenzao wanavyooendesha mambo? Hizi tram huwa wanaziona kabisa,kinatotakiwa kampuni kama UDA/Sumatra iingie urafiki na makampuni yanaoendesha vitu kama hizo tram japo kuwapa utaalam hakuna haja ya kubinafsisha kwa makampuni ya nje.

    Mdau Belgium.

    ReplyDelete
  11. Ndugu wadau,
    Hawa ndugu zetu kule nyumbani(wasomi)tunawaonea bure.Msomi anayeishi kimara anaamka saa 10 alfajiri kwenda kazini.Inamchukua masaa matatu hadi manne kufika kazini.Akiwa njiani anawaza asipate ajali maana magari ya wagonjwa yapo mawili.Ikifika jiono akiwa njiani kurudi nyumbani anawaza sijui atakuta maji yanatoka aoge,au sijui atakuta umeme unawaka?anapokwenda kulala,ukiondoa mbu,anawaza sijui ataingiliwa na majambazi kabla ya kuamka saa 10 alfajiri?Mtu kama huyu unapomzungumzisha"flyovers"au"dual citizenship"sidhani kama ni kumtendea haki.Anaweza kuwa ni msomi mzuri tu lakini"lifestyle" yake inamfanya afikirie matatizo zaidi kuliko hayo madaraja.Wadau hasa tulioko nje naomba tusi wa-push sana hawa wezetu.Nini kifanyike kupunguza foleni,hata mimi sielewi kwa sababu nilisoma masomo tofauti kabisa na engineering. God less Tanzania.

    ReplyDelete
  12. Ni wazo zuri ila naona mwandisi na wadau wa makala hii wanadharau taaluma ya uhandisi kwa wazalendo wa Tanzania.
    Tupo Watanzania wengi tunaoishi nchi zilizoendelea na tunafanyakazi za design na ujenzi wa barabara bora kuliko hizo alizoonyesha mtoa mada. Tanzania tuna matatizo mengi na ujenzi wa flyover unahitaji mambo mengi kama alivyochangia mdau mmoja kuwa hatuna feeder roads za kutosha. Walioko Tanzania wanaona sasa feeder roads nyingi zinajengwa Dsm na baada ya hapo ni hizo flyover. Naomba kama taaluma yako siyo Uhandisi basi usidharau bila utafiti sahihi.

    ReplyDelete
  13. kazi ya injinia moja wapo ni kudizaini nenda ud ukaone watu wanavyodizani tatizo pesa za kujenga mambo hayo na kipi cha kukipa kipaumbele barabara kibao bado mbovu ukajenge mafly over nakubalia na mdau wa dili na za kijijini ili wasafirishe mazao wakulima halafu usizarau mtu kutokana na eneo rangi au kabila iyo ni saini ya kukosa akili timamu hasa kwa mtanzania kama unata amia rwanda kwa mtu akiishi kusoma mtwara hana nafasi ya kutoka ndio nyie mnakimbilia ulaya na saudia arabia mnazani ndio maisha wakati kijijini kwangu moshi kuna watu dasilamu hawaijui na wanapesa mbaya mwisho hakuna zambi kubwa kama kujizarau mwenyewe na vile vile kama ulifeli kuingia ud usimind sio mwisho wa maisha na mcheza kwao hutunzwa na heri mkate mkavu wa nyumbani kuliko nyama ya shari ya pengine walisema wazee mdau njiro a-town

    ReplyDelete
  14. MUNGU ATUSAIDIE TUWEZE KUTANUA MJI/MIJI YETU NA TUACHE UTARATIMBU WA KUJENGA KILA KITU MAHALIPAMOJA. HUWEZI KUAMIHI BADO KUNAWATU/WANAINCHI WANAENDA SOKONI KARIAKOO/MADUKANI/KATIKATI YA MJI KUTOKA UBUNGO NA MBEZI LOUIS N.K (FOLENI MASAA 5 MWENDO WA KWENDA NA MASAA 5 KURUDI)ILI KUJIPATIA MAHITAJI MUHIMU. HUO MUDA NI GHARAMA KUBWA KUPITA "UJENZI WA HIZO BARABARA" (KWASABABU VIONGOZI HAWAJALI/HAWATAKI KUFIKIRIA/WAVIVU WA KUFIKIRIA

    ReplyDelete
  15. Wazo langu kwa Serikali jengeni mikoani kwa ramani ya kisasa kama Mtwara, Tanga, Bagamoyo, ZNZ, Moro, Dom, Mwanza, Arusha, Moshi, Mbeya na kadhalika. Mikoani kuna sehemu nyingi za kujenga kama hivi sababu kuna sehemu za uwazi sio Dar, Dar mpaka waanze kumoboa wata2wekea ucku. Na wakianza kujenga waanze mikoani na Dar iwe ya mwisho, sababu wakianza kuijenga Dar kila m2 atakuja Dar, ila wakianza kujenga Mikoani ata wa2 wa Dar watahama na kuamia mikoani itakayojengwa kisasa. Bongo hamna bara bara ndio maana kuna foleni. Nimetembeala mikoa kadhaa Tz, nimeona magari mengi yapo dar na Dar bara bara sio nyingi mashimo kiboa hivi hawa wakuu wa mkoa wanafanya nini? Wanashindwa ata kufix mashimo ya mikoa yao? Hivi wanajua kwanini wamechaguliwa? Pambafu poteza muda bure, iba ela ya uma.
    Nawakilisha Kigogo

    ReplyDelete
  16. HIVYO VITU VINAHITAJI PESA HATUWEZI KLUJENGA KITU KAMA HICHO HATUNA PESA, SIYO SIRI HUO NI UKWELI, KAMA MADINI PESA YOTE INALIWA NA WAGENI UNADHANI TUTAWEZAJE KUJENGA VITU KAMA HIVYO!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  17. Flyovers Dar zinawezekana kabisa! Nawapinga kwa nguvu zote wale wote wanaosema vingine.

    Unajua, hivi vitu vimeshatumiwa sana na nchi zingine na zime-prove kuwa;

    1. Zinajengeka, na
    2. Zinafanya kazi.

    Wala hamna haja ya kusema kuwa local contractors hawana ujuzi kwani ni kitu kinachofahamika kwamba barabara zote za maana (na hata za kawaida) mara nyingi hujengwa na ma contractor wa nje. Akina kajima, Konoke, Mowlem wote wanaweza kujenga hizi flyovers.

    Tuunge mkono nia ya Raisi wetu ya kupunguza hizi foleni. Bila kufanya hivyo sasa hivi, hali itakuwa ni mbaya sana hapa Dar.

    ReplyDelete
  18. mpaka zijenge Kenya na sisi ndio tuige kujenga flyovers sawa???...
    siwe mna akili fupi... kitu mpaka kifike Nairobi ndio sisi tuanze... achane hizo wanandugu hicho ki2 kinawezekana ila tu nchi yetu kila kitu ni siasa 2u ndio maana Kenya wanatuzindi kwa kila kitu....Wenzetu India wanacopy kutoka Ulaya then wakenya wanakopi kutoka India then na sisi 2nakopi kutoka Kenya ndio maana kila siku 2po nyuma 2u....

    ReplyDelete
  19. Mdau wa juu hapo, kudizaini ni rahisi sana, kuna makampuni chungu mziam wanaweza kukusaidia sio lazima tuwe na elimu hio nyumbani. Tatizo sio dizaini bali feza. Midomo inasema tuna uwezo, benki kuu an serikali ya CCM inasema Kuchinehi.

    ReplyDelete
  20. keep dreaming!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  21. Ukweli ni kwamba serikali inapoteza mabilioni ya hela kutokana na hizo foleni, ni rahisi sana watu ku-argue kwamba no need ya kuwa na fly overs, huko kijijini kunazalisha mazao kiasi gani? And brings the goverment how much revenue?
    Its true we dont have engineer competitive enough to engage into this kind of construction,but you can always bring chines contractors, they have ability to do this. They are doing this in Kenya right now for their new bypass highway project.

    ReplyDelete
  22. sio kwmba ma architectures wetu hawajadesign barabara kama hizo tatizo sio wataalamu tatizo pesa za kutekeleza huo mradi kwa mujibu wa serikali yetu wanatuambia hakuna, kama mpaka leo tumeshindwa kujenga daraja la kivukoni mpaka kigamboni ambapo ni mita chache tu je ndo tutaweza kutekeleza huo mradi? hiyo ni ndoto na itachukua mda sana kutimia, wataalamu tunao tatiza pesa.

    ReplyDelete
  23. Ukitaka fly-over hela yako tu! Hata toka kitandani kwako kwenda sebuleni hela yako!
    Ma-engineer hawatoi hela, hela zinatolewa na Serikali nyambafu wewe!
    makandari wapo dunia nzima wa kuzijenga, ndo bado upo darasani au???

    ReplyDelete
  24. Anony wa 1203 nakupa tano...

    Hivi ule mpango wa makao makuu kuwa dodoma uliishia wapi? Uliyetoa hii mada hukufikiri kwa kina na umeishia kuona kuwa wahandisi ndio mbumbumbu, hapo umekosea...

    Fly over si suluhu ya foleni, kwa ufupi tu ila ukitawanya huduma muhimu ndio suluhu. Serikali ikiamua kuamia dodoma mbona dar mambo yatakuwa mswano. Pata picha mawaziri, makatibu, wafanyakazi wa mawizara yoote hapa mjini wamehamia dodoma unajua ni magari mangapi yamepungua mjini? Fanya tafiti... Au kwa sasa chukulia kuwa TRA wamehamisha ofisi zote za kulipia kodi kwenda bunju, tegeta, mbagala, gongo la mboto, kibamba, unafikiri kutakuwa na foleni mjini pale?

    Tafakari kwa makini kabla ya kutuhumu wahandisi, na unakosea kuwatuhumu wahandisi maana si wao wanaopanga miji bali kuna watu wa taaluma hiyo ambao wanaitwa Town Planners, hawa wakishapanga ndio mipango hii hupelekwa kwa wahandisi kwa ajili ya utekelezaji... Katika hili ifahamike pia kuwa wanasiasa wa nchini humu hawaheshimu sana maamuzi ya wanataaluma hasa wahandisi, watu wa mipango miji na kadhalika na ndio maana nchi inajikuta ikipata changamoto kubwa za kitaaluma. Master plan ya jiji ilifanywa miaka ya 1970s and 80s juu ya ukuaji wa jiji lakini mapendekezo yake hayakuzingatiwa na ndio hapa tumefikia... Pia unakumbuka miaka hiyo hiyo wanataaluma wengi walikmbia nchi? Ni kwa sababu ya maslahi yalikuwa madogo, pia taaluma zao zilikuwa hazipewi umuhimu unaotakikana, na huko walikoenda wameonekana ni vinara katika taaluma zao na wanasifa kubwa...Mfano wa nchi walizoenda ni Botswana na Namibia..

    Mimi ni mhandisi na ninasimama kama mhandisi. Nakushauri usikurupuke jipange....

    ReplyDelete
  25. SWALI MOJA LA MSINGI........ZITABOMOLEWA NYUMBA NGAPI?......mana hilo msilifungie macho kwa maflyover yenu......halafu kumbukeni ujenzi wa twin towers ulivyoiishi kwa watu kushikana uchawi mpaka ikapelekea wengine kugeuzwa mbuzi za kafara.......leo FLYOVERS!

    ReplyDelete
  26. wewe acha utani kwetu napo toka mimi hatuna hata barabara moja ya rami sasa hizo tutaweza wapi? kwanza watujenge kigoma kutoka kibondo kasulu mpaka kigoma kaka ikinyesha mvua kiama sijui kwanini wanatufanyia hivi

    ReplyDelete
  27. Kabla ya kufikiria kujenga fly overs hebu tuangalie hizi barabara mpya zinazojengwa, mfano shekilango road, ilitakiwa ipitishe magari 4 kwa wakati mmoja, lakini ikajengwa vilevile kama zamani, matokeo yake foleni mbaya mno. Hali kadhalika Sam nujoma na Mandela Road, upana ule hautoshi, tunahitaji barabara pana zaidi. Nchi hii si masikini kama tunavyofikiri, tupunguze matumizi makubwa ya serikari na ubinafsi wa viongozi. Hayo tunayoyaona kama ndoto yanawezekana.

    ReplyDelete
  28. SAMAHANI HUU NI MWAKA WA UCHAGUZI HATUWEZI KUWABOMOLEA WANANCHI WETU WAPENZI HAWATATUELEWA KWENYE UCHAGUZI.

    ReplyDelete
  29. tutafika tu

    ReplyDelete
  30. 'insanity' is doing the same thing the same way over and over again and yet one expect different result. Hii si issue ya nyumba ngapi zivunjwe au ugumu gani uliopo...Ila ni lazima hili lifanyike soon or later... Kwa mimi jambo la msingi ni walio na wajibu huu wanajua wanachofanya...au ni sifa tu ya muda wanaitafuta... Maana yangu ni kwamba the same people we are expecting them to implement this, are yet to address the basic fundamentals like barabara nyingi kwenye njia moja, barabara zetu za mitaani, mifumo ya umeme, maji na mawasiliano, madimbwi ya maji, uchafu e.t.c. What if wahusika wakiamua kuweka lami majority ya barabara za mitaani like Oysterbay (imagine Mbezi beach, kinondoni, sinza, magomeni, boko, bungu etc zenye barabara za lami katika mitaa). Patrick ameongelea juu ya uwezo! I beleave uwezo upo, kifedha na kitaaluma, ila kwa nini flyover iwe jangwani, au akiba? na isijengwe kimara au mbezi mwisho, kinyerezi au boko kipawa au mwenge...People and ofcoz business will move any where as long as infrastructure is there. Angalia hiyo picha vizuri...notice eneo iliyochukuwa...na kimsingi hii ni more less like one way type. The 8-style is even worse...ikimaanisha kwamba ubungo flyover means no tanesco station no more..and probably stand ya mkoa pia itabidi ihamee...

    Recommendation:
    The flyovers shouldnt focus on already congested city, where the problem is not on the traffic load but the load distribution (time a car spent in a road to find its way to either parking place or through road to pass) but to focus kwenye maeneo mapya kabisa ambapo siyo nafasi ya kutosha tu, ata uwezo wa kudesign na kupunguza uharibifu wa vile vichache tulivyonavyo ni mkumbwa...
    ---------

    ReplyDelete
  31. ASANTE SANA MDAU WETU KUTOKA NIGERIA KWA MCHANGO MARIDHAWA.TAFADHALI TUJADILI MADA ILIYOWEKWA MBELE YETU NA TUSIJADILI WATU.WAZUNGU WANA MSEMO WAO:"KATA KOTI LAKO KULINGANA NA KITAMBAA CHAKO".
    HUU WAKATI UFAAO KWA MADHAMANA WETU KUKAA NA WAHANDISI WETU ILI WALITAFUTIE SUALA FOLENI MUAFAKA KWA KUWA ATHARI ZAKE KIUCHUMI NI KUBWA SANA.HII NI HASARA KUBWA KUTUMIA ZAIDI YA DAKIKA 150 KUTOKA UWANJA WA NDEGE HADI MTAA WA SAMORA JIJINI DAR ES SALAAM.WAKATI ULIOPITA NILWAHI KUSIKIA MRADI WA BARABARA ZA MZUNGUKO WA PETE PEMBEZONI MWA JIJI LA DAR ES SALAAM.NAONA KAMA MRADI HUO UNAENDELEA KWA UJENZI WA BARABARA ZA JANGWANI HADI UBUNGO,MBEZI LUISI -KINYEREZI-BANANA-KITUNDA HADI MBAGALA RANGI TATU.JET CORNER-YOMBO VITUKA-BUZA HADI TANDIKA.TABATA-VINGUNGUTI-KIWALANI-YOMBO HADI TANDIKA.MBEZI LUISI HADI TEGETA.UWANJA WA NDEGE-GONGO LA MBOTO-KISARAWE HADI MLANDIZI.KWA UCHUMI WETU NA MISAADA YA WAHISANI TUNAWEZA KUPUNGUZA FOLENI KWA KUBORESHA BARABARA ZA PEMBEZONI KWA KIWANGO CHA CHANGARAWE NA LAMI.KILA MWAKA WA FEDHA MANISPAA ZETU ZIJIWEKEE MALENGO YA KUJENGA,KUFUFUA,KUBORESHA NA KUDUMISHA BARABARA ZAKE.KILA KATA IWE NA KAMATI YA MAENDELEO YA MIUNDO MBINU KWA AJILI YA KUSIMAMIA MIRADI YA BARABARA KATIKA KATA.

    ReplyDelete
  32. JE NI KWELI KUWA VIONGOZI WETU AMBAO MPO MADARAKANI HAMUYAONI MATESO HAYA YA FOLENI YANAVYODIDIMIZA UCHUMI WA NCHI YETU NA KUWACHOSHA MASKINI WAOBANANA KWENYE MADALADALA BILA HEWA YA KUTOSHA NA JOTO LA DAR ES SALAAM?AU HIKI NI KILIO CHA SAMAKI BAHARI NA MACHOZI YAKE YANAISHIA HUMOHUMO?

    ReplyDelete
  33. Utendaji wa serikali kuu ukihamishiwa rasmi Dodoma nakuambia Dar itakuwa tambarare.Lakini hapa ni suala la kuthubutu na wala siyo ukosefu wa nini.

    ReplyDelete
  34. SM, lakusikitisha ni kwamba hata tulizo zikuta kama za mwananyamala na magomeni sasahivi ni vumbi/tope kali

    ReplyDelete
  35. Sasa SM wewe unafikiria nini? shida ya watu wetu ni kudhubutu! Hakuna anayetaka kudhubutu kufanya kitu kipya. Kwa hiyo wote ni 'insane'. Inabidi tuwe na watendeje ambao mzee zaidi ana miaka 30. labda hiyo itafaa

    ReplyDelete
  36. DAILY ECONOMIC LOSS = {[(ACTUAL FUEL FROM AIRPORT TO SAMORA)-(FUEL AT 60 KMPH FROM AIRPORT TO POSTA)]*(COST OF UNIT FUEL)* (NUMBER OF CARS IN THAT ROUTE OR SIMILAR) + [(AVERAGE HOURLY RATE)* 3 LOST HOURS ON TRAFFIC JAM PER DAY] * NUMBER OF PEOPLE MOVING FROM SUBURBS TO CITY CENTER}

    ANNUAL ECONOMIC LOSS = COST OF BUILDING ALL DAR FLYOVERS + ALL STREET ROADS + AJIRA ZA KUFA MTU

    ReplyDelete
  37. Yaani huyu mtoa mada ameona kwamba wahandisi hawapo bongo au anamaanisha nini kuweka kwenye mabano (kama wapo). kwa akili yake finyu na ndogo sana ameona kuwa foleni hapa Dar es Salaam inasababishwa na wahandisi. Kwa kweli haya mawazo hafifu kabisa, umefumania hiyo picha na kwa akili yako unadhani kwa ujenzi kama huo foleni zitaisha Dar. pole sana, sijajua una proffessional gani ila mambo mengine yanahitaji macho na akili ya kawaida tu kuyafumbua. Wabongo tunaumiza akili bure tu kuwaza flyover kwa mji kama Dar, maana hata zikijengwa hazitasaidia chochote kama bado serikali haina mawazo mengine ya kupunguza ajali za barabarani zaidi ya kutengeneza matuta ya viazi kwenye barabara. Mtajenga fly over halafu baadaye juu ya flyover mtatengeneza matuta makubwa kama la Stop over, kuna msaada hapo. Labda zijengwe flyover za kuvukia kwenye matuta ya viazi yanayowekwa barabarani.

    ReplyDelete
  38. huyo jamaa wa kwanza hapo juu nadhani hana akili kabisa, eti sisi watanzania elimu yetu ndogo kujenja flyover kama hizo..tuna wataalam wengi tu wapo nje ya nchi na ndani pia, kwani kujenga flyover kunahitaji nini zaidi ya plan na good engineers? nigeria kuna flyovers, ivory coast, mozambique na hata addis ababa sasa wao wamewezi sisi tushindwe tuna nini? kila siku kesi za mafisadi wanaoiibia hii nchi mabilioni ya pesa sasa hayo mabilioni yanatoka wapi? harafu eti sisi ni masikini..kwa kweli hakuna njia nyingine ya kutatua tatizo la foleni hapo dar zaidi ya hili la kujenga flyovers..wadau mnasemaje? tanzania si masikini na wataalam tunao...

    ReplyDelete
  39. Tatizo sio kuwezekana au kutowezekana, tatizo letu hatuna nia ya kufanya hayo mambo na ndio maana tunaona kama hatuwezi, tukiwa na nia kila kitu kinawezekana.....

    ReplyDelete
  40. M-Nigera fikiria upya! Unajua argument yako haina tofauti na kushangaa wagonjwa wa akili walivyozagaa Dar! Ina maana ma-dokta wazalendo hawawezi kutibu au?

    ReplyDelete
  41. nchi ya wenda wazimu watu wa planning ambao wako poor hawana influence hwawezi kupropose proposal zao zikubalike implememntation ifanyike watu ganihao...viongozi nao vipofu wanenda nchi za wenzao hawajifunzi...no one is thinking big than stilling our money...hizi barabara zilitakiwa kuwa zimetengenezwa miaka kumi iliyopita viongozi gani hawna wivu wa maendeleo haya....

    wewe michuzi na vidampa vyako nibanie na huu ujumbe si umezoea!!


    XYZ

    ReplyDelete
  42. Candid ScopeMarch 09, 2010

    USHAURI MUAFAKA SI KUFANYA YALE YALIYO NDANI YA UWEZO WETU KIUCHUMI. PESA YA KUJENGEA DARAJA MOJA INA UWEZO WA KIUTENGENEZA BARABARA YA UREFU WA KM 20 -30.

    KWA MANTIKI HIYO UJENZI WA BARABARA ZAIDI JIJINI AMBAZO UWEZO UNATURUHUSU KIUCHUMI NDO SULUHISHO. TUNAHITAJI BARABARA NYINGI ZINAZOVUKA TOKA MBAGALA KINDONDONI NA TEMEKE ILI MAGARI YAWE NA UHURU WA KUCHAGUA NJIA ZA KUPITA ILI KUPUNGUZA MSONGAMANO.

    KUWE NA HIGHWAY INAYOUNGANISHA DAR NA TANGA ILI MAGARI YAENDAYO MIKOA YA KASKAZINI YAPITIE HUKO KUONDOA MSONGAMNO MOROGORO ROAD.

    PIA BARABARA YA PUGU IJE KUTOKEA MOROGORO.

    KWA AWAMU YA KWANZA BARABARA HIZI ZAWEZA ZIWE ZA KIWANGO CHA KUSHINDILIWA KOKOTO ILI KUWEZA KUMUDU UANDAAJI WAKE KADIRI YA UCHUMI UNAOTURUHUSU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...