ukumbi wa mkutano huo wa kahawa

Mheshimiwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Stephen Wassira (wa pili kutoka kushoto), akiwa na Wajumbe wengine kwenye Mkutano huo ni Bw. Pius Ngeze, Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa (TCB) Adolf Kumburu, Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Professa James Terri, Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa zao la Kahawa (TACRI) na Bwana Yusuf Kashangwa, Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London.

Kama mmojawapo wa wadau wakuu wa zao la kahawa na bidhaa zake, Tanzania iliwakilishwa vyema kwenye Mkutano wa wadau wa bidhaa zitokanazo na zao la kahawa duniani, uliofanyika Nchini Guatemala, Amerika ya Kati kuanzia 26 Februari hadi Machi 5, 2010.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mheshimiwa Stephen Wassira. Wajumbe wengine walikuwa ni Bw. Pius Ngeze, Mwenyekiti wa Bodi ya Kahawa (TCB) Adolf Kumburu, Mkurugenzi Mkuu wa TCB, Professa James Terri, Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa zao la Kahawa (TACRI) na Yusuf Kashangwa, Mkurugenzi wa Kituo cha Biashara cha Tanzania, London.

Lengo kuu la Mkutano huo lilikuwa ni kujadili mikakati endelevu kwa zao na biashara ya kahawa duniani. Kutokana na mada 31 zilizotolewa na wataalam mbalimbali, somo lililoweza kupatikana katika Mkutano huu, linaweza kugawanyika katika maeneo yafuatayo:

Changamoto kubwa na nyingi ziko kwa wazalishaji na kwamba soko kwa bidhaa za kahawa lipo, na halijatoshelezwa.

Hata walaji wenyewe wameshaziona changamoto zilizopo na kwamba kuna hatari ya uzalishaji kutokuwa endelevu ili kukidhi mahitaji yao. Hivyo nao wamebuni mikakati ya kukabiliana na hali hiyo na hasa kwa kuwasaidia wakulima kwa mikopo, teknolojia na masoko.

Changamoto zinazowakabili wazalishaji ni pamoja na mabadiliko ya hali ya hewa, gharama kubwa za uzalishaji ikilinganishwa na kipato kwa wakulima, kilimo kwa ujumla hakiwavutii vijana na hasa kwenye kahawa kutokana na uhaba wa ardhi na bei ndogo apatayo mkulima wa kahawa.
Jawabu la changamoto hizo lilionekana kuwa kuna haja ya kubuni mikakati mbalimbali kwa kila nchi ya kukabiliana nazo.

Hivyo Serikali katika nchi husika, hazina budi kuchukuwa hatua mbalimbali za kuinua uzalishaji wa kahawa kwa kuwasaidia wakulima ili waweze kuinua vipato vyao na kuwawezesha kupunguza umaskini.

Mambo ambayo Serikali zinashauriwa kufanya ni pamoja na :

- Kuwapunguzia gharama za uzalishaji wakulima kwa kutoa ruzuku

kwenye pembejeo, mitambo na mbegu bora.

Kuwajengea mazingia wakulima ya kupata mikopo nafuu, kama wafanyavyo Kenya, India na Colombia.
Kuboresha hali ya miundo mbinu vijijini ili kupunguza gharama za usafirishaji.
Kuendelea kugharamia tafiti za zao la kahawa na hasa kwa lengo la uzalishaji wa mbegu bora zenye tija na zinazoweza kuhimili ukame na magonjwa.

Mkutano huo uliofunguliwa na kufungwa na Rais wa Guatemala Alvaro Colon Cuballeros ulihudhuriwa na wajumbe wasiopungua elfu moja na mia mbili. Hii ni mara ya tatu kufanyika Mikutano kama hii chini ya Mkataba wa 2001 wa bidhaa za Kahawa (ICA2001). Mikutano iliyopita ilifanyika katika miji ya London 2001 na Brazil 2005.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Huyu waziri wetu ndo maana wanamwita "MIKE TYSON" mcheki alivyo-serious, yaani anafaa kweli kuwa internal affairs minister.

    ReplyDelete
  2. Tujipigie debe tupate uenyeji wa mkutano huo. Ni $$$ zitaingia kwa kupitia ugeni wa walima kahawa.

    ReplyDelete
  3. Yupi ni yupi katika hii picha...kwa maana waliotajwa ni wengi kuliko waliomo pichani, au na mpiga picha naye kajitaja? Safi lakini, Kilimo Kwanza

    Mnywa Kahawa
    Kyabakali

    ReplyDelete
  4. Mbona wamekasirika?

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  5. Nagal WashngtonMarch 09, 2010

    Kweli hata mimi nampongeza Kikwete kwa kumchagua Huyu Waziri wewe embu muangalie mkali hata kwenye kupigwa picha ina maanisha hataki mchezo sijui kama wajuu wake wako watundu iweje wakulima wakimuona lazima
    KILIMO KIWE KWANZA

    ReplyDelete
  6. duh! ana sura nzito!!

    ReplyDelete
  7. KATIKA MKUTANO HUO WATANZANIA WALILIDI KWA SUTI.

    ReplyDelete
  8. Waliotajwa hawapo pichani na waliopo hawajatajwa. Huyo wa kulia baada ya waziri ni Balozi Ali Mchumo. Yeye kwa sasa ni Mkuu wa Common Fund for Commodities (Netherlands), na yupo kwenye shirika hilo akiwakilisha serikali ya Tanzania. Watanzania tuko juu!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...