Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Aisha Kigoda akifuatana na Bi Amina mlemavu asiyeona alipotembelea makazi ya wazee na watu walioathirika na ukoma kijiji cha Sukamahela, wilayani Manyoni leo.
Naibu Waziri akisalimiana na mmoja wa wakazi wa makazi hayo katika nyumba zilizokarabatiwa hivi karibuni na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Baadhi ya wakazi wa makzi hayo pamoja wa wananchi wa kijiji cha Sukamahela wakicheza ngoma ya Kigogo katika mkutano wa hadhara ulofanywa na Naibu Waziri Dk. Aisha Kigoda.
Wananchi wa kijiji cha Sukumahela wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizra ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Aisha Kigoda kwenye mkutano wa hadhara ulofanyika kwenye viwanja vya makzi ya wazee na watu wenye ulemavu wa ukoma ya Sukamahela.Muuza mafagio alisitisha kutembeza bidhaa yake akajumuika kumsikiliza.
Naibu Waziri akisalimiana na Bi Christina Lameck makazi wa kijiji cha Maweni, katika hospitali ya Kilimatinde,Hospitali ya Kilimatinde iliyoanzishwa mwaka 1929 na inayomilikiwa na Kanisa la Anglikana hutoa huduma za afya wa wakazi wengi wa wilayani hao. Picha zote na Mdau Cathy Sungura


kijiji cha sukumahela!! watu hapo hawatunzi hela?
ReplyDeleteUchaguzi mkuu Oktoba unakaribia. Tukae mkao wa kula. Ni hayo tu
ReplyDeleteMdau wa Mbezi