Habari ya Kazi Ankal,
Mimi ni mdau mkuu wa blog wako, kuna shida ambayo huwa inanitatiza sijui kama ni mi peke yangu au hata baadhi wateja yamewakuta haya.
Mwaka jana Benki ya Exim imetambulisha huduma mpya au akaunti mpya inaitwa FAIDA akaunti kutokana na matangazo yao wanaonyesha kwamba ukipata hiyo kadi kuna faida nyingi ikiwemo ku nunua bidhaa kwenye mtandao (on-line purchasing), haya matangazo yamenishawishi kufungua akauti ya FAIDA, sasa mpaka leo hii asubuhi hii najaribu kuweka details ya hiyo Faida Card ambayo ni Debit Master Card naambiwa kuwa ajili kwa kununua bidhaa "You have entered an invalid number or partial credit card or debit card number. Please check your entry and try again".
Tafadhali naomba wahusika wa Exim bank watupe statement yao kuhusu hilo suala, kwa sababu wametufanya tuhamishe fedha kutoka kwenye benki nyingine na kuweka kwenye hiyo account tukitaraji kwamba tuta purchase on-line kumbe hamna kitu, sasa huu sio uongo wa ki macho macho na kupoteza uaminifu wenu kwenye jamii ya watanzania?

Nawasilisha Meza kuu....

Wako Mteja wa Faida na Mdau wa Blog ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Pole kwanza kwa hilo ! kwa ufahamu wangu nilizima active hiyo kadi kupitia online bank account au uende bank wafanye hivyo..nadhani ungejaribu kuwasilina nao kabla .Ahsante.

    ReplyDelete
  2. SASA WEWE KWA NINI USIWAULIZE HAO EXIM....WABONGO ACHENI UOGA WENU, HAWA JAMAA MOJA WAPO YA KAZI YAO NI KUWAELEWESHA WATEJA MATUMIZI YA PRODUCT ZAO, SASA KAMA UNAOGOPA KUWAULIZA BASI WATAKUWA WANALIPWA BURE..USIOGOPE KAKA, WANAONGEA HATA KISWAHILI KAMA LUGHA INGINE INASUMBUA....

    ReplyDelete
  3. hizo kadi za bongo hazinunui online ya nje bwana. umeliwa. kadi za bongo nyingi haziko katika mtandao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...